Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Kwa bahati mbaya sijauliza 'nyie wIslamu'.
Nimesema ninatatizwa sana na maelezo na mijadala ya 'wao' na 'sisi'.
Nimeanza kwa kusema Mzee Said, nikaendelea kwenye swali langu.
Lakini pia, wewe sio 'waislam' wewe ni Mzee Said ninayekuuliza swali hapa. Na ninataka kujua elimu yako na 'uhanaharakati' wako unawaweka wapi vijana wa Tanzania katika utu uzima na uzee wao.
Sijataka mawazo ya waislamu. Nikitaka nitapiga simu radio Iman au radio kheri.
Nimetaka mawazo yako kama mzee, mtanzania. Sio mwislam wala mwislam wa bara wala wa pwani.
Tafadhali sana.
Kama huwezi kujibu barazani kwasabau yoyoyte ile, nijibu hata kwa PM. Nitasema nimejibiwa, na nitashukuru.
Wala mimi na wewe si lazima tufanye mjadala katika hili.
Wala sina haja ya kukuletea PM.
Wahusika tumewaeleza na tunaamini wametusikia.
Tuishie hapa.