Uchapakazi wa serikali ya Rais Samia waizima na kuipoteza CHADEMA mitaani

Kwanini hauongelei ACT? Anyway siwezi kukupangia cha kuandika, lakini Chadema inakupa hofu sana kama siyo riziki ya siku kwa kuiongelea. Kuna TLP pia, mkuu wewe ni jinsia gani?
 
muulize mamayenu kule mwanza juz alikua na watu wangapi, tulimkomesha hatasahau na bado 2025 tutamnyoosha kabisa kama mbuz kagoma kwenda.
 
Halafu mwisho wa siku hao unaowasifia wanatoa rushwa kwa wapiga kura wao ili wawachague, ndiyo akili zilizoshindwa kuongoza inchi zinategemea muwekezaji
 
Sasa limekuja suala la ujenzi wa barabara kwa kutumia utaratibu wa EPC + F. Wanavyousifia utaratibu huo ni kama nchi imevumbua muujiza mkubwa utakaomaliza matatizo yote ya ujenzi wa barabara, na kama vile tawala nyingine zote zilizotangulia zilikosa ubunifu.

Ukweli ni kwamba EPC + F, hakuna utawala ambao ungeshindwa kujenga barabara kwa kufuata utaratibu huo kama ungeonekana ni rahisi na wenye tija.

Kwa mchumi mzuri, siyo mchumi wa makaratasi, ujenzi wa barabara kwa utaratibu huu, ndiyo aghali kuliko utaratibu mwingine wowote ambao nchi imewahi kutumia.

Kwa wasioelewa, utaratibu huu wa EPC + F, mjenzi anajenga barabara kwa kutumua pesa yake, halafu Serikali itakuwa inamlipa yule mjenzi taratibu kwa kiwango kilichokubaliwa.

Mjenzi wa barabara anapata wapi pesa?
Mjenzi wa barabara anachukua pesa toka kwenye mabenki na taasisi mbalimbali za fedha.

Mjenzi wa barabara anazichukua pesa toka benki kwa utaratibu gani?
Mjenzi anachukua pesa benki kwa njia ya mkopo. Mkopo ni lazima uwe na riba maana mkopeshaji naye anatafuta faida.

Mjenzi kwa nini akubali kutujengea barabara halafu alipwe taratibu?
Mjenzi ni mfanyabiashara. Anatafuta faida. Hivyo nchi italazimika kumlipa mjenzi kwa kiwango ambacho mjenzi lazima apate faida.

Mjenzi atapataje faida?
Lazima atahakikisha nchi inalipa kufidia riba ya benki alikochujua pesa, plus faida ya kwake yeye mjenzi. Na tukichelewesha, tutalipa na penalty.

Kwa hiyo utaratibu huu wa EPC + F, utatufanya tujenge barabara zetu kwa gharama kubwa kuliko kipindi chochote kile. Kwa wasioupendelea utaratibu huu wangeweza kuuliza, kwa nini ukalipe riba kwa taasisi mbili, yaani kwa benki na mjenzi, wakati kuna uwezekano wa kukopa benki moja kwa moja, ukaokoa riba ambayo ungemlipa mjenzi?

Wakati Waziri Mbarawa akiusifia utaratibu huu kama vile amegundua sayari mpya, hakutoa mchanganuo wowote. Kwa mfano alitakiwa kusema:
1) kwa wakati huu ambao barabara zimekuwa zinajengwa kwa taratibu tofauti na EPC + F, kilometer 1 ya barabara ya lami, gharama ya ujenzi ni sh. ngapi?
2) Kwenye utaratibu huu wa EPC +F, kilometer 1 ya barabara ya lami, itagharimu kiasi gani?

Mkopo siyo pesa ya bure. Na wala huwezi kujisifia kuwa umegundua mbinu mpya ya kukopa. Mateso ya mkopo utayajua wakati wa ulipaji. Uganda wanalalamika sasa hivi, maana kwa mara ya kwanza mwaka huu wa fedha, karibia 40% ya bajeti yao yote itakuwa inagharamia kulipa madeni. Na sisi kwa sababu ni watu ambao uwezo wetu unaishia kushangilia na kupongeza, tunaelekea huko huko. Ifahamike tuna mikopo ya kugharamia miradi kama SGR, bwawa la Mwalimu Nyerere, daraja la Busisi, mikopo ya miaka mingi ya huko nyuma, sasa inakuja na hii ya EPC + F, na kutakuwa na mikopo kuziba pengo la bajeti kila mwaka. Hatuwezi kukwepa kukopa, lakini mwenye weledi anakopa kwa umakini, na siyo kurundika mikopo mingi kwa wakati mmoja kwa sababu tu amepatikana wa kukukopesha.

