Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Umekosea nani kakwambia mie najificha na dini yangu.
Mie najulikana kote kwa hilo.

Hii ni sifa kwangu si jambo mie nikaona aibu.
Siku nyingine kabla ya kutoa uamuzi niulize kwanza.
Mkuu kimsingi kitabu chako kimebebwa ta udini, hilo huwezi kulikana wala kulikwepa, hata waungaji mkono wako wote kwajicho la tatu wamebeba itikadi ya kidini zaidi.
 
Hapo ndipo wewe unapoingia na kuja na kitabu.

Nikiamua kuandika kitabu itakuwa ni kwa ajili ya kuonesha historical inaccuracies, factual errors, and logical inconsistencies katika madai yako. Lengo itakuwa ni kuwasaidia watu ambao wanaposoma kitabu chako wanafikiria wanasoma kitabu cha historia au cha unbiased person kumbe sivyo.
 
Hilo la heshima unaniasa mie?

Huwa si kawaida yangu kujibu wala kusema kila kitu.
 
Lakini mie hilo mbona sikatai.

Kitabu kinasema kwenye jalada "mchango wa Waislam."
 
Mkuu kimsingi kitabu chako kimebebwa ta udini, hilo huwezi kulikana wala kulikwepa, hata waungaji mkono wako wote kwajicho la tatu wamebeba itikadi ya kidini zaidi.

Kimsingi hata nyie itikadi zenu za kidini ndiyo zinawafanya muwadharau hao wazee wazalendo waliopigania uhuru kisa wengi wao ni Waislam huo ndiyo ukweli.
 
Qur'an haitafsiriwi kuchagua kile ukipendacho kisha ukakiegemeza hapo.

Usiingie huko.
Humu si pahala pake.

Mengi ya ukumbusho wa historia nimeweka.
Huna jambo katika hayo yote?
Haaa! kuumbe! Sasa ilikuwaje sheikh Ilunga alipotoa aya ya ''kisasi'' kwa kushawishi mauaji ya maaskofu na mapadre wewe Mohamed Said ukamuunga mkono!
 
Kimsingi hata nyie itikadi zenu za kidini ndiyo zinawafanya muwadharau hao wazee wazalendo waliopigania uhuru kisa wengi wao ni Waislam huo ndiyo ukweli.

Unadhani ili kuyaondoa haya nini kifanyike?
 
.
Nimesoma darasa moja na mwanae aitwae Rashidi, na nilipewa kazi fulani fulani na bintie aitwae Jasmine akiwa ile NGO ya pale mahali na nikaja kukutana tena na Jasmine akiwa South Africa.

Kadri ninavyokusoma baada ya kisa cha kutiwa gerezani babu yako, ndia sasa naanza kuelewa mzizi wa chuki zako kwa Nyerere!, kumbe alifunga babu!.

Kiukweli japo babuyo alipotoka aliwaita watu waongo, Nyerere alikuwa ni mtu wa "intuition", amini usiamini banu yako was planing something evil!, Intuition ya Nyerere ikamshutukia akashughulikiwa ipasavyo!. Na wewe unaweza kujikuta bila mwenyewe kujijua, badala ya kumrith baba ile ya "like father like son", kumbe umemrithi babu with some evil iside you!. Ndio maana siku zote nimekuwa nikuita "a man with a mission" ila sikuwahi kumalizia ni mission gani but now I'm definetely sure, "it is some evil mission!". Umeandika kitabu with ill intention of evil inside you na wanaokisoma kitabu chako, wakisha maliza kukikosoma, "they are not the same again" " the evil inside the writing inahamia kwa hao wasomaji wako" ili mpate kundi kubwa la kutosha, kwa matumaini kuwa siku ya siku itafika, sio tuu uta kamilisha "the evil mission ya babu", bali pia utalipiza kisasi kwa kufungwa kwa babu!. Na dhani kwa kazi nzuri uliofanya hiyo siku haiko mbali!, tutashuhudia matokea ya kazi yako "nzuri". Hongera!, na kwa vile mnaamini ni jihad, hivyo mtapokelewa peponi moja kwa moja!, endeleeni, wish you all the best!. Muenzi Babu!.

