Bwana
Mohamed Said.
Simulizi za maisha binafsi ya wazee wako na harakati za ukombozi wa Tanganyika, zinaweza kuwa sahihi kabisa. Kama "
unatusoma" between lines. Utaona kwamba hatupingi kuwepo kwa hao wazee wako, au ushiriki wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Hata kama ukiandika "Sykes alikula mapapai matatu", au "Salum Abdalah alikuwa anakula
Nsasa na
matoborwa", kama ulivyosimuliwa, sisi hatukupingi.
Mengi ya tunayopinga yapo katika "premises" ambazo zimejengwa katika hisia. Ni katika hisia hizo, ndipo
ULIPOLAZIMISHA kuwepo kwa uadui kati ya Nyerere na Wakristo kwa upande mmoja, na waislam kwa upande mwingine. Umetumia maneno, " inasemekana Mwalimu alikuwa hapendi hiki au kile", , "
it is said that church lobby did this or that"
Na mara nyingine umekuwa uki-
cook conclusions zako ukizifanya kama vile
facts, wakati hazina msingi wowote wa tafiti za kisayansi,. Kwa mfano unasema: "
the truth is that Muslims were not better off than they were 30 years before" Wakati hauoneshi tafiti zozote zinazo
support hiyo "
truth" yako.
Na wakati mwingine, umekuwa kama mtabiri, ambaye unaamini kuwa unayajua mawazo ya watu. Mara nyingi hapa umeonesha kama vile ulikuwa unajua mambo ambayo Nyerere alikuwa anawaza. Nafikiri hii ni hulka yako, ndio maana hata hapa jamvini, mara kadhaa unafikiri unajua tunachowaza, mara "ooh, wamestushwa", mara " ooh, walikuwa hawajawahi kumsikia huyu na yule" Kwa ujumla haya ndio tunapingana nayo. Premises za namna hii ndizo ulizotumia kupandikiza chuki katika jamii. Chuki hii iko
very personal. Ya kwako dhidi ya Nyerere na wakristo (Chanzo cha chuki tunakijua). Lakini ukaona uitumie kupatia pesa kwenye mihadhara, na safari za kimataifa, huku ukishawishi waislam wote wamchukie Nyerere na wakristo. Na hapo hatukubani na wewe.
Sasa tukikubana kwenye hizo "
angles" unasema " ooh mimi nasimulia habari za wazee wangu", " na nyie andikeni kitabu" " sijibu maswali yasiyo na tija" "Mwalimu shaffi alinifundisha nisibizane na wajinga"
Halafu wewe mwenyewe unashangaa kwamba kwa miaka kumi na tano baada ya kutoa kitabu chako, serikali na kanisa hawajakujibu … kwani wao ndio wanalazimishwa "kujibizana na wajinga"???