Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Hivi umemesoma vizuri kituko alichokuuliza? Ungesema tu ndiyo au hapana...

Hapa chini ni bandiko la Mohamed Said

Au ulikuwa una maana ya muasisi wa 'wa jina TANU' kama alivyosema kituko?

Tulizana tatizo unapapara.
 
Wanaukumbi, John Rupia, Said Chamwenyewe, Oscar Kambona, Paul Bomani, Ali Tambwe Mwinyi, Mchango wao TANU ni upi.

Spike Lee:

John Rupia yeye alikuwa mfadhili toka AA hadi TANU.

Rupia alikuwa mmoja wa wanakamati ya TAA Political Sub Committee 1950 pamoja
na Sheikh Hassan bin Amir, Abdu Sykes, Hamza Mwapachu, Said Chaurembo,
Steven Mhando na Dk Vadasto Kyaruzi.

Hii kamati ndiyo iliyokuwa intengeneza mipango ya kuunda TANU.

Mwanasheria wa kamati hii alikuwa Earle Seaton. Huyu Earle Seaton alikuwa rafiki wa
Abdu Sykes na ni yeye aliyemleta katika TAA kuja kuwawekea baadhi ya mambo ya sheria
sawa.

Said Chamwenyewe yeye alikuwa mmoja wa wazee katika TAA na Kamati ya Udhamini ilipokuja
kutembelea Tanganyika mwaka 1948 Mzee Chamwenyewe ndiye aliyetoa maoni ya Watanganyika
kwa niaba ya TAA.

TANU ilipokataliwa kusajiliwa na serikali Abdu Sykes alimtuma Mzee Chamwenyewe kwenda Rufiji
kutoa kadi kwa Warufiji kuwaingiza TANU.

Chamwenyewe alikuwa anakwenda na baiskeli kuanzia Dar es Salaam hadi Rufiji akiingiza watu TANU

Oscar Kambona alikuja Dar es Salaam kujiunga na TANU 1955.
kila kijiji alichopita.

Paul Bomani alikuwa kiongozi wa TAA Lake Province soma habari zake hapa chini kama nilivyoandika
katika kitabu changu:

''From 26 th September, 1953, for almost a month, the committee toured and addressed public meetings, collecting funds in Dodoma, Mwanza, Bukoba, Ukerewe, Tarime, Musoma and Shinyanga.

The president of TAA, Lake Province, Paul Bomani received the three-man TAA committee (Abbas Sykes, Saadan Abdu Kandoro and Japhet Kirilo) and addressed meetings with them in the province.

Bomani told TAA members and all Africans in Mwanza of the importance of contributing generously to the cause.'' [1]


[1] Report ya Lake Province Kwa Kifupi Iliyotolewa na Bwana Abbas K. Sykes, Sykes' Papers. Also see Japhet, op. cit. p.62.


Hii kamati ya TAA ilikuwa ikipita katika majimbo kuwaeleza watu dhulma za Waingereza katika kesi ya ardhi ya Wameru na kuwaeleza kuwa wakati unakaribia wa kuunda TANU.

Ali Mwinyi Tambwe aliingizwa TANU na Zuberi Mtemvu August 1955. Mwaka huo huo Ali Mwinyi, Rajab Diwani na Julius Nyerere walikwenda Lindi kuvunja kuimarisha chama na kufuta propaganda ya Kanisa Katoliki lilikuwa linatisha watu wasijiunge na TANU. Mmoja wa watu waliokuwa wanaipiga vita TANU alikuwa Yustino Mponda, Liwali wa Newala.
 
Naunga mkono

Nyaraka hizo hapo chini zinatosha au niongeze nyingine?

Annual Report of the Secretary of Tanganyika African Association, 7 January, 1951. Sykes' Papers.

