Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Kwa viwango na idadi ya WATANZANIA, Wakristo wamesoma vizuri kuliko Waislamu. DINI ya Kiislam ina mchango wake katika hili kama ilivyo DINI ya Kikristo ingawa sio kwa kubaguana bali kwa desturi na utamaduni wa DINI hizi. Sio NECTA! Hebu msome huyu Binti anaitwa Malala wa Pakistani au vituko na maajabu ya Waislam wa Tuareg kule Mali Kaskazini. Andika tu jina MALALA kwenye mtandao halafu uone yaliyomkumba binti huyu.

Waislam wa TANZANIA ni tofauti na hawa kwa masuala ya elimu?
 

Wanasema ukiwa Mwongo usiwe msahaulifu,
kwa maelezo ya Mzee Mohamed Said ya muda wote ni kuwa Vita ya majimaji na hata ile ya Mkwawa dhidi ya Wajerumani ilikuwa ni vita ya kidini, kwa maana ya Wajerumani walikuwa wanapigana na Waislamu, na kwa maelezo yake ya muda wote ni kuwa Wakristo walikataa kushiriki vita ile kwa sababu walikuwa upande wa Wazungu

Sasa hili la kina Sykes ambao ni Waislamu (walikuja na Uslamu wao kutoka Mozambique) kuja kuwapiga Waislam wenzao tena wakiwa chini ya mwamvuli wa Mjerumani mbona hakuwahi kulieleza?

Kama hichi anachokisema Moh Said ni kweli, basi fitna na kusalitiana miongoni mwa Waislamu wa Tanzania ilianza Zamani maana hata wakina Sykes waliwasaliti Waislam wenzao
 

WC,

Kwanza tatizo lako kubwa kabisa ni kuwa humjui Sheikh Hassan bin Amir
wala huijui historia ya uhuru wa Tanganyika na nafasi ya sheikh katika
maisha ya siasa ya Nyerere.

Ugomvi wa Sheikh Hassan bin Amir na Nyerere ulianza mwaka 1963 Nyerere
alipoanza fitna kutaka kuivunja EAMWS.

Hapo ndipo Nyerere aliposomewa ile hotuba maarufu ''Moto wa Waislam Ukiwaka.''
Msomaji wa hotuba ile alikuwa Katibu wa EAMWS na Muasisi wa TANU Tabora
Bilal Rehani Waikela.

Hotuba ile ilimfedhehesha Nyerere na akalipiza kisasi kwa kumweka Waikela kizuizini
kwa shutuma ya uongo ya kutaka kupindua serikali.

Jambo lingine lilitia hofu Kanisa Katoliki na Nyerere ni ujenzi wa Chuo Kikuu ambacho
EAMWS walikuwa wanapanga kujenga.

Sasa endelea hapa chini:

Dr John C. Sivalon, who in his expose, Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985, [1] unmasks a conspiracy in the government to subvert Islam. Sivalon revealed that the Catholic Church as far back as 1961 was worried by two prospects.

First, was the unity between the Muslim madhheb (sect) of Sunni, Bohora, Ismailia and Ithnasheri in Tanganyika; and the second, was the transfer of the headquarters of the East African Muslim Welfare Society (EAMWS) from Mombasa to Dar es Salaam.

The Church was worried that the resources in the hands of rich Asian Muslim community in East Africa, coupled with the political power of African Muslims, particularly in Tanganyika, would endanger Christian interests in East Africa. The Church therefore declared Islam as its enemy in the country and plotted to thwart its progress.[2]


[1] John C. Sivalon, Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985, (Ndanda, 1992).
[2] Ibid. p 37.

Kusema kuwa Nyerere hakujali nini na nini si kweli.

Nyerere alikuwa Mkatoliki na alikuwa na uadui na Uislam kama alivyoonyesha Sivalon hapo juu.

Katika kuupiga vita Uislam ndiyo akavunja EAMWS, akamfukuza Sheikh Hassan bin Amir na baada ya
kuwa Sheikh Hassan hayupo ndiyo akaunda BAKWATA.

Hapo ndipo alipopanda mbegu ya udini na inatafuna nchi hii hadi leo.

Yapo mengi lakini kwa sasa tuishie hapa.
 

Mpaka sasa hauja-prove kuwa alichokisema mzee Mohamed Said kwenye kitabu chake ni ngano.

