Uchambuzi wa Ndimara Tegambwage, asema “Ithibati na Press Card: Pacha au Pachanga? TUSEMEZANE”

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
KITAMBULISHO au Press Card anayobeba mwandishi wa habari, haina uwezo wa kumpa au kumwongezea elimu, maarifa wala stadi.

Tuseme hivi: Hiki ni kitambulisho tu. Hakina hata uwezo wa kukamilisha, kuongeza au hata kupunguza sifa za mwandishi wa habari. Ni kwa ajili ya kutambulishwa na kutambulika.

Bali mara hii, hupewi Press Card mpaka uwe na diploma ya/katika Uandishi wa Habari. Nadhani wahusika watataka na wataweza kuthibitisha ni kutoka chuo gani; na iwapo chuo hicho – ndani au nje ya nchi – kimesajiliwa rasmi na kina hadhi ya kutoa elimu ya uandishi wa habari.

Tuje kwenye Ithibati. Anayethibitisha kuwa unastahili kupewa Press Card, ndiye anatoa ITHIBATI – uthibitisho na ruhusa. Hii basi ndiyo maana unasikia Press Card na Ithibati vimekuwa pacha; au muzikidansa – pachanga.

Sasa kuna mpagao. Waliokuwa wakiripoti, wakifukua na kuanika taarifa, wakihariri, wakichambua, wakichora katuni, wakitangaza, wakisimamia programu mbalimbali katika redio na televisheni; waweza kupoteza ajira.

Waliokuwa wakiandika na kuhariri, huku wakilea, kuelekeza na kufunza wenye vyeti, diploma na digrii ambao walijiunga nao; waweza kupoteza sifa kwakuwa hawana vitambulisho vyenye Ithibati. Na wao hawana Ithibati. Ni kwakuwa hawana Diploma.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Ithibati (JAB), Patrick Kipangula, amekaririwa na DW – Deutsche Welle akisema (sijaona akikanusha), “…tunawashauri kama mtu hana sifa, basi ajitahidi azipate hizo sifa zilizoainishwa kisheria kisha arudi kwenye kazi yake.”

Kwa mpangilio wa maneno, Kipangula ameeleweka: Kwamba anatoa ushauri. Lakini pia, anatoa tangazo la kufukuza kazi wale wasiokuwa na diploma. Kwa kifuatacho baada ya kauli yake, ni kiza tupu.

Katika mazingira ya “chapuchapu.” Yale ya “mwendokasi.” Yale ya “nipe-nikupe.” Ya kukidhi haja. Ya kurudi haraka kuchukua nafasi yako; ninaona diploma inaweza kupatikana; lakini isiyo ya elimu ya “kiwango cha Diploma” katika uandishi wa habari.

Ni kiza kwa sababu Kipangula anayesema waende kusaka Diploma kisha kila mmoja “arudi kwenye kazi yake,” hana uwezo wa kulinda ajira za anaowaanua katika mamia ya vyombo vya mawasiliano. Wakati mwingine wanaviita vyombo vya habari, hata kama havifanyi kazi ya habari.

Miongoni mwa wanaoanuliwa kama nafaka wakati wingu likitishia kulia, wamekuwa kazini kwa miaka mitano, kumi, hata ishirini au zaidi. Siyo kwamba wamekuwa ving`ang`anizi tu. Siyo kwamba waliwekwa kwa maonesho. Hapana. Wamiliki wa vyombo vyao wanajua, wanathamini uwezo na mtaji wao.

Hao wanaoanuliwa, pamoja na kufanya kazi za uandishi wa habari, wamekuwa wakilea, wakielekeza na kufundisha wanaojiunga na vyombo vyao ambao wanakuja, ama na diploma, digrii au sifa nyingine kitaaluma.

Ni kwa hili, na ndio maana, wamiliki wa vyombo vya mawasiliano, hawajaona umuhimu wa kuwaachia. Utatupaje dhahabu chooni?

Chukua mfano huu. Wewe ni mmiliki wa chombo cha mawasiliano. Unamwacha vipi mwandishi wa habari anayeandika habari na makala zinazopigiwa mfano kwa ubora hata katika vyombo vingine; anayelea, kuelekeza na kufundisha wenzake na “wapya” wanaoingia na wenye sifa za juu za vyuoni hata kuliko yeye? Anayeweka chombo chako sokoni kwa uchambuzi, mahojiano na masimulizi?

Na huyu asingefanya yote haya kama hajifunzi. Maarifa anayowagawia wenzake hayaji kwa sala. Kutakuwepo mito na vijito anamochota ya kwake na yale anayowagawia wengine.

Mfano mwingine. Nani awezaye kuachana na mchorakatuni wa kimataifa kwa misingi kuwa hana diploma? Wahaya wanasema, “kanage nkalonde.” Tafsiri ya haraka: “Katupe nikaokote” – huku mdomo ukibinukia pembeni, jicho likilala kwa kengeza la dharau na pua ikituna utadhani inataka kushindana na Sambu – vyote vikitoa msonyo mrefu wa kusuta – mhvyyy!

Kila mmoja anakahitaji. Kila mmoja anajua hata kakikaa nyumbani, katavuna kutoka kokote duniani. Lakini kangekuwa katika chombo cha wasomaji, watazamaji na wasikilizaji; ubunifu wake – mbali na kuchora – ungerutubisha waandishi wengine, wachoraji, chombo kwa jumla, mazingira na wananchi wanaokitumia. Hukaachii hata kwa shuruti.

