Ndugu yangu Bukyanagandi, ni pigo kubwa sana kwa wanaotafuta "muujiza" ili kumpandisha Nyerere kutoka alipo "mwenyeheri" kumpeleka kwenye "mtakatifu". Muujiza walioutegemea ni kumfanya kuwa yeye ni "super hero" wa Tanganyika aliyeweza kuwakabili wakoloni peke yake na kuipatia Tanganyika Uhuru alioudai yeye pekee. Lingethibitishwa hiilo ni moja kwa moja linampa status Nyerere ya kuwa ni mfanya "miujiza" (miracles) ambao ni kigezo cha u "sainthood".
Ukweli anaouweka wazi Mohamed Said, unaharibu hicho kigezo na ni lazima wagalatia wampinge Mohamed Said kwa nguvu zote. Lakini ukweli ni ukweli haufutiki na muujiza uwe wa kweli basi, si wa kubuni.
Bukyanagandi nafahamu kuwa wewe si Muislaam kama ulivyojieleza katika moja ya post zako, lakini u katika wale waupendao ukweli na inashangaza kuona watu humu wanapinga lakini wanachokipinga hawakioneshi, iliyobaki wanarusha kila istihizai, kejeli, vijembe kwa kuwa tu wanadhani ndio wanafanya "character assassination", laiti angelikuja mmoja wao akasema, Mshume ni wa kabuni hakuwepo, Abdulwahid Sykes hajawahi kumweka Nyerere, Dossa Aziz hajatowa mchango wake katika harakati za kudai Uhuru na wengine wote aliowataja Mohamed Said, japo mmoja wao au habari yao moja wakaipinga, hapo ningewaelewa, lakini tazama na soma kwa makini hilo hukuti.
Ni maradhi tu yaliyomo mioyoni mwao, na kwa uhakika hayapunguwi yanazidi. Unajuwa adui yako kila unapofanikiwa yeye ndiyo huzidi kuumia? ndio hawa wanaopinga, mradi wapinge tu.
Nakuelewa vizuri sana mkuu Zomba analysis yako ni spot on kabisa - ni kweli mimi ni Mkristo wa madhebu ya Kilutheli lakini ukoo wetu una Wakatoliki, Wapagani, Waislaam na Waislaam wa Bukoba wanakuwa Waislaam kupindukia Baba mdogo wangu kwa mfano alipokuwa anakuja kututembela alikuwa anabeba sufuria,vijiko na sahani zake anasema hawezi kutumia sufuria zetu zilizo tumika kupikia nguruwe.
Back 2 the point kuhusu ndugu Mohammed Said - mimi nilikuwa nimekaa kimya bila kuchangia kwa muda mrefu 4 a reason nikiangalia watu wakitetea vitu ambavyo vinaweza kulihingiza Taifa letu kwenye turmoil kwa kuendekeza u-fanatism wa
mtu mmoja. Heading ya post na majibu ya baadhi ya wana jamvi yalionyesha wazi wazi kuna kikundi kulikuwa kimejipanga kumuharibia sifa ndugu Mohammed Said ili aonekane ni mdini, mkabila na mtu hatari ambaye amepania kuligawa Taifa letu kwa misingi ya imani za kidini - wanayasema hayo kimaksudi sio kwamba hawajuhi kwamba ni mambo ya kutunga tu!! Wanafikili Watanzania hawana akili za kuchambua mambo bila ya kuwa swayed na kikundi chochote.
Mimi na Watanzania wenzangu wengi wapenda amani katika Taifa letu tunasikitishwa sana na mbinu za jamaa hawa, hatuzipendi hata kidogo, personally sijawahi kujihisi niko threatened na Waislaam au dini yao. Ndugu Moh alifanya kitendo cha ujasiri - kwanza: Kunyoosha historia ya kweli kuhusu wanaharakati walio husika katika mapambano na wakoloni - wengi wao tukubali walikuwa ni Waislaam na Wakristo wachache kwani tatizo liko wapi hapo, cha ajabu kuna baadhi ya Wakristo
fanatics ambao hawataki kulisikia/kukubali hilo; as far as they are concern
Nyerere ndiye alikuwa
Alpha na Omega - kundi hilo ndilo linamkalia kooni ndugu
Mohammed Said!
