zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,930
Arafat alikutana Camp David wakati wa Bill Clinton ambaye aliingia mamlakani 1988. Hakukuwa na mkutano Camp David enzi za Menachem Begin.
Jimmy Cater?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Arafat alikutana Camp David wakati wa Bill Clinton ambaye aliingia mamlakani 1988. Hakukuwa na mkutano Camp David enzi za Menachem Begin.
Ndugu yangu; mzee wetu kiungwana ameshindwa kujibu haya maswali na kaomba tumruusu aende; kuendelea kumdai ayajibu ni kumpa mzigo asiouweza. Wasomaji wako humu watakuwa wameelewa kwanini hajayajibu maswali mengi na ndio maana tumruhusu tu aende apumzike kidogo. Labda next time hatokuja na madai yale yale tena.
Jimmy Cater?
Nilitoka kidogo, narudi nakuta Maalim wangu wa JF, Mohamed Said, anaaga.
Ni fursa adhyim na ntajitahid kuipitia upya michango yote ya mjadala huu na mingineo na nna uhakika kuwa panapo majaaliwa tutakutana tena katika darsa lingine na wote wapendao kujuwa zaidi ya wayajuwayo.
Amma kwa hakika nafarijika sana kila nnaposikia mitaa ya kwetu, wazee wa mitaani kwetu wakitajwa na hususan Maalim Mohamed Said anapowataja huwa kama nnawaona.
Wengi wa wazee wa Kariakoo wa Gerezani wanaotajwa amma nilibahatika kuwajua na ambao sijabahatika kuwajuwa basi watoto zao amma wajukuu zao amma ndugu zao amma ahli zao nilibahatika kujuana nao.
Nilichojifunza kutokana na mijadala hii iliyoibuka baada ya Mohamed Said kuandika kitabu kinachohusu wazee wetu wa Kariakoo na Gerezani, ni wengi, kama si wote, wanaojikakamuwa kupotosha ni wageni wa Dar Es Salaam, au wakuja, kama si wao basi wazee wao. Na karibu wooote amma si Waislaam amma si Wakristo.
Sijakutana na mwenyeji na mzaliwa wa Dar ambae ametia shaka maandiko (japo kiduchu) ya Mohamed Said.
Nnafuraha kubwa kuona kuwa mleta mada, mpaka dakika za majeruhi, hajaweza kutuonesha ni wapi Mohamed Said alipofanya "uchochezi na dhihaka kwa wapigania uhuru wa Tanganyika na Zanzibar" kama alivyokusudia. Hiyo ni faraja kubwa.
Sina zaidi, ila InshaAllah ntaendelea kuwepo na kupitia tena hii nyuzi na kama kuna panapohitaji kuhojiwa na au kupawekea mkazo, sinto-sita kufanya hivyo. Na patapohitaji nondo, naahidi ntaziteremsha, ya amma hapa ya amma tutapokutana majukwaa mengine.
Napokea muago huo bila kinyongo.
Maalim wangu Mohamed Said, alamsik.
Hapana MM.
Wewe ni muandishi wa habari iwe pro au amateur.
Kwa kudadisi zaidi ungemsaidia Nyerere kutafuta hio audio ya hotuba ili tusikie nani kasema ukweli na nani hakusema ukweli.
Sasa hivi mmetuacha bado kwenye giza sie wafuatiliaji.
Tulichoambulia ni picha tu.
Siwezi kuamini mtu kama Mwanakijiji na yeye anashindwa kuitafuta hio audio.
Na hata kama inauzwa basi kwa uhakika haifikii hata 100$
Tutendeeni haki mmeyaanza sasa tunataka kujua zaidi.
Hamuwezi kutuacha njia panda.
Hata wakati wa Jimmy Carter haikuwa Moshe Dayan. Dayan alikuwa waziri wa ulinzi. Arafat alikutana na waziri mkuu wa Israel.
Kamuulize Faiza Foxy. Nasikia ni binamu yako.
Yericko Nyerere, unaweza msaidia kama una uwezo huo.Nani anayetakiwa kuweka hotuba ya Nyerere ya kile anachodaiwa kusema?
