Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Aisee hii ni ya zamani sijui hadi nitafute kwenye archives zangu... maana vingine vimeshapotea...

Ukiona mtu anakupiga chenga na anatafuta visababu ujuwe alikumbana na asiyoyatarajia. Kama yanavyomkumba Yericko kwenye hii mada.

Usione haya, iweke tu, ndio ukubwa huo.
 
Mohamed Said, kwa ukumbusho tu, majibu ya hii posti hapa chini bado yanasubiriwa, asante.
 
Mohamed Said, kwa ukumbusho tu, majibu ya hii posti hapa chini bado yanasubiriwa, asante.

Hata hayo huyajuwi? ustake kutuchekesha.

Nilifikiri utakuja kusema Mshume ni jina la kubuniwa hakuwepo, wewe unataka tarehe, sijui nini kwa nini. Mohamed Said anakwambia alipoona kitabu cha kivukoni kimewaacha wazee wake na yeye anajuwa kuwa walipigania Uhuru akaamuwa kuandika historia na jinsi wazee wake walivyopigania uhuru. Sasa wewe kama unaona kuna mapungufu katika maandiko ya Mohamed Said kama alivyoona yeye mapungufu kwenye maandiko ya kivukoni hakuanza kuuliza uliza vitu visivyo na maana, aliingia kazini akaweeka mambo sawa kama ayajuavyo. Na leo hii unamjuwa Mashado Plantan ni nani, Mshume Kiate ni nani, Dossa Aziz ni na nani.

Jee, huoni kuwa utatenda wema na wewe badala ya kuja na kuuliza maswali yasiyo na maana ukaanza kuandika ukijuacho? Mwenzako ana kitabu sasa kina miaka 15 na bado kinauzika, na anaalikwa mialiko mbali mbali duniani kuelezea muono wake. Wewe Jee?

Hapo sasa.
 
Mohamed Said, kwa ukumbusho tu, majibu ya hii posti hapa chini bado yanasubiriwa, asante.
Nilikuwa nina ka pendekezo kadogo. Kutokana na kuwepo kwa hoja nyingi ambazo Mohamed Said ameshindwa kuzijibu na urefu wa uzi huu ambao unaweza kuwafanya watu wengi wanaoanza kuangalia leo kutoziona hoja hizo, tujaribu kuzi compile hoja hizo ambazo hazijapata majibu halafu mkuu wetu Yericko Nyerere afanye utaratibu wa kuzibandika pale juu kwenye post yake. Kama hakuna space anaweza hata akaziweka kwenye word doc halafu akazi-attach kwenye post yake. Hizo hoja zikae pale juu ili ziwe kama zinamsuta huku na sisi tukiendelea kumkumbusha...
 
Mag3 katika bandiko lako 2868 nayaangalia yafutayo na yatokanayo na kitabu, majibu na hoja za Mohamed Said.

1. Alichokiandika Mohamed ni kitu alichokuwa na majibu yake na utafiti ulilenga katika kukamilisha kile alichofikiri na si kile alichotafiti.

a) Ameonyesha bias ya uandishi kwa kuelekeza watu kuamini kile alichokusudia na si kile alichokitafiti
b) Aliandika katika mtazamo wa kushambulia ''attack'' kundi fulani la jamii na watu fulani si kutokana na hukumu ya historia bali kile alichodhani kuwa ima yeye au wazazi au ndugu zake hawakutendewa wema au walionewa.
c) Ameshindwa kuthibitisha maandiko yake kwa hoja za kitafiti,kukwepa maswali au hoja zinazoonekana kukinzana na a, b hapo juu.

Hoja: Endapo Mohamed alifanya utafiti asingeweza kuzama katika historia ya uhuru wa Tanganyika kwa kuzama katika TANU na kukwepa historia iliyoanzia karne nyingi. Mathalani, Mohamed hakueleza undani wa AA au TAA kwa kutambua kuwa hilo litaharibu historia nzima anayoidai, wala kulezea harakati nyingine nje ya Dar, mfano Mbiru na Wapare, vyama vya wafanyakazi n.k.

