kakangu ana mabinti zake wameshafika chuo, kawanunulia magari kila mmoja. na amewawekea bili ya mafuta pia. nadhani hapo ndipo tunatofautiana, wengine magari wameyapata miaka 5 baada ya kuajiriwa, wakati mwingine wamezaliwa wanayaona nyumbani, wamefika 18 wametafutiwa leseni walikuwa wanaendesha kwenda sokoni na walipoenda chuo wazazi wao wamewanunuliwa. wakati wewe alichoki toka mwanza huko unasugua barabara hadi uje uajiriwe tena ukae miaka kadhaa mshahara wako uongezeke then ukopee hakohako kamshahara ununue gari. hao ndio huyu aliyeleta mada.
kuna siku kuna mdada fulani wa ofisini hapahapa DSM aliomba tumsogeze nyumbani kwao kwasababu siku hiyo hakuja na gari. ni mtu anajishusha huwezi amini kama sio maskini, tukampakia tukaseme tumpitishe kwao, wapi? nikashangaa anatuelekeza tuelekee Masaki duh, tulienda kumshusha kwenye nyumba hiyo, naomba niishie hapa nisiendelee kusema, nilibaki mdomo wazi. familia ambayo kale kagari ka ofisi yetu wanaweza kununua hata 20 huko. sikuongea kitu ila hata nikikutana naye huwa namwangalia tu kwa kumchungulia manake sisi wengine wachaga nafikiri unajua maisha yetu ni ya kimara, sinza huko na tunajifanya tuna maisha mazuri, nilipelekwa sehemu ambao imetuliaaaaa kama maji ya mtungi. pale hadi ubongo lazima utulie aisee. vijana tutafute hela mabinti zetu wasiliwe kimasihara.