anjo
JF-Expert Member
- Jun 13, 2009
- 299
- 97
Kuna maswali mengi kuliko majibu!
Matatizo au kero zinazoelezwa na Mhe. Magufuli zinatatanisha sana. Hivi Tanzania ina serikali? Kama serikali ipo, inaongozwa na chama gani?
Kero anazoongea kama chama chake kimeshindwa kuzitatua kwa miaka kadhaa, je yeye ataweza kwa miaka 5 au 10?
Itakuwa vigumu sana kwa watu wanaojua kuchambua maswala ya kisiasa kukubaliana na staili ya Mhe. Magufuli. Hawezi kulaumu chama chake na viongozi waliomtangulia na akaonekana ataleta tofauti yoyote wakati akichaguliwa atafanya kazi na watu walewale. Naona kama vile Mhe. Magufuli ameiba sera ya upinzani na amesahau lawama ni za chama chake.
Kwa hotuba anazozitoa, kama kweli kuna upinzani, CCM imeshawapunguzia 50% ya muda wao wa kampeni. Kama watu wanaiba dawa, wananyanyasa raia, matumizi mabaya ya ofisi, ufisadi, nk. ni nani wa kulaumiwa? Bila shaka si Upinzania maana wamekuwa wakitoa shutuma hizo kwa serikali ya CCM.
Hii ni dalili mbaya kwa CCM na upinzani wachukue haya mapungufu kwa kujizatiti.
Anjo