www.immigration.go.tz
Kwa ufupi na uchache unatakiwa uwe na viambata vifuatavyo;-
1. Fomu ya maombi ya passport iliyojazwa na kusainiwa na wewe pamoja na wakili (unajaza online kisha unai print).
2. Barua yako ya kuomba passport (just a simple official letter).
3. Barua ya utambulisho toka serikali ya mtaa.
4. Nakala ya cheti chako cha kuzaliwa.
5. Nakala ya cheti cha kuzaliwa ya mzazi wako mmoja. (Kama hauna unapeleka kiapo yaani affidavit)
6. Namba yako ya NIDA au nakala ya kitambulisho cha NIDA kama unayo.
7. Uthibitisho wa safari (hizi zinatofautiana kulingana na madhumuni ya safari yako). Kwa wewe hapo unaweza kupeleka uthibitisho wa uwezo wa kujilipia gharama za safari, malazi, n.k (Bank statement yenye "mzigo" wa kutosha kufanya hayo).
Kwa uchache ni hayo hapo.
Gharama:
20,000/= (Unalipia wakati unajaza fomu online)
130,000/= (Unalipia benki mara baada ya kupeleka nyaraka zako uhamiaji na zikakaguliwa kuonekana ziko sahihi).
Jumla ni 150,000/=
Hapo sijahesabia gharama za wakili na "lojistiki" zingine ndogondogo.