​kila ninapoangalia kampeni za wagombea wa ccm iwe ubunge au urais huwa naona 60%ya sera zao ni malalamiko either juu ya maendeleo duni tuliyonayo au malalamiko dhidi ya wale wanaoitwa mafisadi na wazembe
mpaka muda huu magufuli ni waziri wa ujenzi na mjumbe wa baraza la mawaziri,Jk ni rais wa nchi hii nae analalamika,samia vile vile
swali langu ni je,kulalamika huku maana yake nini? Kwamba
A)serikali ya ccm imeshindwa Kabisa kuongoza nchi
B) ccm imechoka au imesahau kama inaongoza nchi kama vile mwenyekiti wake alivyosahau kama ni mwenyekiti wa mkutano Mkuu wa ccm
Magufuli anagombea afanye nini kilichoshindwa kufanywa na jk?mbona haelezi ccm na Jk walishindwaje na yeye atawezaje?
Je inatosha kutuambia serikali ya magufuli itafanya hiki na kile bila kutuambia serikali ya kikwete imeshindwaje?