Kama tunalitakia mema Taifa letu, kitu cha kwanza tulikuwa tunapaswa kumshukuru Ndugu Mohammed Said kwa kuwa
muwazi kuhusu
upindishwaji mkubwa wa historia ya wanaharakati, pili kueleza bayana
Waislaam kutotendewa haki katika Taifa lao huru, malalamiko mengi anayo lalamikia Moh yana ukweli ndani yake - Sasa hapo amekosea nini?? Je angehamua kukaa kimya na kufikilia mambo mengine
unfortunate akishirikiana na wenzake mgewafanya nini au mnafikili uwezo huo
hawana? Tatizo tulilo nalo wengi wetu ni kukosa kutafakali mambo kwa kina - hivi inawaingia akilini kwamba mnaweza kupuuzia forever malamiko ya kweli ya madhebu ambayo ni
nusu ya population ya Watanzania???
Mkuu ZOMBA hapa chini nilikuwa namjibu Yericko na WildCard -
nimejaribu kueleza kwa kirefu kwamba Wa Tanzania tukubali na kuwaenzi mashujaa walio shiriki katika mapambano na wakoloni hata kama walioshiriki hatupendi dini zao - ukweli utabaki palepale: God bless U mkuu.
Tukubali kwamba hoja zimemalizika. Tunarudia yaleyale. Niwashukuru mleta mada,
Yericko Nyerere na Mzee
Mohamed Said kwa kujisimamia mwenyewe na kujibu yale alooweza kujibu. Nimshukuru pia kwa kukiri makosa na mapungufu ya kitabu chake. Kwa anadai kitabu kinaendelea kutolewa bila shaka kuna atakalofanya kurekebisha baadhi ya hoja mle hasa ya UDINI aloompakazia Mwalimu na wazee wake.
Nchi yetu itabaki bila DINI kama Mungu, Allah mwenyewe asivyo nayo. WATANZANIA kila mtu ataendelea kuabudu anavyoona inafaa bila ya kumbugudhi mwenzake. Tunapoongelea Taifa letu tusiingize DINI, KABILA ingawa vitu hivi vilikuwepo, vipo na vitaendelea kuwepo.Watanganyika wote kabisa walipigania uhuru wa nchi yao. Historia isingeweza kuwaandika wote. Ambaye hakuandikwa sio kwamba ilidhamiriwa iwe hivo na yeyote. Hamuwezi kukaa na watu mkaunda CHAMA au UMOJA kwa madhumuni na malengo flani halafu ukataka wenzako wote wasahaulike kwa sababu ya DINI zao ambazo uliwakuta nazo. Haingii akilini hata kidogo.Kwa vyovyote vile tumeparurana katika mada hii. Tusameheane. Tubaki WATANZANIA. Hakuna aliyeshinda wala kushindwa. Wengi tuliowajadili humu wametangulia mbele ya haki. Hawakuyaandika karibu yote tulioyajadili na kubishana humu. Hakuna anayejua kwa uhakika kama wangepewa nafasi kama hii tuliopata wangeandika nini. Tumewalisha na kutafunisha maneno mengi tu. Hawakutaka kuonekana wanajikweza kwa kuandika HISTORIA walioitengeneza wenyewe.
Mkuu kwani nani kaleta hoja hii jamvini, au ulishirikiana kikamilifu na mleta hoja aliyepania kuonyesha Dunia kwamba Ndugu Mohammed Said ni mtu hatari sana na mchonganishi!! Inapokuja swala la ndugu Moh, Jericko keeps going in circles na hii si mara yake ya kwanza kuanzisha controversal posts za kumshambulia Mohammed Said bila simile!! Hapa mnajifanya eti hoja hii ifungwe na sijuhi tusameane lakini hapo hapo mnasema kwamba Moh. ni mdini, mkabila, anajikweza kuandika historia alioitengeneza mwenyewe and all vices you can imagine, tuwe wakweli hapa - unataka kueleza wana JF kwamba hakuna kitu chochote alichojifunza kutokana na kitabu/makala ya ndugu Moh; in other words wewe umebobea katika nyanja za historia ya kweli kuhusu Taifa letu, kama kuna ukweli wowote katika hilo mbona uleti jamvini tukaijadili. Mmekazania ku-teardown historia/maoni ya Ndugu Moh. mkiwa na imani kwamba hilo tu litaweza ku-built UP mtizamo wenu - what a folly!
