Taifa lolote liliondelea au linalotaka kuendelea kwa kasi lazima litilie mkazo mambo makubwa matatu: kukusanya kodi, kujenga viwanda na kuimalisha nishati.
Kodi kodi kodi, serikali yako Mh. John Joseph Pombe Magufuli ambayo utaiunda baada ya October, kwa kua naamini wewe ndio utakae shinda na kua Rais wa Jamhuri ya Muungano itilie mkazo ukusanyaji wa kodi, serikali isipokusanya kodi hatutapata maendeleo ya uhakika na kupunguza utegemezi. Na hapa kodi ikusanywe kwa kupunguza mianya ya kodi na kuakikisha makampuni makubwa hayakwepi kodi si kwa kuwaongezea kodi wafanyakazi. Serikali yako ikikusanya kodi itaweza kuwekeza kwenye miradi ya kijamii na kiuchumi kwa asilimia kubwa hivyo basi kusukuma maendeleo ya Tanzania mbele.
Viwanda ni jambo lingine la muhimu Mh. Raisi unaesubili kuapishwa. Tuakikishe tunaweka mazingira mazuri ya kujenga viwanda kwenye miji yetu ili vijana wapate ajira. na hapa serikali inaweza kuja na mkakati wa kupunguza urasimu kwa wawekezaji na kujenga maeneo maalumu ya viwanda, kutumia Public-Private Partnership ili tuwe na viwanda ambavyo vitachochea ukuaji wa kilimo pia,
Pia Mh, Raisi suala la nishati ni zito na lamuhimu sana, bila nishati ya uhakika nchi hii haiwezi kuona mapinduzi ya viwanda. Tunataka nishati nyingi na ya bei nafuu ili kuchochea maendeleo ya taifa letu.
Tanzania yenye neema italetwa na John Pombe Magufuli.
Kwa hakika Manelezu umepotoka kumtukuza mtu binafsi kupita kiwango. Huyo alikuwepo ndani ya serikali zilizopita kwa zaidi ya miaka 20 na hakuna lolote kati ya hayo alilioonyesha ana uwezo wa kulisemea, kulipigia chapuo wala tekeleza.
Kujisahau ndio tatizo sisi watanzania tulio wengi, akijitokeza kiongozi hata katika mitaa, kata n.k zetu basi sisi wote hurudi nyuma na kuanza kumtukuza na kumuachia kila kitu badala kulia mmoja kuchukua nafasi yake kama raia kutimiza wajibu wake wa kuhakikisha mambo yote yankwenda sawia.
Tunatakiwa kubadilika badala ya kumtegemea binadamu mmoja kila mmoja atimize wajibu wake pale alipo.
Utawala bora na maendeleo chanya hutokana na uwepo wa mifumo imara ya
"Checks and balances".
Kutokana na kuimarika kwa upinzani hapa nchini na kuikaba koo kweli kweli CCM, CCM imelazimika kukubali shingo upande kuwa na mgombea ambaye hajalelewa ndani ya CCM, hajawahi kushika wadhifa wowote wa uongozi ndani ya CCM; kwa maana ingine hana tabia na miendendo ya KICCM.
Kwa maneno mengine licha ya CCM kupinga pendekezo la Tanzania kuwa na wagombea binafsi kwa zaidi ya miongo miwili; upinzani umefanikiwa kuifanya CCM kutafuta na kumsimamisha mgombea binafsi ndani yake yenyewe, ndio maana hivi sasa kauli mbiu ya wanaCCm ni CHAGUA MAGUFULI NA SIO CHANGUA CCM.
Kwa kuwa binadamu ni kiumbe chenye mapungufu na kwa kuwa
"Power Corrupts and abosolute power corrupts absolutely" maana yake "Madaraka hulevya na madaraka yasiyo na mipika hulevya maradufu" tunatakiwa tumiarishe taasisi zetu zilizofanikisha Tanzania kuingia katika mabadiliko haya kwa maana ya vyama vya upinzani ili viweze kuendelea kuongoza mabadiliko hayo kwa ajili ya ukombozi wa watanzania.
Tukifanya makosa ya kuwatukuza na kuwaabudu watu binafsi kama tulivyafanya siku za nyuma tutarejea katika mifumuo kandamizi kama ilivyokuwa huko nyuma.