Katika kukomesha swala lililokithiri la rushwa, CCM imetoa ahadi ya kuanzisha mahakama maalumu katika kushughulikia swala hilo , maoni yangu ni kwamba swala hilo halijafanyiwa utafiti wa kina, kwani suluhuhisho hapa si kuanzisha mahakama bali ni kuboresha mahakama zilizopo,Serikali imeshindwa kujenga nyumba za mahakimu, mahakimu wanaishi kwenye nyumba za kupanga, baadhi ya sehemu hakuna majengo ya mahakama, vyombo vya uendeshaji ikiwemo ofisi ya TAKUKURU, DPP na hata polisi Serikali haijafanikiwa kuboresha miundombinu. Sasa ikiwa mahakama zilizopo wameshindwa kuziboresha je ni sahihi kuanzisha nyingine ? ikiwa kama mabaraza ya Ardhi na Kazi mashauri yake yaliondolewa toka mhimili rasmi wa mahakama lakini mpaka leo mashauri yanakaa mda mrefu mahakamani je ni sahihi kufungua mahakama nyingine ? Je na ikiwa tutafungua mahakama maalumu kulishughulikia swala la rushwa kama suluhisho, Je CCM haioni kuwa kuna ulazima mahakama nyingine maalumu zinapaswa kufunguliwa kwa kushulikia matatizo ya madawa ya kulevya, Ujangili, Kubaka, Mauaji,na Ujambazi kwa vile nayo yameshamiri sana katika jamii yetu. Ukisoma vizuri hoja hii utatambua kuwa swala hapa ni kuboresha mahakama kimiundombinu na kimkakati na siyo kufungua mahakama nyingine