Elections 2015 Uchambuzi wa ahadi za mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dr. John Pombe Magufuli

Elections 2015 Uchambuzi wa ahadi za mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dr. John Pombe Magufuli

#VITA DHIDI YA RUSHWA
Serikali itakayoongozwa na Magufuli itaendeleza mapambano ya rushwa kwa kuziba mianya ya rushwa ktk taasisi za umma,kuchukua hatua kali kwa waendeleza rushwa.
Pia kuanzisha mahakama maalumu kwaajili ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi sambamba na kushughulikia kwa ukali tatizo la ubadhilifu,wizi wa mali za umma na matumizi mabaya ya madaraka.
#Chaguo sahihi ni Dr. John Pombe Magufuli kwa mabadiliko ya kweli.
 
#USIMAMIZI BORA
Taswira ambayo magufuli anaweza kuirejesha bila wasiwasi ni usimamizi thabiti wa serikali na nidhamu ya utendaji ndani ya serikali.taswira hi inakuja kwa kuangalia wizara alizopitia magufuli usimamizi wake umekuwa bora sehemu zote alizopita
#chagua john pombe magufuli kwa maendeleo ya kweli
 
sisemi neno, ila mambo haya asijisahau akayafanya mombasa
 
Attachments

  • 1443425252144.jpg
    1443425252144.jpg
    26.2 KB · Views: 80
#VITA DHIDI YA RUSHWA
Serikali itakayoongozwa na Magufuli itaendeleza mapambano ya rushwa kwa kuziba mianya ya rushwa ktk taasisi za umma,kuchukua hatua kali kwa waendeleza rushwa.
Pia kuanzisha mahakama maalumu kwaajili ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi sambamba na kushughulikia kwa ukali tatizo la ubadhilifu,wizi wa mali za umma na matumizi mabaya ya madaraka.
#Chaguo sahihi ni Dr. John Pombe Magufuli kwa mabadiliko ya kweli.

Hayo mapambano ya Rushwa na Uhujumu uchumi atakayoyaendeleza Magufuli yaliazishwa lini na nani Tanzania....!!!!?
 
Kwasababu ya kuokota dodo kwenye michongoma. Lowassa toshaaa
 
Ndg yangu hawa watu hawasikii....subiri Magufuli awaonyeshe tar 25/10/2015
 
Magufuli anatosha watanzania wenzangu,kwa nini tudanganywe na genge la watu wachache wanachumia matumbo yao,sisi wetu magufuli mwadilifu,mchapa kazi na mwenye uzalendo wa kweli,sio ngoyai mfanyabiashara,hatumtaki huyu kwa kuwa atatupoteza
 
Mpambanaji Wa RUSHWA, UFISADI, UBADHILIFU WA MALI ZA UMMA NA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA / OFISI!! Leo Anapita Majimbo Ya Watuhumiwa Wa Vitendo Vya Ufisadi, Ubadhilifu Na Matumizi Mabaya MAMLAKA!! Tumeona Akiwapigia Kampeni HADHARANI, Akiwaomba Watanzania Wa Majimbo Hayo Wawachague Wawe WABUNGE Ndani Ya SERIKALI Yake!! Kuanzia Bariadi ANDREW CHENGE, Muleba Kusini Kwa ANNA TIBAIJUKA, Kule Mara PROF. MUHONGO!! Sasa Huo Ujasiri Hatautoa Wapi!!!!??? Jidanganyeni Wenyewe Tu!! Watanzania Tumeshatambua MFUMO Wa CCM Hauwezi Kuwachukulia Hatua Kali Za Kisheria!! Wakijiuzuru Tu Basi, Tena Wanaombwa Na Mtu Aliyewateua!! Kinachofuata Ni Kuondoa MFUMO Mzima Na Kikundi Chao!!!CCM Wanalindana Kwa Kuogopana Tu, Kila Mmoja Ana Uchafu Wake, Ambao WENGINE Wanaujua!! Hivyo Si Rahisi Kumuonya Na Kuchukuliana Hatua Za Kinidhamu Na Kisheria!! Ndio Tunaona Mafisadi Wa EPA Waliombwa Warudishe MAMILIONI Waliogawana!! Hadi Leo Mafisadi Waliogawana Mabilioni Ya ESCROW KUPITIA Benki 1, Tu Ndio Wametajwa HADHARANI Na Nyingine KIMYAA Hadi Kesho!! Je, Huyo Magufuli Wenu Atakuja Ataweza Kuwataja Na Kuwashitaki!!!?? Je, Ataweza Kuwataja Na Kuwashitaki Waliogawana Mabilioni Kule MEREMETA, DEEP GREEN, WALIOHUSIKA KUNUNUA MABEHEWA CHAKAVU!!?? Kama Ni Kweli Mpambanaji Wa Vitendo Hivyo Mbona Hadi Hajawashitaki Wale WALIOHUSIKA Kumnunulia Meli Mbovu Kwa Billion 8 ( Mv Dar) Hadi Limekwama Kutembea, Na YEYE Akiwa Waziri Wa Wizara Husika Na Alishiriki Kutuonyesha Watanzania Ni Meli Bora!! LEO Eti Aje Kupambana Na MFUMO Huo!! Ndorooobai!! Angeonyesha Mf. Ktk Wizara Yake Kwanzaa Tumpime!!! Hivyo Propaganda Za KUOMBA Kura Tu, Ili CCM Iendelee KUWATAWALA Watanzania!! Watanzania Wameshatambua Kuwa Ni Hadithi Tu!!
 
