Uchambuzi: Tunahitaji ushindi Taifa leo, kocha aanze na mfumo upi?

Uchambuzi: Tunahitaji ushindi Taifa leo, kocha aanze na mfumo upi?

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
34,181
Reaction score
41,563
Ushindi haupatikana bila mikakati thabiti, ukiwa kama mpenzi na shabiki wa soka je unafikiri kocha wetu aanze na mfumo upi?

1. Mfumo wa 5-4 -1 Kujilinda na kupeleka mashambulizi ya kushitukiza kupitia kwa Msuva kutumia zile mbio zake.

2. Mfumo wa 3-5-2 Huu ni kujilinda kama hamna mpira, zile wingi back zinarudi nyuma kufanya cover na mabeki kuwa 5. Lakini hama wana mpira basi zinajaa pembeni na kufanya mfumo kuwa 3- 3- 4 (Striker 4), hasara ya huu ukishapoteza mpira mbele ni kama umekimbiza mwizi hujafunga mlango - faida mnakuwa na ball position kubwa mno hence mnatengeneza chance za kutosha.

3. Mfumo wa miaka yote wa 4-4-2 huu ndiyo unaotumika na makocha wengi duniani, hautashambulia sana wala hutajilinda sana - mfumo huu unatakiwa kuwa na mido wenye uwezo kubwa kale kati.

Kushinda tumesema ni lazima, Je unafikiri Samata aanze kama mido nyuma ya Boko ama aanze kushoto ? sababu kulia kuna Msuva ?

Mwisho nipe list yako? Je utapenda kiraka wa kimataifa Nyoni aanze kati?
 
MOSALA ELEKA MALOBA NA EBELE

Hatuchomoki kwa Wakongo Leo
 
Back
Top Bottom