Kwanza kabisa nimeuliza uchawi ni nini.
Na utajuaje huu ni uchawi na si kitu kingine ambacho si uchawi ila hujakielewa tu.
Hujajibu.
Muandiahi wa riwaya za kisayansi wa Kiingereza Arthur C. Clarke alikuwa na usemi wake mmoja naupenda sana.
Alisema " Any sufficiently advanced technology is indistinguishable from magic".
Yani hata watu kutoka Ulaya walivy9kuja na mambo ya gramophone inayopiga muziki, mababu zetu wakaona muziki na sauti za watu zinatoka katika hiki kibox cha gramophone, waliona uchawi.
Hawa watu wa kutoka Ulaya walivyoweza kutabiri lini jua litapatwa (solar eclipse), kwq kujua sayansi tu, walionekana wachawi.
Sasa, uchawi ni nini na wewe unajuaje huu ni uchawi na si kitu kingine ambacho hukijui tu kama babu zetu walivyokuwa hawajui gramophone na jinsi ya kutabiri solar eclipse?