Kama ilivyo katika mfano wa kwanza hapo juu, wengi wa wanaoanuliwa ni watafutaji, wasakaji, wachimbaji elimu na maarifa; na ndiyo maana wana hazina ya kushiriki na wengine kutoka elimu, maarifa na hekima za wengine; vitabu/mitandao na mazingira.

Tukifika hapa, ndipo tunajiuliza: hivi katika kupata elimu na maarifa kwa walioko kazini, kuna njia moja tu, aina moja tu, mahali pamoja tu na kitu kimoja tu cha kusoma?

Kama wasiokuwa na diploma wameweza kujiendeleza na kufundisha wengine; sasa wao hawawezi kusomea hapohapo kazini kwao na kufikia viwango vinavyohitajika?

Kuna kitu kinaitwa “life-long learning” – usakaji elimu wa maisha yote. Udugu usioisha kati ya maisha ya mtu na elimu, na maarifa; au taaluma Fulani. Elimu inayoendelea au usakaji elimu usiokoma. Hawa wa “miaka mingi” kazini, na waajiri wao bado wanawahitaji; waliishaanza zamani kutekeleza mradi huu binafsi.

Hawa, wala hawapingani na Kipangula. Wanataka mjadala. Je, hawawezi kusomea hapohapo walipo – huku wanasoma na huku wanafanya kazi? Ni lazima watoke nje ya ajira zao ambazo Kipangula hana uwezo wa kuzilinda/kuzitunza mpaka warejee?

Kwa wanaoandika, ni lazima waache kuandika; kana kwamba wanafanya adhabu kwa kosa walilotenda? Ni kosa lipi? Au wawe wanaandika taarifa na habari na kubandika majina bandia; na lipyoto afanye kazi yake – hatimaye taarifa zivuje kuwa huu ni mradi wa JAB?

Kwenda shule ni muhimu, hata kwa wenye umri mkubwa. Viwango ni muhimu pia. Je, katika hili, wataalamu wa Ithibati waliwahi kufanya, au kufikiria kufanya, tathmini ya elimu, maarifa na stadi; kati ya pande hizi mbili: walimu/wataalamu wasiokuwa na diploma; na wanafunzi wao wenye vyeti, diploma na digrii? Kuna upungufu gani, wapi na kuna kitu gani cha kujifunza? Hii ilipaswa kuwa kabla ya amri za Toka! Toka!

Nani atalea, ataelekeza na kufundisha wanaoingia? Nani atalinda/atatunza nafasi za watakaokwenda “kusaka diploma” mpaka watakaporudi? Nani atakuwa anafanya kazi za wajuzi – kulinda haki na hadhi ya chombo ili serikali nyemelezi ikae mbali? Nani ataondolewa pale wasakadiploma watakaporejea; au watakuta chombo kimeyeyuka?

Je, kuna uchunguzi wowote uliothibitisha kuwa hawa wanaoanuliwa, hawana elimu au wana elimu ndogo iliyoleta madhara kwa chombo; au hata kuvunja sheria? Nani atabisha iwapo hili litaitwa ubabe na akili ya viziavizia?

Hii miaka mitano ya kupata diploma iliwekwa kwa utafiti gani ulioonesha kuwa kila mmoja atakuwa na uwezo au atawezeshwa na mwajiri wake, kwenda nje ya eneo la ajira kusaka diploma?

Hivi nani ajuaye kilichosibu waajiri na wataalamu wao katika vyumba vya habari, kutofikia lengo la kuwa na diploma katika miaka mitano kama sheria ya 2016 inavyotaka? Hakuna anayetaka kujua? Hakuna anayetaka kutaarifu? Hakuna anayetaka kusikiliza? Ni kasome…kasome!

Kuna ukweli huu. Kazi zote katika vyumba vya habari, hupita mikononi mwa maripota wa muda mrefu; maripota wakuu, wahariri wa habari; wasanifu; kaimu wahariri na wahariri wakuu. Vibarua hawa hulalamikiwa, husutwa na kulaaniwa kwa kila kosa gazetini, redioni, kwenye skrini ya TV – kila siku, kila wiki, kila mwezi, kila mwaka na siku zote.

Nina ushahidi wa wahariri wakuu, wenye digrii, ambao hawakuwa na vyeti wala diploma za uandishi wa habari. Wasikilize. Bado wanakumbuka ripota mwelekezaji, tena asiye na diploma, alivyokuwa mkali; akidai “uthibitisho” wa ulichoandika, maelezo ya anayetuhumiwa; na kukutolea jicho kali kwa kutoweka alama za uafikishaji katika andiko lako.

Wengine wanakumbuka walivyofunzwa jinsi ya kuandaa uchunguzi wa habari yoyote; kuanzia kutafuta wazo la kuandikia habari kwa chombo chochote; muundo wa hojaji, orodha za watoa taarifa, jinsi ya kukusanya data kwa ajili ya kazi yako; jinsi ya kuandika makala mbalimbali na kuwasilisha.

“Mzee Ndimara, wewe ndio uliniambia kuwa nilionekana kuwa na background nzuri. Nikueleze basi; nilipita mikononi mwa hao ambao hawana diploma lakini ni wakali wa kazi…” ameeleza binti mmoja shahidi wa kazi bora za waelekezaji katika chombo alikoanzia kazi – yeye akiwa na diploma.