Hujaleta ushahidi wowote uliotamba kuwa utaleta

Umekuwa bingwa wa kurukia viroja na si kujadili hoja

Kwa ufupi, umeshindwa kutu-convince na ku-prove madai yako

Somo la bure: Kwa lugha unayotumia kwenye mnakasha, mtu yoyote ambaye hayupo biased atajua kuwa huna nidhamu. Wasomi hawajadili na hawabishani kama unavobishana wewe. Wewe kila saa unarekebishwa na mzee na wana jamvi wengine, lakini unapuuza. Sasa unatulazimu kusema kuwa hukufunzwa uzuri malezi na adabu na familia yako tukufu ikiongozwa na mtakatifu Nyerere
 
Last edited by a moderator:

Nimekuuliza nitajie faida za nyie wasomi wa Kikiristo mmelisaidiaje taifa letu kutoka katika dimbwi la umasikini duniani na vita dhidi ya ufisadi unaniambia habari za Pakistani.

Jaribu na wewe kugoogle ili jina Rev Gene Robinson. Uone maajabu ya Wakiristu halafu rudi uniambie mchango wenu nyie wasomi kwenye taifa letu.

Nasubiri majibu mkuu.
 

K,

Uchambuzi mzuri na ukweli ni huo.
Waislam walipambana na Waislam wenzao.

Hata baada ya uhuru wakati Nyerere anapiga vita EAMWS
aliwatumia Waislam kufanya kazi hiyo.

Huu ndiyo ukweli.

Ila inataka mara kwa mara uangalie na mazingira ndipo utapata
picha kamili.

Babu zetu walipigana katika ukoloni.
Hii ni tofauti na Waislam waliopiga vita EAMWS katika nchi huru.

Katika kitabu changu nimesema maneno haya:

''The fall of the EAMWS evolved around three key
personalities-Adam Nasibu, Sheikh Kassim Juma
and Sheikh Abdallah Chaurembo-and was backed
up by Rashid Kawawa and Abeid Amani Karume.

The hand of Julius Nyerere and that of the Catholic
Church were invisible as they have always been.
''

Yapo mengi sana.
 

Hiyo ndio tunaita Double standard
 
Nijibu tuswali twangu hutu kama hautajali Mzee Mohamed:
-Sheikh Amir alikuwa MTANGANYIKA?
-Unajua kuwa Ukatoliki wa Mwalimu ulikuwa wa ukubwani tu na wazazi wake walikuwa wapagani?
-Kwa nini EAMWS ilikuwa inahamishia makao yake Dar?
-Upo wakati Mwalimu waligombana Prince AghaKhan kwa hilo?
-Kwa nini EAMWS ilikufa hata huko Mombasa?
-Unajua kwamba Padre Sivalon na Shirika lake la Maryknoll Fathers walikuwa marafiki wakubwa wa Mwalimu?
 

Y,

Huenda tatizo ni lugha.

Kwa Kiswahili nikikuambia mathalan, ''Usimjali tunamjua.''
Maana yake ni kuwa vituko vyake vyote vinafahamika si
ajabu.

Maneno haya kwa kawaida huambiwa yule ambae hamjua
Bwana Vituko.

Mdogo wangu basi wewe hujitulizi kutwa kucha ni kuandika
kwa jeuri tu na kuvamia hoja?
 

WC,

Nakuona una ghera ya kujua mambo.
Nakushauri usome kitabu changu.

Hayo maswali yote yana majibu yake mle.
 
Tatizo mtu akisoma kidogo anatumia furs hiyo kuwahadaa jamii yake kubwa ambayo haina kisomo cha kisayansi.. Anawabwatukia .. Mnanyonywaa.. Mnakandamizwaa...!!! Maskini hao basi wanamwaminii wanachotwachotwa tu.. Zambi mbaya sana.. Jehanam itawatafuna
 
Uchuro.Umekiri mwenyewe Rashid Kawawa na Abeid Aman Karume waliunga mkono kuondolewa EAMWS lawama bado unampelekea Mwl Nyerere !.Ikiwa EAMWS ilitishiwa usalama wa taifa ulitaka iachwe.

Hiki kitaasisi vurugu cha Sheikh Ponda kikifutwa leo utasema uislam unagandamizwa.


 
WC,

Nakuona una ghera ya kujua mambo.
Nakushauri usome kitabu changu.

Hayo maswali yote yana majibu yake mle.
Ungejibu kwa kifupi tu. Au unafanya na mauzo ya kitabu chako pia! Nimekisoma sikupata majibu ya hayo.
 

WAPIIII!!!!! Watazitoa wapi historia hiyo???? MashaAllah.

Mungu Akupe Nguvu Na Afya njema Maalim wangu.
 
Ngongo,mwenyezi mungu ana karama zake.
Taratibu Mohamed Said anazidi kuuonyesha ulimwengu Mohamed ni mtu wa aina gani.

