Gwalihenzi
JF-Expert Member
- Oct 21, 2011
- 5,125
- 1,301
Mohamed Saidi, ulikuwa na sababu gani ya kuaga hapa jamvini na sasa unarudi kinyemela?Kwani kuzaliwa kwako Dar es salaam kuna manufaa gani kwa taifa hili unalotaka kuliaangamiza kwa kwa uchochezi wako wa kidini? Au ulifanya juhudi gani ili uzaliwe Dar? kwanini ujivunie kuzaliwa Dar kana kwamba kuzaliwa Dar es Salaam ni "achievement". Sasa angalia majivuno yako yanavyo kuletea mateso;G,
Hivi nyie JF ndiyo kipimo chenu?
Nimekuwekea hapa wewe ili msaidiane nyote wawili mkamilishe hesabu lau kwa uchache sana.
Kuna hili nilikwishaliweka.
Hii kazi ya kuandika sio siri imetangazwa katika Kigoda Cha Mwalimu Nyerere.
Mimi hamtaki kuniaini.
Hebu fanyeni uchunguzi na nyie mjua nini chanzo cha kazi hiyo kisha rejeenikwangu Insha Allah.
Saida Othmann Yahya (mke wa marehemu Prof. Haroub Othman) na Prof. Issa Shivji wanaandika
hivi sasa maisha ya Nyerere.
Hili la kwanza sasa hebu fikeni na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Historia waulize fikra zao
kuhusu kitabu changu.
Hapo ndipo kitovu cha taaluma na utafiti msikalie JF, JF, JF, JF, hapa ni mpata mpatae ndiyo maana
hata Yericko na yeye yumo.
Msitambe kwa kuuliza maswali JF...
Humu kila ''msomi'' uwanja wake hata wale wasomi chekechea.
Mbona hamtii kidole katik ''reviews'' za kitabu?
Ingieni na humo huo ndiyo usomi.
Nyie JF, JF, JF...
Hebu basi ingieni kwenye ''serialisation'' zangu tatu katika The East African.
Hamna la kusema?
Zitafuteni hizo ''series'' mtazipata zilichapwa December 1998.
Maofisa ofsis za serikali walikuwa wanachekea chooni gazetila The East African
wanapasiana kama timu ya Brazili 1970 iliivyokuwa wanapeana pasi.
Ukipenda wanapasiana The East African kama kitabu cha Barzanji.
Nakupeni home work hiyo fanyeni uchunguzi kisha rudini hapa mnambie kuwa
bado mnaamini kuwa John Iliffe, Jonathan Glassman, James Brenan na wengineo,
wasomi hawa mabingwa wa African History waliokifanyia ''review'' kitabu changu walikuwa
wanareview ngano na Cambridge Journal of African History walichapa ngano.
Rudini hapa mnambie The East African katika ''serialisation,'' iliyodumu wiki tatu walikuwa
walikuwa wanafanya kichekesho katika ''serialisation'' ya ngano.
Halikadhalika mje mseme hawa nao Amazon, WH Smith, Africa House (London) hawa wote
waliokuwa wakiuza kitabu changu walikuwa wakiuza unga wa ngano na kuwa waliuziwa mbuzi
ndani ya gunia.
Na hawa wasomaji wa kitabu hiki kinachokwenda toleo la tatu la kitabu ni watu wasiojua kitu.
Hebu piteni humo na jengeni hoja zenu humo.
Basi nyie mmekuwa kazi muijuayo ni kuuliza, kuuliza, kuuliza, ubishi, ubishi, ubishi...
Kujipongeza na kutaka ushindi mwepesi.
Hii haiwezekani.
Ilm sharti usome, upinde mgongo, usome na uandike mambo ya maana yenye tija.
Mwisho nakupeni tanbihi acheni lugha za mitaani za ''JF hapendwi mtu nk. nk...''
Kama ni hizo lugha zingekuwa za maana kutumia mimi ni aula zaidi kuzitumia kwa kuwa sikuzaliwa
kijijini wala kuja kutoka popote.
Nafungua macho niko Dar es Salaam.
Na Dar es Salaam ni bingwa wa kuzua maneno.
Mchochezi Mkuu katimka kakimbia baada ya kugundua kuwa JF si kama uwanja wa mihadhara, watu wanahoji na wanadadisi...sasa wamebaki "cheerleaders" kumlilia kwa kuwaacha wakiwa! Jf kiboko, huko nyuma wako wengi waliokimbia kama yeye na hadi leo hata kuingia humu wanaogopa. Eti hadithi na simulizi za mtaa wa Gerezani zinaitwa historia!...hapana, hapa JF zinaitwa kwa jina lake halisi, ngano.