Uliza baadhi ya wahariri. Watakwambia. Walifanya hivi: Walitundika diploma na digrii zao kutani. Wakaingia vyumba vya habari. Wakakaa chini ya wasio na vyeti. Wakalelewa. Wakaelekezwa. Wakafundishwa, Wakajua. Wakakua. Wakakwea madaraja. Wakawa wahariri. Wakameremeta!

Acha tunong`onezane: Baadhi ya wahariri, wanakiri kuwa hadi kustaafu, hawajawahi kufikia viwango vya baadhi ya walezi, waelekezji na walimu wao ambao hawakuwa na diploma. Wanawaenzi. Kwa nyakati zile na nyakati za sasa za kidijiti.

Kusoma ni muhimu. Nikiwa Mhariri wa Jamii kwa miaka mitano, Mwananchi Communications Limited, nilikuwa ninaongea na waandishi wa habari na kuwauliza: Lini uliajiriwa hapa? Ulikuwa unatoka wapi? Tangu umalize chuo umesoma vitabu vingapi? Msako wa elimu.

Kijana mmoja aliniambia kuwa tangu amalize masomo ya chuo kikuu na kuajiriwa – miaka mitano iliyopita – hakuwa amesoma hata kitabu kimoja. “Ni kuja kazini tu…”

Mwingine aliniambia kuwa kwa miaka mitano amekuwa akisoma kitabu kimoja ambacho hajamaliza; na chenyewe hivi sasa hajui kilipo. Niliumia sana; ingawa niliona wengine wakijisomea vitabu mitandaoni na wengine wakiwa na nakala za vitabu mikononi.

Nikashawishika kaandika makala kwa lengo la kuchochea usomaji; sasa nikipanua eneo hadi kwa wasomaji wa The Citizen – chini ya MCL. Msanifu Mkuu aliipa kichwa: If you don’t read, how do you write? (tafsiri nyembamba: kama husomi, unaandikaje/vipi/nini?). Jisomee: FROM THE PUBLIC EDITOR'S DESK : If you don’t read, how do you write?

Lakini kuna wanaosoma. Wanaojisomea vitabu mbalimbali juu ya uandishi wa habari; misingi ya uandishi kwa wanafunzi; fikra mpya juu ya uandishi katika maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano; aina za uandishi; ufukuaji taarifa, uandishi habari za usuluhishi, uandishi katika mazingira magumu, uchambuzi, uandishi wa habari za siasa… Wanapekua. Wanataka kujua. Wanajielimisha.

Turudi kwenye swali letu la awali: Kwani kusoma kuna njia moja tu, aina moja tu, mahali pamoja tu na kitu kimoja tu cha kusoma?

Mapinduzi ya kiteknolojia katika eneo hili, kwa sasa, yanatosha kuanika wenye uwezo na kuanua waliopitwa na wakati. Ni ujio huu ambao utaondoa malalamiko ya kizembe kuwa “tasnia ya habari imevamiwa.” Haijavamiwa.

Mambo ya kuvamiwa ni kilio cha walioshindwa kujifua na kujipambanua kitaaluma; wanaolialia kuwa kila mmoja mwenye simu ya smati “anajifanya” mwandishi wa habari na mpigapicha.

Ukweli ni kwamba, hao kwa mamilioni, hawafanyi uandishi wa habari. Hao wanaolalamikiwa, wala siyo waandishi wa habari. Ni WAANDIKAJI wanaofurahia kujua kusoma na kuandika; na wanaofurahia uhuru wao wa kujieleza katika mazingira tuliyopigania toka mikaka ya 1980 kwamba, “We Want A Talking Nation; A Talking People!” Tunataka kuwa na Taifa linaloongea. Watu wanaoongea!

Kwahiyo, badala ya kulialia kuwa “taaluma imevamiwa,” waandishi wa kweli wajitahidi kujipambanua, kujitofautisha na waandikaji kwa kujihusisha na mambo mazito na ya maana.

Kwa mfano, habari za uchunguzi, utawala wa kisheria, haki za binadamu, uwajibikaji kwa walioko madarakani na maeneo mengine – utawala, haki, demokrasia – maeneo yanayohitaji ufukuaji na yenye mguso kwa jamii.

Sasa maripota, wasanifu, wahariri wengi walio katika vyombo hivi vya mawasiliano kwa muda mrefu; wakiwa bila diploma lakini wakilea, kuelekeza na kufundisha wenye diploma na digrii, hawastahili kile ambacho serikali inapanga au inatekeleza. Hapana!

Wengi wao wana upeo mpana na maarifa makuu ya kuwamegea wenzao; na siyo kuacha kazi, kwenda kusaka diploma ambayo, huenda wameishaivuka kama kungekuwepo tathmini ya kazi na uwezo wao.

Hapa kuna pendekezo. Siyo langu. Langu nitalitoa mwishoni mwa andiko langu juu ya kusemezana na waandishi wa habari, watawala na wananchi/wadau. Hili ni pendekezo la baadhi tu ya wadau wa habari ambao wamesoma baadhi ya makala zangu. Hili hapa:

“Kwakuwa serikali imetunga sheria – Sheria ya Huduma za Habari 2016 – inayotaka waandishi wa habari kuwa na diploma; basi hiyo iwahusu wanaoingia kazini kwa mara ya kwanza; na wale ambao, kwa tathmini maalum, watakutwa chini ya viwango kitaaluma.

