Uchaguzi 2020 Uchambuzi wa hotuba ya Lissu - Kawe

Uchambuzi wako hauna mashiko.
 
Kwa ujumla wewe umechambua hotuba yake kienyeji hasa. Labda lengo lako lilikuwa tu kukosoa lakini huna uelewa wa kutosha kuhusu uliyoyasema. Labda kwa ufupi tu, ujue yafuatayo:

1) kabla ya awanu hii, mifuko ya hifadhi ya jamii, ilikuwa ikijiendesha na kutoa fao la kujitoa bila tatizo. Tatizo limekuja kutokana na serikali kukopa kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwenye mifuko hii na kisha kutokuwa tayari kulipa madeni. Awamu hii ilipoanza, haikutaka kutoa pesa kuilipa hii mifuko. Wakaamua kuweka sheria ya kuzuia fao la kujitoa, siyo kwa nia ya kumsaidia mfanyakazi bali ni kwa vile hakutaka serikali ilipe madeni kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii. Hii ni mbinu duni sana ya kukabiliana na deni.

2) Kuhusu kuwalipa fidia watu waliobomolewa nyumba, hili lipo wazi sana. Sielewi lina uhusiano gani na utaifishaji wa majengo ya wahindi mwaka 1967 wakati wa utekelezaji wa Azimio la Arusha. Kuwalipa waliobomolewa nyumba kupisha ujenzi wa barabara, ni haki ya walioathirika na ipo kwenye sheria zetu za nchi. Kila anayeondoshwa kwaajili ya kupisha mradi wowote ule, uwe wa serikali, mtu binafsi, kampuni au taasisi yoyote, anastahili fidia. Kutokuwalipa fidia, Rais Magufuli amevunja sheria. Rais badala ya kuwa mfano wa kufuata sheria, anakuwa mfano mbaya wa kukiuka sheria.

3) Kuvutia uwekezaji, nashangaa kusikia kuwa eti kukiwa na vivutio kwa wawekezaji, tutaangukia kwenye tatizo lile lililotokana na sera ya Rais Mkapa ya kuvutia wawekezaji. Ni tatizo gani? Msipende kudanganywa na Rais kuhusiana na uwekezaji, hasa kwenye sekta ya madini. Mambo mengi anayoongea Rais ameyaumba, hayana uhalisia. Rais Mkapa alifanya kazi kubwa sana, na alipata mafanikio makubwa sana, ambayo huyu wa sasa hawezi kufikia hata 25%.

Linganisha performance ya Rais Mkapa na huyu wa sasa kwenye:
1) FDI
2) Employment growth rate
3) Inflation control
4) GDP growth rate
5) Management systems installation

Katika hayo yote, huyu wa sasa hamfikii Rais Mkapa hata kwa 25%.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo akina Lissu walimzushia maneno ya uongo kuwa kaingia mikataba ya unyonyaji?
 
Haya Mambo ya Lissu niya kawaida Sana hayamfanyi awe rais labda udiwani
 
Kabisa anaongozwa na mihemko,Lissu kaongelea fidia kwa wahanga wa serikali ya pombe
 
Huyu mtu alikuwa ughaibuni kwa miaka mitatu hajui muziki wa Magufuli. Ana generalise mambo, ati atafuta kodi 15 kwa wafanyabiashara halafu hazitaji. Wenziwe hata hawamwambii hao wafanyabiashara unaodhani ni mtaji wa kura, Magu alishakutana nao ana kwa ana tena wa nchi nzima na kumalizana nao juu ya kero zao mbalimbali.
 
Kiukweli nchi hii haki haipo, mfano kwenye mifuko ya hifadhi za jamii hela zinaliwa sana, hivi wale waliofukuzwa kwa vyeti feki hela zao za hifadhi zimeenda wapi? Wizi mtupu.lissu akifanikiwa kushinda afuatilie hili
 
Mkuu wafanyabiashara moyoni hawamkubali magu kamwe, ni machoni tu
 
Haya Mambo ya Lissu niya kawaida Sana hayamfanyi awe rais labda udiwani
Kawaida kwako mkuu, kwa mifuko ya hifadhi ya jamii inatumika kudhoofisha wafanyakazi badala ya kuwaimarisha.serikali inachukua pesa zao kujengea miradi.hatari
 
Mkuu wafanyabiashara moyoni hawamkubali magu kamwe, ni machoni tu
Wewe wasema, Magufuli ndio mlezi wa chemba ya wafanya biashara inaliyoasidiwa na Mkapa, anakutana nao mara kwa mara na vinywa vyao vimejaa sifa za Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…