Uchawi vs akili

Naunga mkono na pia nakazia hili swala ebana wako matapeli wanatumia uchawi kupata pesa yaani wale wanasubiri ustaafu au uumwe au uwe na matatizo wakikupoint %90 zalima ulie au ufe kabisa uchawi upo [emoji16]
 

Kwani unafikiria wazungu hawajui uchawi mkuu
Au unadhania imani ya uchawi ni waafrika tu?

Dhana ya uchawi ipo dunia nzima mkuu, watu wanavyozidi kupata maarifa wanakuja kugundua uchawi na imani za mungu ni porojo na wanajikita kwenye mambo ya msingi kuboresha na kurahisisha maisha kisayansi.... hapa ndipo wazungu wanapo tupiga bao

Sisi huku tumekazana na uchawi na kushinda misikitini/makanisani kutafuta favor za maisha kwa “imani”
 
ni muhimu kutambua kwamba sayansi na uchawi sio dhana mbili tofauti kabisa. Kuna baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuonekana kama uchawi lakini yanaelezewa na sayansi. Kwa mfano, watu wanaweza kuonekana kama wanafanya mambo ya ajabu kwa kutumia uchawi, lakini kwa kweli wanatumia ujuzi wa kisayansi (physics, chemistry ,biology)ambao haujulikani kwa watu wengine.



Mfano kwenye Vita vya maji maji 💦


Kama wahehe wange vumbua bullet proof baada ya kujua risasi ni hatari kwao, basi ingewasaidi Sana kupunguza vifo , Lakin kwakuwa hawakuwa na maarifa ya kujizuia na risasi wakamua kuwadaganya wapiganaji Ambao tayar kichwani mwao, Wana Imani za Kichawi, kwamba wakisema maji 💦 basi risasi inageuka kuwa maji 💦,ili kuwa ni trick ya kuwapa morari kwenye uwanja wa Vita japo ni uongo kusema maji na risasi inageuka kuwa maji .


Basi hata na wahehe Nao wangetengeneza risasi ili wawe sawa na wapinzani Wao kwenye medani za kivita, lakini hawakuweza kuujua uchawi uliotumika kutengeneza risasi, ambapo ni physics na kemia
 
Naunga mkono na pia nakazia hili swala ebana wako matapeli wanatumia uchawi kupata pesa yaani wale wanasubiri ustaafu au uumwe au uwe na matatizo wakikupoint %90 zalima ulie au ufe kabisa uchawi upo [emoji16]


Watu wengi wanakuwa na Sonona,hofu, umaskini kwa sababu ya kukosa maarifa sahihi.

Upungufu wa huduma Bora za afya na za kisasa, imepeleke kuwa na matapeli wengi wanaodai kumsaidia kutibu watu ,

Mfano swala la mwanamke kushindwa kupata uzajiuzito , 👈 , hili tatizo limekuwa na utapeli mwingi Sana ,

Lakini si lazima mwanamke abebe ujauzito, anaweza kutumia njia ya chupa kukuza mtoto mpaka miezi 9, Hata hapa Dar hii huduma IPO ni sh million 28 ivi, AU akapandikizwa mwanamke mwingine mwenye uwezo wa kushika Mimba.

Kwa sababu Sio lazima kila wanawake wabebe ujauzito, ni kupoteza Tu Muda na kupunguza uzalisha
ji mali.
 
Mechi ya Azam VS Mashujaa , mlisikia vituko vya uchawi kwenye uwanja wa mashujaa,

Lakin wakafa 3 -0 ,

Pengine walifanya hivyo ili kuwaogopesha Azam, AU wakafikiri kuwa mafuvu, ngozi ndizo zinazo cheza Mpira uwanjani.

Pamoja na kufukia mafuvu,ngozi, lakini havikuwasaidia,

Wasichokijua , Mpira ni utimamu wa Akili na AFYA ya mwili, Katika maximum point.

Nasikia TFF wanafanya uchunguzi ili kubaidi Hilo tukio.

Lazima TFF wawekeze kwenye elimu kuanzia watoto wadogo ili kuwajengea msingi mzuri wa michezo.

Bench la fundi liwe na watu wenye kada za elimu mbalimbali na Sio wazee wa matunguli,

Uchawi unarudisha NYuma maendeleo ya michezo, watu hawafanyi bidii kwenye mazoezi , wanapoteza Muda mwingi kwenye utapeli wa Kichawi.

Michezo , football, swimming, tennis, basketball, cricket, Boxing, etc... Inahitaji elimu ambayo ni sayansi ya michezo.