“Kwa mfano, wenye miaka minne na zaidi kazini, ambao wamekuwa walezi, waelekezaji na walimu kwa miaka mingi (minne na kuendelea); wapate mafunzo maalumu, yanayohusisha mazoezi kikazi; kwa angalau miezi mitatu (kwa mfumo wa saa mbili kwa siku tatu kwa wiki) inayofuatiliwa kwa usimamizi wa wajuzi – ya kuongeza uwezo wao na thamani ya kazi zao; huku wakiendelea na kazi zao; badala ya kutelekeza vyombo ambavyo, ama walishiriki kuunda, kulea au kuimarisha.”

Sheria hii, Sheria ya Huduma za Habari 2016, ni chafu kuliko ile Newspaper ACT ya 1976 iliyofutwa. Hii inastahili kufanyiwa marekebisho makubwa au kufutwa kabisa. Tuijadili katika andiko lijalo.

Andiko la Ndimara Tegambwage
Media Freedom Tanzania
 
Sheria hii, Sheria ya Huduma za Habari 2016, ni chafu kuliko ile Newspaper ACT ya 1976 iliyofutwa. Hii inastahili kufanyiwa marekebisho makubwa au kufutwa kabisa. Tuijadili katika andiko lijalo.📌🔨✌🏿
 
Labda niulize swali yakinifu kwa wajuzi wa taaluma ya habari, swali jepesi tu la kiweledi. Kuna waandishi wana basic certificate in journalism and public relation toka taasisi fulani iliyokuwa imeanzishwa na waandishi nguli na mahiri jijini dar mwaka fulani. Kwa umahiri wao hao waandishi nguli nchini walipika wanataaluma hao kisawasawa mpaka wakawa mahiri katika fani hii. Sasa mtu kama yule aliyepikwa na waandishi nguli na maarufu kama wale na cheti chake kusainiwa na katibu mkuu wa baraza la habari tanzania, hivi mwandishi kama yule unawezaje kumtenga kwa kuwa hana diploma wakati amefanya kazi hiyo miaka zaidi ya kumi akiwa na cerificate tu? Tena kafundishwa na wabobezi mahiri wa uandishi wa habari nchini? Ningeweza kuwataja nguli wale na taasisi yao ya habari waliyoianzisha kufundisha waandishi wapya. Kuna kigogo mmoja ni kinara wa waandishi wa habari nchini niliwahi kumuona pale japo sikuwahi kumuona akifundisha darasani, ina maana naye hazitambui certificate za waandishi waandishi waliowafundisha?
 
Tatizo waandishi wa habari wamegawanyika sana sio wamoja

USSR
 
Kuna wahariri nawajua kwa majina na media wanazofanyia kazi, mmoja kwa sasa ni bosi mkubwa wa jukwaa la wahariri. Hawa wahariri walikuwa wanapokea kazi toka kwa mwandishi asiyejulikana elimu yake ni wa cerificate, diploma au degree, kumbe walikuwa hawana kabisa hata certificate wala kuhudhuria darasa la uandishi wa habari. Ni utashi tu mtu anapenda uandishi, anakuwa na idea, anachora na kuandika kisha anapeleka kazi yake kwa mhariri wa media fulani anaipitia na kuona inafaa kuchapwa, kazi inachapishwa na huyo mwandishi anapata malipo na kuhamasika kufanya kazi bora zaidi na yenye ubunifu zaidi. Hivyo ndivyo waandishi walivyopata umahiri and then mtu anakuja kwenda chuoni akiwa tayari ana uzoefu wa kuandika. Chuoni anaenda kuongeza maarifa na ujuzi mwingine ili tu kupata sifa fulani ya kuongoza taasisi lakini kazi tayari anaijua. Watu walianza kuandika na kutangaza from zero ground, mtu hana hana hata cerificate wala mafunzo yoyote ya uandishi na utangazaji. Kwa nini sasa iwe shughuli ngumu wakati ni kipaji?
 
Hiyo sheria ya huduma ya habari ya mwaka 2016 ifutwe kabisa, ni sheria inayoua ari na moyo wa ubunifu, vinginevyo hiyo sheria itajifia yenyewe automatically kutokana na ukuaji wa kasi wa teknolojia ya habari. Ni kina nani hawa waliokuja na kuleta mawazo ya kutungwa sheria hii kandamizi?
 
Yule bosi baada ya kupanda ngazi akafika juu ndio akang'oa ngazi ili wengine wasifike juu, wakwee kwa taabu kufika juu, huu ni uendawazimu
 
Yawezekana mkachangia kwa hisia lakini ukweli ni kuwa tasnia ya habari ilifana iheshimiwe Badala yake makapuku walijaa news room na kupelekea wenye sifa KUKOSA nafasi Ili halikubariki WAENDE wakasome, mtu km masanja, zembwela kitenge na wengine warudi shule
 
