Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Hapana MM.
Wewe ni muandishi wa habari iwe pro au amateur.
Kwa kudadisi zaidi ungemsaidia Nyerere kutafuta hio audio ya hotuba ili tusikie nani kasema ukweli na nani hakusema ukweli.
Sasa hivi mmetuacha bado kwenye giza sie wafuatiliaji.
Tulichoambulia ni picha tu.
Siwezi kuamini mtu kama Mwanakijiji na yeye anashindwa kuitafuta hio audio.
Na hata kama inauzwa basi kwa uhakika haifikii hata 100$

Tutendeeni haki mmeyaanza sasa tunataka kujua zaidi.
Hamuwezi kutuacha njia panda.
 
Nilitoka kidogo, narudi nakuta Maalim wangu wa JF, Mohamed Said, anaaga.

Ni fursa adhyim na ntajitahid kuipitia upya michango yote ya mjadala huu na mingineo na nna uhakika kuwa panapo majaaliwa tutakutana tena katika darsa lingine na wote wapendao kujuwa zaidi ya wayajuwayo.

Amma kwa hakika nafarijika sana kila nnaposikia mitaa ya kwetu, wazee wa mitaani kwetu wakitajwa na hususan Maalim Mohamed Said anapowataja huwa kama nnawaona.

Wengi wa wazee wa Kariakoo wa Gerezani wanaotajwa amma nilibahatika kuwajua na ambao sijabahatika kuwajuwa basi watoto zao amma wajukuu zao amma ndugu zao amma ahli zao nilibahatika kujuana nao.

Nilichojifunza kutokana na mijadala hii iliyoibuka baada ya Mohamed Said kuandika kitabu kinachohusu wazee wetu wa Kariakoo na Gerezani, ni wengi, kama si wote, wanaojikakamuwa kupotosha ni wageni wa Dar Es Salaam, au wakuja, kama si wao basi wazee wao. Na karibu wooote amma si Waislaam amma si Wakristo.

Sijakutana na mwenyeji na mzaliwa wa Dar ambae ametia shaka maandiko (japo kiduchu) ya Mohamed Said.

Nnafuraha kubwa kuona kuwa mleta mada, mpaka dakika za majeruhi, hajaweza kutuonesha ni wapi Mohamed Said alipofanya "uchochezi na dhihaka kwa wapigania uhuru wa Tanganyika na Zanzibar" kama alivyokusudia. Hiyo ni faraja kubwa.

Sina zaidi, ila InshaAllah ntaendelea kuwepo na kupitia tena hii nyuzi na kama kuna panapohitaji kuhojiwa na au kupawekea mkazo, sinto-sita kufanya hivyo. Na patapohitaji nondo, naahidi ntaziteremsha, ya amma hapa ya amma tutapokutana majukwaa mengine.

Napokea muago huo bila kinyongo.

Maalim wangu Mohamed Said, alamsik.
 

Kamuulize Faiza Foxy. Nasikia ni binamu yako.
 

Nani anayetakiwa kuweka hotuba ya Nyerere ya kile anachodaiwa kusema?
 
Hata wakati wa Jimmy Carter haikuwa Moshe Dayan. Dayan alikuwa waziri wa ulinzi. Arafat alikutana na waziri mkuu wa Israel.

Hiyo niliyokuwekea nyekundu si sahihi na usipotoshe wanaopitia hii mijadala. Moshe Dayan alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wakati wa Jimmy Cater na si Waziri wa ulinzi, Jimmy Cater mwaka 1978 waliposaini mkataba na Anwar Saadat na Menachem Begin, Moshe Dayan alikuwa kiungo muhimu cha kuandika mapatano hayo.

Menachem Begin, Jimmy Carter and Anwar Sadat at Camp David, 1978

In 1977, despite having been re-elected to the Knesset for the Alignment, he accepted the offer to become Foreign Minister in the new Likud government led by Menachem Begin. He was expelled from the Alignment, as a result and sat as an independent MK. As foreign minister in Begin's government, he was instrumental in drawing up the Camp David Accords, a peace agreement with Egypt. Dayan resigned his post in October 1979,
 
Arafat alikutana Camp David wakati wa Bill Clinton ambaye aliingia mamlakani 1988. Hakukuwa na mkutano Camp David enzi za Menachem Begin.

