Mzee Mohamed,
Inawezekanaje RAIS WA KWANZA wa TANU asiwe MUASISI wake. Au kuasisi kuna maana gani? Sisi wengine twatoka bara tusaidie.
Vipi TANU iliundwa inabidi urudi nyuma miaka 25 hadi 1929 pale ilipoasisiwa African Association.
Usiishie hapo uje hadi 1933 ilipoasisiwa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika mwaka 1933.
Vyama hivi viwili viongozi wake walikuwa wamoja.
Nadhani umeona kuwa safari ya Nyerere ya UNO mwaka 1954 aliyekuwa anakusanya fedha
alikuwa Idd Faiz Mafongo ambae alikuwa mweka hazina wa Al Jamiatul na mweka hazina wa TANU
kwa wakati mmoja.
Hii inataka maelezo kwa nini ilikuwa hivi.
Ukitaka mfano hai ni kama vile mweka hazina wa Parokia ndiyo mweka hazina wa TANU.
Jambo kama hili haliji bila sababu.
Sasa kuhusu kuasisiwa kwa TANU azma ilikuwapo miaka mingi toka Vita Kuu Vya Pili na Abdu ndiyo
akishawishi wenzake kuunda chama cha siasa.
Mwaka wa 1950 akiwa katibu aliunda TAA Political Sub Committee.
Hili nimelizungumza sana katika mnakasha huu.
Hiki kilikuwa moja ya kituo katika safari ya kuunda TANU.
Nyerere hayumo katika hiyo kamati.
Mpango wa Abdu ilikuwa kumleta Chief Kidaha Makwaia katika TAA kisha kuunda TANU.
Chief Kidaha hakutaka kujiunga na TAA kwa sababu ambazo ziko wazi.
Mwaka 1952 Nyerere akapelekwa kwa Abdu na Kasella Bantu akiwa na barua kutoka kwa
Hamza Mwapachu ambayo ilieleza sifa za Nyerere.
Kama alivyotoa ile rai ya uongozi kwa Chief Kidaha, Abdu aliitoa ile rai kwa Nyerere.
Nyerere aliafiki na hivyo akawa rais wa TAA mwaka 1953.
Mwaka wa 1954 TANU ikaundwa.
Katika kitabu changu nimesema maneno haya:
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="width: 601"]
...it was during this time that Abdulwahid, for the second time, advised Nyerere to resign from teaching so as to concentrate fully on the work of the Association.
This idea did not appeal to Nyerere, just as it had not appealed to Chief Kidaha Makwaia four years earlier.
But Nyerere had gone a step further than Chief Kidaha. He had at least accepted leadership of TAA.
Nyerere was also aware that TAA was being sustained by patriots who did not number more than four and that he would live on their charity, whatever their good intentions.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"]
What drove the TAA inner circle to insist on Nyerere's assuming TAA's leadership on full-time basis was first, that the Association was then operating more or less as a political party and the governor was aware of it; secondly, the plan was in operation to register as a political party before the end of the year.
TAA was busy working on the draft of the constitution for the new party and plans were under way for the president of the proposed political party to travel to the United Nations to appear before the Trusteeship Council as Japhet Kirilo had done two years before.
It was important that there should be a full-time president when the new party was founded.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Yapo mambo mengi aliyofanya Abdu Sykes na mengi yakihitaji uwezo mkubwa sana wa fedha
kukamilisha.
Naacha wazi akili ya msomaji aamue mwenyewe katika hali kama hii vipi Nyerere aweze kuunda
TANU kwenye mji kama wa Dar es Salaam ile ya 1950.