Nchi nyingi zinazotumia utaratibu wa EPC + F, zinatumia wakandarasi wa ndani. Kwao, hata kama barabara zitajengwa kwa gharama kubwa, mabenki yanayokuwa yamenufaika kutokana na riba ni ya nchini mwao. Wajenzi walionufaika kutokana na riba ni wa nchini mwao. Kwa hiyo hela inakuwa imetoka Serikalini imeenda kwa watu wao. Sisi hela itatoka Serikalini kwenda kwenye mabenki ya nje, pesa itatoka Serikalini kwenda kwa makampuni ya ujenzi ya nje.
 
Halafu mwisho wa siku hao unaowasifia wanatoa rushwa kwa wapiga kura wao ili wawachague, ndiyo akili zilizoshindwa kuongoza inchi zinategemea muwekezaji
Watanzania wanaichagua CCM kwa upendo mkubwa kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi wa na utekelezaji wa ilani yake
 
Kuna maeneo CCM inatumia nguvu kubwa sana kutawala!
Mleta mada u aidanganya CHADEMA ipo imara .Kama kimekufa itisha uchaguzi ambao utahusisha taraubu huyu za uchaguzi.Hapo CCM haiwezi kutoboa!
Kuna Mkoa Fulani Rais Samia alitembelea..siku hiyo Shule za Sekondari za mji huo na maeneo ya jirani takribani kumi na tatu zikifungwa na wanafunzi wakaambia waende kwenye mkutano tena bila ya Sare !
 
Nani kakwambia Mimi naandika kwa ajili ya kupata na kulipwa fadhila
Kwa upuuzi unaoandika hata mtoto wa shule ya vidudu anajua kabisa ama unaandika ili ufurahishe wapuuzi waliopo huko juu ama unaendeshwa na upuuzi tu uliokujaa kichwani mwako mwenyewe
 
Labda wewe na familia yako kwa uzembe wenu ,lakini mamilioni ya watanzania Wana Imani kubwa Sana na mh Rais na serikali yake na wanaendelea kumuunga mkono
sina familia mkuu ila nina watu ninaofahamiana nao mtaani wote wanasema mama hana mipango na kuna remote ipo msoga
 
sina familia mkuu ila nina watu ninaofahamiana nao mtaani wote wanasema mama hana mipango na kuna remote ipo msoga
Watanzania wengi Sana wanaridhishwa na utendaji na uchapa kazi wa Rais Samia.watanzania wanaona kuwa Rais Samia Amekidhi matarajio yao,amekata kiu ya mamillioni ya watanzania na kuleta matumaini katika mioyo ya watu.
 
Kwa upuuzi unaoandika hata mtoto wa shule ya vidudu anajua kabisa ama unaandika ili ufurahishe wapuuzi waliopo huko juu ama unaendeshwa na upuuzi tu uliokujaa kichwani mwako mwenyewe
Hoja hupingwa kwa hoja na siyo viroja
 
 

Attachments

  • 65D35521-6709-4A7A-9894-96F33C237509.jpeg
    51.3 KB · Views: 1
  • E7D424C0-DC29-4654-8E7A-D5B4FBE87924.jpeg
    140.9 KB · Views: 1
Lucas mwashambwa aka chizi waume ZAKO hawalali Kwakuiwaza Chadema halafu wewe unaleta pumba ZAKO hapa kumbuka sie wakubwa ndugu punguza uchizi wako
 
Chawa mlamba mbwata. Umeandika na namba ya tigo kabisa[emoji25][emoji25][emoji25][emoji25]
 
Ifike muda watu kama Mwashambwa, mungu aamue ugomvi mapema, kwani Uchawa wa Aina hii ni hatari kwa rasilimali za nchi yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…