R.M. Kawawa, ‘Comments on Dr Mwanjisi Speaks to TAGSA’, 28 th December, 1951. Sykes' Paper's

Do
ctor Mwanjisi Speaks to TAGSA’ 22 nd December, 1951. Sykes' Papers

The Secretariat Ref. 38515/265 8 th February, 1952. Sykes' Papers.


Sykes to TAGSA Honorary Secretary, to The Honourable Chief Secretary to the Government; Ref. No.1/52/3 10 th January, 1952. Sykes' Papers.


Julius K. Nyerere, President Tanganyika African Association to Governor Edward Twining, 10 th August, 1953. Sykes’ Papers.
 
Nyara hizo hapo chini zinatosha au niongeze nyingine?

R.M. Kawawa, Comments on Dr Mwanjisi Speaks to TAGSA, 28 th December, 1951. Sykes' Paper's

Do
ctor Mwanjisi Speaks to TAGSA 22 nd December, 1951. Sykes' Papers

The Secretariat Ref. 38515/265 8 th February, 1952. Sykes' Papers.


Sykes to TAGSA Honorary Secretary, to The Honourable Chief Secretary to the Government; Ref. No.1/52/3 10 th January, 1952. Sykes' Papers.

Mkubwa Ahsante sana.
 
Mkubwa Ahsante sana.

Ahsante,

Spike hutaki kusikia Ugomvi wa Nyaraka?

TANU wanadai wapewe nyaraka na wenye chama chao wanasema
nyaraka hizi mali yetu zisingekuwa zetu zingefikaje katika majumba yetu.

Ikawa matatizo tayari.
Hapa ndiyo umeanza ule msuguano wa nani kaasisi TANU.

Sisi hapa JF tuandeleza tu vita iliyopiganwa nusu karne iliyopita.

Ndiyo maaana Abdu na mdogo wake Ally wakajikuta wamefutwa katika
historia ya TANU pamoja na baba yao.

Kwa kweli historia ya TANU ina mikasa.

Iliposhindakana kupatikana Nyaraka hizi ndiyo sasa ikaja mpango wa
''kusanya piga moto.''

Kwa kweli mimi sipati tabu ninapoona jamaa zangu hawaamini wanaita ''porojo.''
Kwa hakika vitu kama hivyo vikihadithiwa utavipa jina gani?

Tatizo ni kuwa mikasa hiyo ni ya kweli kwa hiyo haiwezi kuwa ''porojo.''
 
Mkubwa Mohamed Said, napenda kufahamu mengi kuhusu historia ya nchi yetu, nimeshtuka kidogo kuhusu hicho kisa cha kuchoma nyaraka za TANU. Ukipata wasaa tujuze kaka.
 
Vipi TANU iliundwa inabidi urudi nyuma miaka 25 hadi 1929 pale ilipoasisiwa African Association.
Usiishie hapo uje hadi 1933 ilipoasisiwa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika mwaka 1933.

Vyama hivi viwili viongozi wake walikuwa wamoja.

Nadhani umeona kuwa safari ya Nyerere ya UNO mwaka 1954 aliyekuwa anakusanya fedha
alikuwa Idd Faiz Mafongo ambae alikuwa mweka hazina wa Al Jamiatul na mweka hazina wa TANU
kwa wakati mmoja.

Hii inataka maelezo kwa nini ilikuwa hivi.

Ukitaka mfano hai ni kama vile mweka hazina wa Parokia ndiyo mweka hazina wa TANU.
Jambo kama hili haliji bila sababu.

Sasa kuhusu kuasisiwa kwa TANU azma ilikuwapo miaka mingi toka Vita Kuu Vya Pili na Abdu ndiyo
akishawishi wenzake kuunda chama cha siasa.

Mwaka wa 1950 akiwa katibu aliunda TAA Political Sub Committee.
Hili nimelizungumza sana katika mnakasha huu.

Hiki kilikuwa moja ya kituo katika safari ya kuunda TANU.
Nyerere hayumo katika hiyo kamati.