Taifa lolote liliondelea au linalotaka kuendelea kwa kasi lazima litilie mkazo mambo makubwa matatu: kukusanya kodi, kujenga viwanda na kuimalisha nishati.

Kodi kodi kodi, serikali yako Mh. John Joseph Pombe Magufuli ambayo utaiunda baada ya October, kwa kua naamini wewe ndio utakae shinda na kua Rais wa Jamhuri ya Muungano itilie mkazo ukusanyaji wa kodi, serikali isipokusanya kodi hatutapata maendeleo ya uhakika na kupunguza utegemezi. Na hapa kodi ikusanywe kwa kupunguza mianya ya kodi na kuakikisha makampuni makubwa hayakwepi kodi si kwa kuwaongezea kodi wafanyakazi. Serikali yako ikikusanya kodi itaweza kuwekeza kwenye miradi ya kijamii na kiuchumi kwa asilimia kubwa hivyo basi kusukuma maendeleo ya Tanzania mbele.

Viwanda ni jambo lingine la muhimu Mh. Raisi unaesubili kuapishwa. Tuakikishe tunaweka mazingira mazuri ya kujenga viwanda kwenye miji yetu ili vijana wapate ajira. na hapa serikali inaweza kuja na mkakati wa kupunguza urasimu kwa wawekezaji na kujenga maeneo maalumu ya viwanda, kutumia Public-Private Partnership ili tuwe na viwanda ambavyo vitachochea ukuaji wa kilimo pia,

Pia Mh, Raisi suala la nishati ni zito na lamuhimu sana, bila nishati ya uhakika nchi hii haiwezi kuona mapinduzi ya viwanda. Tunataka nishati nyingi na ya bei nafuu ili kuchochea maendeleo ya taifa letu.

Tanzania yenye neema italetwa na John Pombe Magufuli.
 
Kwa hakika Manelezu umepotoka kumtukuza mtu binafsi kupita kiwango. Huyo alikuwepo ndani ya serikali zilizopita kwa zaidi ya miaka 20 na hakuna lolote kati ya hayo alilioonyesha ana uwezo wa kulisemea, kulipigia chapuo wala tekeleza.

Kujisahau ndio tatizo sisi watanzania tulio wengi, akijitokeza kiongozi hata katika mitaa, kata n.k zetu basi sisi wote hurudi nyuma na kuanza kumtukuza na kumuachia kila kitu badala kulia mmoja kuchukua nafasi yake kama raia kutimiza wajibu wake wa kuhakikisha mambo yote yankwenda sawia.

Tunatakiwa kubadilika badala ya kumtegemea binadamu mmoja kila mmoja atimize wajibu wake pale alipo.

Utawala bora na maendeleo chanya hutokana na uwepo wa mifumo imara ya "Checks and balances".

Kutokana na kuimarika kwa upinzani hapa nchini na kuikaba koo kweli kweli CCM, CCM imelazimika kukubali shingo upande kuwa na mgombea ambaye hajalelewa ndani ya CCM, hajawahi kushika wadhifa wowote wa uongozi ndani ya CCM; kwa maana ingine hana tabia na miendendo ya KICCM.

Kwa maneno mengine licha ya CCM kupinga pendekezo la Tanzania kuwa na wagombea binafsi kwa zaidi ya miongo miwili; upinzani umefanikiwa kuifanya CCM kutafuta na kumsimamisha mgombea binafsi ndani yake yenyewe, ndio maana hivi sasa kauli mbiu ya wanaCCm ni CHAGUA MAGUFULI NA SIO CHANGUA CCM.

Kwa kuwa binadamu ni kiumbe chenye mapungufu na kwa kuwa "Power Corrupts and abosolute power corrupts absolutely" maana yake "Madaraka hulevya na madaraka yasiyo na mipika hulevya maradufu" tunatakiwa tumiarishe taasisi zetu zilizofanikisha Tanzania kuingia katika mabadiliko haya kwa maana ya vyama vya upinzani ili viweze kuendelea kuongoza mabadiliko hayo kwa ajili ya ukombozi wa watanzania.

Tukifanya makosa ya kuwatukuza na kuwaabudu watu binafsi kama tulivyafanya siku za nyuma tutarejea katika mifumuo kandamizi kama ilivyokuwa huko nyuma.
 
Kwani Tanzania ya leo ni sawa na ile ya miaka 54 iliyopita? Je, vyama vingi vina umri gani? Je, unajua kwamba lowassa amekuwa waziri kwa miaka 35? Je, umejaribu kumuuliza alifanya nini?

Wapinzani wameazima viongozi. Lowassa ni zao la CCM. Sumaye Anayesemekana kuandaliwa uwaziri mkuu ni zao la CCM. Hata timu ya kampeni ni CCM. Mafuriko ya wabunge wa CCM. Unaongelea upinzani upi? Wa kwenye keyboard au huu wa jf?

Wacha kuishi kwa nadharia

Mkuu nimesoma hii comment yako nikasikitika sana...kwa kifupi tu we ni kichwa maji kabisa....yaani hujui kila kitu...
 
Magufuli hata sera zake amezikita ktk ubabe na vitisho visivyo na maana, labda nikuwahadaa wananchi zaidi, Namfuatilia sana huyu bwana naona CCM wameamua kaburi lao lichibwe na magufuli,anapo tishia watu akidhani anawavutia wananchi kumbe anajifunua surayake halisi na ubabe wakishamba, huyu bwana hafai hata 15% anaweza asipate
 
Back
Top Bottom