Uchebe kasaini kufundisha Singida black stars

Huyu kocha sitamsahau, aliitengeneza Simba Sc ikawa moto yenye vikosi viwili, nakumbuka ile super sub ya Miraj Athuman ilikuwa kazi ya Aussems...

Baadae yule gabachori akaanza wivu wake, anataka yeye ndie apendwe na kutukuzwa kama mungu mtu ndani ya klabu, akamfukuza uchebe bila kosa lolote huku kwa aibu hiyo kazi ya kumfukuza akimuachia dada yake asimamie yeye akakimbilia nje ya nchi.

Kutoka hapo ndio downfall ya Simba Sc ikaanza, kila siku ni kubadilisha makocha tu, timu haina mbele wala nyuma uongozi haueleweki, sajili za hovyo.

Aliyebaki anafanya vizuri atlist ni Ahmed Ally pekee huku nae maneno mengi anayoongea yakigeuka uwongo kwasababu ya kutokuwepo kwa uwiano kati ya mdomo wake na vitendo uwanjani, maneno mazuri huku uwanjani mpira wa hovyo.
 
Kishingo pia alifanya kazi nzuri. Ndiye aliyeiondoa Simba kwenye utamaduni wa kupigwa hamsa πŸͺ¬ Uarabuni.
 
Uchebe ndio mwasisi wa pira biriyani, Kishingo alitembelea nyota yake
Uchebe ndio aliyeanzisha na kuasisi simba imara ya kimataifa. Ile mechi ya Simba Vs Nkana Ni bonge moja la mechi katika historia ya mpira wa Tanzania. Ndio mfumo wa kumtegemea Chama ulianzia hapo na mpaka leo simba bado wanamtegemea chama 🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…