Kwa wale wengine mnaomlaumu Maalim Mohamed Said, naombeni mhurumie, sio kosa lake! hii ni due to "deep rooted neurosis with resentments to revange kwa Nyerere aliyomfanyia babu yake".

Pole sana!.
Pasco.

Mkuu Pasco huwa unanikosha sana na posts zako. Manake wewe kazi yako ni kutoa za uso tu kwa wadini kama Mohamed Said. Kipindi kile umelambishwa BAN kwa kumkorofisha kamanda wangu wa ukweli Molemo nilikumis sana jukwaani. Mungu akupe uhai mrefu Pasco
 
Last edited by a moderator:
Nikiamua kuandika kitabu itakuwa ni kwa ajili ya kuonesha historical inaccuracies, factual errors, and logical inconsistencies katika madai yako. Lengo itakuwa ni kuwasaidia watu ambao wanaposoma kitabu chako wanafikiria wanasoma kitabu cha historia au cha unbiased person kumbe sivyo.

Huwezi, ulimjuwa Mshume kabla hujamsoma Mohamed Said? Maaawe!
 
Mohamed Said,
Baada hoja kuwaishia kinachofanyika sasa ni kukutolea kauli za matusi na kejeli ili ujitoe kwenye munakasha.

Kiukweli wewe ni mvumilivu sana ili nakupa pongezi sana kuvumilia matusi.

Endelea kutoa darsa wala hakuna wa kukufukuza kwa maneno.
 
Last edited by a moderator:
Kimsingi hata nyie itikadi zenu za kidini ndiyo zinawafanya muwadharau hao wazee wazalendo waliopigania uhuru kisa wengi wao ni Waislam huo ndiyo ukweli.

Hao wanaaminishwa na kujazwa ujinga kuwa nyerere ni "mtakatifu" kwa utakatifu asiokuwa nao. Laiti ikionekana historia ya Uhuru ilianzia na kuishia kwa nyerere basi kazi yao ya kuutafuta muujiza wa utakatifu itakuwa imekamilika. Mohamed Said pekee kaisambaratisha hiyo dhanna na kwa hilo usitegemee wagala kuithamini hii jitihada ya Mohamed Said kuweka wazi ukweli. Hawana zaidi ya kuja na kumpinga yeye binafsi na si maandiko yake, sijaona mahali wameweka andiko la Mohamed Said na kusema hili sio sahihi, usahihi ni huu hapa.

Amewaumiza nyoyo na fikra zao vibaya sana kwa kuuonesha ulimwengu kuwa nyerere hakuwa muasisi wa TANU wala muasisi wa Uhuru wa Tanganyika.
 
Maswali haya ya Nguruv3 yamenivutia, sijaona majibu yake. baada ya mihangaiko ya nimejaribu kupitia sijaona majibu.
quote_icon.png
By Nguruvi3

1. Nyerere alikuja kwa mara ya kwanza lini Dar kama ulivyoulizwa?
2. Akienda UNO baada ya kuchangiwa fedha na wazee wako safari yake ilianzia wapi?
3.Halafu ulishaulizwa EAMWS ilianzia wapi na kwanini huko ilikoanzia haipo kwa sasa?
4.Unapozungumzia umoja wa waislam, ni upi huo kati ya Sunni, Shia, Bohora, Ismailia n.k.?
Nini kinashindikana kurudisha umoja huo?
5.Umeulizwa, mlezi wa iliyokuwa EAMWS alikuwa Agakhan, vipi mbona yeye anarudi na kujenga chuo kikuu kingine katika serikali ile ile iliyoua EAMWS 1968?
6.Ushahidi wa kanisa kushinikiza kifo cha EAMWS ni upi?Tusaidiane kumkumbusha Mohamed
sijibu kila kitu.Kubwa ni kuwa siko katika ushindani kwa hiyo hujibu lile lenye tija.
Nikiona swali halina maana huwa sijibu.
Siko humu kushinda mjadala
Siku zote Mohamed ameandika kuhusu tuhuma dhidi ya kanisa na Nyerere. Hilo halina tatizo kama basi ushahidi upo wa kuthibitika. Mathalani amekuwa anadai kuwa kanisa limeua EAMWS bila ushahidi wowote.

