Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
UCHAMISHAJI WA TAASISI ZA UMMA: TISHIO KWA UTAWALA BORA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Katika mfumo wa taifa la kisasa, kuna tofauti kubwa kati ya chama cha siasa, serikali na taifa. Chama cha siasa ni taasisi inayoundwa na watu wenye mtazamo na itikadi fulani za kisiasa. Vyama kama vile CCM, CHADEMA, CHAUMMA Miongoni mwa vyama vingjne.
Serikali ni chombo kinachosimamia uendeshaji wa nchi kwa niaba ya wananchi. Na Taifa ni jumuiya pana ya watu, ardhi, mamlaka na utambulisho wao wa pamoja.
Tatizo huanza pale mipaka kati ya vitu hivi inapofifia. Chama kinapoanza kujiona kuwa sawa na taifa, au serikali inapoanza kutumika kama chombo cha chama badala ya chombo cha wananchi wote, ndipo tunapoanza kuona kile kinachoweza kuitwa uchamishaji wa taasisi za umma.
Uchamishaji ni hali ambapo taasisi, rasilimali au mifumo ambayo inapaswa kuwa ya wananchi wote inaanza kuelekezwa, kudhibitiwa au kutumiwa kwa maslahi ya chama fulani cha siasa. Hiki ndicho ambacho sisi Watibeli hatukitaki. Tunataka jamii ya kiungwana. Mtu akiwa CHADEMA asiwe tofauti na aliye CCM au vyama vingine katika kupewa haki na kutumia na kuhudumiwa na taasisi za umma.
Vurugu zote zinazotokea nchini kwetu ni matokeo ya uchamishaji na michakato yake.
Uchamishaji ni mchakato wa kuhamisha nguvu, utendaji au utambulisho wa taasisi za umma kutoka kwenye msingi wa kutumikia wananchi wote na kuzielekeza kwenye maslahi ya chama.
Katika hali ya kawaida, chama cha siasa kinapaswa kushindana kwa sera, mawazo na uongozi ili kupata ridhaa ya wananchi. Lakini baada ya kupata madaraka, serikali inayoundwa inapaswa kuwa ya wananchi wote, wakiwemo hata wale ambao hawakukipigia kura chama kilichoshinda.
Uchamishaji hutokea pale ambapo taasisi za umma zinaanza kuonekana kama mali ya chama badala ya mali ya taifa. Hapa ndipo hekaheka na vurugu zinaanza. Ukosefu wa haki, unyanyasaji, ukosefu wa uhuru wa kisiasa na kitaaluma unapotea.
Mathalani taaluma za mambo ya ulinzi na usalama katika vyombo vya dola hujikuta wakiwa watumwa wa chama au kikundi fulani hali inayoathiri weledi na uadilifu katika kutimiza majukumu yao.
MAENEO AMBAYL YAKICHAMISHWA HUWA TISHIO KWA UTAWALA BORA NA MWISHOWE TISHIO KWA USALAMA WA TAIFA;
1. UCHAMISHAJI WA TAASISI ZA UMMA.
Utumishi wa umma unapaswa kuongozwa na misingi ya taaluma, uwezo na sheria. Uchamishaji hutokea pale ambapo uaminifu wa kisiasa unakuwa muhimu kuliko uwezo wa kitaaluma.
Mfano ni pale ajira, uteuzi au kupandishwa vyeo kunapoanza kuhusishwa zaidi na ukaribu wa mtu na chama kuliko sifa zake.
Athari yake ni kupunguza ubora wa huduma kwa wananchi. Na yale mambo ya unanijua mimi ni nani kuzuka. Pia uchawa kupamba moto.
2. VYOMBO VYA DOLA
Vyombo kama polisi, jeshi na taasisi za usalama vina wajibu wa kulinda taifa, si kulinda maslahi ya chama fulani.
Endapo wananchi wataanza kuona vyombo hivi vinaegemea upande wa chama fulani, imani yao katika haki na usawa hupungua.
Nguvu ya dola inapokuwa nguvu ya chama, demokrasia huanza kudhoofika. Wafanyakazi, watumishi wa vyombo vya usalama hujikuta wakiwa mateka wa wanasiasa. Hii huwa na athari nyingi. Mojawapo ni imani ya wananchi kwenye vyombo vya dola na usalama hupungua.
Pili, watumishi wa vyombo vya usalama kuishi kwa mashaka, kukosa raha, kukosa amani ya moyo na kutofurahia kazi yao ambayo ni kazi nzuri kama zilivyo kazi zingine. Fikiria askari anajua taaluma na maadili ya kazi yake vinamtaka awe muadilifu, afanye hivi lakini Mimi mtu wa chama fulani ninakuja ninamuamrisha fanya vile. Na sio ombi ni lazima. Hii sio haki kwa watumishi wa dola. Kugeuzwa robots au mbwa.
