Uchawi wa wanawake ni gari, sitosahau gari yangu ya kwanza ilivyogeuka kuwa sumaku ya kuwatumia hadi kuwakinai, Gari! Gari! Gari!

Uchawi wa wanawake ni gari, sitosahau gari yangu ya kwanza ilivyogeuka kuwa sumaku ya kuwatumia hadi kuwakinai, Gari! Gari! Gari!

Watachezewa Sana Kwa Namna Hiyo.
Shida ya kuzaliwa familia maskini zisizo na magari anaonyesha wazi kazaliwa familia ya maskini huyo mleta mada gari kalipatia ukubwani wakati watoti wa matajiri gari Kwao ni kama Doli tu wameanza kuyatumia Toka wakiwa wachanga
 
Pole mleta mada, sikuhizi tunamiliki gari kali kuliko hata nyie wanaume, kwa hiyo ukishi kwa kigezo cha gari utawapata wasiojielewa wanaobabaika na
magari

Zama zimebadilika sana, wanawake wanapambana kuwa namaisha mazuri ambayo sio tegemezi kwa sababu ya mentality kama yako
 
Screenshot_20240213_232815_Google.jpg
 
Haijalishi ni Ist, Passo, Carina, Teza, n.k. dada zetu wengi hasa wanaotembea kwa miguu wanachojua gari ni gari, japo ukiwa na mkoko wa maana inakuwa fresh zaidi kupata kuwapata wazoefu wanaomiliki magari ya kawaida.

Binafsi Nakumbuka takribani miaka 10 iliyopita nilipomaliza chuo nikiwa na 24 nilipata sehem ya kujiegesha kwa kazi ambayo mshahara haukuzidi hata laki 4 lakini kama zali vile kuna ndugu alinipa kigari kinisaidie mizunguko ya mjini, Ilikuwa gari ya kiuchumi inatumia mafuta kidogo hivyo sikuhofia kupiga misele, nilikuwa mtunzaji sana wa gari sikuenda sana gereji, kitu pekee kilichonigharimu ni service nilivyokuwa naifanya baada ya miezi sita

Ehh bwana weee !! wanawake wakikuona una gari tena hasa uwe kijana mdogo haujavuka 30 tayari wanajua una uelekeo mzuri kwenye future yako, wanakuona husband material. kumbe wasichojua mtu anaweza kuwa anaingiza chini ya elf 10 kwa siku ila anaweza kutumia gari, kazidiwa kipato hata kwa dereva wa daladala.

Kimasihara masihara nikaanza kutoa lifti kwa kisingizio cha "Dada nakuomba uingie kwenye gari nikusogeze, jua ni kali / mvua itanyesha" kitu imooo !!! niliwahi kuifanya hii hata kwa crush wangu niliekuwa namsaka kwa muda mrefu huku akinitolea nje, game niliisimamia ukuxha 😂 usiku kucha.

Ukiwa na gari usitumie zile mbinu za kuomba namba kwenye daladala ama mtaani ukiwa unafukuzia kwa mguu ama boda, inabidi ujiongeze thamani, tengeneza business card zako, hii inakupa thamani zaidi na kuwazuzua vilivyo kukuona una piga mishe nzito nzito na unalingana na hadhi wanavyokufikiria, kwamba unaweza hata kuja kuwapa konection, binafsi business card zangu zilikuwa za mchongo niliweka Jina la kampuni la kujitungia, nikajipa cheo mimi ni meneja, cha ukweli kilikua ni namba ya simu tu, akishuka mpe card yako na elf 2 ya boda, uhakika wa kukucheki ni 90 %.

Kugharamika kwa kila pisi inaweza kukucost elf 20 ukiwa na kigeto chako, ukisema uende lodge huko kuna hela ya Ziada ya chumba.

Exit Strategy ni rahisi sana, waweza tu kusingizia mke wako kagundua, cha muhimu usiweke kambi, ukiweka kambi kwa muda mrefu huwezi acha kienyeji.

Umri umeenda na baadhi ya mambo nayo yamekwenda, ilikuwa ni Enzi hizo za ujana ndio nilifanya hio michezo, kwa sasa nina ndinga kali zaidi lakini siwezi hata kufikiria kuigeuza iwe chambo 😂 Enzi hizo hata ukionekana na kabebe kwenye gari unasifiwa na age mates ila kwa sasa hizi Ishu hata nikihitaji Labda niwe na mchepuko wa malengo ya kuwa nae muda mrefu sio kukaa na mtu siku 3, it's more than the action, it's about a serious relationship.
Yeah!...kwenye Uzi wako Kuna chembechembe nyingi za ukweli....Ila kuna baadhi ya Siri za Kambi umeuza mkuu!😅😄😄🙌
 
NI lazima kuwe na madaraja kwenye jamii, huyo Kaka yako kabarikiwa ana mafanikio yake kaweza kuwanunulia "watoto wake" magari mapema ni jambo zuri.

Wengine Tumeanza kuyajua magari tukiwa na 24, wengine miaka 7, wengine 16, wengine 30, wengine 40, wengine hawayajui kabisa.

Wengine wanaona Toyota sio magari parking zimejaa audi, Ford,.. House boy ndio kapewa bmw ya kufata watoto tuition.
Ukizungumzia Toyota be specific ni Toyota gani,kuna Toyota century unaifahamu?
 
Katika wanawake ambao hawapendi magari mimi naongoza. Sio kila mwanamke ana ushamba wa magari jamani.

Basi tu sina namna ila natamani sana yule ninayempenda asiwe na gari. Tuishi maisha ya kawaida kabisa maana mentality za wanaume wengi wenye magari ndio kama hizi… wanawake.
Maisha ya roho juu siyawezi.
Ngoja nikupakie kwenye toyota century yangu,halafu tuone kama hutapenda
 
Mimi nilimkosa mdada wa maana kabisa kisa kuwa na gari, anasema angependa tuanze chini wote, nilishangaa sana

Kwahiyo mleta mada, huo mkweche wako utakukosesha dhahabu za maana huko ukichekelea kubeba mawe.
Chini ya kila mtu inategemea,chini ya mtoto wa bakhresa sio chini yangu
 
Katika wanawake ambao hawapendi magari mimi naongoza. Sio kila mwanamke ana ushamba wa magari jamani.

Basi tu sina namna ila natamani sana yule ninayempenda asiwe na gari. Tuishi maisha ya kawaida kabisa maana mentality za wanaume wengi wenye magari ndio kama hizi… wanawake.
Maisha ya roho juu siyawezi.
Unanifaaa
 
Back
Top Bottom