Uchambuzi wa Soka: Nani bora zaidi kati ya Mwalimu Kashasha na Dr. Leakey?

Uchambuzi wa Soka: Nani bora zaidi kati ya Mwalimu Kashasha na Dr. Leakey?

Leaky Abdalla ndie mchambuzi wa kandanda aliekamilika hapa nchini anaeuchambua mpira kwa lugha adhimu ya kiswahili na aliefasaha kabisa.

Mwalimu kashasha zaidi kajikita kwenye sayansi ya mpira simzuri sana kwenye uchambuzi bali vile vionjo vyake ndio vinavyotia raha nahakika asilimia kubwa ya watanzania hawamwelewi kwenye yale maneno anayotumbukizia.

Leaky anajua historia na records na kuwafahamu wachezaji wengi pamoja na tabia zao nje na ndani ya uwanja tuliomfuatilia tokea kipindi hicho tunaujua ubora wake.
 
Huyo mwl kashasha akielezea goli la kichwa utamsikia "pale ilikua head bending tactically heart controllel kwenye movement in order to score organism[emoji23][emoji23][emoji23]
Dakika za nyongeza anakwambia ni injury time[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwanza hongera JF kwa kurudi hewani

Ningependa kujua mtazamo wa watu juu ya wachambuzi hawa wawili wa soka hapa Tanzania.

Mwalimu Kashasha na Dr. Leakey, Wamekuwa wakichambua soka stesheni ya TBC wakati huu wa kombe la dunia. Kwa kweli Mwalimu Kashasha kwa mtazamo wangu kamuacha mbali sana Dr. Leakey. Licha ya Mwalimu Kashasha kuwa na technical jargons za soka ila anajua kuuchambua mpira kiufundi zaidi

Dr. Leakey sioni akichambua mpira upande wa mbinu za mchezo bali yeye ni masimulizi ya kawaida tu kama ya kupiga stori kijiweni kuhusu soka.

Je wewe wadhani nani ni zaidi?
Tofauti zao hizo ndio zinawafanya wapendwe zaidi. Hakuna aliyemuacha mwenzake
 
Dr. Leakey ni mchambuzi mzuri mwenye kujua history na pia anatia hamasa kuendelea kufuatilia game hata ukiwa kilaza kiasi gani kwenye soka basi ukimsikiliza dr Leakey urafurahi
 
Nilianza kumfuatilia na kupenda maelezo yake kwa mara ya kwanza
Kwenye fainali za kombe la Dunia 1998, kati ya Ufaransa na Brazil. Hakika hautochoka kumsikiliza

Bado hajatokea mwingine kama yeye. Nakumbuka kuna kipindi tunaangalia mpira TBC lakini Dr.Leakey alikuwa anatoa dondoo kabla ya mechi Channel Ten, tumamsikiliza kwanza kisha tunahamia TBC kuangalia mpira.
 
Back
Top Bottom