Please revisit headig ya hoja ya Jericko, hiko je? highly derogative isn't it!! Je hii ni bahati mbaya au? - Kwa nini tushangae alicho kuja zungumza baadae! Yuko obsessed na Mohammed Said
as if Moh is some MONSTER, sijawahi kusikia
Mohammed Said eating anyone dead or alive sasa tatizo liko wapi!! - watu waogope kuzungumza wanayo yajuwa kwa kuogopa kuzungumzia
a virtual demi-GOD?
Kumbukeni kwamba Watanzania ni waelewa wa mambo, wana akili za kuchambanua mambo na kujua ukweli huko wapi, kama Jericko unaona Mohammed kaandika historia ambayo afikiani nayo kwa nini andiki historia ya kwake mbadala ukatuletea hapa jamvini tuakaijadili, ninacho kishuhudia humu ni baadhi ya wana JF specifically mleta hoja ana jump from tree 2 tree looking 4 anything however
infinitesimal za kuweza kum-pin down Ndugu Moh -
come rain or shine!!
Yaani hoja za Jericko kwa ndugu Mohammed wakati mwingine zinakuwa highly incoherent - mpaka watu tunapoteza -track unacho taka kuzungumzia ni nini hasa! Hata Mohammed mwenyewe nimeona akimkumbusha politely kama kawaida yake Moh, kwamba ndugu Jericko wakati mwingine anatumbukiza hoja nyingine ambazo azina mtililiko mzuri, kila mtu mwenye akili timamu anajua kwamba hiyo ni a clever ploy ya Ndugu Jericko ya kujaribu kumtega tega Ndugu Moh - forgetting kwamba this GUY(Moh) is capable of smelling a rat a MEGA miles away, there's no way u can play Ndugu Moh on your little finger - tukubaliane jamaa anajua mambo mengi -
his creed notwithstanding, oh yes kipengele hicho ndicho naona mahasimu wake wanakitumia kwa hila kumzulia mambo na kumuhukumu! Mnaweza kutuonyesha ni wapi Moh amezungumzia kwamba anataka Tanzania hiwe Islamic Republic, wapi kanzungumizia mambo ya ukabila? Nyinyi ndio mnapalilia mambo ya ukabila nmasema sijuhi yeye ni Mmanyema, sijuhi walio anzisha TAA ni Wazaramo/Warufiji/Wamanyema ambao hawakwenda shule wanywa kahawa tu!! Sijuhi Ukoo wa Sykes asili yao ni Wazulu!! Kwa nini mnakazania hilo, tukianza kuulizana asili zetu nani atakuwa na haki ya kuitwa Mtanzania labda watu walio zaliwa pwani na katikati ya Tanzania, mbona hamna ubavu wa kuhoji asili ya Mwalimu Nyerere – nimesoma na mtoto wake Minaki kwa hiyo najua ninacho zungumza hapa.
Sijaona popote ambapo mkuu Moh akimlazimisha mtu kusoma makala yake, kama kuna watu awataki kumsikiliza basi wana hiari ya kumpuuzia na ku-move on, lakini sio kumkosea heshima, kumtukana na kibaya zaidi kuonyesha kiburi cha wazi wazi.
Mambo mengine yanashangaza sana! Hivi wewe na mwenzako nani kawapa a blank cheque ya kuwasemea Watanzania wenzako wenye akili timamu ili tumuone Ndugu Mohammed Said ni mtu wa kuogopwa kama ukoma - yaani nyinyi mnaji-appoint kwenye posts za kuwa
Judge, Jury and executioner all rolled into ONE mlipania kumu hukumu ndugu Moh
in a Kangaroo court! Eti "unamshukuru kwa kukiri makosa na mapungufu ya kitabu chake" – unaweza kutuonyesha ni wapi amekili makosa na mapungufu ya kitabu chake!!! .
