Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Hakuna sababu ya kukebehi wala kukejeli dini ya mtu yeyote ili kufanya hoja za mtu ziwe na nguvu. Hoja za Mohammed Said zinajibika kwa hoja zenye nguvu zaidi na tumeweza kuonesha hilo tayari mara kadhaa. Sasa kama mtu huwezi kujibu au kuuliza maswali huna sababu ya kushambulia imani ya watu wengine au kuita watu wengine majina.

Bw. Said kwa muda mrefu alikuwa anategemea kupata uwanja huru ambapo wasikilizaji wake wengi walikuwa hawana nafasi ya kumuuliza maswali na kama walimuuliza maswali yalikuwa ni kutoka katika kutofahamu - hawakuwa na cha kusimamia. Hivyo akisema "Nyerere alikuja Dar kwa mara ya kwanza mwaka 1952" hakuna mtu wa kumuuliza na wanashangaa kwa tabasamu; akisema "Nyerere alificha historia ya viongozi wa Kiislamu" wasikilizaji wanashangaa kwani anarusha rusha majina ya watu maarufu; maskini wa Mungu hawajui kuwa walikuwepo Wakristu miongoni mwao... anacheka anaendelea na habari nyingine ambapo wasikilizaji wake wanaonekana kushangazwa na wengine kujaa na hamaki!!

Sasa kaja kwenye home of the Great thinkers; hapendwi mtu, haogopwi mtu - hoja hujibiwa kwa hoja na siyo vioja.. anatoa madai ambayo sehemu nyingine yangewashtua watu hapa watu hawashtuki anaulizwa maswali! Anatoa madai anaulizwa ushahidi anakimbia na kukwepa kiufundi (with technicality). Sasa amefika mahali anadai ati yeye hataki kushawishi watu waamini - unabaki kujiuliza sasa kwanini unaandika kama hutaki watu waamini! - hajibu.

Histohisia yake imeoneshhwa kuwa haina msingi wowote katika historia; zaidi ya masimulizi ya watu kupambana na kuelezana na tena masimulizi ya watu waliuoumizwa hisia zao. Nyerere aliwasema hawa vizuri tu mwaka 1966 kwamba wengine walipigania uhuru wakiamini kuwa baada ya uhuru watapewa vyeo au nafasi fulani; walipokosa nafasi hizo ndio wakamgeuka Nyerere. Wakarudi na udini ule ule waliokuwa nao miaka karibu kumi nyuma, udini ambao Bw. Mohammed Said mwenyewe ametusimulia - japo hakutaka kwenda kuuliza kwanini!
 
Huyo ndie Shehe Mohamed Said, tukimkosoa kwa uchochezi wake anasema kuwa twamtetea Nyerere kwasababu ni mkristu wenzetu,
 
Mohamed Said, Mzee Mwanakijiji, THE BIG SHOW, Pasco, Nguruvi3, Jasusi, Fundi Mchundo,

..Wamisionari wa Maryknoll nao wanadai kwamba walikuwa wakimuunga mkono Nyerere ktk harakati za kudai uhuru.

..jamani kuna mambo mengi sana yamejificha ktk historia ya harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

..kuna umuhimu wa kuweka mambo yote haya in the open bila kuingiza ukakasi wa udini.




source: Maryknoll Africa - History: Buffaloes - Politics


 
Last edited by a moderator:

JK,

Ikiwa Maryknoll waliunga mkono harakati za kudai uhuru wa Tanganyika sawa hakuna mtu wa kupinga hilo.

Hakuna mwenye haki ya kukataa hilo.

Mie kwa kutambua hilo la yaliyojificha ndipo nikaandika kitabu.

WR Duggan na JR
Civille wameandika kitabu ''Tanzania and Nyerere,'' Maryknoll New York, Orbis Book, 1976. Atakae na asome hicho kitabu wala mimi sina haja ya kusema mengi.

Kitabu hiki kimo katika bibliografia yangu.
Nimekisoma chote.

Kitabu hiki kipo Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Huo mchango wa Maryknoll unaozungumzwa hapa ukumbini umo humo.
Atakae ende akausome humo.

Lakini anaetaka kujua khasa waliochangia narudia tena waliochangia uhuru wa Tanganyika watake wasitake lazima wasome kitabu changu.

Wala si suala la udini.
Haiwezekani kutaja mchango wa Mufti Sheikh Hassan bin Amir ukaacha kutaja wanatarika wa Qaudiriyya.

Huu ndiyo ukweli wenyewe hata kama unauma.


 
Huyo ndie Shehe Mohamed Said, tukimkosoa kwa uchochezi wake anasema kuwa twamtetea Nyerere kwasababu ni mkristu wenzetu,

Yericko kauli hiyo si yangu.
Huenda umechanganya.

Mimi kuna maneno huwa sisemi kwa kuwa siyo katika fikra wala msamiati
niliyozoea.
 