Nina hakika waliofuatilia mjadala huu kwa makini watakuwa wamejifunza mengi lakini tusije tukawashangaa wale ambao wameambulia sifuri...uelewa watu hutofautiana, wapo ambao wataendelea kulalamikia mtihani badala ya mapungufu yao, oh tunaonewa! Common sense is not that common otherwise id.io.ts would have no domicile! Wapo wanaoamini kwa akili finyu kwamba wanatoa darsa kumbe ni wao wanapewa darasa!
Baada ya maswali yangu kwa mchochezi kukosa majibu, na mimi naaga nikiwaachia uwanja the Barubaru's, the zomba's, the vichwangumu and company. You are free to go ahead and dance yourselves lame...unfortunately the music has long stopped playing!
Haya msome na huyu na uzijibu hoja hizi;
Asalaam Alekum, Shalom, Peace be apon you guyz!..
damn hivi bado nyie wadanganyika mnazungumzia maswala ya Nyerere, Uislaam na Ukristu?... ama kweli mzungu alituweza sana kutupachika wingu hili ktk bongo zetu.... Dah! ama kweli adui yetu mkubwa ni kutawaliwa kifikra haswaaaa!
Kwako Muhammed Said, Hakuna mtu apaswaye kuitwa Muislaam ikiwa hajajisalimisha kwa Mwenyezi Mungu (Total submission to God), hizi habari za watu kuzaliwa ktk Uislaam wa majina na ukoo na nasaba, kuvaa kanzu na kubaraghashia hauwezi kutumiwa kama ushahidi hata mbele ya Mwenyezi Mungu isipokuwa wale walojinafsisha mioyo yao na wakafuata waloamrishwa na vitabu bya Mwenyezi Mungu..Na ndio maana wapo wale waliofuata vitabu enzi za Nabii Issa (Yesu) na kabla ya Muhammad waliitwa Masara na kwa sababu moja tu kwamba walifuata kitabu na wakawasamilisha kwa Mwenyezi Mungu...Hii inarudi nyuma hadi wakati wa Ibrahim walikuwepo walojisalimishakwa Mwenyezi Mungu na wakatofautiana na baba, mama au kaka zao wa tumbo moja..
Kwa hiyo mkuu wangu, ni dhambi kubwa sana kujaribu kuutafsiri Uislaam kama Wakristu maana hawa ni kundi la watu waliomfuata Yesu ama Wayahudi (Jews) ambao ni kundi la watu waliokubali kumfuata Judea, Uislaam ni dini ambayo humfuati mtu isipokuwa unajisalimisha kwa Mwenyezi Mungu na kufuata yale uloamrishwa. Infact Muslims are not followers of Muhammad bali Muhammad ni mjumbe tu (messanger)...Hizi habari za kuleta jamii ya waislaam kwa kuzaliwa ama kwa sababu anaitwa Abdul, Ally, Omar na kutuweka sote kundi moja ni ujinga mwingine kufuata utamaduni wa watu wengine ilihali ukweli sivyo!
Binafsi yangu nachukia sana mtu anapotaka kutumia dini kuhalalisha ujinga ambao ndio sababu kubwa ya hao unaowaita waislaam kuwa nyuma. Na nimeshakwambia sana tu ya kwamba ikiwa enzi ya Nyerere ni asilimia 5 tu waliweza kupata nafasi ya kuendelea ma na masomo shule za juu, ulitegemea Waislaam wangapi wachaguliwe na kwa kigezo gani? yaani unataka kunambia asilimia 95 ya watoto waloshindwa kuendelea na masomo wote waliokuwa Waislaam!!..
Kama swala ni ELIMU leo hii basi lizungumzwe na tusitake sana kukwepa ukweli maana lipo wazi kabisa na Nyerere hayupo duniani. Tumeujenga mfumo huu mpya sisi wenyewe tena kwa matusi na rais akiwa Mwinyi sasa iweje Nyerere ndiye wa kulaumiwa?..Ama rais anapokuwa Muislaam jina basi hakuna makosa isipokuwa yule mwenye jina la kizungu?
Hebu angalia na kigongo kingine hiki hapa!
Hoja kuu ya Mohammed said ni kwamba waislamu hawajafaidi matunda ya uhuru kama wakristo ilihali wao ndio haswa waliopigania uhuru huo. Lakini wengi wa wapigania uhuru hao wa gerezani kama siyo wote na kama ilivyoainishwa na MS mwenyewe hakuna hata kumbukumbu zao kuendesha political rally hata Morogoro, leave alone Nkasi, Karagwe, Magu au Tunduru. Hiyo haimaanishi mchango wao hautambuliwi so is to others waliokuwa maeneo mbali mbali ya Tanganyika. Shukrani kwa walioleta ushahidi wa ziada katika kurekebisha historia iliyopindishwa. Anyways!
Tulishayaongea haya 2010/2011 mpaka tukafika hitimisho mbalo lilikuwa je kama kuna hilo tatizo la mfumo kristo au waislamu kubaguliwa suluhisho lake ni nini? Tukamuuliza Mohammed Said, je ianzishwe affirmative action?, MMM akamuuliza kwa nini basi wasianzishe political movement? Mpaka leo Mohammed Said hajatoa suluhisho ya nini kifanyike kuhusu hiyo anayoiita dhulma. Zaidi zaidi ni tishio kwamba wanatoa tahadhari kwamba serikali isipoliangalia hili yatakayotokea huko baadae tusijelaumiana. Na hapa ndiyo hoja ya mfumo kristo inapojikoroga. Iweje serikali ile ile inayodaiwa kuongozwa na kusimamiwa na mfumo kristo ishughulikie hicho kinachoitwa dhulma dhidi ya inaowadhulumu??
Nilimuuliza Mohammed Said wakati ule atupe japo mfano wa nchi ambayo madaraka na ajira serikalini zinatolewa kwa kufuata uwiano wa kidini ili ikibidi tukajifunze huko. Hajajibu mpaka leo.
Kuhusu Nyerere kunyima jamii fulani elimu, nilimuuliza pia ni kwa nini 1990 kulikuwa na shule nyingi binafsi wilaya ya Rungwe (Na nilizitaja) kulinganisha na mkoa mzima wa Dar es Salaam na Pwani? Hajajibu mpaka leo. Nilitoa mfano specific wa Rungwe ili kuua hoja ya ukatoliki maana wilaya ya Rungwe by then na very likely hata leo ilikuwa na waumini wa RC wasiozidi 10% ya total population.
Nilimuuliza Mohammed Said ni kwa nini Haroub Othman aliendelea kutoa lectures kuhusu intellectualism na uongozi wa mfano wa Nyerere????? Hii ni baada ya MS kutuambia HO alikasirika sana (In a sense alianza kukosa imani na Nyerere) baada ya kujua ukweli wa historia ya uhuru wa Tanganyika kama isimuliwavyo na yeye Mohammed Said. Mfano wa lectures za HO inazozingumzia ni ile aliyoitoa October 14, University of Cape Town, South Africa – Mwalimu Julius Nyerere: An intellectual in power (Unaweza bofya juu ya hiyo title kupata ziada ya kilichosemwa). Mohammed Said hajajibu mpaka leo?
Nilimuuliza MS kuwa inadaiwa wenye mfumo Kristo chaguo lao la uraisi in 2010 elections ilikuwa Dr. Slaa, Kilichotokea wote tunafahamu. JK alishinda, je hii haimaanishi kushindwa au kutokuwepo huo unaodaiwa kuwa mfumo Kristo wenye nguvu za ajabu wa kuamua nani asome nani asisome, nani awe raisi au waziri na nani asiwe, na aajiriwe serikali na nani asiwe. Mohammed Said hajajibu mpaka leo.
Kilichoniondoa mjadalani wakati ule ni pale MS (Mwenye bandiko) alipoonekana kuishiwa hoja na kudai ooh! Angalia nyie mko wangapi, mie peke yangu lakini bado hamniwezi. Mara ooh! Kama hamkubaliani na hoja ndani ya kitabu chake andikeni na nyie vitabu vyenu juu ya historia za wazee wenu. Ikawa sasa si kuelimishana bali kushindana. Nimepitia humu naona ndio huko huko mjadala ulikoelekea.
All in all ni kwamba huu mjadala hautakuwa na maana kama facts na opinions hazitenganishwi na pia mjadala kuhusu nini kifanyike kwa hiyo dhulma inayodaiwa kuwepo. Kutishana na kukebehiana hakutatufikisha kokote kama taifa. Unless kama mjadala huu ni burudani tu. Lakini pia ndugu zangu tusisahau individual responsibility, maana hapo ndio kwenye suluhisho la kudumu.
Babu Mohamed upo hapo?