Kwanza hongera JF kwa kurudi hewani
Ningependa kujua mtazamo wa watu juu ya wachambuzi hawa wawili wa soka hapa Tanzania.
Mwalimu Kashasha na Dr. Leakey, Wamekuwa wakichambua soka stesheni ya TBC wakati huu wa kombe la dunia. Kwa kweli Mwalimu Kashasha kwa mtazamo wangu kamuacha mbali sana Dr. Leakey. Licha ya Mwalimu Kashasha kuwa na technical jargons za soka ila anajua kuuchambua mpira kiufundi zaidi
Dr. Leakey sioni akichambua mpira upande wa mbinu za mchezo bali yeye ni masimulizi ya kawaida tu kama ya kupiga stori kijiweni kuhusu soka.
Je wewe wadhani nani ni zaidi?