**** mmoja hivi sasa ana nafasi kubwa huko serikalini. Nafikiri ni Afisa habari wa mkoa.
Baada ya digrii yake aliajiriwa na gazeti kubwa maarufu la.kiswahili wakati huo, akiwakilisha ofsi ya mkoa x.
Katika kipindi cha miezi tisa ya kutumikia.nafasi hiyo, msomo.hiyu aliandika story mbili ambazo pia ziliishia kuwa "filler".
Katika kituo hocho hicho cha mkoa x kulikuwa na "reporter" kijana ambaye bila.shaka hakufika kidato cha kwanza.
Huyu kijana alikuwa akiongoza kwa kuandika "vigongo" vikiibika kila.mara kama.lead stories.
Alichikiwa sana na vigogo wa serikali kwa kuibua mambo yao, lakinj pia akipigwa vita kubwa na mkuu wake.wa kituo.kwa kilichokuwa kikewlezwa.kuwa kujipendekeza kwa wahariri na kumpendelea!
Msomi.huyo alijifuta kazi.mwemyewe na leo yuko mstari wa mbele kupigia chapuo ithibati kama.ndiyo inayoandika habari, huku akikificha kwenye kichaka cha usomi na mgongo wa serikalini ambako hawana cha kuonyesha, baada ya kuua MAELEZO.NA SHIHATA.
 
Yawezekana mkachangia kwa hisia lakini ukweli ni kuwa tasnia ya habari ilifana iheshimiwe Badala yake makapuku walijaa news room na kupelekea wenye sifa KUKOSA nafasi Ili halikubariki WAENDE wakasome, mtu km masanja, zembwela kitenge na wengine warudi shule
unaanza vipi kuwachuria kitenge na zembwela kindezi hivi? Spoti leo na super mix unavijua vema vipindi hivi? Mjuba acha dharau
 
Nilisoma na kijana mmoja toka pemba, huyo kijana alikuwa na elimu ya msingi tu lakini aliibuka wa pili kwa kufanya vema kwenye uandishi akiwaacha mbali wenye elimu ya chuo kikuu. Hizi diploma na degree ni mbwembwe tu wala hazifanyi vema field na si vibaya mtu kuwa nazo watu wakasome tu ila si kutimua na kuzuia wenye vipaji kuchora, kuandika na kutangaza
 
Hii sheria ya huduma za habari haikuangazia mukhtadha wa habari kwa upana wake, walikurupuka na kuitunga na hatimaye JAB ikaja kuanzishwa, ni balaa ifutwe
 
Hii ndio taaluma pekee nayoona watu wake hawataki kwenda darasani mnachekesha sana ukitaka kuwa mwandishi usiekuwa na hizo qualifications wanazotaka huzuiwi act kama "kanjanja journalist" post makala zako Facebook na Tweeter au hapa jukwaa pendwa kama sie akina kambwinde ila kama unataka kuwa pro nenda darasani fani yenu nyi jamaa mnapenda kulialia sana yule jamaa aliekuwa anajitambulisha kwa jina la kitoweo alikuwa anatangaza anakaa juu ya meza kaa litoto kumbe darasa hamna, nendeni darasani nyie acheni kujiliza
 
Nilisoma na kijana mmoja toka pemba, huyo kijana alikuwa na elimu ya msingi tu lakini aliibuka wa pili kwa kufanya vema kwenye uandishi akiwaacha mbali wenye elimu ya chuo kikuu. Hizi diploma na degree ni mbwembwe tu wala hazifanyi vema field na si vibaya mtu kuwa nazo watu wakasome tu ila si kutimua na kuzuia wenye vipaji kuchora, kuandika na kutangaza
Hao wenye hizo elimu wakienda " field" practical, jubaki kushangaa. Wanayofundišhwa vyuoni na ukweli ulivyo.
Baya zaidi hao "Walimu" hawajitokezi kuka kuangalia maendeleo ya wanafunzi wao na hata kuongea na wasimamizi wao.
wanachofanya ni kuchukua madodoso waliuotumia babu zao na kuwapatia hao wanafunzi ili zijazwe na hao wasimamizi
Yaliyoko kwenye madososo ni tofauti na kilichopo, wao wamejifungia vyuoni.

Wati wasome lakini wanachosoma kinakwendana na hali ilivyo.mtaani? Wanatoa mazao ambayo yakionyesha karatasi ya digriii ya ufaulu wa juu wanaweza kujisimamia?
Mnafeli wapi kuelewa umuhimu wa wa kipaji na uzoefu na kung'ang'ania elimu ya kuingia asubuhi na kutoka jioni kwa miaka 2 ili kupata diploma?
 
Hii ni taaluma mtambuka, sio kama ualimu na udaktari
 
Hii ni taaluma mtambuka, sio kama ualimu na udaktari
 
KITAMBULISHO au Press Card anayobeba mwandishi wa habari, haina uwezo wa kumpa au kumwongezea elimu, maarifa wala stadi.

Tuseme hivi: Hiki ni kitambulisho tu. Hakina hata uwezo wa kukamilisha, kuongeza au hata kupunguza sifa za mwandishi wa habari. Ni kwa ajili ya kutambulishwa na kutambulika.

Bali mara hii, hupewi Press Card mpaka uwe na diploma ya/katika Uandishi wa Habari. Nadhani wahusika watataka na wataweza kuthibitisha ni kutoka chuo gani; na iwapo chuo hicho – ndani au nje ya nchi – kimesajiliwa rasmi na kina hadhi ya kutoa elimu ya uandishi wa habari.

Tuje kwenye Ithibati. Anayethibitisha kuwa unastahili kupewa Press Card, ndiye anatoa ITHIBATI – uthibitisho na ruhusa. Hii basi ndiyo maana unasikia Press Card na Ithibati vimekuwa pacha; au muzikidansa – pachanga.

