Nimekuwa nikitamani sana kujua nini maana ya Mfumo Kristo, na kama ni kitu halisi lakini kwa bahati mbaya sijawahi kupata jibu zuri. Yupo mwanaJF anayeitwa Mkandara, aliwahi kuniambia kuwa ni mfumo uliotumiwa na serikali za kikoloni, kutawala kwa kupendelea ukristo na kubagua wasio wakristo. Bw Mkandara alionyesha wasiwasi kuwa bado chembechembe za mfumo kristo hadi sasa, japo hakuweza kutoa mifano. Niliwahi tena kuendesha mjadala kwenye thread moja humu na mwanaJF anayeitwa Ami (sina uhakika kama nimekumbuka jina vizuri), ambae nae alionyesha hisia za uwepo wa mabaki ya mfumo kristo, lakini hakuweza kunipa mifano stahiki.
Binafsi niko very interested kujua kama mfumo kristo ni kitu kinacho exist hadi leo, au leo tunashuhudia tu makovu yake? Interest yangu kwa kiasi fulani inatokana na kwamba mimi ni mwalimu katika mojawapo wa taasisi za juu za elimu Tz, na huwa najiuliza kwa nini hadi sasa (miaka 50 baada ya kuondoka wakoloni) bado ratio ya waislamu darasani ni ndogo sana ukilinganisha na wakristu? Mzee
Mohamed Said, nimejaribu kusoma maandiko yako mengi humu JF, kwa bahati mbaya sijawahi kusoma maandiko yake mengine. Katika hayo niliyosoma sijapata kuona
sharp evidences za uwepo wa mfumo kristo hadi leo, na namna unavyoathiri maendeleo ya waislamu kielimu.
Nimefanya observation ndogo kwenye matokeo ya form four mwaka jana, nikajaribu kulinganisha ufaulu katika shule za serikali katika wilaya ya Morogoro vijijini (ambako wengi ni waislamu) na za wilaya ya Moshi vijijini (ambako wengi ni wakristo). Siwezi nikasema kuwa tofauti niliyoiona inatokana moja kwa moja na dini zao. Nilifikiria yapo mambo kama mazingira ya kufanyia kazi na kadhalika. Swala ambalo naomba Mzee Mohamed unisaidie, je ni kwa vipi serikali inaweza kufanya, bila upendeleo au bila kuwakandamiza wakristo, kuhakikisha ufaulu katika maeneo na shule zenye waislamu wengi sio tofauti na maeneo na shule zenye wakristo wengi?
Je, ni juhudi zipi ambazo waislamu wanaweza kuzifanya, wao kama wao, kuhakikisha watoto wao wanakuwa na ufaulu zaidi katika mitihani?
Tunaheshimu historia, lakini hatuwezi kuibadilisha, je leo tunaweza kurekebisha vipi yale ambayo yanayoathiriwa sasa na historia, hususan yale ambayo yalibagua kundi fulani la watu, ha hapa tukiongelea zaidi waislamu katika elimu?
Mimi ni mkristo, lakini nimeuliza maswali haya kwa sababu kama nilivyosema awali, ni mwalimu katika taasisi ya elimu ya juu, na siku moja niliwahi kukwaruzana na mwanafunzi wangu ambaye ni muislamu ambapo, japo niliona ni kutokana na utoto wake, lakini sina uhakika kama namna nilivyo handle suala lile ilikuwa sahihi hasa ukizingatia sina uelewa wa kutosha na hiki kinachoitwa mfumo kristo...