Uchambuzi wa Mkataba wa kuendesha bandari ya Dar es Salaam kati ya Tanzania na Dubai

Uchambuzi wa Mkataba wa kuendesha bandari ya Dar es Salaam kati ya Tanzania na Dubai

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nime usoma na ku translate na nimeulewa vyema.
Poleee wee km umedandia baada ya kudadavuliwa ni wee pekee.
Kwa akili zipi ulizonazo wewe zaidi ya ushabiki maandaz? 😆😆😆

Ukivyoudoma.ukaelewa nini? Miaka 100 au?
 
Kumbe ubaguzi tu unakusunbuwa, wewe kwenu wapi?

"Kule zenji" kama ghuelewi mkataba na Dubai walianza na eyapoti, wa bandari ukafatia.

Mbona ni zamani mpaka imekuwa historia, wewe ulikuwa umelala?
Ghuelewi ❎= uelewi ☑️

Eyapoti❎ = Airport ☑️
 
Ehe ehe tupeni faida mnazopata nyie omba omba wahead! Tuondoleeni biashara ya utumwa hapa!
Kwa hayo mawazo yako hautoacha kuwa mtumwa.

 
Ghuelewi ❎= uelewi ☑️

Eyapoti❎ = Airport ☑️
 
Ngoja waarabu waichukue bandari ya Dar es salaam ndo mtajua hamjui.
Kazi zoote za maana zitakuwa zao, na happy ndo mtatumikishwa Kama watumwa,?
Nasema hivi mtakuja kuwa watumwa ndani ya nchi yenu.
Eti tumeshindwa kuisimamia hiyo bandari hadi tunaleta waarabu waje wasimamie, kweli?
 
Mnaingizwa mkenge na nketa mada na nyinyi mnauvaa kichwa kichwa, Mleta mada ameleta vipande tu vya mkataba na kuwalisha maoni yake.

Aweke mkataba kamili.

Huyu ni wale wale tu, kina ndugai na bashiru.
Kwanini mleta mada peke yake? Wewe unaetetea, kwanini na wewe usilete hivyo unavyosema tukaona au unatoa kwa utashi wako? Sasa kuna maana gani ya kumpinga mleta mada ilihali angalau yeye kajitahidi kuleta hata kipande cha huo mkataba.

Sio wajibu wenu / wako / serikali kuweka wazi watu wakajadili kwa uwazi? Kila mtu akaona? Ingekuwa ni vyema na wewe ukaleta angalau vipande vya hayo unayotetea tukaona pia?
 
faiza faiza faiza FaizaFoxy hua na appreciate sana unachosemaga hapa jf ila kwa hili umefeli. Wewe unawaza positive unasahau kuna negative tena negative n nyng kuliko positive. Mkataba hauna duration, mkataba hautavunjwa hata kama wakifanya makosa makubw kias gn, hakuna mkataba wenye vipengere hivo unaotegemea ukubebe .Obvious wanajua madudu watayoyafanya ndo mana wamesema hata wakoseeje mkataba hauvunjwi yote n kujidefend tu.Unawaza ndio sawa tnaingia kimataifa lakn je tnafaidikaje na huko ilhali mwenzetu ndio anaetuongoza na anatotal control. Naona kbs tz inakua dumping place yao and this marks the official beginning of neo- colonialism in tz.
 
Huu mkataba unaiingiza rasmi Tanzania kwenye biashara za Kimataifa.

Wenye uelewa wa biashara za Kimataifa watalielewa hilo.

Mambumbumbu wa biashara mtabaki bandari imeuzwa, imeuzwa.

Imeuzwa kupelekwa wapi?
Bibi acha kuzingua, ina maana kabla ya hapo hakuna biashara za kimataifa zimekuwa zinafanyika kupitia hiyo bandari? huna uelewa kwamba hiyo bandari inapitisha mizigo ya mataifa mbalimbali yanayotuzunguka, au ni biashara gani ya kimataifa unayoongelea. Acha kuleta porojo zako za udini kwenye mambo yenye maslahi mapana kwa taifa.​
 
Mkataba Kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya DPW ya Emirates Dubai umeacha maswali mengi na kuamsha hisia za kudai Katiba mpya kwa nguvu zote.

Ni mkataba ambao ulisainiwa kwa mwendokasi bila kuchukua tahadhari juu ya madhara yake yaliyo dhahiri. Mkataba huu haukubaliki kwa sababu nyingi Sana.

Moja , ni mkataba wa milele kwa sababu hauna ukomo. Najua wapo waliosema ni wa miaka 100 na wapo waliosema ni wa miezi 12.

Hawa wote sijui wametoa wapi huo muda wa mkataba. Ibara ya 23 ya mkataba na randama zake (appendixes) zake hakuna popote zinaonyesha mkataba huu ni wa muda gani. Hii inaweza kutafsiriwa kuwa ni mkataba wa kudumu.

