Nimemuuliza mtu.
Nimemuambia hivi.
Babu zetu waliokuwa hawajui umeme, redio, kutabiri kupatwa kwa jua etc, walipokutana na watu kutoka Ulaya, waliojua vitu hivi, waliwaona watu hawa wachawi. Waliwaona "mizungu".
Ukichukua neno "mzungu" ukiondoa herufi z unapata neno "mungu".
Waliwaona wana nguvu za kichawi.
Kwa sababu hawakuelewa sayansi na teknolojia.
Ungewachukua hawa babu zetu kutoka miaka 140 iliyopita, ukawaweka leo na kuwaonesha tunavyowasiliana kwenye internet, mpaka kwa videocalls, wangesema ni uchawi.
Sasa na hawa watu wanaosema wameona uchawi leo, wanajuaje hawajakutana na vitu wasivyovijua tu, lakini ambavyo si uchawi?
Mpaka sasa sijajibiwa.