Uchimbaji wa maduka ya chini kwa ajili ya kuongeza sehemu ya maduka unatajwa kuwa chanzo cha kuporomoka kwa jengo kariakoo

Uchimbaji wa maduka ya chini kwa ajili ya kuongeza sehemu ya maduka unatajwa kuwa chanzo cha kuporomoka kwa jengo kariakoo

Kwa jinsi nilivyoelewa, ni kwamba Jengo Hilo la Ghorofa lilijengwa Kwa plan ya kawaida tu, ikiwa na Ghorofa kadhaa...!

Ila kutokana na Tamaa za Wamiliki, na inaonekana ni mchezo wa kawaida Kariakoo Kwa Majengo mengi Kwa Sasa.
Mmiliki akaamua kuchimba Chini ili apate kujenga Frame zitazokua Underground, bila kuzingatia Usalama na plan ya Jengo...!

Matokeo yake hata zile Nguzo zilizoshika Jengo zikawa weak, na kupelekea Jengo kuanguka.....!

Serikali ingeanza kufanya Uchunguzi coz ni majengo mengi Sasa wanaamua kuchimba Underground wakati Jengo lilishajengwa na kuisha zamani.
Na hapa ndipo tatizo lilipo, wengi wanafosi kujenga chini wakati jengo lilishakamilika toka muda matokeo yake ndio haya.
 
Kwa mujibu wa mashuhuda, ghorofa hilo lilianguka ghafla saa tatu na dakika tano asubuhi wakati mafundi ujenzi walipokuwa kazini wakitoboa kwa ajili ya kuongeza sehemu ya maduka.

"Tulianza kusikia kelele za mtikisiko, kisha kwa ghafla jengo zima likaanguka. Wananchi wameshindwa kujiokoa na zoezi la ujenzi lilianza tangu jana hivyo angetaka urahisi angebomoa tu jengo lote," amesema mmoja wa mashuhuda, Harrison Shayo.

Mfanyabiashara mmoja ambaye hakujitambulisha kwa majina, ameeleza kuwa uchimbaji wa maduka ya chini ndio chanzo cha jengo la ghorofa kuporomoka katika eneo la Kariakoo, mtaa wa Congo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema hadi sasa mtu mmoja amefariki dunia na wengine 28 wameokolewa katika ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo jijini Dar es Salaam.​

Soma pia: Ghorofa limeporomoka Kariakoo asubuhi ya leo Novemba 16

View attachment 3153698
View attachment 3153756


Chanzo: Bongo FM, Mwananchi
Naona watu wengi hawaelewi wakisikia neno"walikua wanachimba chini undergroun"

Ipo hivi magorofa ya zaman unakuta kule chini kulikua ni stoo hata mbili au unakuta chini pote kulikua stoo sasa mmiliki anaamua kubadili zile stoo za under ground kuwa maduka kama magorofa meng ya kisasa yanayojengwa kkoo wanajenga maduka kuanzia chini..

Sasa wanaanza kuchimba kubomoa zile kuta ili wapange vyumba vidogo vidogo vya maduka yawe hata 20,, huu ubomoaji kule chini huwenda walivunja hata nguzo bahati mbaya maana hatujui..

Ushauri wangu magorofa yanayojengwa Kkoo underground zinapawa kuunganishwa mfano unaingia dukan chini kuna kuwa njia ya chini kwa magorofa yanayofuatana hata tatzo likitokea inakuwa rahisi watu kutoka.

Baadhi ya magorofa mapya naona yameunganishwa hivi unaweza ingia gorofa ukaona njia inanyooka mpka kwenye gorofa linafuata.
 
Wata
alam ujenzi/wahandisi watueleze kitaalmu ni kwa % ngap hii inaweza sababisha jengo kuporomoka!?,na kama ni hatari je serikali haikulijua hilo na wametoboa majengo mangap mpaka sasa!?
Asilimia 100.
Na hapa ndipo tatizo lilipo, wengi wanafosi kujenga chini wakati jengo lilishakamilika toka muda matokeo yake ndio haya.
Sahihi, lile Jengo lilikua Mzigo wa Mabalo ya Nguo kila Floor, lilikua kama Ghala.
 
Nyie wote mnajiongelea tu hamjui kitu, issue ni huyo Sosteli aliyenunua hilo jengo na tamaa zake, km ukiangalia vizuri kule juu kwenye lile jengo aliongeza floor moja ni baada ya kutaka kulijenga upya wenzie waliokuwa na asilimia 20 ya umiliki kugoma, ndio akaforce kujenga juu kisha kuanza kujenga underground. Katika kuchimba hao mafundi wakagonga bim mzigo ukashuka.

Hilo jengo lina miaka zaidi ya 20 hata kuongeza floor juu tayari ilikuwa ni red flag. Ila sasa viongozi nao wanatoa tu vibali na rushwa wakipewa wanaweka usalama wa watu hatarini, na sisi wafanyabiashara ndio hatuelewi tunawaza pesa tu..!!
 
Jana nilikukumbuka sana sema na mimi nilikuwa na hekaheka kuna mdogo wangu yuko kariakoo eneo hilo kila nikipiga Simu yake ilikuwa haipatikani nilichanganyikiwa mno ila ni mzima.
Acha wifi yangu jana ilikuwa hatari haya mambo ni mazito, mimi jana nilichelewa kwenda nilitanguliza vijana km kawaida yangu..
Nilivyopigiwa simu niliacha gari nikachukua boda naona km nachelewa mana hiyo ndio mitaa yangu, nimelala nimechoka..
Nashukuru wazima na sio jengo letu lililobomoka ila haya mambo yasikie kwa wengine..

Sasa hivi watu wanalia wamepoteza watoto na huku mizigo na wana mikopo bank 😥😭
 
Back
Top Bottom