Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mohamed Said mzee wangu, hebu jaribu kuwa mstaarabu hata kama huna, jibu maswali yaliyoletwa kwako na Yericko Nyerere. Acha kutafuta pa kutokea kwa kuomba msaada kwa watu kama zomba au Ritz, ambao umaarufu wao humu unakuja kwa sababu za uchochezi tu, hakuna lingine. Mimi niko interested sana na swali kwamba Somalia na sehemu nyingine duniani ambako majority ni waislamu, je, matatizo yao chanzoni Nyerere? Jibu hilo pamoja hoja zoote za Yericko Nyerere ili angalau tujue kuwa hukuandika kwa sababu za kidini wala hukutumwa na Mzulu (Ally Sykes). Ufahamu kuwa watu wanafuatilia sana uzi huu, wengine hatukulala tukitegemea muda wowote utatoa jibu au majibu. Sasa huu ni muda wa kazi maliza mada hii kwa kutoa jibu, maana wengine twaendesha vyombovya moto na bado twachunguliachungulia humu kuona jibu lako. Usifikiri wote humu jamvini ni wastaafu, wengine tuna miaka 30 mbele kabla ya kustaafu na LAZIMA utufanyie favour. Jibu angalau hilo swali moja tu kwanza, ili tufahamu kuwa wewe ni mdini ama laa, na kama ni mdini naachana na hii thread kabisa. Je, Nyerere ni chanzo cha matatizo ya waislamu wote hapa duniani? Maana koote ambako waislamu ni wengi ni matatizo makubwa na hilo lipo wazi kabisa, Nyerere alimwaga sumu?
 
Unajijua kuwa wewe ni mjuvi?

Unatuthibitishiaje kuwa watu wote wanakusoma wewe tu?

Hivi wachangiaji wote hawanamaana kwa watazamaji hao 22,000 isipokuwa wewe tu


Punguza munkar na hasira ili uipe nafasi hewa iweze kufikiri kwa umakini sana na kutoa lugha za busara katika kuendeleza mnakasha huu kama alivyobainisha Mohamed Said.

Hakika kuna mengi sana tulioishi huko enzi za Nyerere tumejifunza na kuyakumbuka. Tunamshukuru sana Mohamed Said kwa darsa hili ambalo mimi binafsi nimeprint pg zote kwa faida yangu na vizazi vyangu kujionea Tanzania ikoje....

Pole sana YR
 
Mzee Mohamed,
Inawezekanaje RAIS WA KWANZA wa TANU asiwe MUASISI wake. Au kuasisi kuna maana gani? Sisi wengine twatoka bara tusaidie.
 
Mkuu Pasco naunga mkono wazo lako niko tayari kuchangia,uandaliwe utaratibu wa haraka sana kuacha haya mambo ya kijinga yaendelee bila kufanyiwa kazi itakuwa ni dhambi kubwa kwa kizazi kijacho.
Siku zote kitabu cha kitaaluma (academic book) kinaandikwa kutokana na mwandishi / waandishi wake wanafanya utafiti na sio tu kukusanya habari kama unavyosema na kuziweka katika kitabu kisha ukaita cha kitaaluma. ndio maana kila wakti unasikia Mohamed Said anaitwa katika makongamano mbalimbali ya kitaaluma kutetea kitabu/ maandiko yake kwa kutoa mihadhara.

Nakushauri na wewe mjipanga kwayo kwani kinyume mtaotea na kuitwa kitabu cha hekaya za Abunuwasi.

Fanyeni au fikireni kitaalamu zaid na punguzeni jazba ili kuongeza busara katika maamuzi yenu
 
Waislam wenye mtazamo chanya kama nyinyi mmejificha wapi? Mbona sauti zenu zimefunikwa na akina Mohamed Said, Ustaadh Ilunga, Shehe Ponda na wengine kama hao?
 

Hakika maneno adhimu kabisa haya. Wengi wamejawa na jazba na hasira kiasi cha kupoteza uvumilivu na busara katika majadiliano. Lakin siku zote ukweli ni ukweli tu hakuna jinsi.

Tuombe Mola busara itawale wache jazba tuzidi pata darsa.
 
Yericko Nyerere.

