Uchebe afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumshambulia Shilole

Uchebe afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumshambulia Shilole

IMG-20200406-WA0006.jpg
 
Sahv uchebe azipuzie media maana naye kutwa kuhojiwa, dem anataka kumkomoa amsweke Ndani asijisikie burdan

Ova
 
Ikifika hatua unamwambia mwanamke neno hatii, mpaka unampiga, my dear brother, uncle, father, katafute atakae kusikiliza na kukuheshimu.
Mwanamke akikupenda na kukuheshimu, atakutii. Ukiona heshima yake kwako unaipambania, hakuamkii mpaka umwambie kama mtoto mdogo, "wewe mbona huniamkii", anakuongelea shit, hakushirikishi tena mambo yake, kula kona bro, wanawake dunia hii wapo rundo, ukifeli kupata wa maana nicheki nitakuunga kwa wife material wa kila rika. Usimpige mwanamke, utafungwa bro.
 
serikali somtimes mna kiherehere ?
sasa kama aliyepigwa hajashtaki nyie yanawahusu nini ? au kesi zimeisha ?
 
karma is a bitch. kipindi anampiga Nuhu mziwanda hadharani yeye alichekelea tu. kipigo kimemrejea yeye na anajikuta nunda kushtaki mahakamani. huyu dada ange rewind kumbukumbu zake angejisikia aibu sana kwa kumpiga kofi nuhu.
 
Dar es Salaam.

Ashiraf Geuza maarufu' Uchebe' amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na kosa la kumjeruhi Zuwena Mohamed maarufu 'Shilole' na kumsababishia maumivu makali.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Serikali, Chesensi Gavyole mbele Hakimu Mkazi Hudi Hudi, alidai kuwa Julai 6, 2020 maeneo ya Dar Estate Kinondoni jijini Dar es Salaam mshtakiwa huyo alimpiga Zuwena Mohamed sehemu ya kichwa na shingoni na kumsababishia maumivu makali.

Hata hivyo mshtakiwa huyo alikana shtaka linalomkabili. Gavyole alidai kuwa upelelezi umekamika na aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine.

Hakimu Hudi alisema dhamana ipo wazi mshtakiwa anatakiwa awe na wadhamini wawili ambao wanatakiwa kuwa na barua inayotambulika na watasaini bondi ya Sh2 milioni pamoja na mshtakiwa.

Mshtakiwa huyo alikidhi masharti ya dhamana shauri hilo limeahirishwa hadi Septemba 23, 2020 itakapokuja kwa ajili ya usikilizwaji wa hoja za awali.
Polisi wamefanyia kazi mambo ya mitandaoni?
 
Back
Top Bottom