Ni kweli unaweza kuwa miaka mia lakini pia hakuna Cha kuzuia uwe wa miaka 1000.

Pili, mkataba huu unanguvu kuliko Sheria za Tanzania pamoja na Sheria za kimataifa ( Takes precedent over national and international law)

Mathalani Ibara 23( 4) hairuhusu kuvunja mkataba huu hata pakiwa na ukiukwaji mkubwa ( material breach) au kukitokea hali inayopelekea mkataba usitekelezeke ( fundamental change of circumstances) ambalo ni Takwa la mkataba wa kimataifa uitwao Vienna Convention on the Law of Treaties,1969 ambao Tanzania imejifunga nao.

Sasa hii tafsiri yake ni kwamba baada ya kusaini mkataba huu hata Dubai wakikiuka kabisa hatuwezi kujitoa. Hicho ni kitu Cha ajabu mno dunia itatushangaa.


Mbaya zaidi mkataba hausemi je una nafuu ili mbadala ukiachilia mbali kuvunja mkataba.

Kifungu Cha 23( 4) kinaenda mbali zaidi na kusema ikitokea sababu yeyote inayotambulika kwenye Sheria za kimataifa ya kupelekea kuvunja mkataba bado mkataba huu hautavunjwa.Tafsiri yake ni kwamba tumeingia kwenye shimo ambalo halina pa kutokea( coup de sac) .

Tatu , mawanda ( scope ) ya mkataba pia ni mapana, ni Kama hayana ukomo. Ibara ya 2(1) itaruhusu muwekezaji kujenga na kuendesha miradi ya bandari za Bahari na maziwa yote.

Mkataba unakwenda mbali zaidi hata kwenye kile kinachoitwa logistic parks na trade corridors ambazo bahati mbaya hazijatafisiriwa kwenye mkataba.

Kwa namna mkataba huu ulivyo sisi tutakuwa tumepoteza udhibiti wa bandari zote za bahari na maziwa yote.

Mkataba ungeweka wazi ni bandari zipi hasa kwa sababu kwa namna ya Sasa hata usalama wa nchi unaweza kuwekwa rehani.

Nne , mkataba hausemi sisi tutapata nini( consideration) kwa maana ya faida za mradi. Je sisi tutakusanya Kodi tu? Au tutakuwa wabia?

Tano , mkataba hauonyeshi nafasi ya mamlaka ya bandari( TPA) ni ipi katika uendeshaji wa mkataba. Kumbuka kwa mujibu wa sheria TPA ndo chombo chenye mamlaka ya kuendesha bandari zote. Sasa je mkataba huu umefuta sheria hiyo? Kwa mamlaka gani?

Mkataba hauelezei kuhusu usalama wa mapato yetu bandarini na nafasi ya vyombo vya ulinzi na usalama kwaajiri ya usalama wa nchi yetu hasa kwenye marine.

Nafasi pekee ya TPA kwa mujibu ya randama ya kwanza imeachiwa kuendesha na kusimamia " DHOW AND WHARF TERMINAL" ya bandari ya Dar es Salaam.


Sita , pamoja na kuweka kipengele Cha local content ili kunufaisha wazawa kwenye ajira na manunuzi kwenye ibara 13( 2) ibara hiyo haina maana yoyote Kwanza kwa sababu haiweki wazi kwamba threshold ya wazawa kwenye ajira itakuwaje.

Pili hata procurement( manunuzi) ya vitu au items au huduma zinazopatikana ndani hailindwi na mkataba kwa sababu kwa mujibu wa ibara ya 6(2) ya mkataba huu serikali yetu hauruhusiwi kufanya usumbufu wowote (interference) yoyote hata kwenye manunuzi yanayokiuka Sheria isipokuwa tu Kama yanahatarisha usalama( safety and security).

Sasa je wakiamua kuagiza mbao Dubai wakati hapa nchini zipo utawazuia kwa kigezo Cha usalama?

Saba , mkataba hausemi nani atawajibika kulipa fidia yoyote inayotokana na utekelezaji wa mradi pamoja na watumishi ambao ajira zao zinaweza athiriwa na mradi.

Nane , pamoja na kwamba ibara ya 26 ya mkataba inaelekea kuruhusu reservation utagundua kwa namna ibara ya 24 ilivyo imepoka kwa mkono mwingine haki ya reservation iliyopo kwenye ibara ya 26 hivyo sioni uwezekano wa nchi yetu kufanya reservation kwenye makubaliano bila kukwaza mkataba.

Kwa namna ya mkataba huu tukifanya reservation Sasa ivi inaweza kupelekea nchi iingie kwenye mgogoro wa kukiuka mkataba.