Sasa kuna mpagao. Waliokuwa wakiripoti, wakifukua na kuanika taarifa, wakihariri, wakichambua, wakichora katuni, wakitangaza, wakisimamia programu mbalimbali katika redio na televisheni; waweza kupoteza ajira.

Waliokuwa wakiandika na kuhariri, huku wakilea, kuelekeza na kufunza wenye vyeti, diploma na digrii ambao walijiunga nao; waweza kupoteza sifa kwakuwa hawana vitambulisho vyenye Ithibati. Na wao hawana Ithibati. Ni kwakuwa hawana Diploma.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Ithibati (JAB), Patrick Kipangula, amekaririwa na DW – Deutsche Welle akisema (sijaona akikanusha), “…tunawashauri kama mtu hana sifa, basi ajitahidi azipate hizo sifa zilizoainishwa kisheria kisha arudi kwenye kazi yake.”

Kwa mpangilio wa maneno, Kipangula ameeleweka: Kwamba anatoa ushauri. Lakini pia, anatoa tangazo la kufukuza kazi wale wasiokuwa na diploma. Kwa kifuatacho baada ya kauli yake, ni kiza tupu.

Katika mazingira ya “chapuchapu.” Yale ya “mwendokasi.” Yale ya “nipe-nikupe.” Ya kukidhi haja. Ya kurudi haraka kuchukua nafasi yako; ninaona diploma inaweza kupatikana; lakini isiyo ya elimu ya “kiwango cha Diploma” katika uandishi wa habari.

Ni kiza kwa sababu Kipangula anayesema waende kusaka Diploma kisha kila mmoja “arudi kwenye kazi yake,” hana uwezo wa kulinda ajira za anaowaanua katika mamia ya vyombo vya mawasiliano. Wakati mwingine wanaviita vyombo vya habari, hata kama havifanyi kazi ya habari.

Miongoni mwa wanaoanuliwa kama nafaka wakati wingu likitishia kulia, wamekuwa kazini kwa miaka mitano, kumi, hata ishirini au zaidi. Siyo kwamba wamekuwa ving`ang`anizi tu. Siyo kwamba waliwekwa kwa maonesho. Hapana. Wamiliki wa vyombo vyao wanajua, wanathamini uwezo na mtaji wao.

Hao wanaoanuliwa, pamoja na kufanya kazi za uandishi wa habari, wamekuwa wakilea, wakielekeza na kufundisha wanaojiunga na vyombo vyao ambao wanakuja, ama na diploma, digrii au sifa nyingine kitaaluma.

Ni kwa hili, na ndio maana, wamiliki wa vyombo vya mawasiliano, hawajaona umuhimu wa kuwaachia. Utatupaje dhahabu chooni?

Chukua mfano huu. Wewe ni mmiliki wa chombo cha mawasiliano. Unamwacha vipi mwandishi wa habari anayeandika habari na makala zinazopigiwa mfano kwa ubora hata katika vyombo vingine; anayelea, kuelekeza na kufundisha wenzake na “wapya” wanaoingia na wenye sifa za juu za vyuoni hata kuliko yeye? Anayeweka chombo chako sokoni kwa uchambuzi, mahojiano na masimulizi?

Na huyu asingefanya yote haya kama hajifunzi. Maarifa anayowagawia wenzake hayaji kwa sala. Kutakuwepo mito na vijito anamochota ya kwake na yale anayowagawia wengine.

Mfano mwingine. Nani awezaye kuachana na mchorakatuni wa kimataifa kwa misingi kuwa hana diploma? Wahaya wanasema, “kanage nkalonde.” Tafsiri ya haraka: “Katupe nikaokote” – huku mdomo ukibinukia pembeni, jicho likilala kwa kengeza la dharau na pua ikituna utadhani inataka kushindana na Sambu – vyote vikitoa msonyo mrefu wa kusuta – mhvyyy!

Kila mmoja anakahitaji. Kila mmoja anajua hata kakikaa nyumbani, katavuna kutoka kokote duniani. Lakini kangekuwa katika chombo cha wasomaji, watazamaji na wasikilizaji; ubunifu wake – mbali na kuchora – ungerutubisha waandishi wengine, wachoraji, chombo kwa jumla, mazingira na wananchi wanaokitumia. Hukaachii hata kwa shuruti.

Kama ilivyo katika mfano wa kwanza hapo juu, wengi wa wanaoanuliwa ni watafutaji, wasakaji, wachimbaji elimu na maarifa; na ndiyo maana wana hazina ya kushiriki na wengine kutoka elimu, maarifa na hekima za wengine; vitabu/mitandao na mazingira.

Tukifika hapa, ndipo tunajiuliza: hivi katika kupata elimu na maarifa kwa walioko kazini, kuna njia moja tu, aina moja tu, mahali pamoja tu na kitu kimoja tu cha kusoma?

Kama wasiokuwa na diploma wameweza kujiendeleza na kufundisha wengine; sasa wao hawawezi kusomea hapohapo kazini kwao na kufikia viwango vinavyohitajika?

Kuna kitu kinaitwa “life-long learning” – usakaji elimu wa maisha yote. Udugu usioisha kati ya maisha ya mtu na elimu, na maarifa; au taaluma Fulani. Elimu inayoendelea au usakaji elimu usiokoma. Hawa wa “miaka mingi” kazini, na waajiri wao bado wanawahitaji; waliishaanza zamani kutekeleza mradi huu binafsi.

