Uchawi vs akili

Uchawi vs akili

Nachojua kwamba wakoloni walitushinda kwasababu tulishidwa kutumia uchawi kwa akili,badala yake tukatumia uchawi kama uchawi...hicho ndicho kinacho tusumbua mpaka hivi leo kuonakwamba uchawi mbaya kumbe tunashidwa kutumia akili kwenye kutumia uchawi ipasavyo na kuangukia kwenye umasikini na mangojwa ya ajabu.
Naunga mkono na pia nakazia hili swala ebana wako matapeli wanatumia uchawi kupata pesa yaani wale wanasubiri ustaafu au uumwe au uwe na matatizo wakikupoint %90 zalima ulie au ufe kabisa uchawi upo [emoji16]
 
Nachojua kwamba wakoloni walitushinda kwasababu tulishidwa kutumia uchawi kwa akili,badala yake tukatumia uchawi kama uchawi...hicho ndicho kinacho tusumbua mpaka hivi leo kuonakwamba uchawi mbaya kumbe tunashidwa kutumia akili kwenye kutumia uchawi ipasavyo na kuangukia kwenye umasikini na mangojwa ya ajabu.

Kwani unafikiria wazungu hawajui uchawi mkuu
Au unadhania imani ya uchawi ni waafrika tu?

Dhana ya uchawi ipo dunia nzima mkuu, watu wanavyozidi kupata maarifa wanakuja kugundua uchawi na imani za mungu ni porojo na wanajikita kwenye mambo ya msingi kuboresha na kurahisisha maisha kisayansi.... hapa ndipo wazungu wanapo tupiga bao

Sisi huku tumekazana na uchawi na kushinda misikitini/makanisani kutafuta favor za maisha kwa “imani”
 
ni muhimu kutambua kwamba sayansi na uchawi sio dhana mbili tofauti kabisa. Kuna baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuonekana kama uchawi lakini yanaelezewa na sayansi. Kwa mfano, watu wanaweza kuonekana kama wanafanya mambo ya ajabu kwa kutumia uchawi, lakini kwa kweli wanatumia ujuzi wa kisayansi (physics, chemistry ,biology)ambao haujulikani kwa watu wengine.



Mfano kwenye Vita vya maji maji 💦


Kama wahehe wange vumbua bullet proof baada ya kujua risasi ni hatari kwao, basi ingewasaidi Sana kupunguza vifo , Lakin kwakuwa hawakuwa na maarifa ya kujizuia na risasi wakamua kuwadaganya wapiganaji Ambao tayar kichwani mwao, Wana Imani za Kichawi, kwamba wakisema maji 💦 basi risasi inageuka kuwa maji 💦,ili kuwa ni trick ya kuwapa morari kwenye uwanja wa Vita japo ni uongo kusema maji na risasi inageuka kuwa maji .


Basi hata na wahehe Nao wangetengeneza risasi ili wawe sawa na wapinzani Wao kwenye medani za kivita, lakini hawakuweza kuujua uchawi uliotumika kutengeneza risasi, ambapo ni physics na kemia
 
Naunga mkono na pia nakazia hili swala ebana wako matapeli wanatumia uchawi kupata pesa yaani wale wanasubiri ustaafu au uumwe au uwe na matatizo wakikupoint %90 zalima ulie au ufe kabisa uchawi upo [emoji16]


Watu wengi wanakuwa na Sonona,hofu, umaskini kwa sababu ya kukosa maarifa sahihi.

Upungufu wa huduma Bora za afya na za kisasa, imepeleke kuwa na matapeli wengi wanaodai kumsaidia kutibu watu ,

Mfano swala la mwanamke kushindwa kupata uzajiuzito , 👈 , hili tatizo limekuwa na utapeli mwingi Sana ,

Lakini si lazima mwanamke abebe ujauzito, anaweza kutumia njia ya chupa kukuza mtoto mpaka miezi 9, Hata hapa Dar hii huduma IPO ni sh million 28 ivi, AU akapandikizwa mwanamke mwingine mwenye uwezo wa kushika Mimba.

Kwa sababu Sio lazima kila wanawake wabebe ujauzito, ni kupoteza Tu Muda na kupunguza uzalisha
ji mali.
 
Mechi ya Azam VS Mashujaa , mlisikia vituko vya uchawi kwenye uwanja wa mashujaa,

Lakin wakafa 3 -0 ,

Pengine walifanya hivyo ili kuwaogopesha Azam, AU wakafikiri kuwa mafuvu, ngozi ndizo zinazo cheza Mpira uwanjani.

Pamoja na kufukia mafuvu,ngozi, lakini havikuwasaidia,

Wasichokijua , Mpira ni utimamu wa Akili na AFYA ya mwili, Katika maximum point.

Nasikia TFF wanafanya uchunguzi ili kubaidi Hilo tukio.

Lazima TFF wawekeze kwenye elimu kuanzia watoto wadogo ili kuwajengea msingi mzuri wa michezo.