Ukisoma kitabu chake ameeleza kwa uchungu na undani sana kuhusu siku za mwisho za Platan na Abdul Sykes.
Jinsi walivyofariki wakiwa na fadhaa iliyotokana na kudhalilishwa, kuhujumiwa na kuzodolewa na Nyerere.

Kwa wale wanaosoma mistari tu bila kutumbukiza chembe ya fikra hakika hasira zitapanda jinsi gain huyu ‘’ muovu, dhwalim na shaitwan Nyerere alivyo’’

Sasa anafunguka kuwa Dr Lugazia alifariki akiwa na kinyongo, Denis Phombeah, Dr Mwanjisi, Dr Kyaruzi, Kidaha Makwaia na Chief Lugusha.Hii maana yake ni nini!

Ni ushahidi kuwa kama Nyerere alifanya ubaya basi ulikuwa across the board na dini si kigezo.
Mohamed Said anashuhudia mwenyewe si mimi.

Kwa ‘’mtafiti’’ Mohamed haya aliyajua wakati anaandika kitabu, si kweli kuwa ameyajua jana kwasababu source zake ambazo ni masimulizi ya wazee wake wametangulia mbele ya haki.

Ameandika kuhusu kifo cha Sykes na jinsi Nyerere alivyokuwa na wakati mgumu kwenda kumzika, hakuandika kuhusu wengine kwa kujua kuwa ingeharibu dhana na makusudi ya kitabu chake. Huu ndio unafiki tunaousema kila uchao

Kitu kibaya zaidi kilichonisukuma niandike hapa ni kuonyesha jinsi gain Mohamed alivyokuwa mzushi.
Anasema Nyerere alikataza ugomvi wake na Dr Kyaruzi usiwekwe wazi.
Mohamed hakuwahi kumhoji Nyerere hata siku moja.

Dr Kyaruzi amefariki miaka 13 baada ya Nyerere na ilikuwa mwaka jana. Mohamed hakuwahi kumhoji hata siku moja kupta ushahid wa meneno yake.
Yet ameweza kujua kuhusu kuzuiwa kwa Dr Kyaruzi kusema kisa cha ugomvi! Inaingia akilini kweli!!

Ni uongo na uzushi kama huo ndio aliotuambia kuhusu mazungumzo ya Mwalim na Malima ambayo Mohamed hakueleza mwisho wake, tunachojua ni picha tu zilitolewa chumbani na Nyerere basi Malima akatokea mlango wa uani bila kuaga!

Ni uongo kama huo amemsingizia Prof Othman Haroub alipokwenda kumuona mwalimu. Hatujui mwalim alijibu nini tunachojua ni kuwa prof alitokea mlango wa uani na kuruka ukuta akatokomea kufuatana na ngano hii ya kusadikika.

Ni hulka ya Mohamed kuzushia marehemu maneno na ni mbaya sana katika dini na imani.
Sijui kwanini Mohamed amegeuza dini kuwa ushabiki na si imani.

Tuendelee kumshukuru mwenyezi mungu, si mnaona jinsi Mohamed anavyokiri, anavyokana na anavyoonyesha kile alichokificha?

Si mwenyezi mungu ndiye alifichua siri ya Maryknoll ambayo haikusemwa?

Mohamed, muogope mwenyezi mungu! Mwenyezi mungu si Simba au Yanga.

Mohamed wajukuu zako watasoma maneno yako na watapita ulipopunzika wakisema huyu ndiye msanii, mzushi na bingwa wa upotoshaji. Watakusifu babu alikuwa kiboko kwa kamba!
 
Umetuletea bandiko refu sana la Gazeti la Raia Mwema, sijui hilo ndiyo umebandika kuthibitisha kichwa cha habari au ndio bado unahaha baada ya kula zile za "Camp David"?
Ya Camp David tena? wahenga wanasemaje vile? Ficha ujinga wako. Tangu Lini Menachem Begin akawa Moshe Dayan?
 
Amedandia hoja bila kusoma chanzo cha hoja hiyo!


[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=+2]Abdallah Rashid Sembe (1912-1999)[/SIZE][/FONT][FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1][/SIZE][/FONT][FONT=Arial,Helvetica][SIZE=+1]Shujaa wa Azimio la Tabora la mwaka 1958

UMESHAWAHI KUMSIKIA AU KUMSOMA KTK KITABU CHOCHOTE UKIONDOA CHA MZEE MOHAMED SAID HUYO MZEE???
[/SIZE][/FONT][FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1][/SIZE][/FONT]
 


Mbaya zaidi maneno yake hayana hata ushahidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…