Uchamishaji unaweza kumfanya binadamu akawa hana thaman. Hasa thamani ya ndani kabisa.
3. VYOMBO VYA HABARI VYA UMMA
Vyombo vya habari vinavyomilikiwa na umma vina wajibu wa kuwahudumia wananchi wote.
Uchamishaji hutokea pale chombo cha habari kinapokuwa zaidi kama chombo cha mawasiliano cha chama kuliko chombo cha taarifa kwa umma.
Matokeo yake ni kupungua kwa nafasi ya mijadala huru na maoni mbalimbali.
Hii itakufanya uone taarifa za chama kimoja zikipewa nguvu huku za vyama vingine vikipuuzwa na kutoripotiwa.
Wamiliki wa media na vyombo vya Habari kuogopa, kutokuwa huru kufanya kazi zao kwa weledi. Huku waandishi wa habari wakijikuta katika hali ngumu ya mateso. Na hii hufanya kazi hizo zote kupoteza hadhi na heshima mbele ya umma.
Ndio yale unakuta nyakati za uchaguzi mkuu. Habari za vyama vya upinzani haziripotiwi na kupewa uzito huku Habari za chama kikuu zikipewa uzito.
4. Rasilimali za Taifa
Mali za umma kama majengo, magari, fedha na miundombinu vimeundwa kwa ajili ya wananchi wote.
Vinapotumiwa kama mali za chama kwa shughuli za kisiasa, mpaka kati ya mali ya taifa na mali ya chama huvurugika.
Hii huleta matumizi mabaya ya rasilimali ambazo wananchi wote wanapaswa kunufaika nazo.
Inaweza kutokea mtu mwenye ushawishi akataka kuitisha mkutano katika jengo au uwanja fulani wa umma. Akanyimwa kibali huku wa chama kingine akipewa.
Au unakuta chama kimoja kinauhuru wa kutumia magari ya serikali na rasilimali za serikali. Huku chama kingine kikizuiwa kufanya hivyo. Hiyo sio sawa.
5. Taasisi za Sheria na Usimamizi
Taasisi kama mahakama, vyombo vya uchaguzi na mamlaka za udhibiti zinapaswa kuwa na uhuru wa kutekeleza majukumu yao.
Uchamishaji wa taasisi hizi unaweza kuathiri imani ya wananchi katika haki, uchaguzi na utawala wa sheria.
Hii inaenda sambamba, watumishi na viongozi wakuu wa taasisi za sheria, ikiwemo mwanasheria Mkuu, Waendesha mashtaka, Mahakimu na majaji kuteuliwa na kupewa nafasi hizo kwa kuangalia uchama kuliko majukumu yao kwa haki.
Utawala bora unategemea misingi kama uwazi, uwajibikaji, usawa, sheria na ushiriki wa wananchi.
Uchamishaji unaweza kuathiri misingi hiyo kwa njia mbalimbali:
Kama, hudhoofisha usawa
Wananchi wanaweza kuanza kuhisi kuwa haki na huduma zinategemea upande wao wa kisiasa badala ya kuwa haki yao kama raia.
Pili, hupunguza uwajibikaji
Taasisi inapokuwa karibu sana na chama, viongozi wake wanaweza kujiona wanawajibika zaidi kwa chama kuliko kwa wananchi.
Tatu, hudhoofisha demokrasia
Demokrasia si uchaguzi pekee, bali pia uwepo wa taasisi huru zinazolinda haki za wote.
Nne, hupunguza imani ya wananchi
Wananchi wakipoteza imani kwamba taasisi za umma ni zao wote, huanza kujitenga na mfumo wa utawala.
Katika demokrasia, chama kinaposhinda uchaguzi kina haki ya kutekeleza ahadi zake kwa wananchi.
Tatizo linatokea pale chama kinapotumia taasisi, sheria au rasilimali za umma kama mali yake binafsi na kuwanyima wengine nafasi sawa.
Kulinda mipaka kati ya chama, serikali na taifa ni kulinda misingi ya haki, demokrasia na utawala bora. Na haya ili yafanyike. Tunahitaji Katiba mpya itakayounda mifumo bora yenye nguvu ya kulinda maslahi ya wananchi na taifa letu kwa ujumla. Na sio kulinda kukundi fulani cha watu.
Mimi Nimemaliza.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam