Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar



Kumekucha...Mohamed Said, hebu tupe kisa cha huyu Sheikh.
 
TUNATOA POLE KWA WADAU WOTE KUFATIA KIFO DOKTA VEDASTO KYARUZI ALIYEBUNI JINA LA TANZANIA NA ALIWAHI KUWA RAIS WA TAA. MIAKA YA 50.


Mdau Erick akimlisha keki dokta Kyaruzi wakati wa uhai wake.

MAKALA YA MDAU UPENDO ERICK BAADA YA KIPO CHA DOKTA KYARUZI
Si watanzania wengi sana wa kizazi cha miongo baada ya Uhuru wanaomfahamu au wamesikia habari za Dokta Vedasto Mzungu Kyaruzi, Mtanzania Mzalendo na Mwanamapinduzi, Msomi wa awali wa kiwango cha Udaktari wa Binadamu ndani ya Tanganyika. Nafasi ya wengi kumjua Dokta Kyaruzi imepotea kutokana na kuwa na Taifa lisilo na misingi mizuri ya kutambua michango na kuona ufahari juu ya uzalendo wa watu wake.

Ninamshukuru Mungu kwa kunipa nafasi ya kuwa karibu na Dokta Kyaruzi. Amekuwa rafiki na mlezi wangu; akiningoza vema jinsi ya kukua kitaaluma, kuishi na watu, makundi na jamii mbalimbali. Nakumbuka wakati wa hafla ya kunipongeza kwa kuhitimu Shahada ya Kwanza, Dokta aliniusia kwa msisitizo kwamba; Waafrika wengi wanadhani kuhitimu masomo ndo mwisho wa elimu katika fani husika. Kwake kuhitimu kulimaanisha mwanzo mpya wa kusoma fani kiundani zaidi, kujisajiri katika Journals, Periodicals, na Newsletters ili kuhakikisha anakwenda sambamba na kukua kwa maarifa katika tasnia yake. Ndipo alipopata kunijulisha maana ya neno "Practitioner" linalowekwa mbele ya vyeo vya Madaktari, Wahasibu, Wanasheria na fani zingine huko kwenye nchi zilizoendelea.

Pia, daima Daktari hakuacha kuniusia juu ya siasa na nafasi ilipotokea alinikutanisha na wanasiasa wakongwe mmoja wapo akiwa ni marehemu Abdulnoor Suleiman. Siku zote aliniambia na kunikanya kuwa, kama nia ya mtu kujiunga na siasa ni kujilimbikizia mali basi mtu huyo amekosea njia maishani. Katika ushiriki wake kwenye siasa, alithamini sana haki iliyompa mtu uhuru maishani kuliko mali ambayo ingemkosesha amani na heshima kwenye jamii. Mara kwa mara alisema; mtu akigonga mlango wa nyumba yake usiku wa manane atajua ama ni jirani kapata shida au kuna mtu anataka maelezo kapotea njia. Hawezi kuogopa kama wanasiasa wa siku hizi walafi ambao likiwatokea haraka uhisi "mambo yameharibika". Mbele ya nyumba yake mara nyingi alijipumzisha Mbeba-Mkaa, Mlevi aitwaye Rostamali. Dokta alipenda kumtumia Rostamali kama mfano wa watu wasiokuwa na hofu juu ya maisha yao. Wanaopata pesa yao kihalali kwa kusota, wakaitumia wapendavyo na kisha kuishi kwa amani wakilala nje bila kumhofia mtu yeyote na hata mdudu kama mbu naye asiwadhuru! Katika mfano huu alipenda kuhitimisha kwa kuniuliza, ni mwanasiasa gani (huu ulikinukiliwa enzi za Mkapa lakini bado una uhai) anaishi nyumba isiyo na geti kubwa, uzio wa umeme, walinzi wenye silaha, mbwa wakali na Je, ana amani kuliko mimi au Rostamali?

Kulingana na kumbukumbu ya masimulizi mbalimbali, Dokta Kyaruzi ni miongoni mwa Watanganyika watatu wa kwanza kabisa kupata dalaja la Udaktari wa Binadamu. Na wa kwanza alitoka ukoo wa Kichifu pale Gera-Ishozi, Bukoba. Dokta Kyaruzi alikuwa miongoni mwa Maktaba zinazotembea. Ni mmoja wa watu waliomfahamu Mwl. J.K Nyerere fika tuliokuwa tumebaki nao. Kwa mara ya Kwanza Dokta walikutana na Mwl. Nyerere Tabora mwaka 1939 wakati Dokta akisoma St. Mary (Kwa sasa Milambo Sec. School) na Mwl. naye alikuwa akisoma Tabora School (Sasa Tabora Sec. School). Walibahatika kuwa wote tena katika masomo ya Elimu ya Juu huko Makerere-Uganda. Na kwa pamoja walishiriki siasa za ukombozi kupitia tawi la TAA Chuo Kikuu cha Makerere, Dokta akiwa kama Katibu wa Tawi. Waliporejea nchini kila moja alikwenda kwanza kutumikia fani aliyosomea huku akijipanga vema kushiriki siasa za ukombozi. Dokta Kyaruzi alikwenda kufanya kazi Kingolwira wakati Mwl alikwenda kufundisha Tabora Boys. Baadaye hisia za ki-harakati ziliwarejesha Dar es Salaam na kuwakutanisha tena katika uongozi wa juu wa TAA huku Dokta Kyaruzi akikwea mpaka Uenyekiti wa chama mwaka 1949. Kama TAA ndiyo ilizaa TANU na TANU ikarithiwa na CCM basi utashangaa mbona Muasisi huyu hakuvuma na wala hukusikia habari zake kama usikiavyo habari za kina Sykes, Bibi Titi, n.k. Hili nakuachia uchunguze mwenyewe! Miongoni mwa wanasiasa ambao Daktari amekufa akiwakumbuka kwa kumkumbuka au kuthamini harakati zake ni Prof. Mark James Mwandosya. Mwaka 2005 wakati Prof. Mwandosya akiwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi alifunga safari kwenda kumsalimu Daktari. Baada ya mazungumzo, Prof. Mwandosya alimwachia Daktari zawadi ya simu ya mkononi aina ya NOKIA. Ni jambo ambalo hakulisahau mpaka uhai unamtoka.

Baada ya uhuru, Mwalimu J.K Nyerere alimteua Dokta Kyaruzi kuwa Mwakilishi wa Kwanza wa Tanganyika huru kwenye Umoja wa Mataifa, NY-Marekani. Kutokana na uhaba wa wasomi baadaye Mwl alimuhitaji na hivyo Dokta Kyaruzi alirejea nchini na kuwa Msaidizi wa Mwl-Ikulu. Kulitokea uchonganishi kati ya wasaidizi wa Mwl uliojikita katika majungu ya madaraka. Na Mwl kwa kutolichunguza vema akafanya uamuzi wa kumrejesha Dokta Kyaruzi kufanya kazi kwenye taaluma yake. Hivyo Dokta Kyaruzi alipangiwa kuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kazi ambayo aliripoti mara moja na kuitenda kwa moyo wake wote mpaka kustaafu utumishi wa umma. Aliporejea nyumbani Bukoba baada ya kustaafu alianzisha Zahanati iliyoangaliana uso kwa uso na duka la Nyegera Waitu. Kulingana na ugwiji aliokuwa nao katika masuala ya wanawake (Gynecology) huduma yake ilivuta watu kutoka sehemu mbalimbali za nchi na hata toka nchi jirani. Kipindi ziwa Rwelu (viktoria) likiwa ndo njia kuu ya usafiri kati ya Kagera na mikoa mingine, hakuna meli ingefika asubuhi bila kuwa na wagonjwa wanaokuja kupata huduma kwa Dokta Kyaruzi. Pamoja na huduma yake hii lakini pia aliendelea kutoa mchango wa Elimu, Uzoefu na Maarifa yake kupitia majukwaa mbalimbali. Lakini ushiriki wake katika harakati za kisisasa ulikomea katika uandishi wa makala kwenye gazeti la Rai. Dokta amekuwa mjumbe na baadaye Mwenyekiti wa Bodi la Hospitali ya Mkoa wa Kagera kwa muda. Na katika kipindi chake mabadiliko makubwa katika miundombinu, rasilimali watu na huduma yaliweza kufanyika.

Hata katika umri wake wa mauti (miaka 91), Dokta ni mtu aliyeishi kwa kanuni na malengo. Siku yake iligawanywa kikanuni na haikubadilika iwe jua, umande ama mvua. Siku yake daima ilianza kwa kuhudhuria misa ya asubuhi. Baada ya misa hurudi nyumbani kupata kifungua kinywa na kujiandaa kwenda kazini. Saa saba alipata mlo wa mchana na kupumzika kwa saa na kisha kwenda kazini. Jioni alipenda kumpleleka mbwa wake ziwani na aliporejea alikaa bustanini kupata kikombe cha kahawa. Baada ya mazungumzo na mgeni ama kama muda wa sala ungefika angali bado na wageni, basi angeomba udhuru na kwenda kusali na aliporejea alifikia mezani kwa mlo wa usiku. Mara baada ya chakula iwe cha mchana au usiku, Dokta asingeweza kuhimili nguvu ya usingizi hivyo kila baada ya mlo tendo lililofuatia lilikuwa ni kupumzika.

Dokta Kyaruzi alijaliwa uzao wa watoto wane (4). Miongoni mwao, wawili (Patrick na Christina) aliwapata kwenye ndoa ya kwanza na Mama wa Kiganda. Mama huyu walifahamiana wakati Dokta akisoma Makerere. Patrick alisomea urubani na Tina ni mtaalamu wa kushona mavazi aliyebokea. Mama Patrick alifariki kwa saratani zaidi ya miaka 35 iliyopita. Baada ya msiba huu Patrick na Tina ambao hawakuwa wakiishi Tanzania waligundua msongo uliompata Baba yao. Walibaini kuwa iwapo msongo usingetafutiwa njia mbadala mapema, basi ungempelekea Baba yao mauti mapema zaidi. Hivyo kwa pamoja wakamsihi Dokta aoe mwanamke mwingine. Huu ulikuwa ni wakati mgumu mwingine kwa Dokta Kyaruzi kuufanyia maamuzi. Baada ya kitambo Dokta Kyaruzi aliafiki kufunga ndoa na mke ambaye amepata kuzaa naye watoto wawili; wa kike (Adela-Ngonzi) na wa kiume ( Edween-Shubi)-Ni wiki chache tu Dokta Kyaruzi alikuwa amepata mjuu kupitia Adela ambaye kwa bahati mbaya sana mauti yamemkuta kabla ya kumtia machoni. Pia mjukuu wa Dokta aitwaye- John Patrick Kyaruzi, aishiye nje wiki jana tu ndo alikuwa amekata tiketi ya kuja Tanzania mwishoni wa mwezi kumsalimu Babu yake! Huzuni iliyoje?

Katika ndoa ya pili Dokta Kyaruzi hakudumu kabla ya kupata jaribu lingine kubwa. Wakati ndoa inaanza kurejesha furaha na utulivu katika maisha yake, Patrick (mwanae mkubwa) aliyekuwa rubani wa ndege Marekani alipata ajali angani na ndege kuteketea. Kilichoshuhudiwa na kuzikwa ni majivu! Ukifuatilia vema maisha ya familia ya Dokta Kyaruzi utaduwaha kubaini mlolongo wa ajali za ndege na hasara zake katika mali na watu wa familia.

Katika maisha yake yote pamoja na utitiri wa fursa alizokuwa nazo, Dokta Kyaruzi alimiliki nyumba mbili tu; moja Kyaka-Mutukula na nyingine Miembeni-uwanja wa ndege, Bukoba. Nyumba ya Kyaka ilitunguliwa na ndege wakati wa vita ya Kagera na ile ya miembeni iliunguzwa upande kwenye ile ajali ya ndege ya Jeshi ya mwaka 1997. Wale mtakaokumbuka, pamoja na nyumba kuungua upande, Dokta Kyaruzi alipoteza magari yake mawili (Toyota Stout na Jeep) papo hapo. Pia vifaa vya Zahanati yake ambayo alikuwa ameihamishia nyumbani viliharibika na kupelekea huduma kufungwa. Hizi ajali na matokeo yake huniumiza sana hadi leo. Hata mara zote Dokta Kyaruzi alipokuwa akizirejea katika masimulizi, zimekuwa zikiniacha na simanzi kubwa. Kiufupi, HAKUNA FIDIA YOYOTE ALIYOPEWA Dokta Kyaruzi katika ajali hizi! Si kwa sababu yoyote ile ya msingi bali ni kutokana na ukiritimba na rushwa ambazo yeye hakuwa tayari kuafikiana nazo. Katika upanuzi wa uwanja wa ndege uliofanyika hivi karibuni, Dokta Kyaruzi alitakiwa kubomoa na kuondoka toka nyumba hii ya Miembeni. Kwa tabia yake ya kupenda kutenda na kutendewa haki alimanusura anyimwe hata kile kiduchu cha fidia aliyopewa. Mpaka pale Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi alipoingilia kati.

Ndugu na Jamaa tunamlilia mpendwa wetu Dokta Kyaruzi. Na kwa tabia ninahakika na viongozi wa Serikali-Kitaifa nao sasa watanakshi salamu na hotuba zao. Binafsi hisia zangu zinahama haraka kutoka kwenye huzuni na kujawa na furaha na amani ya moyo. Ni kwa kuwa imani yangu inanituma kuamini kuwa Dokta Kyaruzi hakufa bali ametwaliwa kwenye makazi ya kudumu akafurahie milele kifuani mwa Ibrahim baada ya kuyashinda majaribu makuu ya ulimwengu huu. Siku zote nimeyatathmini maisha ya Dokta Kyaruzi kwa kuyamithilisha na miasha ya Ayubu mtumishi wa Mungu. Naamini hata katika kulifanya simulizi langu kuwa fupi kadri niwezavyo bado umeweza kung'amua mateso na majaribu aliyopitia Dokta Vedasto Kyaruzi.

Hapo kwenye blue kazi ya Mohamed Said.

Mwandishi analalamika nani atawakumbuka kuandika historia ya waliopotezwa.
 

MM,

Sijui vipi unapata tabu na mimi.

Kwangu mimi nikizungumza dini namuona Allah.
Nikuzungumzia Waislam namzungumza Allah.

Kwangu mimi hiki si kitu cha kuona aibu.
Kwangu mimi Uislam ni kitu adhim.

Na katika kitabu changu nilitaka kuanza na
Bismillah Rahman Rahim...

Publisher akasema haifai.
Tulivutana sana katika hilo.

Baada ya kukueleza haya bado utakuwa na tabu kunifahamu?
 

Ritz,

Nilimwandikia Dk. Vedasto Kyaruzi taazia mara tu nilipopata taarifa ya kifo chake.
Naiweka hapa ili wanaukumbi wamjue shujaa huyu aliyesahauliwa na historia:

DK. VEDASTO KYARUZI DAKTARI MWANAHARAKATI WA TAA
Na Mohamed Said
Utangulizi
Katika moja ya misiba mikubwa iliyoikumba Tanzania ni kukosekana kwa historia inayoweza kuaminika kuhusu mashujaa wake waliopigania uhuru kutoka kwa Waingereza. Gazeti la Raia Mwema (Mei 23 - Mei 29, 2012) limefahamisha umma kuhusu kifo cha Dk. Vedasto Kyaruzi na kwa muhtasari wakaweka sifa zake.

Kwa bahati mbaya sana sifa walizoweka hazikuwa za kweli kwa kiasi fulani. Mfano ni pale makala iliposema Dk. Kyaruzi ndiye aliyemwachia uongozi Nyerere katika TAA na kuwa alikuwa rais wa kwanza wa TAA.

Ukweli ni kuwa Nyerere na Dk. Kyaruzi hawakupata kukutana katika uongozi wa TAA kwa hiyo isingewezekana kwa Dk. Kyaruzi kumwachia Nyerere uongozi. Wakati Nyerere anaingia TAA Makao Makuu, Dar es Salaam mwaka 1952 Kyaruzi alikuwa keshaondoshwa Dar es Salaam na wakoloni kapelekwa Nzega na chama kilikuwa chini ya uongozi wa Abdulwahid Sykes akiwa katibu na kaimu rais. Abdulwahid ndiye aliyeikabidhi TAA kwa Nyerere mwaka 1953.

Jingine ni kuwa Kyaruzi wala hakuwa rais wa kwanza wa TAA kwani chama kilianzishwa Dar es Salaam mwaka 1929 kikijulikina kama African Association na wakati huo Dk Kyaruzi alikuwa bado mtoto mdogo.

Mwaka wa 1948 ndipo kilipokuja badilishwa jina na kuitwa Tanganyika African Association (TAA) Kwa nia njema kabisa naweka hapa maisha ya siasa ya Dk. Kyaruzi kama nilivyoyaandika katika moja ya sura za kitabu changu "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924
- 1968..."

Katika makala haya nimefanya mabadiliko hapa na pale ili kumwezesha msomaji kufuatilia siasa za TAA kama zilivyokuwa wakati wa uongozi wa Dk. Kyaruzi mwaka wa 1950.


Juhudi za Kubadili Uongozi Mkongwe wa TAA Uliochoka, 1949 - 1950


Kwa miongo miwili kuanzia mwaka wa 1929 Chama cha African Association kilikuwa mikononi mwa viongozi watu wazima sana mfano wa Mzee bin Sudi na Mwalimu Thomas Sauti Plantan ambae alikuwa rais wa chama hicho mwaka wa 1949. Mzee bin Sudi na Kleist Sykes walipata vilevile kuwa rais na katibu wa African Association na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika kwa wakati mmoja katika miaka ya 1930. Vyama hivi viwili vilikuwa vikifanya harakati zake kwa karibu na ushirikiano mkubwa kwa kuwa viongozi wake walikuwa viongozi wa ngazi ya juu katika vyama hivyo viwili.

Siasa za kikoloni zilikuwa zikibadilika na kwa hivyo zilihitaji damu change kama za akina Dk. Kyaruzi zenye mawazo na mbinu mpya ili kuongoza harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Serikali ya kikoloni ilikuwa kila uchao inabadili mitindo, hila na mbinu za ukandamizaji ili kuendeleza utawala wake. Ukitazama mwelekeo wa siasa na mazingira ya wakati ule, uongozi wa wazee katika African Association, kwa hali yao na kutokana na mambo yalivyokuwa yakiwakabili, walikuwa hawana uwezo wa kukabiliana na changamoto ya ukoloni. Lakini pamoja na yote hayo, wazee hawakutaka kuachia madaraka.

Jambo hili lilizusha mvutano baina ya wazee na wanasiasa vijana. Vijana hawa walikuwa akina Abdulwahid na Ally Sykes (ambao baba yao, Kleist Sykes ndiye aliyeasisi African Association), Tewa Said Tewa, Stephen Mhando, Waziri Dossa Aziz, James Mkande, na wale madaktari watano - Vedasto Kyaruzi, Joseph Mutahangarwa, Luciano Tsere, Michael Lugazia na wengineo. Haya yalikuwa ni mapambano baina ya kizazi kipya na kile cha kale. Vita Kuu ya Pili ilikuwa imemalizika na ukoloni katika Tanganyika sasa ukawa unakabiliwa na changamoto mpya kutoka kwa vijana wasomi toka Chuo cha Makerere na askari wa Tanganyika waliopigana Burma katika Vita ya Pili Vya Dunia chini ya King's African Rifles (KAR).


Katika mvutano huu wa madaraka kwa upande wa vijana waliokuwa wakiinukia alikuwepo kijana wa Kidigo kutoka Tanga aliyehitimu Makerere, Hamza Kibwana Mwapachu. Mwapachu alikuwa ameajiriwa na Idara ya Maendeleo ya Jamii kama 'Assistant Welfare' Officer (Msaidizi wa Ustawi wa Jamii), Ilala Welfare Centre mjini Dar es Salaam. Historia ya Mwapachu katika siasa ilianza Makerere College, Uganda ambako alijihusisha na mambo ya siasa wakati alipokuwa mwanafunzi. Mwaka wa 1947 Mwapachu akiwa Tabora alichaguliwa kuwa katibu wa African Association, Julius Nyerere akiwa naibu wake.

Mwapachu na Abdulwahid walikuwa na usuhuba mkubwa. Mwaka wa 1950 Mwapachu alikuwa na umri wa miaka 32 na Abdulwahid alikuwa na umri wa miaka 26, mdogo kwa Mwapachu kwa miaka sita. Vijana hawa wawili walikuja kugeuza mwelekeo wa TAA na wakaingiza ndani ya chama hicho aina mpya ya uongozi na ushawishi uliokuwa haujapata kuonekana katika historia ya Tanganyika. Lakini wote wawili walifariki dunia katika ujana. Na wote wawili wakaja kusahauliwa na historia. Hakuna kati yao ambaye hii leo jina lake linahusishwa na historia ya Tanganyika ingawa wao ndiyo waliomvuta Nyerere katika TAAna siasa za Dar es Salaam ya miaka ya mwanzo ya 1950.

Kupitia vijana hawa wawili ndipo historia ya Dk. Kyaruzi ilipoanza. Uongozi wake ulikuwa mfupi katika TAA lakini uongozi huo ulifanya makubwa na kubadilisha sura ya harakati. Katika siku zake za mwisho Dk. Alipata kumwambia mmoja wa watoto wa Hamza Mwapachu kuwa, "Kama si mipango waliyoweka baba yako na Abdulwahid mwaka 1950 tusingelipata uhuru mwaka 1961."


Ofisi ya Mwapachu pale Ilala ilikuwa kituo cha mijadala ya siasa nyakati za mchana. Jioni vikao hivyo vya majadiliano vilihamia Tanga Young Comrades Club. Hiki ilikuwa kilabu maarufu ya vijana wa mji kukutana. Kilabu hii ilikuwa New Street (sasa Mtaa wa Lumumba) karibu na ofisi ya TAA. Mijadala ya siasa nyumbani kwa Abdulwahid au katika ofisi ya Mwapachu Ilala au Tanga Club kidogo kidogo ikawa inaingia katika nadharia ya vipi vijana wangeweza kuuondoa madarakani uongozi wa Mwalimu Thomas Sauti Plantan ndiye aliyekuwa rais wa katibu wake Clemet Mohammed Mtamila.

Si kwamba Tanganyika wakati ule ilikuwa na uhaba wa maswala ambayo yangeweza kuamsha mijadala ya siasa. Kulikuwa na mambo kadhaa ambayo kama yangetumiwa kwa ustadi na uongozi wa TAA, shida hizo zingeweza kuleta kwa watu hisia za manung'uniko na chuki dhidi ya serikali ya kikoloni. Vitu ambavyo TAA ingeweza kuvitumia kuwafitini Waingereza dhidi ya wananchi. Unahitaji tu kuzipitia tahariri za Ramadhani Mashado Plantan katika gazeti lake alilokuwa akihariri mwenyewe lililojulikana kama "Zuhra" ili kuweza kufahamu siasa ilivyokuwa ikitokota chini kwa chini Tanganyika katika miaka ya 1950.

Rais wa TAA Mwalimu Thomas Plantan na damu yake ya Kizulu ya kupenda vita, baada ya kuwa yupo kwenye nchi yenye amani, aliielekeza bunduki yake porini kuwinda wanyama. Hakuwa na muda kama rais wa TAA kushughulika na masuala ya TAA. Uhodari wake katika kuwinda bado hadi miaka ya 1970 iliweza kushuhudiwa nyumbani kwake Mtaa wa Masasi, Mission Quarters. Kuta za nyumbani kwake zilikuwa zimepambwa na mafuvu ya vichwa vya wanyama aliowaua huko porini Mwalimu Thomas Plantan hakuwa na muda wa kuitisha mikutano au kushughulikia mambo ya TAA kwa sababu alitumia wakati wake mwingi porini. Makao Makuu ya TAA mjini Dar es Salaam yalikuwa kama vile yamegubikwa na usingizi mzito.

Barua kutoka matawini hazikuwa zikijibiwa. Baya zaidi, hakukuwepo na mawasiliano yoyote na Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa, mjini New York ambalo ndilo lilikuwa likiitawala Tanganyika kama nchi ya udhamini. Juu ya haya ndani ya TAA na uongozi wake kulikuwa na hali na sura nyingi za ukinzani. Schneider Abdillah Plantan mmoja wa viongozi wa TAA alikuwa siku nyingi amekwishaonyesha chuki yake dhidi ya Waingereza na kwa ajili hiyo akawekwa kizuizini wakati wa Vita Vya Pili kwa kuonyesha msimamo wa kumuunga mkono Hitler dhidi ya Waingereza.

Yeye mwenyewe mwaka 1914 alipigana Vita vya Kwanza vya Dunia dhidi ya Waingereza akiwa askari katika jeshi la Wajerumani akiwa na ndugu yake Kleist Sykes (wakati ule akijulikana kama Kleist Plantan), Mashado Plantan alikuwa na gazeti lake "Zuhra" ambalo lilikuwa ndiyo sauti ya African Association.

Lakini watu hawa walikuwa wazee na wamechoka. Hawakuwa na jipya katika siasa mbali na kuuchukia utawala wa kikoloni.
Walipochoshwa na uongozi huu wa wazee na walipoona hakuna lolote la maana liliokuwa siku moja wakati wa alasiri, Abdulwahid na Mwapachu bila ya kumshauri mtu yeyote wakitokea Tanga Club, New Street, walivamia ofisi ya TAA na kufanya mapinduzi kwa kumtoa msobe msobe Clement Mtamila ofisini kwake.

Abdulwahid alikuwa bingwa wa ngumi wa Tanganyika na Kenya katika kikosi chake wakati wa vita. Hakupata tabu sana kumtoa nje ya ofisi Mtamila. Baada ya vurugu hii ambayo ilikuwa gumzo la mji kwa wakati ule wazee walisalimu amri na wakaamua kuitisha uchaguzi. Maofisa Wazungu kutoka serikalini walihudhuria mkutano huu kama mbinu ya kuwatisha vijana waliokuwa wakishinikiza mageuzi katika TAA. Bila woga Schneider Plantan aliwakabili na kuwaeleza kuwa uchaguzi utafanyika watake wasitake. Shneider alipigwa risasi mguuni vitani kwa hiyo alikuwa akichechemea. (Katika moja ya sifa zake ni kuwa alikuwa mtu shujaa sana. Hamuogopi yeyote. Shneider ndiyo mtu pekee katika historia aliyesimama uso kwa uso na Nyerere na Shneider akamtukana Nyerere nyumbani kwake Msasani huku akimtazama usoni).

