Khalifavinnie
JF-Expert Member
- May 19, 2017
- 2,796
- 2,367
duu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
police Akataka Alipe Faini Kipindi Kile Tshs 30000/=Kuna Jamaa Alikuwa Anauguliwa Na Mke Wake
Akaazima Pikipiki Akiwa Na Tshs 30000/= Cash
Akampakia Mkewe Kumpeleka Hospital Kasulu
Barabarani Akakutana Na Police Akadaiwa Licence
Hana Akajieleza Kuwa Mkewe Yu Hoi Anawahi Hospital Apate Tiba
police Akataka Alipe Faini Kipindi Kile Tshs 30000/=
Akamwambia Ndiyo Pesa Hiyo Tu Anayo Kwaajil Ya Matibabu. Police Akasema Hutoki Usipolipa
Akamuomba Sana Akakataliwa
Akalipa Akaenda Zake Hapo Hana Pesa
aliporudi Nyamnyusi Police Alikuwa Akivaa Uniform Anawashwa Mwili Wote Akivua Sawa
Changamoto Sasa Yule Askari Atampata Wapi Yule Jamaa
Hujamalizia connection pmShukia Makanya Same mbali sana
Nimezaliwa Makanya
Nimekulia na Kusomea Makanya kuanzia chekechea, shule ya msingi mpaka Kidato cha nne,
Niliondoka Makanya nilipofaulu Kidato cha nne.
Makanya ndio kwetu, Makanya ndio watu wangu, nami ni mtoto wao.
Hayo unayosema yapo Kwa kiasi,
Makanya Ushirikina na Uchawi upo na unaathari labda Kwa wageni wasio wazawa.
Makanya inamchanganyiko wa Makabila kutokana na kilimo cha zao la Mkonge.
Wenyeji wengi ni Wapare,
Lakini pia kuna
Wamasai, wasambaa, Wachaga kidogo, Warundi, Wanyambo, Wasukuma, NK.
Pia wapo wanyiramba.
Uchawi Kwa kiasi kikubwa unapatikana Milimani ambapo ipo Mashariki mwa kamji Ka Makanya.
Wasambaa na watu wa Tanga wameongeza nafasi ya UCHAWI katika mji huo wenye ukame.
Makanya ndio Makao makuu ya Biashara ya Mirungi Afrika Mashariki.
Mirungi hiyo itokayo Milimani hasa Tae, Suji, Parane na Chime ina ladha inayopendwa na watumiaji ukilinganisha na Mirungi ya Kenya na Somalia.
Uchawi pia unaisaidia Biashara hiyo ya Mirungi kuendelea kuexist mbali na Rushwa.
Polisi Wanoko wasiotaka Rushwa hukipata cha mtema kuni wakifuatilia Wauza Mirungi huko Milimani.
Hivyo hujikuta wanapata madhara na kuamua kuacha au huamishwa kabisa kituo cha kazi.
Kipindi nakua, baadhi ya ajali za barabarani zilihusishwa na Uchawi na Ushirikina.
Makanya pia ni moja ya miji iliyojaliwa Madini ya Mawe ya Nasi(Gypsum stone) ambapo hutumika kutengeneza Saruji(Cement).
Ipo dhana katika mji huo kuwa Migodi ya Jasi inaathiri unyeshaji wa Mvua.
Watu wa Makanya kipindi nakua waliamini kuwa Mvua inahamishwa na wenye Migodi ya Mawe Jasi.
Ni kawaida Makanya Wingu Jeusi kutanda lakini upepo ukatokea na kupeperusha mawingu hayo na mvua kugoma kunyesha.
Hata hivyo, kitaaluma Tabia nchi ya Makanya na tambarare ya magharibi ya wilaya ya SAME ni SEMI-ARID DESERT.
Hivyo sifikiri uhaba wa Mvua Makanya unaotokana na uchawi na Ushirikina Bali ni tabia ya nchi ya eneo hilo
AINA ZA UCHAWI ULIOPO MAKANYA KULINGANA NA ASILI;
1. Uchawi wa Wapare wenye asili ya Milimani sio Tambarare
2. Uchawi wa kisambaa
3. Uchawi wa kizigua na Kibondei
4. uchawi wa Kimasai unaotokea magharibi ya Mji wa Makanya ambapo kuna Mji wa Ruvu.
5. Uchawi wa Kirundi kutokana na Wakazi wa Makanya wenye Asili ya Burundi ambao wengi walikuja kufanya vibarua kwenye mashanba ya Mkonge
6. Uchawi wa Wanyambo na Wasukuma. Hawa pia walikuja Kama vibarua vya Mkonge.
7. Uchawi chotara
Ambao kutokana na mchanganyiko wa Makabila Makanya kuna uchawi chotara.
Wachimba Jasi wanaotaka Maeneo mengine ya Tanzania wamechangia kiasi katika uchawi huu.
Msamiati Kama Zongo ni moja ya maneno ya kawaida Makanya.
Kuvunja Jungu, n.k
Makanya na Hedaru ni moja ya miji Maarufu wilayani Same na pia inaongoza Kwa ujanja ujanja.
Sisi Wana Makanya tunapendana mno,
Nasubiri mkuuNakuja huko
Aisee umemaliza kila kitu. Big UpNimezaliwa Makanya

Wilaya ya Same siyo Same mjini
We jamaa acha imani za ajabu,hii ni ajari ya kweli,hii ni gari ya kampuni ya northern engineering,HQ yao ipo sakina arusha,gari hii ilikuwa imepaki kwenye mnara,juu mlimani,ilikuwa haijawekwa handbreak,ikaserereka,Huwa nacheka sana baadhi ya watu wakipinga kwa nguvu zote kuwa hakuna uchawi. Hawa hawajatembea wakajionea kwa macho yao na kushuhudia live kabisa, SIO KUSIMULIWA.