Hawa, wala hawapingani na Kipangula. Wanataka mjadala. Je, hawawezi kusomea hapohapo walipo – huku wanasoma na huku wanafanya kazi? Ni lazima watoke nje ya ajira zao ambazo Kipangula hana uwezo wa kuzilinda/kuzitunza mpaka warejee?

Kwa wanaoandika, ni lazima waache kuandika; kana kwamba wanafanya adhabu kwa kosa walilotenda? Ni kosa lipi? Au wawe wanaandika taarifa na habari na kubandika majina bandia; na lipyoto afanye kazi yake – hatimaye taarifa zivuje kuwa huu ni mradi wa JAB?

Kwenda shule ni muhimu, hata kwa wenye umri mkubwa. Viwango ni muhimu pia. Je, katika hili, wataalamu wa Ithibati waliwahi kufanya, au kufikiria kufanya, tathmini ya elimu, maarifa na stadi; kati ya pande hizi mbili: walimu/wataalamu wasiokuwa na diploma; na wanafunzi wao wenye vyeti, diploma na digrii? Kuna upungufu gani, wapi na kuna kitu gani cha kujifunza? Hii ilipaswa kuwa kabla ya amri za Toka! Toka!

Nani atalea, ataelekeza na kufundisha wanaoingia? Nani atalinda/atatunza nafasi za watakaokwenda “kusaka diploma” mpaka watakaporudi? Nani atakuwa anafanya kazi za wajuzi – kulinda haki na hadhi ya chombo ili serikali nyemelezi ikae mbali? Nani ataondolewa pale wasakadiploma watakaporejea; au watakuta chombo kimeyeyuka?

Je, kuna uchunguzi wowote uliothibitisha kuwa hawa wanaoanuliwa, hawana elimu au wana elimu ndogo iliyoleta madhara kwa chombo; au hata kuvunja sheria? Nani atabisha iwapo hili litaitwa ubabe na akili ya viziavizia?

Hii miaka mitano ya kupata diploma iliwekwa kwa utafiti gani ulioonesha kuwa kila mmoja atakuwa na uwezo au atawezeshwa na mwajiri wake, kwenda nje ya eneo la ajira kusaka diploma?

Hivi nani ajuaye kilichosibu waajiri na wataalamu wao katika vyumba vya habari, kutofikia lengo la kuwa na diploma katika miaka mitano kama sheria ya 2016 inavyotaka? Hakuna anayetaka kujua? Hakuna anayetaka kutaarifu? Hakuna anayetaka kusikiliza? Ni kasome…kasome!

Kuna ukweli huu. Kazi zote katika vyumba vya habari, hupita mikononi mwa maripota wa muda mrefu; maripota wakuu, wahariri wa habari; wasanifu; kaimu wahariri na wahariri wakuu. Vibarua hawa hulalamikiwa, husutwa na kulaaniwa kwa kila kosa gazetini, redioni, kwenye skrini ya TV – kila siku, kila wiki, kila mwezi, kila mwaka na siku zote.

Nina ushahidi wa wahariri wakuu, wenye digrii, ambao hawakuwa na vyeti wala diploma za uandishi wa habari. Wasikilize. Bado wanakumbuka ripota mwelekezaji, tena asiye na diploma, alivyokuwa mkali; akidai “uthibitisho” wa ulichoandika, maelezo ya anayetuhumiwa; na kukutolea jicho kali kwa kutoweka alama za uafikishaji katika andiko lako.

Wengine wanakumbuka walivyofunzwa jinsi ya kuandaa uchunguzi wa habari yoyote; kuanzia kutafuta wazo la kuandikia habari kwa chombo chochote; muundo wa hojaji, orodha za watoa taarifa, jinsi ya kukusanya data kwa ajili ya kazi yako; jinsi ya kuandika makala mbalimbali na kuwasilisha.

“Mzee Ndimara, wewe ndio uliniambia kuwa nilionekana kuwa na background nzuri. Nikueleze basi; nilipita mikononi mwa hao ambao hawana diploma lakini ni wakali wa kazi…” ameeleza binti mmoja shahidi wa kazi bora za waelekezaji katika chombo alikoanzia kazi – yeye akiwa na diploma.

Uliza baadhi ya wahariri. Watakwambia. Walifanya hivi: Walitundika diploma na digrii zao kutani. Wakaingia vyumba vya habari. Wakakaa chini ya wasio na vyeti. Wakalelewa. Wakaelekezwa. Wakafundishwa, Wakajua. Wakakua. Wakakwea madaraja. Wakawa wahariri. Wakameremeta!

Acha tunong`onezane: Baadhi ya wahariri, wanakiri kuwa hadi kustaafu, hawajawahi kufikia viwango vya baadhi ya walezi, waelekezji na walimu wao ambao hawakuwa na diploma. Wanawaenzi. Kwa nyakati zile na nyakati za sasa za kidijiti.

Kusoma ni muhimu. Nikiwa Mhariri wa Jamii kwa miaka mitano, Mwananchi Communications Limited, nilikuwa ninaongea na waandishi wa habari na kuwauliza: Lini uliajiriwa hapa? Ulikuwa unatoka wapi? Tangu umalize chuo umesoma vitabu vingapi? Msako wa elimu.