Bench la fundi liwe na watu wenye kada za elimu mbalimbali na Sio wazee wa matunguli,

Uchawi unarudisha NYuma maendeleo ya michezo, watu hawafanyi bidii kwenye mazoezi , wanapoteza Muda mwingi kwenye utapeli wa Kichawi.

Michezo , football, swimming, tennis, basketball, cricket, Boxing, etc... Inahitaji elimu ambayo ni sayansi ya michezo.

Kila kitu ni elimu, sayansi Tusikurupuke
 
Uchawi na akili ni vitu viwili tofauti. Uchawi ni imani katika nguvu za kiroho au za kichawi, wakati akili ni uwezo wa kufikiri na kuelewa.

Uchawi
  • Ni imani katika nguvu za kiroho au za kichawi.
  • Huweza kutumika kwa madhumuni mbalimbali, kama vile kusababisha madhara, kushawishi matukio, au kupata utajiri.
  • Hauna msingi wa kisayansi.

Sayansi

Sayansi ni mfumo wa ujuzi unaotegemea uchunguzi, majaribio, na ubunifu. Sayansi inatumia mbinu za mantiki na ushahidi ili kuelewa ulimwengu unaotuzunguka.

Sifa za sayansi

Uchunguzi: Sayansi huanza na uchunguzi wa ulimwengu unaotuzunguka. Wanasayansi hutumia akili zao na hisia zao ili kutambua mifumo na uhusiano.
Majaribio: Wanasayansi hutumia majaribio ili kupima nadharia zao. Majaribio yanasaidia wanasayansi kuthibitisha au kukataa nadharia zao.
Ubunifu: Sayansi inahitaji ubunifu. Wanasayansi wanahitaji kuwa na uwezo wa kufikiria nje ya boksi na kutoa nadharia mpya.

Akili

  • Ni uwezo wa kufikiri na kuelewa.
  • Huweza kupimwa kwa kutumia vipimo vya akili.
  • Ina msingi wa kisayansi.

Tofauti kati ya uchawi na akili

Uchawi unategemea imani, wakati akili inategemea ushahidi.

Uchawi unategemea imani katika nguvu za kiroho au za kichawi ambazo haziwezi kuthibitishwa. Akili, kwa upande mwingine, inategemea ushahidi wa kisayansi.

Uchawi unahusisha matumizi ya nguvu za kiroho au za kichawi, wakati akili ni uwezo wa kufikiri na kuelewa.

Uchawi mara nyingi huhusisha matumizi ya dawa za jadi, spell, au uaguzi. Akili, kwa upande mwingine, ni uwezo wa kufikiri na kuelewa, Bila kujali kama inahusisha matumizi ya nguvu za kiroho au za kichawi.

Uchawi hauna msingi wa kisayansi, wakati akili ina msingi wa kisayansi.

Uchawi hauna msingi wa kisayansi na hawezi kuthibitishwa. Akili, kwa upande mwingine, ina msingi wa kisayansi na inaweza kupimwa kwa kutumia vipimo vya akili.

Maoni ya watu mbalimbali kuhusu uchawi na akili.

Watu wengine wanaamini katika uchawi, wakati wengine hawaamini kabisa. Watu wanaoamini katika uchawi wanaweza kuamini kwamba uchawi unaweza kutumika kwa madhumuni chanya au hasi.

Watu ambao hawaamini katika uchawi wanaweza kuamini kwamba uchawi ni udanganyifu au kwamba hakuna ushahidi wa kisayansi wa kuunga mkono kuwepo kwake.

Watu wengi wanaamini kwamba akili ni muhimu kwa kufanikiwa katika maisha. Akili inaweza kusaidia watu kufikiri kwa ubunifu, kutatua matatizo, na kufanya maamuzi sahihi.

Kama uchawi unamanufaa ungetusaidia kusitawaliwe na wakoloni, lakini ni kwamba wakoloni walituzidi akili, (maarifa).

Nilikuwa natoa ushauri Kwa JF Kwamba kuwe na jukwaa la Mada za Kichawi , nguvu za Giza.

Na jukwaa la intelligence libaki na Mada zenye utafiti wa kisayansi.
Hoja nyingine hii kuhusiana na akili inapatikana haoa #9
 
Uchawi ni taaluma iliyoshindwa kuthibitishwa kisayansi. Mfano kwenda Marekani kwa nusu saa.

Lakini uenda uchawi ungetumiwa vizuri ungekuwa na manufaa... Ubaya wa uchawi ni kuuana, kulogana... Yani uchawi ni sambamba na Roho mbaya ya kuwafelisha watu, wakati Sayansi ni sambamba na roho nzuri ya kusaidia wengine
Sayansi pia imejaa roho mbaya nakusababishiana matatizo!! Ww fikilia kikundi cha watu kina amua kukaa maabara nakuamua kutengeneza magonjwa!! Alf baada ya muda wana kaa tena wanatengeneza tiba yake ili wapate
Maokoto [emoji1787] sayansi na uchawi nisawa na mohamed kumuita mudi..[emoji3578]
 
Sayansi pia imejaa roho mbaya nakusababishiana matatizo!! Ww fikilia kikundi cha watu kina amua kukaa maabara nakuamua kutengeneza magonjwa!! Alf baada ya muda wana kaa tena wanatengeneza tiba yake ili wapate
Maokoto [emoji1787] sayansi na uchawi nisawa na mohamed kumuita mudi..[emoji3578]

Sayansi na dini ni kipi kimesababisha maafa zaidi mkuu?

