Ndugu zangu watanzania,
Kasi ya utekelezaji wa ilani ya CCM, uchapakazi wa serikali ya CCM,ujenzi wa miradi kila Kona ya nchi yetu, mafuriko ya maelfu ya ajira kwa vijana hapa nchini kumeizima Kama mshumaa mikutano na harakati zote za CHADEMA mitaani. Kwa Sasa haieleweki Kama chama kipo au kimehifadhiwa kabatini, ni chama ambacho ni Kama kinamtegemea mwenye kigoda akitoe mfukoni na kukionyesha kwa watu.
Mbwembwe zote za chopa zimezima ghafla, hii ni baada ya kuona chama kinapuuzwa mitaani hasa baada ya wananchi kutambua ya kuwa ni chama kilicho jaa na kusheheni wasaka tonge, wababaishaji, watu waliokosa Dira na muelekeo,watu wasio na maono Wala malengo mikakati, watu wasio na mipango, sera na ajenda za kugusa maisha ya watu.
Imefikia hatua viongozi wake wamekuwa wakilalamika kuwa wanapuuzwa na kutopewa Umuhimu wa habari na taarifa zake na vyombo vya habari hapa nchini.hii Ni kutokana na ukweli kuwa chama hicho kilichokosa mizizi na uhai kimeshindwa kujuwa na kufahamu Mahitaji ya watanzania ni yapi? Ajenda na Sera zinazogusa maisha ya watanzania Ni zipi? Kiu ya watanzania Ni Nini? Mahitaji ya makundi mbalimbali katika jamii Ni yapi? Ni chama kinachoshindwa kwenda na wakati,Ni chama kilicho nyuma ya wakati na kuwa na ajenda zisizo endana na wakati.
Ndio maana kimekataliwa na watanzania kwa kuwa watanzania wanahitaji mambo ambayo chama hicho hakiyazungumzi zaidi ya kuweka kipaombele katika Mambo ambayo yatakipa Ruzuku za kutafuna Kama mchwa.mambo ambayo watanzania wanahitaji ndio mambo ambayo serikali ya CCM inatekeleza na kuyafanya kila Siku na hivyo kugusa mioyo ya Watanzania.
Watanzania wanahitaji maji Safi na salama karibu Yao, wanahitaji wakienda hospitali wapokelewe vizuri,wakute wahudumu wakutosha,wakute vifaa Tiba, sawa na kupewa huduma iliyobora na kwa ukarimu, watanzania wanahitaji kuona vijana na watoto wao wanapata Elimu iliyo Bora, ajira kwa vijana wao, Miundombinu iliyobora na inayopitika misimu yote ya mvua na jua, huduma za umeme mpaka vijijini, gharama nafuu za bidhàa Kama mafuta ya kula. Nishati ya petrol, disel, mafuta ya taa, sabini, sukari, unga,Michele n.k.fursa nzuri za kiuchumi kwa kila mwenye kujituma, mzunguko mzuri wa fedha mitaani, mfumuko mdogo wa Bei,nauli ndogo zisizoleta maumivu, ukadiriaji wa mapato unaozingatia haki, demokrasia na utawala Bora, haki kwa kila mtu mbele ya Sheria, mazingira mazuri ya biashara na wepesi wa kufanya biashara nchini.
Mambo hayo na mengine mengi ndio yamekuwa ajenda za CCM wakati na muda wote,ndio imekuwa kipaombele Cha serikali ya CCM katika kuleta Tabasamu, furaha na matumaini katika mioyo ya watanzania,ndio imekuwa kazi inayofanywa na serikali wakati wote,ndio kazi ya kila siku inayofanywa na viongozi wa chama na serikali ya CCM na kila kiongozi anatambua huo ndio wajibu wake namba moja.
Ndio maana CCM inaendelea kuaminika,kukubalika,kupendwa, kuongoza na kuchaguliwa katika kila uchaguzi, ndio maana upinzani inapata taabu Sana katika kupenya kwenye mioyo ya watanzania, ndio maana ya upinzani kukosa uungwaji mkono kutoka katika makundi mbalimbali katika jamii na ndio maana ya CCM kuwa na uhakika wa Kuendelea kuongoza Taifa letu kwa miaka mingi Sana ijayo na kukosa mbadala wake.
Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.