Usipotoshe wana JF. Menachem Begin ndiye alisaini mkataba wa kwanza wa maridhiano baina yake na Anwar Saadat mwaka 1979 wakati wa Jimmy Cater (akiwa kinara wa mkataba huo). Nimeweka na picha. Na makubaliano hayo yaliyoanzia Camp David 1978 (ndiyo yalipelekea Anwar Sadat na Menachem Begin kupewa kwa pamoja tuzo ya Nobel mwaka 1978) na kufikia kilele na kusainiwa na wote watatu White House mwaka 1979 na ndiyo pia yalichochea Jimmy Cater kupewa tuzo ya Nobel mwaka 2002.



President Jimmy Carter, center, with Egyptian President Sadat, left, and Israeli Prime Minister Begin, right, during a signing ceremony for the Camp David Peace Accords at the White House in 1979. Carter was awarded the Nobel Peace Prize in 2002 for his humanitarian efforts and success in bringing Egypt and Israel to the peace table in 1979. mk/mk/UPI

Read more: http://www.upi.com/Top_News/World-N...-David-dead/UPI-48831335870834/#ixzz2JVUJxyu3
 

Jee, ulikuwa unamjuwa Mshume Kiate kabla ya kumsoma Mohamed Said?
 

Ushajibiwa mara chungu nzima, tuyarudishe majibu uliyopewa?
 

Zomba,
Wewe ndiye uliyepotosha. The issue was Arafat versus Moshe Dayan. Kaitafute picha yao basi.
 

Dah.!.......Bob Mkuu sana ..........heshima mbele!!

Mkuu mbona umepotea sana hapa JF?...........shukrani sana kwa elimu.......
 
Yaani Begin ndiye Moshe Dayan? Anayehitaji darasa ni wewe.

Uzuri wa JF kama moderators hawajachakachuwa kila kitu kinakuwapo, soma ulichoandika na nilivyokujibu na kukupa darsa:

Uliandika hivi:

By Jasusi


Arafat alikutana Camp David wakati wa Bill Clinton ambaye aliingia mamlakani 1988. Hakukuwa na mkutano Camp David enzi za Menachem Begin.

Nikakupa hint:

Jimmy Cater?

Hukunielewa kuwa nilikuwa nakusaidia kiuungwana, ndio maana nilikuwekea jina tu la Jimmy Cater bila maelezo, ili urejeshe kumbukumbu zako, ukajibu bila kufikiri:


Nikakupa darsa baada ya kuona kuwa kumbe huelewi unachokiandika na hata unaposaidiwa kwa kupewa hint bado unajifanya mjanja:


Nikakuta kwingine tena ulianza kupotosha kwa hili:
By Jasusi

Arafat alikutana Camp David wakati wa Bill Clinton ambaye aliingia mamlakani 1988. Hakukuwa na mkutano Camp David enzi za Menachem Begin.

Nikaamuwa nikupe darsa lingine kwa kuwa huelewi unachokisema:


Sasa unarusha nini? vitu viko kinagaubaga.
 
Hi hi hii, Jasusi, wewe unampa darasa, yeye zomba anadai anakupa darsa...kulemaa kuko aina nyingi!

Nna uhakika hata wewe umejifunza na darsa fupi nililompa Jasusi, rejea post.

Naona hukutaka kujibu post niliyokuuliza hapo juu? au mkuki kwa nguruwe kwa binaadam mchungu?
 
Barubaru,

Mtu kama Mzee Jumbe Tambaza mwenye historia Dar es Slaa kwa wasiomjua eneo la Muhimbili Hosptal lilikuwa mali yake. Leo hii hayumo hata kati ya wale wanachama 20 wa mwanzo wa TANU.


maajabu ya Dunia yahilahi.

Hata Bibi Titi Mohamed ambaye ndie kiongozi wa kwanza wa umoja wa akina mama wa TANU na mhamasishaji mkubwa sana wa Tanu katika mikoa ya Dar na Pwani hususan Rufiji leo hii hatambuliki kabisa.


Kwa kweli kuna mengi sana yalifichwa na Al Akhi Mohamed Said ametufungua macho.


Mchambuzi.

Mimi nilikuwa naomba unitajie members wa Baraza la wazee wa TANU la kwanza kabisa labda majina yaliyosahaulika katika waasisi yanaweza kuwemo humo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…