Mpango wa Abdu ilikuwa kumleta Chief Kidaha Makwaia katika TAA kisha kuunda TANU.
Chief Kidaha hakutaka kujiunga na TAA kwa sababu ambazo ziko wazi.

Mwaka 1952 Nyerere akapelekwa kwa Abdu na Kasella Bantu akiwa na barua kutoka kwa
Hamza Mwapachu ambayo ilieleza sifa za Nyerere.

Kama alivyotoa ile rai ya uongozi kwa Chief Kidaha, Abdu aliitoa ile rai kwa Nyerere.
Nyerere aliafiki na hivyo akawa rais wa TAA mwaka 1953.

Mwaka wa 1954 TANU ikaundwa.

Katika kitabu changu nimesema maneno haya:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] ...it was during this time that Abdulwahid, for the second time, advised Nyerere to resign from teaching so as to concentrate fully on the work of the Association.

This idea did not appeal to Nyerere, just as it had not appealed to Chief Kidaha Makwaia four years earlier.

But Nyerere had gone a step further than Chief Kidaha. He had at least accepted leadership of TAA.

Nyerere was also aware that TAA was being sustained by patriots who did not number more than four and that he would live on their charity, whatever their good intentions.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] What drove the TAA inner circle to insist on Nyerere's assuming TAA's leadership on full-time basis was first, that the Association was then operating more or less as a political party and the governor was aware of it; secondly, the plan was in operation to register as a political party before the end of the year.

TAA was busy working on the draft of the constitution for the new party and plans were under way for the president of the proposed political party to travel to the United Nations to appear before the Trusteeship Council as Japhet Kirilo had done two years before.

It was important that there should be a full-time president when the new party was founded.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Yapo mambo mengi aliyofanya Abdu Sykes na mengi yakihitaji uwezo mkubwa sana wa fedha
kukamilisha.

Naacha wazi akili ya msomaji aamue mwenyewe katika hali kama hii vipi Nyerere aweze kuunda
TANU kwenye mji kama wa Dar es Salaam ile ya 1950.

Seuse nyerere mwenyewe kakiri kuwa wakati huo alikuwa hata Kiswahili hakijui vizuri.
 
Nimetoa tafsiri ya mwasisi hapo juu hebu isome mkuu

Soma upate hekima kijana, wewe unaweza kuijuwa maana ya muasisi ("mwasisi" si sahihi) na kujidai kuitolea tafsiri kuliko tunaofundishwa kiarabu (madrasah) kabla hatujajuwa hata kuongea sawa sawa? Unanchekesha - courtesy FaizaFoxy.

Msome Mohamed Said kaamuwa kumwaga vitu ambavyo si wewe tu, bali hata waliokufundisha somo la historia hawavijui.
 
Bwana Mohamed Said.

Simulizi za maisha binafsi ya wazee wako na harakati za ukombozi wa Tanganyika, zinaweza kuwa sahihi kabisa. Kama “unatusoma” between lines. Utaona kwamba hatupingi kuwepo kwa hao wazee wako, au ushiriki wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Hata kama ukiandika “Sykes alikula mapapai matatu”, au “Salum Abdalah alikuwa anakula Nsasa na matoborwa”, kama ulivyosimuliwa, sisi hatukupingi.

Mengi ya tunayopinga yapo katika “premises” ambazo zimejengwa katika hisia. Ni katika hisia hizo, ndipo ULIPOLAZIMISHA kuwepo kwa uadui kati ya Nyerere na Wakristo kwa upande mmoja, na waislam kwa upande mwingine. Umetumia maneno, “ inasemekana Mwalimu alikuwa hapendi hiki au kile”, , “it is said that church lobby did this or that”
Na mara nyingine umekuwa uki-cook conclusions zako ukizifanya kama vile facts, wakati hazina msingi wowote wa tafiti za kisayansi,. Kwa mfano unasema: “the truth is that Muslims were not better off than they were 30 years before” Wakati hauoneshi tafiti zozote zinazo support hiyo “truth” yako.