Hivi karibuni amekuwa akijaza watu fikra za kuwa bila wazee wake Nyerere asingekwenda UNO.

Tunawashukuru sana wazee wake kwa mchango huo.

Baada ya ukweli kuanza kudhihiri Mohamed amekubali kuwa John Rupia ni mmoja wa watu waliotoa mchango katika harakati za uhuru ikiwa ni pamoja na kuchangia gharama za usafiri wa Nyerere kwenda UNO

Mohamed sasa anakiri kuwa kuna wafuasi wa kanisa waliOchangia ticket (yeye anasema mara moja).
Mohamed aliujua ukweli huu kwasababu alishawahi kusema kuwa amekwenda New York na kukutana nao(ushahidi upo JF)

Kwasababu tu ngano hii ililenga katika kuwadhalilisha baadhi ya watu waliochangia uhuru wa nchi hii, Mohamed hakutHubutu kuandika mchango wa ticket moja wa shirika la Marknoll.
Ameuficha kwasababu ukitoka hadharani atakuwa ameondoa maana halisi ya historia aliyokusudia na siyo iliyokuwepo.

Kitendo cha kuendelea kulaani kanisa huku akijua hilo si kweli na badala yake kuficha ukweli ni unafiki na ulaghai.
Ameupumbaza umma unaotembea na majenereta kusikiliza hotuba zake huku akiwa na siri moyoni.

Hii maana yake ni nini! Maana yake ni kuwa hata zile shajara, makabrasha na mafaili aliyoyaona peke yake kwa akina Sykes huenda kuna mambo mengine hakutaka kuyaweka hadharani kama alivyoficha hili la shirika la Maknoll.

Ni Mohamed huyo huyo ameficha ukweli wa lini Nyerere alifika Dar es Salaam, ameficha ukweli wa kwanini sheikh Amir alitimuliwa, ameficha ukweli kwanini kulikuwa na jaribio la kumuondoa Nyerere mara 2 kabla ya uhuru.
Mohamed ameficha ukweli kwanini EAMWS ilikufa huko ilikoanzia, ilianza lini na washirika wake walikuwa nani.

Pamoja na kuficha ukweli, bado amekuwa kinara wa kubambikia marehemu maneno. Ameshindwa kuthibitisha lini Nyerere alisema hataki historia ya Kleruu na Sykes. Ameshindwa kuthibitisha ushiriki wa kanisa katika kuua EAMWS.

Mohamed kwa kutumia vibaya kalamu yake ameupotosha umma kuwa Nyerere alianza siasa baada ya kuonana na Abdul Sykes, kushonewa suruali kariakoo na kufundishwa kula chapati! Ney! imethibitika ni uzushi uliobobea, Nyerere alianza siasa akiwa Makerere, amevaa mavazi kuanzia Musoma, Makerere, Tabora, Scotland na hakuwahi kutembea na vibwenda

MO hakuwahi kumhoji Nyerere achilia mbali kuomba appointment ya kumuona. Alichobaki kutuambia ni maneno ya Marehemu Prof Othman ambayo pia hakumlizia Nyerere alimjibu nini.
Alichobaki ni kutueleza kuhusu Nyerere kutoa picha na kumuonyesha Malima baila kutuambia Malima alijibu nini.

Mohamed akamsingizia Malima kuwa ndiye aliyeanzisha namba za mitihani. Tulipotaka ushahidi hoja hiyo kaiondoa katika agenda zake! sasa kimyaa! Ulikuwa uzushi tu usio na thibitisho.

Mzee Said anatuambia Nyerere asingefanikiwa kwasababu alikuwa mkristo na hawakukubalika Dar es Salaam.
Tunaushahidi kuwa viongozi wa kisiasa kama Clement Mtamila na Vedastus Kyaruzi walikubaliwa kuongoza chama cha kisiasa ndani ya mji ule ule unaosemekana Nyerere asingeweza.

Mohamed anasahau kuwa Nyerere alikuwa katibau wa AA Tabora mji uliokuwa na Waislam wengi na msisimko wa siasa za nchi yetu naykati hizo.