Sasa limekuja suala la ujenzi wa barabara kwa kutumia utaratibu wa EPC + F. Wanavyousifia utaratibu huo ni kama nchi imevumbua muujiza mkubwa utakaomaliza matatizo yote ya ujenzi wa barabara, na kama vile tawala nyingine zote zilizotangulia zilikosa ubunifu.
Ukweli ni kwamba EPC + F, hakuna utawala ambao ungeshindwa kujenga barabara kwa kufuata utaratibu huo kama ungeonekana ni rahisi na wenye tija.
Kwa mchumi mzuri, siyo mchumi wa makaratasi, ujenzi wa barabara kwa utaratibu huu, ndiyo aghali kuliko utaratibu mwingine wowote ambao nchi imewahi kutumia.
Kwa wasioelewa, utaratibu huu wa EPC + F, mjenzi anajenga barabara kwa kutumua pesa yake, halafu Serikali itakuwa inamlipa yule mjenzi taratibu kwa kiwango kilichokubaliwa.
Mjenzi wa barabara anapata wapi pesa?
Mjenzi wa barabara anachukua pesa toka kwenye mabenki na taasisi mbalimbali za fedha.
Mjenzi wa barabara anazichukua pesa toka benki kwa utaratibu gani?
Mjenzi anachukua pesa benki kwa njia ya mkopo. Mkopo ni lazima uwe na riba maana mkopeshaji naye anatafuta faida.
Mjenzi kwa nini akubali kutujengea barabara halafu alipwe taratibu?
Mjenzi ni mfanyabiashara. Anatafuta faida. Hivyo nchi italazimika kumlipa mjenzi kwa kiwango ambacho mjenzi lazima apate faida.
Mjenzi atapataje faida?
Lazima atahakikisha nchi inalipa kufidia riba ya benki alikochujua pesa, plus faida ya kwake yeye mjenzi. Na tukichelewesha, tutalipa na penalty.
Kwa hiyo utaratibu huu wa EPC + F, utatufanya tujenge barabara zetu kwa gharama kubwa kuliko kipindi chochote kile. Kwa wasioupendelea utaratibu huu wangeweza kuuliza, kwa nini ukalipe riba kwa taasisi mbili, yaani kwa benki na mjenzi, wakati kuna uwezekano wa kukopa benki moja kwa moja, ukaokoa riba ambayo ungemlipa mjenzi?
Wakati Waziri Mbarawa akiusifia utaratibu huu kama vile amegundua sayari mpya, hakutoa mchanganuo wowote. Kwa mfano alitakiwa kusema:
1) kwa wakati huu ambao barabara zimekuwa zinajengwa kwa taratibu tofauti na EPC + F, kilometer 1 ya barabara ya lami, gharama ya ujenzi ni sh. ngapi?
2) Kwenye utaratibu huu wa EPC +F, kilometer 1 ya barabara ya lami, itagharimu kiasi gani?
Mkopo siyo pesa ya bure. Na wala huwezi kujisifia kuwa umegundua mbinu mpya ya kukopa. Mateso ya mkopo utayajua wakati wa ulipaji. Uganda wanalalamika sasa hivi, maana kwa mara ya kwanza mwaka huu wa fedha, karibia 40% ya bajeti yao yote itakuwa inagharamia kulipa madeni. Na sisi kwa sababu ni watu ambao uwezo wetu unaishia kushangilia na kupongeza, tunaelekea huko huko. Ifahamike tuna mikopo ya kugharamia miradi kama SGR, bwawa la Mwalimu Nyerere, daraja la Busisi, mikopo ya miaka mingi ya huko nyuma, sasa inakuja na hii ya EPC + F, na kutakuwa na mikopo kuziba pengo la bajeti kila mwaka. Hatuwezi kukwepa kukopa, lakini mwenye weledi anakopa kwa umakini, na siyo kurundika mikopo mingi kwa wakati mmoja kwa sababu tu amepatikana wa kukukopesha.
Nchi nyingi zinazotumia utaratibu wa EPC + F, zinatumia wakandarasi wa ndani. Kwao, hata kama barabara zitajengwa kwa gharama kubwa, mabenki yanayokuwa yamenufaika kutokana na riba ni ya nchini mwao. Wajenzi walionufaika kutokana na riba ni wa nchini mwao. Kwa hiyo hela inakuwa imetoka Serikalini imeenda kwa watu wao. Sisi hela itatoka Serikalini kwenda kwenye mabenki ya nje, pesa itatoka Serikalini kwenda kwa makampuni ya ujenzi ya nje.