Na wakati mwingine, umekuwa kama mtabiri, ambaye unaamini kuwa unayajua mawazo ya watu. Mara nyingi hapa umeonesha kama vile ulikuwa unajua mambo ambayo Nyerere alikuwa anawaza. Nafikiri hii ni hulka yako, ndio maana hata hapa jamvini, mara kadhaa unafikiri unajua tunachowaza, mara “ooh, wamestushwa”, mara “ ooh, walikuwa hawajawahi kumsikia huyu na yule” Kwa ujumla haya ndio tunapingana nayo. Premises za namna hii ndizo ulizotumia kupandikiza chuki katika jamii. Chuki hii iko very personal. Ya kwako dhidi ya Nyerere na wakristo (Chanzo cha chuki tunakijua). Lakini ukaona uitumie kupatia pesa kwenye mihadhara, na safari za kimataifa, huku ukishawishi waislam wote wamchukie Nyerere na wakristo. Na hapo hatukubani na wewe.

Sasa tukikubana kwenye hizo “angles” unasema “ ooh mimi nasimulia habari za wazee wangu”, “ na nyie andikeni kitabu” “ sijibu maswali yasiyo na tija” “Mwalimu shaffi alinifundisha nisibizane na wajinga”
Halafu wewe mwenyewe unashangaa kwamba kwa miaka kumi na tano baada ya kutoa kitabu chako, serikali na kanisa hawajakujibu … kwani wao ndio wanalazimishwa “kujibizana na wajinga”???
 
Last edited by a moderator:
Bwana Mohamed Said.

Simulizi za maisha binafsi ya wazee wako na harakati za ukombozi wa Tanganyika, zinaweza kuwa sahihi kabisa. Kama "unatusoma" between lines. Utaona kwamba hatupingi kuwepo kwa hao wazee wako, au ushiriki wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Hata kama ukiandika "Sykes alikula mapapai matatu", au "Salum Abdalah alikuwa anakula Nsasa na matoborwa", kama ulivyosimuliwa, sisi hatukupingi.

Mengi ya tunayopinga yapo katika "premises" ambazo zimejengwa katika hisia. Ni katika hisia hizo, ndipo ULIPOLAZIMISHA kuwepo kwa uadui kati ya Nyerere na Wakristo kwa upande mmoja, na waislam kwa upande mwingine. Umetumia maneno, " inasemekana Mwalimu alikuwa hapendi hiki au kile", , "it is said that church lobby did this or that"
Na mara nyingine umekuwa uki-cook conclusions zako ukizifanya kama vile facts, wakati hazina msingi wowote wa tafiti za kisayansi,. Kwa mfano unasema: "the truth is that Muslims were not better off than they were 30 years before" Wakati hauoneshi tafiti zozote zinazo support hiyo "truth" yako.

Na wakati mwingine, umekuwa kama mtabiri, ambaye unaamini kuwa unayajua mawazo ya watu. Mara nyingi hapa umeonesha kama vile ulikuwa unajua mambo ambayo Nyerere alikuwa anawaza. Nafikiri hii ni hulka yako, ndio maana hata hapa jamvini, mara kadhaa unafikiri unajua tunachowaza, mara "ooh, wamestushwa", mara " ooh, walikuwa hawajawahi kumsikia huyu na yule" Kwa ujumla haya ndio tunapingana nayo. Premises za namna hii ndizo ulizotumia kupandikiza chuki katika jamii. Chuki hii iko very personal. Ya kwako dhidi ya Nyerere na wakristo (Chanzo cha chuki tunakijua). Lakini ukaona uitumie kupatia pesa kwenye mihadhara, na safari za kimataifa, huku ukishawishi waislam wote wamchukie Nyerere na wakristo. Na hapo hatukubani na wewe.