Arafat alikutana Camp David wakati wa Bill Clinton ambaye aliingia mamlakani 1988. Hakukuwa na mkutano Camp David enzi za Menachem Begin.
Ndugu yangu; mzee wetu kiungwana ameshindwa kujibu haya maswali na kaomba tumruusu aende; kuendelea kumdai ayajibu ni kumpa mzigo asiouweza. Wasomaji wako humu watakuwa wameelewa kwanini hajayajibu maswali mengi na ndio maana tumruhusu tu aende apumzike kidogo. Labda next time hatokuja na madai yale yale tena.
Hebu Spike Lee, naomba kama hajakuacha mkiwa, mkumbushe ajibu maswali yangu haya. Maanake naona anaanza kujikaanga mwenyewe kwa mafuta yake na hata internet etiquette inaanza kumpa taabu kuifuata...font hizo!... ni zaidi ya zile za THE BIG SHOW! Hiyo si dalili nzuri. Maswali yenyewe haya;
Asante, naendelea kusubiri (remember the vulture is a patient bird)...hii ni safari ya tatu namkumbushia.
Usipotoshe wana JF. Menachem Begin ndiye alisaini mkataba wa kwanza wa maridhiano baina yake na Anwar Saadat mwaka 1979 wakati wa Jimmy Cater (akiwa kinara wa mkataba huo). Nimeweka na picha. Na makubaliano hayo yaliyoanzia Camp David 1978 (ndiyo yalipelekea Anwar Sadat na Menachem Begin kupewa kwa pamoja tuzo ya Nobel mwaka 1978) na kufikia kilele na kusainiwa na wote watatu White House mwaka 1979 na ndiyo pia yalichochea Jimmy Cater kupewa tuzo ya Nobel mwaka 2002.
President Jimmy Carter, center, with Egyptian President Sadat, left, and Israeli Prime Minister Begin, right, during a signing ceremony for the Camp David Peace Accords at the White House in 1979. Carter was awarded the Nobel Peace Prize in 2002 for his humanitarian efforts and success in bringing Egypt and Israel to the peace table in 1979. mk/mk/UPI
Read more: Egyptian candidate says Camp David 'dead' - UPI.com
Nimekupa darsa lingine kuhusu Moshe Dayan hapo juu, ulipotosha kama kawaida yako.
Asalaam Alekum, Shalom, Peace be apon you guyz!..
damn hivi bado nyie wadanganyika mnazungumzia maswala ya Nyerere, Uislaam na Ukristu?... ama kweli mzungu alituweza sana kutupachika wingu hili ktk bongo zetu.... Dah! ama kweli adui yetu mkubwa ni kutawaliwa kifikra haswaaaa!
Kwako Muhammed Said, Hakuna mtu apaswaye kuitwa Muislaam ikiwa hajajisalimisha kwa Mwenyezi Mungu (Total submission to God), hizi habari za watu kuzaliwa ktk Uislaam wa majina na ukoo na nasaba, kuvaa kanzu na kubaraghashia hauwezi kutumiwa kama ushahidi hata mbele ya Mwenyezi Mungu isipokuwa wale walojinafsisha mioyo yao na wakafuata waloamrishwa na vitabu bya Mwenyezi Mungu..Na ndio maana wapo wale waliofuata vitabu enzi za Nabii Issa (Yesu) na kabla ya Muhammad waliitwa Masara na kwa sababu moja tu kwamba walifuata kitabu na wakawasamilisha kwa Mwenyezi Mungu...Hii inarudi nyuma hadi wakati wa Ibrahim walikuwepo walojisalimishakwa Mwenyezi Mungu na wakatofautiana na baba, mama au kaka zao wa tumbo moja..
Kwa hiyo mkuu wangu, ni dhambi kubwa sana kujaribu kuutafsiri Uislaam kama Wakristu maana hawa ni kundi la watu waliomfuata Yesu ama Wayahudi (Jews) ambao ni kundi la watu waliokubali kumfuata Judea, Uislaam ni dini ambayo humfuati mtu isipokuwa unajisalimisha kwa Mwenyezi Mungu na kufuata yale uloamrishwa. Infact Muslims are not followers of Muhammad bali Muhammad ni mjumbe tu (messanger)...Hizi habari za kuleta jamii ya waislaam kwa kuzaliwa ama kwa sababu anaitwa Abdul, Ally, Omar na kutuweka sote kundi moja ni ujinga mwingine kufuata utamaduni wa watu wengine ilihali ukweli sivyo!