Lakini Maryknoll ni Shirika la Kanisa Katoliki; Na umeandika kuwa Kanisa lilikuwa halikuwa mstari wa mbele kupinga ukoloni. Unapoelezea safari ya Nyerere UN unaweka mkazo kuwa ni wazee wako waliochangia sana - japo hujaweza kuonesha wazi ni kiasi jumla kilichangwa kwa safari hiyo kulinganisha na kiwango kilichochangwa na wengine (wakiwemo hawa MM).

Ndio maana wengine tunakuambia hujaandika historia. Umeficha na kufuta vitu vingine vyote ambavyo vingefanya simulizi lako lisinoge.

Itabidi unapoandika toleo jipya uweke masahihisho ya simulizi lako kuzingatia ukweli huu ambao unajulikana sasa. Utawatendea haki wasomaji wako.

Na unaposema "waliochangia khasa" una maana gani? maana kuna wengine hawakuchangia 'khasa' au mchango wao ni negligible?
 

MM,

Hunifahamu.

Haiba yangu si ya kutisha.
Hata kama ningelitaka niogofye watu nisingelifanikiwa.

Allah hakunijalia haiba hiyo.
Hilo la kupendwa...

Ngoja nikudokolee kuhusu hilo la kupendwa.

Mama yangu ananikhadithia anasema nilipokuwa mdogo
akinichukua kwenye shughuli akifika tu uani kila mwanamke
anataka kunibeba...

Wananigombania ''Huyu mume wangu mie huyu mume wangu mie...''
Wamanyema wake kwa waume tuna maumbile tofauti sana na makabila
mengine...

Vipi utampenda mtu usiyemwona.
Kwa hiyo hayo yote mawili mie hayanienei.

Hayo mengine uliyosema wala sina haja ya kuyajibu.
Sioni kama ukumbi utapata manufaa achilia mbali kuburudika.
 

MM,

Una haraka sana.
Mara nirekebishe kitabu kwa safari moja iliyochangiwa na Maryknoll?

Hilo tu basi?

Kwa tiketi moja kanisa lishakuwa mstari wa mbele?

Sasa kanisa likishakuwa hapo mbele hebu nijibu Sheikh Hassan bin Amir,
Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Mohamed Yusuf Badi na hawa wanatariqa
Quadiriyya tuwasogeze upande upi?

Umeshajiuliza Maryknoll walichangia safari ipi na ya mwaka gani
na nguvu ya TANU ilikuwaje?

Hiyo nguvu ilikuwa inatoka wapi?

Baada ya kuchangia hiyo safari msaada wao mwingine ni upi?
Msaada kwa TANU au msaada kwa Nyerere?

Hivi unajua ni kiasi gani cha fedha walichotoa wale wachangiaji
wanaojuliokana na TANU walikuwa wakikifadhili chama toka enzi
za TAA 1950...Dossa, Abdu, Ally, Rupia kisha Mshume Kiyate,
Mwinjuma Mwinyikambi, Mohamed Jumbe Tambaza na wengine wengi.

Hivi unajua Abdu Sykes mara moja katika maisha yake aliwahi kufilisika
kwa ajili ya TANU?

Dossa kafa masikini kwa ajili ya TANU?

Hiyo tiketi moja ya Maryknoll imekuwa kisa cha kipofu na tembo.

Nadhani ushajua nini maana ya ''khasa.''
Ukienda katika kamusi ya Kiswahili ya TUKI utapata ''hasa.''

Watu wa pwani hatutamki hivyo hiyo ni lafidh ya watu wa bara.
Sie tunatia ''khe" ni ngumu kutamka kwa asiyezoea.
 
Dah hongereni sana Wakuu wote kwa kudumisha mnakasha..........

Huwezi linganisha gogovivu discussion style na JF discussion style........hapa ukileta maneno watu hawakuachii ipite hivi hivi.........haangaliwi mtu usoni......
 

Unanikimbiza kwa maneno yasiyopendeza ''huu ujinga,'' ''comedy'' ''mwanameka.''
Mimi si mjinga hata wasonipenda watanitetea kwa hilo.

Hutaki kusikia jina la Zena bint Farijallah.
Huyu ni ''sweetheart'' wangu bibi (nyanya) yangu.

Kawaona wote na kasikia yote.

Ondoa hamaki rejesha adabu na staha.
Jitulize.

Endapo unataka tufanye mjadala wa maana.
Ikiwa umezoea kutupiana maneno na wengine.

Siyo mimi.

Narudia toa ghadhabu tuliza fikra zako na Insha Allah nitakujibu yote ulouliza.
Makuzi yangu hayakuwa sawa hata na vijana wengine wa Dar es Salaam.

Niliishi kati ya ''who's who'' in Dar.

Nimewajua watu kama Peter Colmore, Jim Bailey katika umri mdogo sana.
Hawa ni Wazungu.

