Nguruvi3,
Wewe unaponda maandishi ya Mohamed Said na kuyaita ngano yako kwako sijui tuyaitaje.
Unasema udini ulikuwepo toka kabla ya uhuru sijui umeipata wapi wewe na Nyerere sijui tumuamini nani.
Pitia tena hotuba ya Nyerere anavyowaelezea wazee wa Dar es Salaam wakati wa TANU na harakati za kupigania uhuru.
Nyerere mwenyewe anakiri fadhira za Wazee wa Dar es Salaam kuna kipindi anasema alikuwa Mkiristu peke yake lakini wanamtendea wema wewe leo unasema walikuwa wadini.
Angalia hizo picha wazee walivyokuwa na mahaba na Nyerere.
Ritz, mimi hata siku moja sikuwahi kusema wazee wetu walikuwa wadini. Kinyume chake nimekuwa natetea kuwa hawakuwa wadini ndio maana waliweza kufanya kazi across the board. Nimetolea mifano ya akina Sykes, Mshume, Rupia, Lugazia Kyaruzi, Kawawa, Chaurembo, Yufu Ngozi n.k. na mara zote nimesema wazee wetu tunawashukuru, sio tunawapongeza tu bali tunawashukuru sana!
Aliyeonyesha kuwa kulikuwa na udini ni Mohamed Said. Mohamed anasema miaka 1950 kulikuwa na radical moslems kwa maneno yake, waliotaka kumuondoa Nyerere katika uongozi wa chama kwasababu ya ukristu wake.
Tafadhali sana naomba uelewe ni Mohamed Said siyo maneno yangu.
Mohamed akaeleze kisa cha kuundwa kwa AMNUT na radicals.
Mohamed akasema kuwa bila Abdul Sykes Nyerere asingeweza kufanikiwa kwasababu kwa nyakati hizo mkristo hakukubalika. Hayo si maneno yangu ni ya Mohamed yakishadidia kuwa Mohamed aliona suala la udini kuanzia nyuma.
Hata pale ilipothibitika kuwa Kyaruzi na Mtamila waliwahi kuwa viongozi ndani ya jiji la Dar badio Mohamed ameshikilia kuwa Nyerere asingeweza kufanikiwa. Hii maana yake ni kuwa kulikuwa na udini kwa mtazamo wake
Kwa muktadha huo na ushahidi wa maneno ya Mohamed nasimama kusema kuwa Mohamed anajua udini ulikuwepo kuanzia zama hizo kwahiyo si haki kusema udini uliletwa na Nyerere.
Sijatuhumu wazee wetu, ninachofanya ni analysis ya maneno ya Mohamed na jinsi anavyo skew information.
Matokeo ya spinning ni kuwanyooshea kidole wale anaowatetea.
Mimi nimeandika kuanzia mwaka 2011 katika minakasha kuhusu maneno ya Nyerere alivyokiri.
Hata katika uzi huu nimeandika hayo kama unanisoma vizuri.
Post iliyopita nimesema kuwa Nyerere amekiri katika kitabu chake ''we must run..'' kwa kuwataja wazee.
Mimi ni miongoni mwa watu waliokariri maneno ya Nyerere hata kabla kipande hakijawekwa.
Nimekuwa napinga dhana kuwa Nyerere aliwadharau wazee hawa na nimepinga dhana kuwa wazee walimdharau yeye.
Kwahiyo hapo unafanya spinning ku-discredit maandishi yangu lakini wasomaji wananielewa nasimamia nini.
Narudia, anayejenga dhana ya wazee hawa kuwa wadini ni Mohamed Said Abdallah Salum muyukwa Samtungo.
Siyo Nguruvi3 au Nyerere. Msome Mohamed vizuri.
Ama hili la kuita ngano, hilo ninabaki nalo kwasababu kila mtu ana mtazamo wake kuhusu maandishi ya Mohamed.
Wapo wanaomeza na wapo wanaofikiri. Inategemea mtu yupo upande gani wa mtazamo.
Lakini Ritz, hivi kama si ngano wewe ulijua kuwa shirika la dini la Maknol liliwahi kutoa ticket kwa Nyerere kusafiri kwenda UNO? Mbona hilo halisemwi na Mo? Hivi unajua kanisa lilishiriki vipi kuua EAMWS? unalo jibu wewe! maana Mo hana.
Ritz, Mo anasema Nyerere alikuja Dar 1952 ukweli si huo, je hiyo si ngano?
Ninabaki kusema kuwa Mohamed ameandika ngano hii kwa kutumia majina ya watu, nyakati na matukio ambayo ni ya kweli akiwa na lengo lake lililo nje ya ukweli uliokusudiwa bali aliokusudia ili kujenga mazingira anayotaka.
Kwa mintaarafu hiyo nasoama kitabu chake tofauti na wewe, kama unaona ni maandiko matakatifu hilo ni juu yako.
Mimi naona ngano! Nitty gritty!