Mohamed amemsingizia Nyerere kuwa alisema hamjui Abdul Sykes katika hotuba ya kuaga wazee.
Hotuba imewekwa, Mohamed yule yule aliyenukuu hotuba ya Nyerere anataka uthibitisho wa hotuba ile ile aliyonukuu eti kwa audio.

Sijui alinukuu misukule au nini!
Flip flop zote ni kutapa tapa kwasababu hana pa kutokea na taratibu ngano inajichuja na mashudu yanaelea.

Mohamed hakuwahi kumhoji Abdul Sykes kwasababu alikuwa na umri wa miaka 16, na haionekani kama alikuwa tofauti kimtazamo na fikra. Anachosimulia ni third part story ndio maana huchagua nini cha kujibu na mara nyingi hukwama.

Nyerere akifika Dar kwa mara ya kwanza Mohamed hajazaliwa na alipokutana na Sykes Mohamed alikuwa kichanga, kushuhudia kuwa Nyerere alishonewa suruali ni dharau sana, kumsingizia na kumwekea maneno mdomoni ni dhihaka kubwa lakini Kuupotosha umma ni ukosefu wa maadili ya kiroho '' moral authority''.

Usikimbie Mohamed, tupo hapa kuusaidia umma kukuelewa wewe na lengo lako kwa amani na usatwi wa taifa hili.
 
Hao wanaaminishwa na kujazwa ujinga kuwa nyerere ni "mtakatifu" kwa utakatifu asiokuwa nao. Laiti ikionekana historia ya Uhuru ilianzia na kuishia kwa nyerere basi kazi yao ya kuutafuta muujiza wa utakatifu itakuwa imekamilika. Mohamed Said pekee kaisambaratisha hiyo dhanna na kwa hilo usitegemee wagala kuithamini hii jitihada ya Mohamed Said kuweka wazi ukweli. Hawana zaidi ya kuja na kumpinga yeye binafsi na si maandiko yake, sijaona mahali wameweka andiko la Mohamed Said na kusema hili sio sahihi, usahihi ni huu hapa.

Amewaumiza nyoyo na fikra zao vibaya sana kwa kuuonesha ulimwengu kuwa nyerere hakuwa muasisi wa TANU wala muasisi wa Uhuru wa Tanganyika.

Kuna mfuasi mmoja wa nyerere, anaitwa Mag3,

Anasema hao wazee wote walikuwa wasaidizi wa Nyerere.

Nguruvi3, yeye hataki kabisa kusikia majina ya hao wazee anawaita kina mwanameka.
 
Last edited by a moderator:
Mohamed Said Popo mstahafu mwenzangu wa bandari ila anakula kwa ulaini pesa anazolipwa na Ally Sykes[mzulu] ili uiandike na kuitukuza familia yake. kelele tu kila kukicha za kuonewa je mpaka sasa umefanya nini kurekebisha hii hali au utaishia kupiga keleel tu? hao mabwana zako akina Sykes mapesa waliyonayo kuna shule au taasisi yoyote wameanzisha kusaidia hao waislamu wenu wanaodhulumiwa?
 
Mohamed Said,
Baada hoja kuwaishia kinachofanyika sasa ni kukutolea kauli za matusi na kejeli ili ujitoe kwenye munakasha.

Kiukweli wewe ni mvumilivu sana ili nakupa pongezi sana kuvumilia matusi.

Endelea kutoa darsa wala hakuna wa kukufukuza kwa maneno.
Mkuu unaposema watu wameishiwa hoja basi jaribu kuonyesha ni wapi na wapi. Hoja nyingi zimetolewa hapa lakini ni Mohamed Said ndiyo ameshindwa kutoa majibu ya hoja hizo. Utakuwa na upungufu mkubwa sana kama hilo hulioni. Cha msingi ni na nyinyi mjaribu kumsisitizia mzee wetu atoe majibu ya hoja maana wengine akili zetu siyo za kushikiwa...hatuwezi kuamini tu kwa kuambiwa tuamini kama wewe na wenzako mnavyofanya. Kuwa mkweli bhana...
 
Back
Top Bottom