Binafsi yangu nachukia sana mtu anapotaka kutumia dini kuhalalisha ujinga ambao ndio sababu kubwa ya hao unaowaita waislaam kuwa nyuma. Na nimeshakwambia sana tu ya kwamba ikiwa enzi ya Nyerere ni asilimia 5 tu waliweza kupata nafasi ya kuendelea ma na masomo shule za juu, ulitegemea Waislaam wangapi wachaguliwe na kwa kigezo gani? yaani unataka kunambia asilimia 95 ya watoto waloshindwa kuendelea na masomo wote waliokuwa Waislaam!!..
Kama swala ni ELIMU leo hii basi lizungumzwe na tusitake sana kukwepa ukweli maana lipo wazi kabisa na Nyerere hayupo duniani. Tumeujenga mfumo huu mpya sisi wenyewe tena kwa matusi na rais akiwa Mwinyi sasa iweje Nyerere ndiye wa kulaumiwa?..Ama rais anapokuwa Muislaam jina basi hakuna makosa isipokuwa yule mwenye jina la kizungu?
Yaani Begin ndiye Moshe Dayan? Anayehitaji darasa ni wewe.
Jimmy Cater?
Hata wakati wa Jimmy Carter haikuwa Moshe Dayan. Dayan alikuwa waziri wa ulinzi. Arafat alikuthttps://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/383235-uchochezi-wa-mohamedi-said-na-dhihaka-kwa-wapigania-uhuru-wa-tanganyika-na-zanzibar-160.html#post5579623ana na waziri mkuu wa Israel.
Hiyo niliyokuwekea nyekundu si sahihi na usipotoshe wanaopitia hii mijadala. Moshe Dayan alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wakati wa Jimmy Cater na si Waziri wa ulinzi, Jimmy Cater mwaka 1978 waliposaini mkataba na Anwar Saadat na Menachem Begin, Moshe Dayan alikuwa kiungo muhimu cha kuandika mapatano hayo.
![]()
Menachem Begin, Jimmy Carter and Anwar Sadat at Camp David, 1978
In 1977, despite having been re-elected to the Knesset for the Alignment, he accepted the offer to become Foreign Minister in the new Likud government led by Menachem Begin. He was expelled from the Alignment, as a result and sat as an independent MK. As foreign minister in Begin's government, he was instrumental in drawing up the Camp David Accords, a peace agreement with Egypt. Dayan resigned his post in October 1979,
Usipotoshe wana JF. Menachem Begin ndiye alisaini mkataba wa kwanza wa maridhiano baina yake na Anwar Saadat mwaka 1979 wakati wa Jimmy Cater (akiwa kinara wa mkataba huo). Nimeweka na picha. Na makubaliano hayo yaliyoanzia Camp David 1978 (ndiyo yalipelekea Anwar Sadat na Menachem Begin kupewa kwa pamoja tuzo ya Nobel mwaka 1978) na kufikia kilele na kusainiwa na wote watatu White House mwaka 1979 na ndiyo pia yalichochea Jimmy Cater kupewa tuzo ya Nobel mwaka 2002.
President Jimmy Carter, center, with Egyptian President Sadat, left, and Israeli Prime Minister Begin, right, during a signing ceremony for the Camp David Peace Accords at the White House in 1979. Carter was awarded the Nobel Peace Prize in 2002 for his humanitarian efforts and success in bringing Egypt and Israel to the peace table in 1979. mk/mk/UPI
Read more: Egyptian candidate says Camp David 'dead' - UPI.com
Barubaru,
Mtu kama Mzee Jumbe Tambaza mwenye historia Dar es Slaa kwa wasiomjua eneo la Muhimbili Hosptal lilikuwa mali yake. Leo hii hayumo hata kati ya wale wanachama 20 wa mwanzo wa TANU.