Uchambuzi wa press ya kwanza ya Polepole: Amevuta ushawishi, ameweza kujenga hoja, amefungua mjadala

Mambo yao ya CCM wayamalize huko huko CCM, mbona CDM nao walimaliza mambo yao huko huko CDM na Mbowe akajikuta yuko nje
 
Ni wakati Mzuri sana kupima uwezo wa chama tawala kukabiliana na mawazo hasi.Siasa za ndio mzee si rafiki kwa maslahi mapana ya nchi yetu yenye dira ya kuwa na uchumi wa 1 trillion baada ya miaka 25 kuanzia leo
 
Ni kwamba wahuni wanatumia uwepo wa "Paskali" kufanya mambo Yao. Na sio kuendeleza nchi, au ktk kivuli cha kufanya vitu Kwa ajili ya nchi, ni wao kuchukua Chao mapema.

Yale yalioteteresha mifuko ya hifadhi ya jamii pensheni na kiinuo mgongo, ndio hayo hayo yaliofanyika kuteteresha Bima ya afya, na baada ya hapo kuteteresha trc, ATCL, Bandari NK nk
 
Kwa hiyo Ccm na serikali vimetekwa na wahuni?.....yaani wahuni wana nguvu kuliko serikali yenye Dola?...maajabu haya..
 
Pia alingusia kuhusu mwana Ccm mzee Malisa alivyo hoji kuhusu uhuni uliofanywa Dodoma Kikwete kuondoka na mpira kwapani, hakutendewa haki kufukuzwa chama, kwa sababu Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, " hoja hupingwa kwa hoja"
 
Kwa hiyo lila mtu anaogopa? Kuanzia wakubwa hadi wadogo? Sasa hao wakubwa na wao wnaamwogopa nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…