Mfano, angeandika kwa undani kuhusu AA na TAA ni dhahiri asingekuwa na hoja ya Nyerere kufundishwa siasa mwaka 1952 ili hali twajua kuwa alianza siasa miaka 6 kabla ya hapo tena katika uwakilishi wa jimbo kama Tabora.
Hilo peke yake lingetosha kupunguza nguvu za ziada anazompatia Abdul Sykes.

Ni kwasbabu ya kuonyesha bias, Mohamed amejikuta anaficha ukweli wa historia ya kweli.
Kwa vile lengo ni kushambulia kundi fulani, bwana Said ameacha makusudi mchango wa shirika la Maryknoll huku akiufahamu vema.

Kibaya zaidi ameenda mbali na kuudharau kwa kusema ni 'ticket' moja. Wakati akiudharau mchango huo Mohamed ameutukuza sana mchango wa ticket moja uliofanywa na wazee wake. Hapa ukweli upo wapi katika double standard kama hii.

Ili kukamilisha lengo alilokusudia,Mohamed amewaandika washiriki wa uhuru wasio katika kundi lake kwa dhalili ya hali ya juu. Amewataja kwa imani zao kama viambatanisho vya majina yao na kuacha mchango wao katika mapambano.

Katika hilo la bias, Mohamed ameandika kurusa za kutosha kuhusu Mwapachu kuliko alivyomwandika Mtamila aliyekuwepo kabla ya Mwapachu. Mo amemuelezea Mshume Kiyate kiasi kwamba Rais wa TAA Dr Vedastus Kyaruzi mchango wake hauonekani.

Kila mmoja alikuwa na mchango na si sahihi kuufanya mchango fulani bora kuliko mwingine hasa kwa kuangalia majina na viambatanisho vya imani zao. Hilo linaondoa hata hoja dhaifu iliyokuwepo.

Mohamed ameshindwa kuthibitisha madai yaliyomo ndani ya kitabu chake. Hata pale alipojaribu, MO alikwenda nje ya taratibu za utafiti na kanuni za asili za ''kisheria'' natural justice.

Mathalani, amelituhumu Kanisa kuhusika na mambo mengi maovu na mengi yaliyozuia harakati.
Ameshindwa kuthibitisha ushiriki wa kanisa, kinyume chake kunukuu habari za mtu mwingine ambaye kimsingi angekuwa chanzo cha utafiti wa ushahidi na si yeye kuwa ushahidi(sivalon).

Kwa vile uandishi wake ni katika misingi ya ''attack'' na siyo academic, Mohamed ameshindwa kutetea hoja zake kimantiki.
Mfano, hajaeleza kwanini ilipangwa njama ya kuondoa Nyerere katika uongozi wa TANU mara mbili wakati huo akiwa hana uongozi wa nchi au vyombo vya dola na akiwa chini ya baraza la wazee wa TANU waliokuwa wazee wake.

Moh ameshindwa kutetea hoja ni kwanini ukristo wake ulionekana kikwazo hata kabla ya kuingia madarakani na kwanini majaribio hayo yalipangwa. Pengine hapa alitaka kuficha hisia za udini ambazo ni sehemu ya malalamiko yake ya leo.

Mo ameshindwa kututhibitishia mkakati wa Nyerere kuumaliza Uislam na kuingiza ukristo ulianza lini na kwa mbinu gani.
Kinyume chake ametumia kifo cha EAMWS kumtupia lawama kama sehemu ya ukristo na kanisa.
Ameshindwa kututhibitishia ushiriki wa kanisa kwa ushahidi hivyo kubaki kuamini ndivyo ilikuwa.