Sasa tukikubana kwenye hizo "angles" unasema " ooh mimi nasimulia habari za wazee wangu", " na nyie andikeni kitabu" " sijibu maswali yasiyo na tija" "Mwalimu shaffi alinifundisha nisibizane na wajinga"
Halafu wewe mwenyewe unashangaa kwamba kwa miaka kumi na tano baada ya kutoa kitabu chako, serikali na kanisa hawajakujibu … kwani wao ndio wanalazimishwa "kujibizana na wajinga"???

Nanren,

Ndugu yangu hata wewe huna sababu ya kujibizana na mjinga.
Hiki kitabu ni cha miaka mingi sasa.

Kisikushughulishe.
 
nanren,

ndugu yangu hata wewe huna sababu ya kujibizana na mjinga.
Hiki kitabu ni cha miaka mingi sasa.

Kisikushughulishe.

umemjibu vema sana,japo wao wanakuja kwa jazba na kejeli ili wakutoe kwenye mstari ila nakupongeza sana kwa jins unavojituliza na kuwajuza wajinga mambo wasiyoyajua,,
stil hatujaona criticisms zenye tija kutoka kwao.
 
Nikiikumbuka Tanzania nakumbuka ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI WA CCM. Na wakti huo Mwenyekiti ni CCM ni Nyerere. Kwa kufikiri kidogo tu utaona huyu alikuwa Mungu mtu yaani zidiume fikra zake zote hata zikiwa za kuangamiza Taifa lake.Kweli enzi za Nyerere tulijifunza na kuona mengi
Mkuu baadae sijuhi walishtuka nini walikukuja rekebisha kidogo msemo huo ukuwa "ZIDUMU FIKIRA SAHII ZA MWENYEKITI WA CCM" wakaongezea neno sahihi!!! Mtu uwezi kuamini kama tulikuwa tunaishi in real au virtual WORLD wakati huo!
 
nimetoa tafsiri ya mwasisi hapo juu hebu isome mkuu

ile hotuba uliyotuahid ya kwamba utakwenda tbc kuifuatilia vipi mbona muda unazid kutaradadi??
Pia swali letu mbona nalo hulijibu yericko? Linalouliza "wewe una uhusiano gani wa moja kwa moja na julius kambarage nyerere?tujibu basi yericko nyerere..!
 
Mkubwa Mohamed Said, napenda kufahamu mengi kuhusu historia ya nchi yetu, nimeshtuka kidogo kuhusu hicho kisa cha kuchoma nyaraka za TANU. Ukipata wasaa tujuze kaka.

Spike,

Insha Allah.

Unashangaa hilo.

Mbona na sisi tuna ''Watergate'' yetu?

Lakini ikawa hola.
Nyaraka zimehamishwa.

Jamaa hawakupata kitu.

Hivi hujiulizi imekuwaje Abdu Sykes na
mdogo wale Ally waje kupewa medali
baada ya nusu karne ilahali wao ndiyo
vinara wa kuasisi TANU?

Hilo halikushangazi?

Inner circle ya mipango ya TANU ni
Abdu, Ali, Dossa, Rupia na Nyerere.

Hao wa wajumbe mikoani waliitwa kuja kukamilisha
ratiba.

Na hiyo katiba wala hawakuandika walinakili katiba ya
Convention Peoples Party (CPP) ya Nkrumah.

Mahali pa CPP wakaweka TANU.
Itafute katiba ya CPP halafu iangalie na ile ya TANU 1954.

Earle Seaton hawamtaji lakini huyu ndiye aliyekuwa akimpa
mipango Abdu Sykes vipi aendeshe mambo ya sheria katika
TAA kuwapiga kitanzi Waingereza.

Hii ilikuwa toka 1950 Seaton alimtia sana moto Abdu aende
Marekani akasome.

Kuna kitu cha ajabu hapa kwa Seaton.
Insha Allah tutafute muda nitakuwekea.

Seaton akiogopa kusema habari za Abdu hadharani.