Mwezi Machi mwaka 1950, katika Ukumbi wa Arnatouglo, kijana wa Kihaya, Dk. Vedasto Kyaruzi alichaguliwa kuwa rais wa TAA na Abdulwahid Sykes katibu wake. Dk. Kyaruzi alipochukua uongozi, TAA ilikuwa na shilingi 87.00 Barclays Bank, Dar es Salaam. Huu ndiyo ulikuwa mwisho wa wazee, kuongoza TAA. Vilevile ndiyo ukawa mwanzo wa uzalendo na utaifa Tanganyika. Abdillah Schneider Plantan na mdogo wake Ramadhani Mashado Plantan walimuuunga mkono Dk. Kyaruzi katika kuipa TAA uhai mpya ingawa aliyetolewa madarakani alikuwa kaka yao mkubwa Mwalimu Thomas Sauti Plantan. Hivi ndivyo Dk. Kyaruzi alivyoingia katika uongozi wa TAA.

Dk. Kyaruzi Katika Kamati Ndogo ya Siasa Ndani ya TAA, 1950 - 1951


Hakuna nyaraka zozote zinazoonyesha kama African Association ilikuwa imetayarisha mpango wa kushughulikia hali ya siasa. Kuelewa mwelekeo wa siasa wakati ule inabidi mtu atazame mwenendo wa viongozi wa TAA na jinsi walivyokuwa wakiyashughulikia mambo tofauti yaliyokuwa yakiwadhili wananchi. Jambo la kwanza walilofanya Dk. Kyaruzi na Abdulwahid Sykes mara tu baada ya kuingia madarakani ni kuunda TAA Political Subcommittee (Kamati Ndogo ya Siasa ya TAA) iliyomjumuisha Sheikh Hassan bin Amir kama mufti wa Tanganyika na Zanzibar; Dk. Kyaruzi, Mwapachu, Said Chaurembo aliyekuwa liwali wa mahakama ya Kariakoo; John Rupia na Stephen Mhando. Kazi ya kamati hii ilikuwa ni kushughulika na masuala yote ya siasa katika Tanganyika.

Kuundwa kwake ndiyo hasa ulikuwa mwanzo wa siasa za dhahiri katika Tanganyika na mwanzo wa harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.
Kwa kipindi cha miaka ishirini na moja African Association ilifanya kazi chini ya katiba isiyokuwa ya siasa. Kwa mara ya kwanza mwaka 1950, TAA chini ya uongozi mpya, ilijipa hadhi ya chama cha siasa, siyo kwa kubadilisha katiba yake bali kwa kuunda kamati ya siasa ndani ya chama. Kamati hii ilikuwa na watu wenye kuwakilisha maslahi na uwezo tofauti, wakiwa halikadhalika wanatokana na uzoefu na hali tofauti.

Sheikh Hassan bin Amir Muunguja alikuwa ndiye mufti wa Tanganyika na aliwakilisha Waislam ambao hasa ndiyo waliokuwa wakiongoza mapambano dhidi ya serikali. Said Chaurembo aliwakilisha Wazaramo wa Dar es Salaam na vitongoji vyake. John Rupia kutoka Mission Quarter alikuwa mfanya biashara tajiri na mfadhili wa chama. Stephen Mhando Mbondei kutoka Muheza alijulikana kwa misimamo mikali aliwawakilisha wasomi wa Makerere, Dk. Kyaruzi akiwa mmojawapo.

Uongozi huu ndiyo ulioweka msingi wa kuundwa kwa TANU chama kilichokuja kung'oa ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika.
Baada ya kuunda kamati hii uongozi wa TAA ulianza kuyaandikia matawi ya TAA ili kuyahuisha. Jambo kubwa lililokabili TAA na ile kamati ya siasa ilikuwa ni hadhi ya Tanganyika kama nchi ya udhamini chini ya Umoja wa Mataifa. Uongozi wa TAA ulimuingiza katika kamati ya siasa Earle Seaton, mwanasheria kutoka Bermuda aliyekuwa akikaa Moshi ili aishauri kamati kuhusu mambo ya sheria ya katiba. Seaton alitakiwa kuishauri jinsi ya kuliendea shauri la kutaka Uingereza itoe uhuru ili Tanganyika ijitawale yenyewe kwa kuwa nchi hiyo haikuwa koloni, bali nchi chini ya udhanini wa Umoja wa Mataifa.