Kijana mmoja aliniambia kuwa tangu amalize masomo ya chuo kikuu na kuajiriwa – miaka mitano iliyopita – hakuwa amesoma hata kitabu kimoja. “Ni kuja kazini tu…”

Mwingine aliniambia kuwa kwa miaka mitano amekuwa akisoma kitabu kimoja ambacho hajamaliza; na chenyewe hivi sasa hajui kilipo. Niliumia sana; ingawa niliona wengine wakijisomea vitabu mitandaoni na wengine wakiwa na nakala za vitabu mikononi.

Nikashawishika kaandika makala kwa lengo la kuchochea usomaji; sasa nikipanua eneo hadi kwa wasomaji wa The Citizen – chini ya MCL. Msanifu Mkuu aliipa kichwa: If you don’t read, how do you write? (tafsiri nyembamba: kama husomi, unaandikaje/vipi/nini?). Jisomee: FROM THE PUBLIC EDITOR'S DESK : If you don’t read, how do you write?

Lakini kuna wanaosoma. Wanaojisomea vitabu mbalimbali juu ya uandishi wa habari; misingi ya uandishi kwa wanafunzi; fikra mpya juu ya uandishi katika maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano; aina za uandishi; ufukuaji taarifa, uandishi habari za usuluhishi, uandishi katika mazingira magumu, uchambuzi, uandishi wa habari za siasa… Wanapekua. Wanataka kujua. Wanajielimisha.

Turudi kwenye swali letu la awali: Kwani kusoma kuna njia moja tu, aina moja tu, mahali pamoja tu na kitu kimoja tu cha kusoma?

Mapinduzi ya kiteknolojia katika eneo hili, kwa sasa, yanatosha kuanika wenye uwezo na kuanua waliopitwa na wakati. Ni ujio huu ambao utaondoa malalamiko ya kizembe kuwa “tasnia ya habari imevamiwa.” Haijavamiwa.

Mambo ya kuvamiwa ni kilio cha walioshindwa kujifua na kujipambanua kitaaluma; wanaolialia kuwa kila mmoja mwenye simu ya smati “anajifanya” mwandishi wa habari na mpigapicha.

Ukweli ni kwamba, hao kwa mamilioni, hawafanyi uandishi wa habari. Hao wanaolalamikiwa, wala siyo waandishi wa habari. Ni WAANDIKAJI wanaofurahia kujua kusoma na kuandika; na wanaofurahia uhuru wao wa kujieleza katika mazingira tuliyopigania toka mikaka ya 1980 kwamba, “We Want A Talking Nation; A Talking People!” Tunataka kuwa na Taifa linaloongea. Watu wanaoongea!

Kwahiyo, badala ya kulialia kuwa “taaluma imevamiwa,” waandishi wa kweli wajitahidi kujipambanua, kujitofautisha na waandikaji kwa kujihusisha na mambo mazito na ya maana.

Kwa mfano, habari za uchunguzi, utawala wa kisheria, haki za binadamu, uwajibikaji kwa walioko madarakani na maeneo mengine – utawala, haki, demokrasia – maeneo yanayohitaji ufukuaji na yenye mguso kwa jamii.

Sasa maripota, wasanifu, wahariri wengi walio katika vyombo hivi vya mawasiliano kwa muda mrefu; wakiwa bila diploma lakini wakilea, kuelekeza na kufundisha wenye diploma na digrii, hawastahili kile ambacho serikali inapanga au inatekeleza. Hapana!

Wengi wao wana upeo mpana na maarifa makuu ya kuwamegea wenzao; na siyo kuacha kazi, kwenda kusaka diploma ambayo, huenda wameishaivuka kama kungekuwepo tathmini ya kazi na uwezo wao.

Hapa kuna pendekezo. Siyo langu. Langu nitalitoa mwishoni mwa andiko langu juu ya kusemezana na waandishi wa habari, watawala na wananchi/wadau. Hili ni pendekezo la baadhi tu ya wadau wa habari ambao wamesoma baadhi ya makala zangu. Hili hapa:

“Kwakuwa serikali imetunga sheria – Sheria ya Huduma za Habari 2016 – inayotaka waandishi wa habari kuwa na diploma; basi hiyo iwahusu wanaoingia kazini kwa mara ya kwanza; na wale ambao, kwa tathmini maalum, watakutwa chini ya viwango kitaaluma.

“Kwa mfano, wenye miaka minne na zaidi kazini, ambao wamekuwa walezi, waelekezaji na walimu kwa miaka mingi (minne na kuendelea); wapate mafunzo maalumu, yanayohusisha mazoezi kikazi; kwa angalau miezi mitatu (kwa mfumo wa saa mbili kwa siku tatu kwa wiki) inayofuatiliwa kwa usimamizi wa wajuzi – ya kuongeza uwezo wao na thamani ya kazi zao; huku wakiendelea na kazi zao; badala ya kutelekeza vyombo ambavyo, ama walishiriki kuunda, kulea au kuimarisha.”

Sheria hii, Sheria ya Huduma za Habari 2016, ni chafu kuliko ile Newspaper ACT ya 1976 iliyofutwa. Hii inastahili kufanyiwa marekebisho makubwa au kufutwa kabisa. Tuijadili katika andiko lijalo.

Andiko la Ndimara Tegambwage
Media Freedom Tanzania
Natafuta nakalaya kitabu chake dula la kaya
 
Back
Top Bottom