Lakini pia ameshindwa kutetea hoja za EAMWS kwanini ilikufa huko kwingine na ni nani alihusika kuiua.
Kwa vile hoja yake haisimami yenyewe, Mo amewashirikisha baadhi ya waislam kama sehemu ya njama.

Iwe iwavyo mtu aliyekuwa na mtazamo tofauti na malengo ya MO huyo alikuwa kibaraka. Alikuwa kibaraka kama Amir Kweyamba aliyekuwa kachero wa serikali, lakini wale waliokula njama dhidi ya serikali walibaki kuwa waislam safi.

Mo ameupotosha umma mara nyingi katika hali ya kujenga hoja na pengine kuficha ukweli.
mfano, si kweli kuwa Nyerere alikuja Dar mwaka 1952, si kweli kuwa alionana kwa mara ya kwanza na Sykes mwaka 1952, si kweli kuwa viongozi wa TAA hawakumjua, si kweli kuwa alianza siasa mwaka 1952, si kweli aliandikiwa hotuba bila kujua alikwenda UNO kusema nini akiwa msomi mkubwa ndani ya TANU.

Ni katika upotoshaji huo, Mohamed ameacha kwa maksudi mchango uliotolewa na wazawa wengine wasio na imani kama yake. Amejikuta akikweza watu kwa majina ili kuficha majina yasiyompendeza.
Mfano, tunauthamini mchango wa Yusuf Ngozi lakini je, Yusuf alikuwa katika nafasi aliyokuwa nayo Dr Vedastus Kyaruz, Clement Mtamila, Stephen Mhando, Cecil Matola, Dunstan Omar na wengine ?

Mifano na hoja ni nyingi sana lakini kwa ufupi nimalizie kwa kusema, alichoandika Mohamed ni kutumia majina, nyakati na matukio ili kupata nafasi ya kushambulia sehemu ya jamii yetu kwa kudhalilisha na kudharau michango yao.
Hili limefanyika kwa kutumia majina kama Nyerere au kwa shambulizi la dini.

Amefanya hivyo kwa kuhadaa kuhusu utafiti kwasababu alijua kile alichokusudia kabla ya kuanza utafiti.
Mohamed amefanya hivyo ili kujenga uhalali wa kundi fulani juu ya umiliki wa nchi na kupitia hilo apenyeze madai yake ambayo mengi hayana uthibitisho kama kilivyo kitabu chake.

Sehemu kubwa ya maandiko yake yanatokana na ''third party'' na wengi aliowahoji ima walikuwa na duku duku au walieleza ukweli ambao Mo hapendi uwekwe hadharani. Ameshindwa kutuwekea shajara alizosoma na akitaka tuamini kile kilichomo ndani ya shajara. Kanuni za uandishi hasa wa kitafiti hazikubaliani na hilo.

Ili kuhakikisha kuwa jamii aliyokusudia kuieleza ina amini na haipati nafasi za kuhoji hoja zake, Mohamed ametumia sehemu kubwa ya utafiti wake na maandishi kujenga chuki, kuleta farki na uhasama.

Ametumia dhana kuhusu kile marehemu walichokifikiri hata kama hakuwahi kuwahoji na ameshindwa kuwahoji walio hai ili kupata upande wa pili.

Mo anafahamu kuwa sehemu rahisi sana ya kufikia malengo yake ni kutumia dini. Hili analifanya kwa njia ya ''sisi dhidi yao''

Ushahidi kuwa ameshindwa kutetea hoja zake,amepotosha, ameficha baadhi ya ukweli na ameshindwa kujibu hoja au maswali na pale alipojaribu alifanya hivyo kwa udhaifu, unatueleza kilichomo ndani ya mistari aliyoandika.
Na hapa ndipo taifa linapopaswa kutupia jicho.
 

