Kudadeki, kwenye huu Uzi ndio nimepata majibu ya kibubu changu namie
Kuna mwaka fulani wakati ndio naanza maisha, niliwahi kuishi kigogo basi baada ya kupata ahueni ya maisha nikaenda kukaa mbezi baada ya kupiga deal la bumkubaa
Sasa nilipofika Mbezi na kufanya Tathmini ya maisha nikaona kulipa Kodi mbona itakuja itakuwa utata badae me nimezoea Kodi zangu za 30k
Wakati naishi kigogo niliwahi kuona Mzee fulani hivi anauza vibubu kwake, hivo nikapanga siku ya kwenda na nikanunua kimoja Kwa ajili ya kukusanya pesa ya kulipa Kodi
Basi kweli bana, nikawa najitahidi kila siku lazima niweke hela kuanzia 2000 kuendelea, nikafanya hivo Kwa miezi 2 mfululizo bila kusimama ata siku 1, nilipanga ikifika miez 3 ndio nivunje nitoe hela ya Kodi
ila bahati mbaya kabla ya kufika miez 3 nikawa nimepata msiba, nikaona nivunje tu kibubu ili nitumie ile pesa kama nauli ya kwenda Mkoa, ilikuwa imefika kama siku 78 hivi
Ohoooo si nikakitoa bana ili nichukue mafao, kudadeki baada ya kuvunja nakuta 6500, na hapo tangu nihamie hayo makazi mapya nilikuwa sijawahi kupeleka mshkaji wala Manzi
Ikabidi nikae tu niegemee ukuta maana sina nauli wala sina tumaini la kulipa Kodi, nikawaza na kuwazua kama steringi wa kihindi ila haikunisaidia chochote
Dahh sikuwahi kupata majibu ya hela yangu ilienda wapi hadi leo kwenye Uzi huu ndio nimepata Mwanga kuwa huenda ni kweli hivi vibubu waga vimefungwa Visimbuzi