Mmi ushauri wangu kwako kama unataka kuanza kufanya utafiti hu utakuwmwongozo mzuri sana kwako kuanzia utafiti wako. Unaweza anzia kwa mama Nyerere kisha wengine ili kuisafisha au kuichafua zaidi historia ya JKN
 

Nakushauri tu saizi tupo post ya 124 usikurupuke kuandika anza kusoma kuanzia post ya kwanza utajifunza vitu vingi sana. Ulikuwa unajua kuwa Nyerere siyo muasisi wa TANU.
 
Mohamed Said, nauliza jengo la ofisi za African Association, miaka ya 1930 wakati wa Gavana Sir Donald Cameron, lilikuwa wapi?
 
Last edited by a moderator:

Unaweza kukurupuka bila kufanya utafiti mzuri ukatoa kitabu kikawa kama Novel ya Shigongo.
 

Sina murkali ndugu yangu, nimemsihi tu ndugu Mohamed Said apunguze ujuvi!

Kama umeweza kutoa nakala ngumu hilo jambo la heri sana, hicho ndicho tulikuwa tunakitaka!
 
Mohamed Said, nauliza jengo la ofisi za African Association, miaka ya 1930 wakati wa Gavana Sir Donald Cameron, lilikuwa wapi?

Jengo la AA lilikuwa hapohapo Lumumba/Kariakoo Street zamani New Street.

Hilo jengo la ghorofa lilikuja kujengwa baadae lakini kabla ya uhuru wakati
Dossa akiwa Mweka Hazina na msaidizi wake Abbas Sykes.

Katika majengo hayo yote hakuna kumbukumbu yoyote ya waasisi wa AA wala TANU.
 
Nakushauri tu saizi tupo post ya 124 usikurupuke kuandika anza kusoma kuanzia post ya kwanza utajifunza vitu vingi sana. Ulikuwa unajua kuwa Nyerere siyo muasisi wa TANU.

Mkuu Rtz, usituangushe bwana, inakuwaje Nyerere sio mwasisi wa TANU na wakati huohuo anaKuwa ni raisi wa kwanza wa TANU?
, naona kuna mambo mawili unayoyachanganya hapa, kuna kuasisi Chama na kuna kutumia jina la TANU,
Nyerere alikuwa ni raisi wa TAA kabla ya TANU na walipoamua kuibadilisha TAA na kuunda chama kingine Nyerere alikuwa ni miongoni mwa hicho chama,,,,

Tulishajadili hili kwenye mnakasha ule wa Mag3, kwamba majina yalikuwa mengi yaliyoletwa kama pendekezo, lakini mwisho wa siku jina la TANU ndilo lilipita na Nyerere anelezea wazi kabisa kuwa jina hilo ni pendekezo la kina Syskes, sipati picha unaposema Nyerere sio Mwasisi wa TANU, au una Maaana sio mwasisi wa JINA TANU?
 
Wanaukumbi, John Rupia, Said Chamwenyewe, Oscar Kambona, Paul Bomani, Ali Tambwe Mwinyi, Mchango wao TANU ni upi.
 
Yericko Nyerere.

Mmi ushauri wangu kwako kama unataka kuanza kufanya utafiti hu utakuwmwongozo mzuri sana kwako kuanzia utafiti wako. Unaweza anzia kwa mama Nyerere kisha wengine ili kuisafisha au kuichafua zaidi historia ya JKN

Si mimi tu bali wewe na Mohamed twaweza kushiriki vema katika haya!
 
Kweli chizi anaona wenzio ndio machizi....... we ulieleta mada hii Ni mdini wa kwanza manake hoja zako ziegemea upande fulani.... kama sio jibu basi takwimu alizo toa wimbilambele...... Halafu uachane kabisa na hizi mambo manake wengine tunakuheshimu sana
 
Mzee Mohamed,
Inawezekanaje RAIS WA KWANZA wa TANU asiwe MUASISI wake. Au kuasisi kuna maana gani? Sisi wengine twatoka bara tusaidie.

Vipi TANU iliundwa inabidi urudi nyuma miaka 25 hadi 1929 pale ilipoasisiwa African Association.
Usiishie hapo uje hadi 1933 ilipoasisiwa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika mwaka 1933.

Vyama hivi viwili viongozi wake walikuwa wamoja.

Nadhani umeona kuwa safari ya Nyerere ya UNO mwaka 1954 aliyekuwa anakusanya fedha
alikuwa Idd Faiz Mafongo ambae alikuwa mweka hazina wa Al Jamiatul na mweka hazina wa TANU
kwa wakati mmoja.

Hii inataka maelezo kwa nini ilikuwa hivi.

Ukitaka mfano hai ni kama vile mweka hazina wa Parokia ndiyo mweka hazina wa TANU.
Jambo kama hili haliji bila sababu.

Sasa kuhusu kuasisiwa kwa TANU azma ilikuwapo miaka mingi toka Vita Kuu Vya Pili na Abdu ndiyo
akishawishi wenzake kuunda chama cha siasa.

Mwaka wa 1950 akiwa katibu aliunda TAA Political Sub Committee.
Hili nimelizungumza sana katika mnakasha huu.

Hiki kilikuwa moja ya kituo katika safari ya kuunda TANU.
Nyerere hayumo katika hiyo kamati.

Mpango wa Abdu ilikuwa kumleta Chief Kidaha Makwaia katika TAA kisha kuunda TANU.
Chief Kidaha hakutaka kujiunga na TAA kwa sababu ambazo ziko wazi.

Mwaka 1952 Nyerere akapelekwa kwa Abdu na Kasella Bantu akiwa na barua kutoka kwa
Hamza Mwapachu ambayo ilieleza sifa za Nyerere.

Kama alivyotoa ile rai ya uongozi kwa Chief Kidaha, Abdu aliitoa ile rai kwa Nyerere.
Nyerere aliafiki na hivyo akawa rais wa TAA mwaka 1953.

Mwaka wa 1954 TANU ikaundwa.

Katika kitabu changu nimesema maneno haya:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="width: 601"] ...it was during this time that Abdulwahid, for the second time, advised Nyerere to resign from teaching so as to concentrate fully on the work of the Association.

This idea did not appeal to Nyerere, just as it had not appealed to Chief Kidaha Makwaia four years earlier.

But Nyerere had gone a step further than Chief Kidaha. He had at least accepted leadership of TAA.

Nyerere was also aware that TAA was being sustained by patriots who did not number more than four and that he would live on their charity, whatever their good intentions.

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] What drove the TAA inner circle to insist on Nyerere's assuming TAA's leadership on full-time basis was first, that the Association was then operating more or less as a political party and the governor was aware of it; secondly, the plan was in operation to register as a political party before the end of the year.

TAA was busy working on the draft of the constitution for the new party and plans were under way for the president of the proposed political party to travel to the United Nations to appear before the Trusteeship Council as Japhet Kirilo had done two years before.

It was important that there should be a full-time president when the new party was founded.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Yapo mambo mengi aliyofanya Abdu Sykes na mengi yakihitaji uwezo mkubwa sana wa fedha
kukamilisha.

Naacha wazi akili ya msomaji aamue mwenyewe katika hali kama hii vipi Nyerere aweze kuunda
TANU kwenye mji kama wa Dar es Salaam ile ya 1950.
 
[QUOTEL=Yericko Nyerere;5557757]Si mimi tu bali wewe na Mohamed twaweza kushiriki vema katika haya![/QUOTE]

FUTA KWANZA NENO NGANO KATIKA MATAMKO YAKO,,,
KAMA UNATAMBUA UMUHIM WAKE NA UNAHITAJI MCHANGO WAKE USINGEANZA KUBEZA KWANZA,
LILE SWALI LILILOHOJI YA KWAMBA UNA UHUSIANO GANI NA NYERERE BADO HUJAJIBU YERICKO NDUGU YANGU,
TUNAOMBA JIBU.
 
Nilichogundua wengi hawajui maana ya Mwasisi/kuasisi has hasa katika dhana ya vyama vya siasa!

Katika dhana ya siasa, "kuasisi" ni kuongoza kwa mara ya kwanza kundi lenye malengo fulani

Hivyo kiongozi wa awali huitwa mwasisi na waambata wake pia huitwa waasisi wa cha chama hicho, lakini katika uso wa wengi, ni kiongozi tu ndie huonekana zaidi!

Ikiwa ni kampuni au NGOs basi mwasisi wake huwa ni mmoja tu!
 
Mohamed Said,

Mimi bado nipo kwa huyu mzee Idd Faiz mweka hazina wa TANU mwaka 1959.

Kama sikosei Katibu Mkuu alikuwa Oscar Kambona na Makamu wa rais wa TANU John Rupia.

Inakuaje huyu mweka hazina watu wamemtupa hata kupewa heshima yeyote.
Kwani Oscar Kambona alipewa heshima gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…