Mkuu Said umenichekesha sana, umenikumbusha mengi kuhusu Binadamu huyu ambaye alikuwa aogopi kusema ukweli aogopi DORA i.e Moh Ali! Jamaa huyu alikuwa mtu wa matani sana na alikuwa na mbinu nyingi za kuwahamasisha watu waje kuangalia mapambano yake na kumuongezea kipato, hakuwa na akili za kawaida yule: Kuna msemo wake ulio kuwa unawahacha wasikilizaji hoi - he goes " I'm so MEAN I can make MEDICINE SICK" hata sijuhi maneno alikuwa anayatoa wapi! "I ain't got no quarrel with them Viet Cong".


Back 2 the point, Ndugu SAID sijuhi ni watu wangapi wamekuelewa sentensi yako ya mwisho? Lakini mimi nimekuelewa sana.
 

Hoja au maswali yasiyo na mpango? kwani ni lazima ajibu kila upuuzi na ujinga anaoulizwa? kishasema kama anaona swali halina maana halijibu. Na wewe na wenzako wakuja, kama mnaona kuna mapungufu katika historia aliyoandika Mohamed Said, kwanini hamkai mkaandika kitabu chenu kwa muono wenu? Ulikuwa unamjuwa Tosiri kabla ya kumsoma Mohamed said? Ulikuwa unajuwa kuwa TANU ilibuniwa Burma kabla ya kumsoma Mohamed Said? Ulikuwa unajuwa kuwa Mwapachu alikuwa boss wake Nyerere katika chama huko Tabora?
 
Sweke,

Yeshakuwa ya kusutana?
Kwa mila za sie watu wa pwani huo ni mwiko.

Wanaume hatusutani.
 
Kilemba?



Naamini mpaka leo hii vazi lao la heshima wahehe ni kilemba na kanzu, hapo Chief Abdallah Mkwawa ndani ya Ihraam na Kilemba ananikumbusha Wasudan huyu.

Umesema vema ABDALLAH na siyo Mwamnyanyi
 

Lingekuwa jambo jema sana kama tutafanya hivyo,

Nitaajitahidi kuiweka vema na kila msomaji aone kwa macho yake ya nyama!
 

Nguruvi3,

Wale Waislam ambao mnaowaandika humu wavivu hawana elimu, wavaa vipendo, watu wa kahawa tu, wavaa mateneti, watu wa ubwabwa tu, wana akili za madrasa watu wakulalamika hawataki kusoma unawaweka kundi gani.
 
Last edited by a moderator:
Lingekuwa jambo jema sana kama tutafanya hivyo,

Nitaajitahidi kuiweka vema na kila msomaji aone kwa macho yake ya nyama!

Unaona kama umepata pakupumulia, wapi? ulijidai kuruka kwenda Iringa huko ukakutana na ma uppercut ya uhakika, ukaanza oooh, wewe hujui historia ya machifu, lakini ukaufyata hukuendelea, unakumbuka ulipojidai unamjuwa chifu wa huko ukaulizwa "Abdu Mkwawa?" ukabana kimya kama hukuona.

Nakuonea huruma sana kujitosa kwenye maji yaliyokuzidi kimo na kuogelea hujui. Naona wenzako wamekutupia tyubu ujivutevute, ukisha pata pumzi njoo na jingine.

Tunasubiri, ulisema ukimaliza la Mkwawa utakuja na la Abushiri, vipi? maji marefu? Naona la Mkwawa umeomba ukatafute data kama ulivyoomba kuleta klip ukaingia mitini wala huiongelei, nna uhakika na la Mkwawa limekuwa ni knockout ya ki Tyson (zile za raundi ya kwanza) kwako. Pole sana, lakini usikate tamaa, jitahidi ndio ukubwa huo.
 
Lingekuwa jambo jema sana kama tutafanya hivyo,

Nitaajitahidi kuiweka vema na kila msomaji aone kwa macho yake ya nyama!

1) Usisahu kutuwekea na majina ya wale waasi walipewa msamaha na Nyerere na wengine wengi kupewa vyeo na mabalozi kama ulivyosema mwenyewe.

2) tuwekee na gari la kwanza la Nyerere uliosema kapewa na Mariale.

