WC,
Kwanza tatizo lako kubwa kabisa ni kuwa humjui Sheikh Hassan bin Amir
wala huijui historia ya uhuru wa Tanganyika na nafasi ya sheikh katika
maisha ya siasa ya Nyerere.
Ugomvi wa Sheikh Hassan bin Amir na Nyerere ulianza mwaka 1963 Nyerere
alipoanza fitna kutaka kuivunja EAMWS.
Hapo ndipo Nyerere aliposomewa ile hotuba maarufu ''Moto wa Waislam Ukiwaka.''
Msomaji wa hotuba ile alikuwa Katibu wa EAMWS na Muasisi wa TANU Tabora
Bilal Rehani Waikela.
Hotuba ile ilimfedhehesha Nyerere na akalipiza kisasi kwa kumweka Waikela kizuizini
kwa shutuma ya uongo ya kutaka kupindua serikali.
Jambo lingine lilitia hofu Kanisa Katoliki na Nyerere ni ujenzi wa Chuo Kikuu ambacho
EAMWS walikuwa wanapanga kujenga.
Sasa endelea hapa chini:
Dr John C. Sivalon, who in his expose,
Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985, [1] unmasks a conspiracy in the government to subvert Islam. Sivalon revealed that the Catholic Church as far back as 1961 was worried by two prospects.
First, was the unity between the Muslim
madhheb (sect) of Sunni, Bohora, Ismailia and Ithnasheri in Tanganyika; and the second, was the transfer of the headquarters of the East African Muslim Welfare Society (EAMWS) from Mombasa to Dar es Salaam.
The Church was worried that the resources in the hands of rich Asian Muslim community in East Africa, coupled with the political power of African Muslims, particularly in Tanganyika, would endanger Christian interests in East Africa.
The Church therefore declared Islam as its enemy in the country and plotted to thwart its progress.[2]
[1] John C. Sivalon,
Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985, (Ndanda, 1992).
[2]Ibid. p 37.
Kusema kuwa Nyerere hakujali nini na nini si kweli.
Nyerere alikuwa Mkatoliki na alikuwa na uadui na Uislam kama alivyoonyesha Sivalon hapo juu.
Katika kuupiga vita Uislam ndiyo akavunja EAMWS, akamfukuza Sheikh Hassan bin Amir na baada ya
kuwa Sheikh Hassan hayupo ndiyo akaunda BAKWATA.
Hapo ndipo alipopanda mbegu ya udini na inatafuna nchi hii hadi leo.
Yapo mengi lakini kwa sasa tuishie hapa.