Baada ya kufatilia uzi huu kwa muda mrefu bila ya ku-comment chochote leo nataka niwe MUWAZI kwa kusema "the truth of the matter ni kwamba mind set za wengi wetu ndizo zitakuja kulihingiza Taifa letu kweye machafuko yasiyo kifani" tusije tukajidanganya hapa kwamba madhehebu ya kislaam
(half or more ya Tanzania population ni wa madhehebu haya) the Nation cannot afford kuto kuwatendewa haki forever-kama kuna baadhi yenu wenye fikila za kuwapuuzia 4ever 'am afraid kuwambieni kwamba you are
DEAD WRONG na itakuja kutu-cost dearly, I am not a scare monger lakini ukweli unabaki pale pale.
Repeate - tunapaswa kumshukuru Mungu kwamba at least amajitokeza mtu msomi na mchambuzi anaye weka mambo wazi kuhusu historia ya Taifa letu na kero wanazo kumbana nazo ndugu zetu Waislaam nchini, ambazo nyingi ni za kweli; badala ya ku-address kero zao sisi tunabaki tuna wabeza beza na kuwa kejeli. Mtu ungetegemea wana JF na raia wengine wenye kuitakia amani nchi yetu wangeishauri Serikali yetu Tukufu iyavalie njuga maswala ya KERO za Waislaam ili tusije kujikuta tunapigana siku za usoni - hatari hiyo ya kuchezea kiberiti karibu na
Gunpowder KEG nyinyi hilo amulioni, tumejaa dhalau TU.
Labda nimalizie kwa kusema kwamba, kitu kilicho msukuma Ndugu Moh. Said kuandika kitabu chake kinatokana na matukio ya kweli aliyo wahi kushuhudia au kusimuliwa na wazazi wake au wetu wengine wenye lika la wazazi wake au zaidi, kingine zaidi kilicho msukuma kuandika kitabu ni kile cha Serikali ya awamu ya kwanza kutowataja raia wote walioshiriki kikamilifu katika kupinga ukoloni wa Waingereza ambao hata jina la mzazi wake halikutajwa, je ingelikuwa ni wewe unalipenda Taifa lako bila ya kutukuza mtu mmoja ungefanya nini kuhusu uposhaji mkubwa wa historia? Nimesoma darasa la kwanza mpaka la saba kwenye somo la historia yetu sikuwahi kusikia majina aliyo taja Ndugu Moh, mfano Dr.Kyaruzi na Dr. Rugazia walijulikana huko Bukoba kama Doctors of medicine, lika letu hakuna aliye kuwa anajuwa kwamba waliwahi kuhusika na harakati za ukombozi, lakini mbona Moh kawataja kwenye kitabu chake, lakini niliona kulikuwa na watu wanamlahumu eti he didn't go far enough kuwazungumzia madaktari hao wakristo! Kichekesho kabisa, mnamlahumu Moh lakini amsemi chochote kuhusu Serikali ya awamu ya kwanza ambayo Mkristo mwenzao hakuwataja popote na wote walisoma Makerere. Nani wa kulahumiwa katika hilo – Moh aliye wataja kidogo au Serikali ya awamu ya kwanza iliyo kaa KIMYA?
Watu tulishuhudia juzi juzi hapa ndio busara za JK zilitumika kwa kuwatunuku nishani mashujaa wetu hawa waliokuwa wamefutwa kwenye historia ya Taifa letu, kumbuka imelichukua Taifa letu takribani miaka 50 na ushee kutaja/kukumbuka mashujaa hao! Ndugu Moh. alishawataja zaidi ya miaka15 iliyopita na wengi walio tajwa kwenye kitabu cha ndugu Moh walitunukiwa nishani, mbona hilo amlisemi - mmekazania
UDINI X3.
Tukumbuke kuna Raia ambao wali wahi kupitia zahama zinazo fanana fanana na za baba yake Ndugu Mohammed Said na wenzake wakati wa utawala wa awamu ya kwanza, wako wengi walio fanyiwa vitendo ambavyo havipendezi kibinadamu usione wamekaa kimya kama bado wako hai au ndugu zao mkafikili ni wajinga. Sio vizuri kujaribu ku-muzzle watu wasiseme wanacho kijua, waacheni wafunguke kwa maslahi ya kurekebisha historia ya kweli kuhusu Taifa letu.