Kwa ujumla wewe umechambua hotuba yake kienyeji hasa. Labda lengo lako lilikuwa tu kukosoa lakini huna uelewa wa kutosha kuhusu uliyoyasema. Labda kwa ufupi tu, ujue yafuatayo:
1) kabla ya awanu hii, mifuko ya hifadhi ya jamii, ilikuwa ikijiendesha na kutoa fao la kujitoa bila tatizo. Tatizo limekuja kutokana na serikali kukopa kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwenye mifuko hii na kisha kutokuwa tayari kulipa madeni. Awamu hii ilipoanza, haikutaka kutoa pesa kuilipa hii mifuko. Wakaamua kuweka sheria ya kuzuia fao la kujitoa, siyo kwa nia ya kumsaidia mfanyakazi bali ni kwa vile hakutaka serikali ilipe madeni kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii. Hii ni mbinu duni sana ya kukabiliana na deni.
2) Kuhusu kuwalipa fidia watu waliobomolewa nyumba, hili lipo wazi sana. Sielewi lina uhusiano gani na utaifishaji wa majengo ya wahindi mwaka 1967 wakati wa utekelezaji wa Azimio la Arusha. Kuwalipa waliobomolewa nyumba kupisha ujenzi wa barabara, ni haki ya walioathirika na ipo kwenye sheria zetu za nchi. Kila anayeondoshwa kwaajili ya kupisha mradi wowote ule, uwe wa serikali, mtu binafsi, kampuni au taasisi yoyote, anastahili fidia. Kutokuwalipa fidia, Rais Magufuli amevunja sheria. Rais badala ya kuwa mfano wa kufuata sheria, anakuwa mfano mbaya wa kukiuka sheria.
3) Kuvutia uwekezaji, nashangaa kusikia kuwa eti kukiwa na vivutio kwa wawekezaji, tutaangukia kwenye tatizo lile lililotokana na sera ya Rais Mkapa ya kuvutia wawekezaji. Ni tatizo gani? Msipende kudanganywa na Rais kuhusiana na uwekezaji, hasa kwenye sekta ya madini. Mambo mengi anayoongea Rais ameyaumba, hayana uhalisia. Rais Mkapa alifanya kazi kubwa sana, na alipata mafanikio makubwa sana, ambayo huyu wa sasa hawezi kufikia hata 25%.
Linganisha performance ya Rais Mkapa na huyu wa sasa kwenye:
1) FDI
2) Employment growth rate
3) Inflation control
4) GDP growth rate
5) Management systems installation
Katika hayo yote, huyu wa sasa hamfikii Rais Mkapa hata kwa 25%.
Sent using
Jamii Forums mobile app