Dini ndio chanzo kikubwa cha migogoro duniani..... kuanzia enzi hizo crusade hadi jihad na hadi sasa

Sayansi imeleta mapinduzi makubwa sana duniani
 
Nimefanya tafiti mkuu uchawi ni uowoga unao ambatana na matatizo ya akili
Kabisa mkuu ,tena ni ugonjwa wa kuambukiza, unakuta mtu anaongelea uwepo wa majini , ukimuuliza aliyaona wapi hakuna kitu .
 
Kuna kipindi fulani cha nyuma , nilitafuta nyumba ya kupanga huko tanga kwa kazi fulani iliyonileta apo.

Nikapata nyumba fulani nzuri sana , wakazi wa eneo , wakaniambia hiyo nyumba haikaliwi na mtu ina mashetani yanakupiga usiku.

Niliichukua ile nyumba nikakaa zaidi ya miezi sita kwa elfu 30 tu kw mwezi nyumba nzima .

Sikuona chochote , wakazi wa huo mtaa kila mtu alikua ananiogopa [emoji38][emoji38]
 
Sayansi na dini ni kipi kimesababisha maafa zaidi mkuu?

Dini ndio chanzo kikubwa cha migogoro duniani..... kuanzia enzi hizo crusade hadi jihad na hadi sasa

Sayansi imeleta mapinduzi makubwa sana duniani
Ni kweli imeleta mapinduzi ila na madhara makubwa vile vile.

Silaha za kutisha,

Sasa hivi ndio tunaenda kwenye hatari zaidi mnatengenezewa mpaka manukato, vipodozi na vitu vingine vya kubadilisha hormone zenu muwe na matamanio kama wanawake
 
Kuna kipindi fulani cha nyuma , nilitafuta nyumba ya kupanga huko tanga kwa kazi fulani iliyonileta apo.

Nikapata nyumba fulani nzuri sana , wakazi wa eneo , wakaniambia hiyo nyumba haikaliwi na mtu ina mashetani yanakupiga usiku.

Niliichukua ile nyumba nikakaa zaidi ya miezi sita kwa elfu 30 tu kw mwezi nyumba nzima .

Sikuona chochote , wakazi wa huo mtaa kila mtu alikua ananiogopa [emoji38][emoji38]
Tanga maeneo gani
 
Ni kweli imeleta mapinduzi ila na madhara makubwa vile vile.

Silaha za kutisha,

Sasa hivi ndio tunaenda kwenye hatari zaidi mnatengenezewa mpaka manukato, vipodozi na vitu vingine vya kubadilisha hormone zenu muwe na matamanio kama wanawake

Mkuu haya yote yanatokea kwa sayansi kwasababu HAKUNA MUNGU
 
Mwafrica ni mtu aliepotea kutokana na husuda na kutamani vya majirani ili hali hajui hata jirani kafikaje hapo. Hao mnaowaita sijui technlogical advanced sijui kitu gani utagundua it's all bullshit. Ukweli ni kuwa wao wamegraduate kutoka uchawi mpaka kwenye advanced level ya kuongea na baba wa uchawi kabisa( devil himself) na kuwapa mifumo mipya ya kuwahadaa wajinga kama waafrika. Kwanza vijana wengi wa Afrika wataangukia pabaya katika umasikini mkubwa na wengi mpaka leo hawajui direction yao ni ipi maana hawana imani ila wanaabudu sayansi ambayo nayo hata hawaijui ni matope tu kichwani. Mtu hana imani na hana ujuzi wa hicho anachokiamini ndo maana ukifuatilia vijana wengi wa 90's bado ni masikini wakati enzi hizo wazee walikuwa wanatoboa miaka 18+ tu. Halafu na vijana wengi wamenyweshwa madawa sana utotoni na marituals kibao wengine wako kwenye mikataba ya wazazi wao na maagano ya shetani hivyo hawajui wanaishije ndo kutwa kuwaita watu wajinga kwa kuwa ni imani thabiti kama ya dini. Mfano mmoja wamarekani mnaowaita sijui advanced sijui upuuzi gani lakini rituals wanazofanya daily hasa wale iconic figures wao utashangaa ni vitu gani. Mfano tunaita washed up industries kama Hollywood kuna ritual maarufu ya kuvaa dresses (magauni na skirt) kwa male celebrities ambapo utaona madili ya movie yanamwagika kwa celebrity husika( hii mfano mastar kibao walishaiaddress na wakapotea kwenye game kweli)

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom