THE BIG SHOW
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 16,950
- 13,527
kweli chizi anaona wenzio ndio machizi....... We ulieleta mada hii ni mdini wa kwanza manake hoja zako ziegemea upande fulani.... Kama sio jibu basi takwimu alizo toa wimbilambele...... halafu uachane kabisa na hizi mambo manake wengine tunakuheshimu sana
[QUOTEL=Yericko Nyerere;5557757]Si mimi tu bali wewe na Mohamed twaweza kushiriki vema katika haya!
Kituko,Mkuu Rtz, usituangushe bwana, inakuwaje Nyerere sio mwasisi wa TANU na wakati huohuo anaKuwa ni raisi wa kwanza wa TANU?
, naona kuna mambo mawili unayoyachanganya hapa, kuna kuasisi Chama na kuna kutumia jina la TANU,
Nyerere alikuwa ni raisi wa TAA kabla ya TANU na walipoamua kuibadilisha TAA na kuunda chama kingine Nyerere alikuwa ni miongoni mwa hicho chama,,,,
Tulishajadili hili kwenye mnakasha ule wa Mag3, kwamba majina yalikuwa mengi yaliyoletwa kama pendekezo, lakini mwisho wa siku jina la TANU ndilo lilipita na Nyerere anelezea wazi kabisa kuwa jina hilo ni pendekezo la kina Syskes, sipati picha unaposema Nyerere sio Mwasisi wa TANU, au una Maaana sio mwasisi wa JINA TANU?
Hapo humsaidii chochote huyo mzee wenu hasidi na mchochezi, unazidi kumfanya aonekane kituko na husuda zake!Maswali yako hayana tija. Nilifikiri unaleta hoja kuwa hiki ulichoandika siyo sahihi na sahihi ni hiki hapa. Wewe utamjuwa Abdul Wahid kuliko MS? Usitake kuleta viroja.
Nilichogundua wengi hawajui maana ya Mwasisi/kuasisi has hasa katika dhana ya vyama vya siasa!
Katika dhana ya siasa, "kuasisi" ni kuongoza kwa mara ya kwanza kundi lenye malengo fulani
Hivyo kiongozi wa awali huitwa mwasisi na waambata wake pia huitwa waasisi wa cha chama hicho, lakini katika uso wa wengi, ni kiongozi tu ndie huonekana zaidi!
Ikiwa ni kampuni au NGOs basi mwasisi wake huwa ni mmoja tu!
Unafadhaishwa na unachokiita matusi, lakini madhara ya uchochezi wako hayo huyaoni? amakweli huna aibu mzee muovu wewe!Adolay,
Huu ndugu yangu ni mjadala tu tunabadilishana mawazo hapana haja
ya kunitukana.
Mimi naandika na wanangu wanasoma michango yangu na majibu
yenu.
Mimi ni mtu mzima sasa yanapokuja matusi huwa wanangu wanafadhaika
na mimi pia.
Ondoa ghadhabu huu ni mjadala tu tushindanishe hoja tukiwa hatukubaliani
basi tunasonga mbele na nukta nyingine.
Huu ndiyo ustaarabu.
Huu ndiyo uungwana.
Loo! mpiga debe anakelele kuliko mwenye chombo!Wewe umekuja kwa papara ukala za uso unatafuta pakutokea huna. Hivi ulifikiri nyerere ndio muasisi wa TANU?
FUTA KWANZA NENO NGANO KATIKA MATAMKO YAKO,,,
KAMA UNATAMBUA UMUHIM WAKE NA UNAHITAJI MCHANGO WAKE USINGEANZA KUBEZA KWANZA,
LILE SWALI LILILOHOJI YA KWAMBA UNA UHUSIANO GANI NA NYERERE BADO HUJAJIBU YERICKO NDUGU YANGU,
TUNAOMBA JIBU.
Kwani Oscar Kambona alipewa heshima gani?
Kumbe hayo ndiyo yanayokufanya umchukie Nyerere!Rashid Heri Baghdelleh.
Angalia ''spelling'' yako unakosea.
Baghdelleh alikuwa rafiki ya baba yangu akija hata nyumbani kwetu.
Mara ya mwisho kaja nyumbani baba hayupo akaacha salamu.
Ndiyo mara yangu ya mwisho kumtia machoni akiwa hai.
Illipigwa simu nyumbani kumuarifu baba yangu kuwa Rashid Heri Baghdelleh
amepata ajali ya gari Arusha na kufariki.
Kwa nini nasema haya hapa ukumbini ni kutaka kuwajuvya kuwa watu hawa
mimi kwa hakika ni wazee wangu.
Tuendelee...
Mwaka 1964 Baghdelleh alikuwa ndiyo Mkuu wa Mkoa Tabora.
Huo ndiyo mwaka babu yangu kafungwa jela Uyui kwa ''kutaka kupindua serikali.''
Baba yangu anamuuliza Baghdelleh ''Vipi Rashid ni kweli mzee alikuwa na mipango
na wanajeshi kuangusha serikali?''
Baghdelleh anatingisha kichwa anamwambia baba, ''Sikiza Said mzee atatoka hakuna
kitu kama hicho wewe nakuomba vuta subra tu...''
Lakini uongo huu ulienezwa sana na baadhi ya watu waliuamini hadi leo.
Ndiyo babu yangu sasa baada ya kutoka kifungoni akawa anawaita baadhi ya watu ''waongo.''
Waongo kwa kuwa walimsingizia alikuwa anaandaa jeshi kupindua serikali ya Nyerere wakati
haikuwa kweli.
Alhamdulilah najua mengi sana katika historia ya nchi hii.
Hapo humsaidii chochote huyo mzee wenu hasidi na mchochezi, unazidi kumfanya aonekane kituko na husuda zake!
Hivi umemesoma vizuri kituko alichokuuliza? Ungesema tu ndiyo au hapana...Kituko,
Haya maneno ya Nyerere "Baada ya miezi 13, hapo 1954 tukaanzisha TANU. Jina hili lilipendekwezwa na kina Abbul Sykes. Walikuwa wamefikiria tangu zamani, walipokuwa askari Vitani huko Burma (Vita vya pili)"
Mwaka 1945 mkesho wa Krismas Abdulwahid na James Mkande, mdogo wake Ally pamoja na askari wengine walifafanya makubaliano ya kuunda chama hapo wametoka Chitangong wakielekea Imphal, Burma.
Kwa ufupi mimi nayajua hayo kama kuna mwingine anajau chochote basi tuzidi kujifunza.
Hapa chini ni bandiko la Mohamed Said
Au ulikuwa una maana ya muasisi wa 'wa jina TANU' kama alivyosema kituko?TAA was busy working on the draft of the constitution for the new party and plans were under way for the president of the proposed political party to travel to the United Nations to appear before the Trusteeship Council as Japhet Kirilo had done two years before.
It was important that there should be a full-time president when the new party was founded.
Kituko,
Haya maneno ya Nyerere "Baada ya miezi 13, hapo 1954 tukaanzisha TANU. Jina hili lilipendekwezwa na kina Abbul Sykes. Walikuwa wamefikiria tangu zamani, walipokuwa askari Vitani huko Burma (Vita vya pili)"
Mwaka 1945 mkesho wa Krismas Abdulwahid na James Mkande, mdogo wake Ally pamoja na askari wengine walifafanya makubaliano ya kuunda chama hapo wametoka Chitangong wakielekea Imphal, Burma.
Kwa ufupi mimi nayajua hayo kama kuna mwingine anajau chochote basi tuzidi kujifunza.
Hii itasidiaje kufuta uovu na uzandiki wa mzee wenu Mohamedi Saidi dhidi ya vijana wa kiislam?Unaweza kututajia wanachama 20 wa mwanzo wa TANU. Unamjua Clement Mtamila alikuwa nani kwenye TANU.
LAHAULAA..!
HIVI UMEKIONA ULICHOKIANDIKA?
YAN KWAMBA KUASISI NI KUONGOZA KWA MARA YA KWANZA KUNDI LENYE MALENGO FULANI?NI KWELI?
MFANO WATU WAPO KWENYE MCHAKATO WA KUANZISHA NGOs FLANI,KISHA BAADA YA KUKAMILISHA KILA KITU MWISHONI IKATOKEA WAKAMPATA MTU AMBAE WAO WANAONA NI ANAFAA KUWA MWAKILISHI AMA MSEMAJI WAO KWA NIABA YAO,NDIO UNATAKA KUTUAMINISHA YA KWAMBA HUYO MKARIBISHWA MWISHONI, ETI KWA KUWA TU NDIYE ALIKUWA KIONGOZI WA KWANZA WA NGOs HIYO BASI HUSTAHIKI KUITWA MUASISI MKUU?
CHUTAMA YERICKO..
Kaka, Nyerere mwenyewe anakiri kuwa jina la TANU walikuwa wamelifikiria tangu zamani, wewe unatuambia yalikuwa majina mengi mezani wakachagua TANU. Unaweza kukutajia hayo majina mengine ambayo yalikuwa mezani tuyafahamu. Chama cha kina Nyerere TAWA kilikuwa cha wanafunzi peke yao.Kaka Ritz,
Hakuna anayekataa hilo hata Nyerere naye alikuwa na Chama chake pale Makerere kabla ya kukivunja na kuwa tawi la TAA
mimi ninachopinga ni kwa wewe kusema Nyerere hakuwa mwasisi wa TANU, sio wote waasisi wa CCM ndio waliobuni hilo jina, jina lilibuniwa na wachache lakini waasissi wa chama ni wengi, same na TANU, Nyerere, Rupia, Syskes na wengine walikuwa waasisisi wa TANU na ndio maana kadi ya Nyerere ni namba moja kwa kuthibitisha hilo, Nyerere ni mwasisi wa TANU lakini si mwasisi wa hilo jina, majina yalikuwa mengi mezani na yalibuniwa na watu mbalimbali lakini jina lililopita ni hilo la TANU
Naihurumia jamii ambayo imelishwa hizi ngano za Mohamed Said kwa muda wa miaka 15 na yenyewe ikapokea hizo ngano kama zilivyo. Huyu mtu hana nukuu yoyote iwe ya John Sivalon, Andulwahid Sykes wala hiyo listi ndeeefu ya anaowaita wazee wake. Anayotetea yeye ni mawazo yake aliyokaa akayatunga kwa malengo maalum hasa pale alipowasoma aliowakusudia na kutambua mapema kuwa watayapokea mazima mazima bila hata kujiuliza.
Nina wasi wasi na hizo anazozitaja kama nyaraka za Abdulwahid Sykes kama zipo na anazinukuu kama zilivyo, watu wa aina yake ndivyo walivyo, wachochezi. Nikitoa mfano ameombwa alete nukuu ya kitabu cha Sivalon kama kilivyo kuthibitisha maneno anayodai kuyasoma humo lakini kashindwa...kama kawaida ya mbea amebakia kujiuma. Kama tusingepata hiyo hotuba ya Nyerere ambayo imemuumbua mchana kweupee, bado angekazania tu uongo wake kuwa Mwalimu hakuwataja wazee wake.
Kuhusu nyaraka za hao wazee wa Mohamed Said ambazo anadai anazo, hata siku moja hajawahi kuzitoa popote pale, ziko tu kichwani kwake na hakuna mtu amewahi kumdai sauti wala video kuzithibitisha. Uwezekano mkubwa upo kuwa aliziandika yeye mwenyewe na kwa njia aliyotaka. Yeye leo pamoja na kutolewa hotuba ya Mwalimu kwa Wazee wake bado anadai uthibitisho wa sauti na ikiwezekana video. Sasa na mimi leo namwomba na yeye atuletee hapa sauti za wazee wake wakisema na kutenda anayodai Mohamed Said.
Sasa maajabu ya hawa wazee wa Mohamed Said! Sisi tukiongelea wazee wetu Watanganyika wa sehemu zote kusini hadi kaskazini, magharibi hadi mashariki, yeye amekazania wazee wake wa Gerezani Dar es Salaam (ukanda), tukiwataja wazee wetu Watanganyika wa makabila yote makubwa kwa madogo, yeye amekazania wazee wake Manyema na Wazulu (ukabila) na tukiwaenzi wazee wetu Watanganyika wa dini zote pamoja na wasio na dini, yeye amekazania wazee wake wa Kiislaam (udini).
Mwisho nina ombi kwa jukwaa (hii ni JF)...imeonekana kitabu/vitabu alivyoandika Mohamed Said havina ukweli na kama upo ni asilimia kidogo sana, sasa tusiishie hapa...tuende next step...wapotoshaji kama yeye adhabu yao ipo. Their works have to be discredited as academic dishonesty...a deliberate attempt to falsify, fabricate data, records, or information. Taasisi, Waandishi na wachapishaji wote aliowawekea maneno mdomoni kwa nukuu zisizo sahihi, juhudi zifanyike wajulishwe hatua ziweze kuchukuliwa. Nawapa changamoto wana JF.
unachokosa ni hapo kwenye ubinafsi/uboramimi unaposema mkaribishwa!
Mwalimu hakuwa mkaribishwa, kijana funguka!
Hatuwezi shindana nao kwa midomo, vita yetu iko shuleni watakaohitimu hawatawasikiliza tena na Jua lao hao linaelekea kuzama.Waislam wenye mtazamo chanya kama nyinyi mmejificha wapi? Mbona sauti zenu zimefunikwa na akina Mohamed Said, Ustaadh Ilunga, Shehe Ponda na wengine kama hao?
Nimetoa tafsiri ya mwasisi hapo juu hebu isome mkuukama ni kwa hoja zile ulizozitoa,nadhan utakubaliana na ndugu moh said ya kwamba julius hakuwa mwasisi,unakubali au unakataa??
Once again,yericko nyerere,una uhusiano gani wa moja kwa moja na julius,babu yako,mjomba wako,mzee wako kiukoo ama uhusiano wako nayeye ukoje??