Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Hakuna sababu ya kukebehi wala kukejeli dini ya mtu yeyote ili kufanya hoja za mtu ziwe na nguvu. Hoja za Mohammed Said zinajibika kwa hoja zenye nguvu zaidi na tumeweza kuonesha hilo tayari mara kadhaa. Sasa kama mtu huwezi kujibu au kuuliza maswali huna sababu ya kushambulia imani ya watu wengine au kuita watu wengine majina.
Bw. Said kwa muda mrefu alikuwa anategemea kupata uwanja huru ambapo wasikilizaji wake wengi walikuwa hawana nafasi ya kumuuliza maswali na kama walimuuliza maswali yalikuwa ni kutoka katika kutofahamu - hawakuwa na cha kusimamia. Hivyo akisema "Nyerere alikuja Dar kwa mara ya kwanza mwaka 1952" hakuna mtu wa kumuuliza na wanashangaa kwa tabasamu; akisema "Nyerere alificha historia ya viongozi wa Kiislamu" wasikilizaji wanashangaa kwani anarusha rusha majina ya watu maarufu; maskini wa Mungu hawajui kuwa walikuwepo Wakristu miongoni mwao... anacheka anaendelea na habari nyingine ambapo wasikilizaji wake wanaonekana kushangazwa na wengine kujaa na hamaki!!
Sasa kaja kwenye home of the Great thinkers; hapendwi mtu, haogopwi mtu - hoja hujibiwa kwa hoja na siyo vioja.. anatoa madai ambayo sehemu nyingine yangewashtua watu hapa watu hawashtuki anaulizwa maswali! Anatoa madai anaulizwa ushahidi anakimbia na kukwepa kiufundi (with technicality). Sasa amefika mahali anadai ati yeye hataki kushawishi watu waamini - unabaki kujiuliza sasa kwanini unaandika kama hutaki watu waamini! - hajibu.
Histohisia yake imeoneshhwa kuwa haina msingi wowote katika historia; zaidi ya masimulizi ya watu kupambana na kuelezana na tena masimulizi ya watu waliuoumizwa hisia zao. Nyerere aliwasema hawa vizuri tu mwaka 1966 kwamba wengine walipigania uhuru wakiamini kuwa baada ya uhuru watapewa vyeo au nafasi fulani; walipokosa nafasi hizo ndio wakamgeuka Nyerere. Wakarudi na udini ule ule waliokuwa nao miaka karibu kumi nyuma, udini ambao Bw. Mohammed Said mwenyewe ametusimulia - japo hakutaka kwenda kuuliza kwanini!