Tisa , hata kuridhiwa kwa mkataba huu na Bunge tayari umefanyika nje ya muda.

Ibara ya 25(2) ilitaka mkataba uridhiwe ndani ya siku 30 tu na leo ni zaidi ya miezi Saba.

Kumi , kwa mujibu wa ibara ya 8(3) (c ) mkataba huu ni kama unatoa umiliki wa ardhi kwa mwekezaji kinyume na Sheria ya ardhi.

Kwa mujibu wa sheria ya Ardhu Sura ya 113 Kampuni ya kigeni hairuhusiwi kumiliki ardhi Tanzania.

Tulitegemea mkataba useme ardhi zitakuwa chini ya TPA au mamlaka nyingine za serikali na wao watapata derivative rights badala ya kuwapa ardhi kwa mgongo wa lease hold.
 

Attachments

  • 27AD9A88-732F-4AE5-AF15-0AD2E0E29F23.jpeg
    27AD9A88-732F-4AE5-AF15-0AD2E0E29F23.jpeg
    55.1 KB · Views: 3
Kwa akili zipi ulizonazo wewe zaidi ya ushabiki maandaz? [emoji38][emoji38][emoji38]

Ukivyoudoma.ukaelewa nini? Miaka 100 au?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sasa km kuandika vizuri hujui, ndo ushindane na mie?? Nitolee stress zako hapa.
 
Job alikuwa jikoni huko alicho ona ndicho alichosema ww ujinga Ni hujui Mambo yabiki maandazi ...ukipewa pesa ya bando na posho unashabikia nchi ipelekwe kokote ewe mtu ww..aliamua kuuza shamba ameamua kuanza na miti na vitu vya thamani vilivyomo lakin job alisema..mwisho vikiisha na airport Nayo inafuatia , migodi...alisema job.
Mimi wangu ujinga, wewe wako ujanja mbadala uko wapi?
 
Job alikuwa jikoni huko alicho ona ndicho alichosema ww ujinga Ni hujui Mambo yabiki maandazi ...ukipewa pesa ya bando na posho unashabikia nchi ipelekwe kokote ewe mtu ww..aliamua kuuza shamba ameamua kuanza na miti na vitu vya thamani vilivyomo lakin job alisema..mwisho vikiisha na airport Nayo inafuatia , migodi...alisema job.
Uko wapi huo mkataba?

. Alikuwa jiko la mwendazake.
 
Mkataba Kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya DPW ya Emirates Dubai umeacha maswali mengi na kuamsha hisia za kudai Katiba mpya kwa nguvu zote...
This is smart thinking siyo kama wale CHADEMA na Maria Space
 
Kwanza kwanini umejitokeza leo kutetea ili Hali kesho Bunge litakaa kwa shughuli hiyo?

Kujitikeza kwako kutetea huu mkataba as an individual ndiyo kuna leta maswali. Mbona nguvu ni kubwa hivi?

Mbona kama kuna kiwewe?

Nisingeliandika kama ungekuwa unahojiwa na chombo cha habari lakini kuitisha press kutetea ndiyo wengi tunona nyie lomolomo ndiyo mnatangulizwa kuweka mamb Sawa. Ungelitulia ukasubiri kesho nafasi unayo Bungeni.

Mimi siwezi kukubali kusikia porojo zako kwenye press ili Hali mkataba huo umeandaliwa na wasomi wakubwa wanaojua namna ya kula kwa wasiojitambua.

Kweli nisikilize porojo ili Hali wewe hujui hata kutamka neno" contractual term" kwa usahihi.

Hivi mh. Msukuma ule mkataba ukiusoma wewe utaulewa unamaanisha Nini kweli?

Ndugu tulia kwanza jambo lichakatwe hizi porojo ni kwasababu tumeruhusu kuingia mjengoni Sifa moja wapo ni "anayejua kusoma na kuandika kiswahili"

Wewe siyo mtaalamu wa SHERIA

Tukienda kwa pupa, kesho akiingia Rais mzalendo akaona kuna madudu kwenye mkataba akataka kuvunja ndiyo utaona wanakamata mali zetu ZILIZOPO nje ya nchi.

Msukuma tulia kaka, Wacha bunge lipitie kesho na Bunge la wananchi nalo halipo nyuma tunafuatilia. Hatutaki yajirudie Yale ya migodi namna tulivyopigwa. Kila tukijaribu Jamaa wanakimbilia MIGA.

Msukuma Mimi Nina nusu ya umri wako, napenda nami watoto wangu wakute nchi ikiwa vizuri.

Acha tujue, je ni lifetime au ni miaka 100 au la!

Mungu ibariki Tanzania 🇹🇿
 
Back
Top Bottom