[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Nilichogundua wengi hawajui maana ya Mwasisi/kuasisi has hasa katika dhana ya vyama vya siasa!

Katika dhana ya siasa, "kuasisi" ni kuongoza kwa mara ya kwanza kundi lenye malengo fulani

Hivyo kiongozi wa awali huitwa mwasisi na waambata wake pia huitwa waasisi wa cha chama hicho, lakini katika uso wa wengi, ni kiongozi tu ndie huonekana zaidi!

Ikiwa ni kampuni au NGOs basi mwasisi wake huwa ni mmoja tu!
Si kweli!
Waswahili tukisema muasisi au katika lafidhi nyingine mwasisi tunamaanisha kuwa ni; mtu mwenye kuliwekea msingi jambo(i.e mwanzilishi).

Mfano, kama wewe utajenga msingi wa nyumba halafu ikatokea sababu yoyote ile na kuiacha halafu baadaye mimi nikaja kuijenga ile nyumba kutokea pale wewe ulipouacha msingi, basi wewe utakuwa ni MWASISI wa ile nyumba na mimi ninakuwa ni MJENZI (au mjengaji) wa nyumba ile.

Tumeona maneno ya nyerere katika kuwaaga wazee wa Dar ,hotuba inatufahamisha waziwazi kuwa NYERERE SI MUASISI WA TANU.

Umefeli tena unapotuambia katika "dhana ya kisiasa"! lau kama ungekuwa ukijua maana ya neno dhana basi usingejaribu hata "kutafsiri"


*Umeitoa wapi tafsiri ya neno Muasisi uliyotuletea hapa jamvini?
 
umemjibu vema sana,japo wao wanakuja kwa jazba na kejeli ili wakutoe kwenye mstari ila nakupongeza sana kwa jins unavojituliza na kuwajuza wajinga mambo wasiyoyajua,,
stil hatujaona criticisms zenye tija kutoka kwao.

Kaka mimi ni mtu mzima.

Na kama wasemavyo Waswahili.
Utu uzima dawa.

Mimi azma yangu ni kueleza kila kitu nikijuacho
kuhusu wazee wangu walivyopigania uhuru wa
Tanganyika.

Hii ni fursa adhim sana.
Siwezi kuipata kirahisi kama hivi.

Namshukuru sana Yericko kwa kufungua zile nyuzi mbili.
Ile ya Maaskofu na hii yangu ya Mchochezi.

Mwisho wa mnakasha nataka Insha Allah niwe nimewaelimisha
wanajamvi.
 
Una uhakika sio NECTA?
Sina lakini najua kama wamejiwekea asilimia zakupitisha hakuna shida.
Tuseme wanapitisha 10% ya watahiniwa wote wa ki-Islamu, hivyo dawa ni kuongeza idadi ya wahitimu. Hii ina maana kuwa 10% ileile lakini idadi ya wahitimu ni wengi.
 
Nyaraka hizo hapo chini zinatosha au niongeze nyingine?

Annual Report of the Secretary of Tanganyika African Association, 7 January, 1951. Sykes' Papers.

R.M. Kawawa, ‘Comments on Dr Mwanjisi Speaks to TAGSA’, 28 th December, 1951. Sykes' Paper's

Do
ctor Mwanjisi Speaks to TAGSA’ 22 nd December, 1951. Sykes' Papers

The Secretariat Ref. 38515/265 8 th February, 1952. Sykes' Papers.


Sykes to TAGSA Honorary Secretary, to The Honourable Chief Secretary to the Government; Ref. No.1/52/3 10 th January, 1952. Sykes' Papers.


Julius K. Nyerere, President Tanganyika African Association to Governor Edward Twining, 10 th August, 1953. Sykes’ Papers.

Hapa ndio mzee Said unapokuwa huwatendei haki wasomaji wako; umetuwekea vichwa vya habari tu. Why don't you scan these documents and make them public for anyone to see?
 
Back
Top Bottom