KERO Ucheleweshwaji wa malipo ya 'Booms' unakwamisha shughuli za Wanafunzi wa Chuo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Bodi ya Mkopo Heslb inatupa wakati mgumu sana hasa wanafunzi tunaotokea familia ya vipato vya chini, maana wanafanya kazi kama wanavyojisikia wao Bali si kama wajibu wao wanafunzi tunalala njaa hatuna pesa.

Lakini pia kupata allocation inafanyika mapema lakini sasa pesa ya kujikimu inakuwa mwendo wa Kobe.

Kwa mfano mimi hapa ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) sijalipwa pesa ya matumizi, na harafu hiyo pesa ndo tulio wengi tunasubiria kulipwa ili kuwezesha kulipia gharama za moja Kwa moja yaani direct cost, na dirisha linafunguliwa la pili nalo linafungwa tar 30/11/2024 na hii inapelekea kuahirisha masomo kwa sababu ya watumishi wachache wazembe katika office za HESLB.

Jamani Mamlaka husika tunaomba itusaidie tunateseka na tunaishi kama hatuna mkopo kwa sababu wanajisahau sana hawa watumishi
Vyuoni hamjui wajibu wenu mnasibiri asante kutoka kwa serekali, nyie kama wasomi lini mmekaa kuzungumzia yatokeayo nchini mpo mpo tu kama firigisi ya binadam
 
Mkuu wachuo cha udsm si juzi tu hapa ametamba kwamba mama mitano tena
 
Bodi ya Mkopo Heslb inatupa wakati mgumu sana hasa wanafunzi tunaotokea familia ya vipato vya chini, maana wanafanya kazi kama wanavyojisikia wao Bali si kama wajibu wao wanafunzi tunalala njaa hatuna pesa.

Lakini pia kupata allocation inafanyika mapema lakini sasa pesa ya kujikimu inakuwa mwendo wa Kobe.

Kwa mfano mimi hapa ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) sijalipwa pesa ya matumizi, na harafu hiyo pesa ndo tulio wengi tunasubiria kulipwa ili kuwezesha kulipia gharama za moja Kwa moja yaani direct cost, na dirisha linafunguliwa la pili nalo linafungwa tar 30/11/2024 na hii inapelekea kuahirisha masomo kwa sababu ya watumishi wachache wazembe katika office za HESLB.

Jamani Mamlaka husika tunaomba itusaidie tunateseka na tunaishi kama hatuna mkopo kwa sababu wanajisahau sana hawa watumishi
Kijana hamna mwaka HESLB washakuwa serious ww pambana tu uone namna ya kutoboa kulia lia haisaidii.
Nakumbuka 2017 nipo 4th year Ardhi na Ada sijamalizia imebaki wiki nifanye final dessertation presentation ilibidi nifanye dili haramu mno kupata ile hela.(Niliowapiga Pc naamini walinisamehe)
Haya maisha
 
Mama e zao Heslb wanataka vijana waibe na wengine wauze chini ili walipe ada bila hivyo dirisha linafungwa njoo mwakani
 
Crdb wana account ya scholar ile unaweza kopeshwa boom ukisubiri hela iingie.
 
Sasa kujitapa kote kule kuwa Kuna mabilioni kadhaa washayapanga, kama hawana pesa si waseme tu wanafunzi wajue moja na siyo kuwaacha na dilemma.
 
Waongo ni siasa tu.mwenye boom shida ambae ana boom shida.
 
Back
Top Bottom