Last week kuna picha ilitrend mitandaoni ikionesha gari la Landcruiser pickup likiwa limekita pua juu ya paa la nyumba ya udongo na kudumbukia ndani. Achana na ubora na uimara wa nyumba ambayo pamoja na kuathirika kwenye paa lake lakini kuta zimebaki salama licha ya kuangukiwa na gari lenye uzito wa tani hivi.
Baada ya picha ile kuzagaa mitandaoni kuna wanahabari walichukua muda kwenda kupata ukweli na uhalisia wa tukio zima na wakatuletea na video! Katika video husika mashuhuda wakalihusisha tukio zima na imani za kishirikina! Mwenye gari kampuni ya minara ya Arusha kaingia mitini na kulitelekeza gari lake ambalo liliserereka lenyewe likapata support ya waya za umeme na kwenda kuishia kujikita kwenye nyumba husika. Hakukuwa na vifo wala majeruhi licha ya kwamba wakati wa tukio kuna mtoto alikuwa kalala ndani.
Mimi nilikuwa mitaa ya huko mwanzoni mwa mwaka huu. Nilienda kwenye mishe zangu personal. Nilienda Milima ya kati ya Hedaru na Same eneo linaitwa makanya Kijiji cha TAE. Kwa hakika kule niliukuta ushirikina katika uhalisia wake.
Kule mahakama ya haki ni ushirikina hakuna dhuluma, hakuna wizi, hakuna kugeukana hakuna kusalitiana. Ukizingua kwenye hayo moto utakuwakia. Kule ni heshima, adabu, ukweli na uaminifu.
Wizi wa bodabida ni tatizo kubwa Tanzania lakini sio Makanya wala Tae. Wakati naelekea Tae tukapita mahali porini kuna bodaboda imeegeshwa kwenye mti nikaambiwa ina wiki mbili hapo na mwenyewe alitoa tu taarifa kwa ndugu zake kuwa ilimuishia mafuta. Akaiacha hapo akauchapa mpaka Makanya akaenda zake aendako.
Safari yangu ya Tae ilinikutanisha na mambo ya ajabu lakini mengine ya kutisha. Kwa kifupi Tae kunaogopeka kati ya vijiji vyote vya kule. Tae mpaka leo hakuna usafiri wa Jumuiya kwenda na kurudi Makanya licha ya kwamba kuna umbali wa kama Kilometers 20 hivi huko ni boda au kuuchapa na ni kupanda ama kushuka milima na vilima.
Magari yaendayo Tae ni kwa ajili ya waendao kwa waganga wa kienyeji, misiba, shughuli za kiserikali na miradi.
Tae kuna vilinge maarufu vya kuua, kuharibu, kutengenezwa mambo yako. Na wakuu wake hawaingiliani bali wanashirikiana. Nikiwa kule nilishuhudia nyumba zilizoachwa na wahanga wa usaliti kwenye siasa.
Wahanga wa usaliti kwenye biashara (mirungi, bhangi na gongo)
Wahanga wa wizi mbalimbali
Wajuaji nknk
Nilikaa Tae siku tatu tuu lakini niliyoyaona kule yanafaa kuandikiwa kitabu kizima!
Tukirudi kwenye ajali husika tujihoji haya. Kwanini mmiliki kaamua kuitelekeza gari yake ya mamilioni pale?
Je, dereva wake kakimbilia wapi?
Je, wafanyakazi wa kampuni kuna mahali waliharibu?
Bado natafuta wasaa nifike eneo la tukio. Na nikienda huko nitawaletea mrejesho.
View attachment 1828122
Hiyo gari iliserereka kutoka mlimani,kazi za minara ya simu,ni tukio la kawaida kabisaIli uzi uendelee kunoga yabidi DEREVA wa gari atafutwe ajieleze nini kilitokea, ni matumaini yangu kampuni husika itamjengea nyumba mama.
Mkuu niMekucheki PM
Mkuu Mshana Jr huku ndio nyumbani au ndio ulikochukulia jiko?Haya ndio mazingira ya Tae. Ni milimani kwenye baridi kali lakini kukiwa na greenish nzuri na vijito vinavyotiririsha maji meupe masafi.. Hizi picha niliwahi kutupia hapa JF kule SELFIKA[emoji2]
View attachment 1828124View attachment 1828125View attachment 1828126
Hii ndio video husika ya tukio zima. Dereva kama angepatikana angetupa insights za nini kilitokea dakika zile za mwisho. Je, alienda chobingo? Je, ajali ilimtaka yeye? Je, dereva naye yuko fit?
View attachment 1828123
Nalutafuta nduguMshana umezingua sana, Tae kuna ushirikina kiasi hicho..sikubaliani na wewe hata kidogo Ila najua unaaminika zaidi so sitatumia nguvu nyingi kupinga hoja yako ya ushirikina huko juu milimani. Yaani kifupi ni kuwa Tae, Chome, Suji, Vudee nk hakuna ushirikina kwa level uliyoongea, umefanya bonge la exaggeration... lakini tukubaline hivyo tu kwamba ushasema hivyo...
Mimi najua ushirikina upo zaidi pare ipi, Ila sio upande uliotaja!
Haaaaaq[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Lushoto kuna Wasambaa hakuna wapare wa Lushoto... Ningesimulia kila kitu kwa siku 3 nilizokaa kijijini Tae si mngesema nimeweka vinegar kabisa....!!?[emoji23]
Kuna watu tayari leo wanaenda huko ikiwapendeza nao wataleta mrejesho wao...