Ushawasikia?

Nimeingia katika sehemu ambazo wengi wa umri wangu walikuwa wanazisikia tu.
Nashukuru.

Ndiyo maana nikawa mjanja.

Mimi nikukimbie wewe kwa kipi ulichokuwanacho?
 
Sawa, jibu hoja sasa sisi wengine tupo kimya tunafuatilia darsa kwa umakini
 
Umekosea nani kakwambia mie najificha na dini yangu.
Mie najulikana kote kwa hilo.

Hii ni sifa kwangu si jambo mie nikaona aibu.
Siku nyingine kabla ya kutoa uamuzi niulize kwanza.
 
MM,

Una haraka sana.
Mara nirekebishe kitabu kwa safari moja iliyochangiwa na Maryknoll?

Hilo tu basi?

Unaona sasa! kwako hilo ni dogo na halihitaji kutajwa kwenye kitabu chako. Lakini kwa mtu anayetaka kuandika historia hilo pia ni jambo la muhimu kwani mwanahistoria yuko interested na historical facts. This one sir is a historical fact and deserve a mention - hata kama ni kwa kupita tu. Ukifanya hivyo siyo kwamba unaonesha kanisa kwa mwanga mzuri au wakristu kwa mwanga mzuri la hasha; unaitendea historia haki.

Kwa tiketi moja kanisa lishakuwa mstari wa mbele?

Unaona sasa; hakuna aliyesema kanisa limekuwa 'mstari wa mbele'. Tunachosema na kumbe tayari ulikuwa unakijua kanisa na watumishi wa kanisa (mapadre wakiwemo) walikuwa interested kuona Tanganyika inakuwa huru vile vile na wao pia hawakusita kutoa michango yao na kama waliitoa kwenye parokia zao basi inaweza kutajwa ni michango ya wakristu vile vile.


Sasa kanisa likishakuwa hapo mbele hebu nijibu Sheikh Hassan bin Amir,
Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Mohamed Yusuf Badi na hawa wanatariqa
Quadiriyya tuwasogeze upande upi?

Hili ni tatizo jingine mkubwa wangu; unafikiri tunasema hivi dhidi ya wazee wetu hawa. La hasha! Tutakuwa si waungana kabisa na siyo wa kweli wa historia. Kama umetusoma vizuri utaona kuwa hakuna hata mmoja wetu mmoja kati ya wanaopinga simulizi lako ambaye amesema jambo baya la kebehi au la kuwashusha wazee wetu hawa, mashujaa na waasisi wa taifa letu. Hutasikia kwa mfano miye nikisema jambo baya kwa Sheikh Amir, Tambaza, Mshume Kayeta n.k Siwezi kufanya hivyo kwani mchango wao kwenye historia yetu haufutiki.

Hivyo, tunapokosoa histohisia yako tunafanya hivyo siyo dhidi ya wazee wetu Waislamu walioshiriki katika kupigana uhuru chini ya uongozi wa baba wa taifa Mwalimu Nyerere. Huo ni ukweli wa historia hatuwezi kuukana. Usisome hoja zetu kwa macho ya "sisi dhidi ya wao"; kwamba wanaokuhoji basi wanataka wazee Waislamu wasitambuliwe mchango wao.

Umeshajiuliza Maryknoll walichangia safari ipi na ya mwaka gani
na nguvu ya TANU ilikuwaje?

Mbona hilo limeandikwa mara nyingi tu na bahati nzuri ninayo hotuba nzima ya Nyerere pale UN na ukisoma hata utangulizi wake ilisemwa wazi kuwa fedha za kumpeleka Nyerere UN zilichangwa kutoka vyanzo mbalimbali. Imeandikwa hivi; "The fare and other expenses were collected from Party Members in the capital" (Freedom and Unity pp.35). Hii ilikuwa kwenye kikao cha March 7, 1955. Na hata kwenye mkutano wake UN wa Disemba 20, 1956 bado MM walitoa mchango vile vile na waliendelea kumpatia misaada mbalimbali.

Hiyo nguvu ilikuwa inatoka wapi?
Baada ya kuchangia hiyo safari msaada wao mwingine ni upi?
Msaada kwa TANU au msaada kwa Nyerere?

sasa hili indilo jukumu lako kama mwandishi wa historia; ulitakiwa kutafuta jibu linaweza kusaidia kwenye hoja yako.


Lakini wapo kati ya hawa kwa maelezo yako mwenyewe walikuwa wanamsaidia Nyerere moja kwa moja na si TANU tu; je siyo kwamba wengine walimsaidia Nyerere wakijua kwa kufanya hivyo wanaisaidia TANU?
 
Bila shaka sasa unapata picha ya ushiriki wa kanisa katika kisa nilichokieleza pale juu kuhusu kanisa na Uhuru wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…