Kila kitu ni elimu, sayansi Tusikurupuke
 
Hoja nyingine hii kuhusiana na akili inapatikana haoa #9
 
Sayansi pia imejaa roho mbaya nakusababishiana matatizo!! Ww fikilia kikundi cha watu kina amua kukaa maabara nakuamua kutengeneza magonjwa!! Alf baada ya muda wana kaa tena wanatengeneza tiba yake ili wapate
Maokoto [emoji1787] sayansi na uchawi nisawa na mohamed kumuita mudi..[emoji3578]
 

Sayansi na dini ni kipi kimesababisha maafa zaidi mkuu?

Dini ndio chanzo kikubwa cha migogoro duniani..... kuanzia enzi hizo crusade hadi jihad na hadi sasa

Sayansi imeleta mapinduzi makubwa sana duniani
 
Nimefanya tafiti mkuu uchawi ni uowoga unao ambatana na matatizo ya akili
Kabisa mkuu ,tena ni ugonjwa wa kuambukiza, unakuta mtu anaongelea uwepo wa majini , ukimuuliza aliyaona wapi hakuna kitu .
 
Kuna kipindi fulani cha nyuma , nilitafuta nyumba ya kupanga huko tanga kwa kazi fulani iliyonileta apo.

Nikapata nyumba fulani nzuri sana , wakazi wa eneo , wakaniambia hiyo nyumba haikaliwi na mtu ina mashetani yanakupiga usiku.

Niliichukua ile nyumba nikakaa zaidi ya miezi sita kwa elfu 30 tu kw mwezi nyumba nzima .

Sikuona chochote , wakazi wa huo mtaa kila mtu alikua ananiogopa [emoji38][emoji38]
 
Sayansi na dini ni kipi kimesababisha maafa zaidi mkuu?

Dini ndio chanzo kikubwa cha migogoro duniani..... kuanzia enzi hizo crusade hadi jihad na hadi sasa

Sayansi imeleta mapinduzi makubwa sana duniani
Ni kweli imeleta mapinduzi ila na madhara makubwa vile vile.

Silaha za kutisha,

Sasa hivi ndio tunaenda kwenye hatari zaidi mnatengenezewa mpaka manukato, vipodozi na vitu vingine vya kubadilisha hormone zenu muwe na matamanio kama wanawake
 
Tanga maeneo gani
 
Ni kweli imeleta mapinduzi ila na madhara makubwa vile vile.

Silaha za kutisha,

Sasa hivi ndio tunaenda kwenye hatari zaidi mnatengenezewa mpaka manukato, vipodozi na vitu vingine vya kubadilisha hormone zenu muwe na matamanio kama wanawake

Mkuu haya yote yanatokea kwa sayansi kwasababu HAKUNA MUNGU
 
Mwafrica ni mtu aliepotea kutokana na husuda na kutamani vya majirani ili hali hajui hata jirani kafikaje hapo. Hao mnaowaita sijui technlogical advanced sijui kitu gani utagundua it's all bullshit. Ukweli ni kuwa wao wamegraduate kutoka uchawi mpaka kwenye advanced level ya kuongea na baba wa uchawi kabisa( devil himself) na kuwapa mifumo mipya ya kuwahadaa wajinga kama waafrika. Kwanza vijana wengi wa Afrika wataangukia pabaya katika umasikini mkubwa na wengi mpaka leo hawajui direction yao ni ipi maana hawana imani ila wanaabudu sayansi ambayo nayo hata hawaijui ni matope tu kichwani. Mtu hana imani na hana ujuzi wa hicho anachokiamini ndo maana ukifuatilia vijana wengi wa 90's bado ni masikini wakati enzi hizo wazee walikuwa wanatoboa miaka 18+ tu. Halafu na vijana wengi wamenyweshwa madawa sana utotoni na marituals kibao wengine wako kwenye mikataba ya wazazi wao na maagano ya shetani hivyo hawajui wanaishije ndo kutwa kuwaita watu wajinga kwa kuwa ni imani thabiti kama ya dini. Mfano mmoja wamarekani mnaowaita sijui advanced sijui upuuzi gani lakini rituals wanazofanya daily hasa wale iconic figures wao utashangaa ni vitu gani. Mfano tunaita washed up industries kama Hollywood kuna ritual maarufu ya kuvaa dresses (magauni na skirt) kwa male celebrities ambapo utaona madili ya movie yanamwagika kwa celebrity husika( hii mfano mastar kibao walishaiaddress na wakapotea kwenye game kweli)

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…