Nilipokuwa darasa la nne/tano nilikuwa na muongozo mzuri sana shuleni.. ufahulu mzuri sana.. madaftari safi yaani nilikuwa kitoto fulani hivi cha mfano ,,, nakumbuka nilikuwa nikiitwa officin kama mfano watoto watukutu wakiitwa wazazi wao kwa makosa fulani fulani ..
Tulikuwa tukiishi nyumba moja ya kupanga na wazazi wetu huko mabibo .. wapangaji tulikuwa wengi wengi .. na kulikuwa na bibi mmoja ana mtoto wake ana umri unafanana na mimi.. na tulikuwa tupo sawa ki-darasa lakini hatukukuwa tukisoma shule moja..
Kwa mujibu wa mama anasema alikuwa akiadithia maendeleo yangu ya shule anapopata nafasi ya kukaa na huyo mama.. daah aliniponza kumbe bila ya kujua .. niliumwaga ugonjwa wa ajabu wakuu hakuna mfano na sijasikiaga mpaka leo mtu anaumwa ule ugonjwa tena wala kuona..
Usiku nilipokuwa nimelala nashituka usiku mkubwa saa kati ya saa 8 ,9 au 10 naanza kuwewe seka mithili ya haya mapicha ya mazombi wanavyokuwa wakitembea na kutetemeka sasa wawe wanaenda kasi zaidi yaani.. huwa naamka natetemeka naelekea kwa wazazi na kuwaamsha na hali hiyo ikiwa inaendelea wazee huwa wanaanza kunisomea mpaka hali inakata.. mimi huwa nalia sana baada ya hiyo hali kukata nawauliza wazazi hii ni nini? Wazazi hasa mama nae anaanza kulia hajui nini? Afanye hali ilidumu zaidi ya mwaka bila mafanikio yeyote tulienda hospital zaidi ya 6 lakini haku kuwa na tiba yeyote wazazi walikuwa wakiulizwa hamna magonjwa ya kurithi ninyi “ walikuwa wanasema yaani hakuna ugonjwa kama huo... haibu ilinikuta na shuleni nilipitiwa kwa kulala ugonjwa ukanikuta akaenda kuitwa mwalimu... daaah acheni tu.. mwalimu akaniruhusu na kunipa watu wanipeleke nyumbani.. na kuniambia nipumzike nyumbani siku tatu then niende na mzazi.. baada na kwenda na mzazi
Mwalimu alikuwa anamwambia Baba kuwa mwanao alikuwa na maendeleo mazuri na miezi hii ya karibu amekuwa akifanya vibaya bila ya kujua chanzo ni nini? Ila juzi ameumwa hapa na ugonjwa wa ajabu sana .. bado sijajua kama hilo ni tatzo em nielezee kama hiyo hali inamtokea mara kwa mara au laaah .. Baba alimwambia ni kila siku anapolala lazima imkute mpaka siku nyingine anaogopa kulala... mwalimu akamwambia bana mkizembea kwa mwanenu kwa haya tanayomkuta sio tu kufeli tu darasana mtamkosa kabsa mwanenu.. naandika hii Message.. machozi yakinibbujika.. mwalimu akamuuliza baba kuwa huu ugonjwa una mda gani? Baba akamwambia.. mwalimu alisikitika sana na kuchukua namba za Baba kwa mawasiliano zaidi...
Ilikuwa tukienda ugenini kutembea wakati wa likizo kazi ilikuwa hiyo hiyo ya kuumwa baada ya kulala.. nilikuwa mtoto asiyekuwa na furaha mda wote.. nilikuwa dhaifu kimwili tena.. nilikuwa sili chakula kwa wakati .. mvivu hata kwenda shule nilikuwa na hali mbaya sana..
Sisi ni waislam... nakumbuka nilipeleka kwa sheikh mmoja ambae namkumbuka mpaka leo na kuelezewa jinsi hali inavyonitokea na akawaambia wazazi kuwa kuna kitu katupiwa kichafu na aliwaelezea mpaka alienitupia hicho kitu na akawaambia ni kwa ajili tu ya wivu tu wa maendeleo ya shuleni.. nia ya icho kitu kichafu ni kumzubaisha na kumchosha kumtesa tu asiwe na raha na amani na automatically atafeli shuleni basi tukaanza tiba pale pale
Akanisomea baadhi ya aya katika baadhi ya sura katika qur-an na akawaambia wazee awe anatafuna punje moja mpaka tatu kabla ya kulala za kitunguu swahumu.. na kuwaambia hali ikiendelea njoeni nae tena.. uwezi amini siku ile ile ya kwanza sikuumwa tena baada ya kusomewa na kutumia kitunguu swahumu kabla ya kulala.. baada ya wiki ilibidi tuame.. na ile hali haikurudia tena