3) Utuwekee na kiasi cha pesa alichopewa Nyerere na Mariale kwenda UNO kama ulivyotuambia hapo mwanzo.
 
Lakini muheshimiwa mwanakijiji mwandishi alisha sema anarudisha wazee wake walio ondelowa kwenye historia ya taifa letu, sasa aandike wengine ambao walisha ingizwa katika historia ama sio wazee wake ili iweje?
 

Kwa Abushuri Bin Salim Bin Harith wa Pangani ndiyo hawezi kabisa.
 
Lakini muheshimiwa mwanakijiji mwandishi alisha sema anarudisha wazee wake walio ondelowa kwenye historia ya taifa letu, sasa aandike wengine ambao walisha ingizwa katika historia ama sio wazee wake ili iweje?

Kuwarudisha maanayake ni kuuwaunganisha na waliopo si kuwatenga tena!

Alichokifanya Mohamed Said hakina tofauti na anachokilalamikia!
 

B,

Katika biographies zangu ninazozipenda na huzirudia kuzisoma baada ya muda ni hii ya
Muhammad Ali ''The Greatest My Own Story,'' ''Ghandi'' Robert Payne, ''Long Walk to
Freedom'' Nelson Mandela na ''Malcom X,'' Alex Hailey.

Ali alikuwa na kipaji cha kutunga mashairi ya papo kwa papo akakujibu swali kwa mashairi.
Hii akiwamaliza sana waandishi wa magazeti.

Nilifika Madison Square Garden, New York hapa ndipo 1971 Ali alipopigana na Joe Frazier katika
kile kilichoitwa ''Fight of the Century.''

Kuna picha kubwa sana ya Ali na Frazier ''in action'' pigano hili Ali alipigwa.

Huchoki kuitazama ile picha.
Ali good looking and at his best.

Kuna movie zake mbili moja kacheza mwenyewe ''The Greatest'' 1977 na nyingene kacheza
jina limenitoka la actor wake.

Unaweza kuzipata bure katika torrentz.
 
Kwa Abushuri Bin Salim Bin Harith wa Pangani ndiyo hawezi kabisa.

Mmeathiriwa na Mohamed Said,

Nilishasema juu ya mambo ya kichifu Mohamed Said hataniweza, anahitaji msaada wa haraka, na nikaongeza kuwa hata kama muumba amuongezee miaka 60 mingine mbele katika uhai wake, basi kwamambo yahusuyo uchifu na himaya zake afrika atabaki kuwa msikilizaji wangu tu!

Nasema tena upya kuwa historia ya Mkwavinyika Mwamuyinga haijui,

Hajui kwanini alijua kusoma na kuandika Kiarabu, eti anasema alizaliwa akiwa Muislamu????

Hivi pale Rungemba alipolala Mnyigumba baba yake mzazi wa Mkwavinyika Mnyigumba paliwahi kuwa na chembe la uislamu?

Mohamed Said nakujuza tu kuwa jina la Abdala kwa chifu Mkwawa alilipata akiwa tayari ni chifu na alilipata baada ya mahusiano mazuri na waarabu waliokuwa wakimuuzia nguo na vitu vingine, ndipo akajua kusoma na kuandika na akaiga kuswali kiarabu!

Walipokuja Wajerumani nao pia walimfundisha tamaduni zao za kusali na kusoma na kuandika,

Nenda pale Kalenga kuna maandishi mengi sana ya kijerumani,

Kumbuka Mkwawa Mnyigumba kwa dini alikuwa muamini wa DINI za ASILI/Jadi

Na maandishi ya Mkwawa yote ni mawasiliono ya barua kati yake na wajerumani

Na zaidi kuna mahali maalumu alipokuwa akisali kwa KIKRISTU (kijerumani)

Nakusihi na kukuonya Mohamed Said usijifungie kiudini tu, utasinyaa kwa kila jambo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…