Mwaka wa 1948 Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa tayari lilikuwa limetuma ujumbe wake wa kwanza kuzuru Tanganyika. Lakini hakuna jambo lolote la manufaa lilipatikana kutoka kwa ujumbe huo. Makao Makuu ya TAA mjini Dar es Salaam chini ya Dk. Kyaruzi na Abdulwahid ikiungwa mkono na kamati ya siasa sasa ilikuwa ikiamka kutoka kwenye usingizi mzito. Kilichotakiwa ilikuwa ni kupata maswala yakutoa changamoto kwa akili za wale wasomi vijana. Uongozi wa chama cha TAA haukuwa na haja ya kuangaza mbali. Changamoto ilikuja kwa sura ya Constitutional Development Committee (Kamati ya Mapendekezo ya Katiba) iliyoundwa na Gavana Edward Twining na mgogoro wa ardhi ya Wameru.


Uingereza ilikuwa ikitawala Tanganyika chini ya kifungu 76 na 77 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Kama mamlaka tawala Uingereza ilitarajiwa kuanzisha na kuendeleza maendeleo ya siasa, uchumi na ya kijamii ya Tanganyika hadi kufikia wakati ambao watu wake wangekuwa tayari kujitawala. Lakini Waingereza walifanya khiyana na hawakutimiza ahadi hiyo. Walijihusisha na kulinda maslahi yao wenyewe ya kikoloni na yale ya watu weupe wachache na wakaendelea kuwapuuza Waafrika waliokuwa wengi na wenye nchi. Labda kwa kuanua ngoma juani, Gavana Twining alikaribisha mapendekezo kutoka kwa watu mashuhuri, vyama vya ustawi wa jamii na Native Authorities, kutaka mapendekezo ya jinsi Tanganyika itakavyotawaliwa.

Kamati ya siasa ya TAA ilipeleka mapendekezo yake ambayo yalitiwa sahihi na wajumbe wote wa kamati ya siasa. Sheikh Hassan bin Amir, Abdulwahid Sykes, Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, John Rupia, Stephen Mhando na Said Chaurembo. Katika taarifa yake ya TAA ya mwaka ya 1950 Abdulwahid aliandika:
"Kwa ajili ya maslahi ya Waafrika na kulinda maslahi ya chama hiki na yale ya jumuiya ya Waafrika kwa ujumla, chama kimeweka wakili atakayeshauri juu ya mambo ya sheria. Wakili huyo ni Bwana E. E. Seaton wa Moshi. Mara kwa mara amekiandikia chama hiki juu ya masuala mbali mbali ya siasa, na kwa kiasi kikubwa ushauri wake umesaidia wakati chama hiki kilipokuwa kikitayarisha mapendekezo juu ya katiba."

Uongozi wa Dk. Kyaruzi na Abdulwahid ulitambua kuwa matatizo mengi kuhusu haki za Waafrika yalikuwa masuala ya kisheria ambayo yalihitaji ushauri wa wanasheria. Kwa mara ya kwanza kwa msaada wa Seaton, TAA kilitoa hoja zake zilozotiwa nguvu na ukweli hoja na kwa tarakimu zilizoonyesha udhalimu ndani ya mfumo wa kikoloni ambao ulikuwa kinyume na Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Memorandum ya TAA kwa Constitutional Development Committee ambayo Pratt amesema iliandikwa kwa utaalamu wa hali ya juu na uongozi wa makao makuu ya Tanganyika African Association ilipendekeza kuwa ndani ya Baraza la Kutunga Sheria Waafrika watashika nusu ya viti kwa miaka kumi na mbili na baada ya hapo ipigwe kura kuwachagua wajumbe.


Hitimisho


Katika miaka hii ya karibuni nimesoma makala kadhaa ambazo Dk. Kyaruzi akifanyiwa mahojiano na waandishi wa magazeti tofauti na katika kila makala Dk. Kyaruzi hakuacha kuweka msisitizo kuwa yeye ndiye aliyemuachia TAA Nyerere. Hiki ni kitu ambacho mimi kama mtafiti na mwandishi wa historia ya uhuru wa Tanganyika kilikuwa kikinitaabisha sana. Kilichokuwa kikinipa shida ni kuwa nilikuwa nikifahamu kuwa Dk. Kyaruzi aliingia katika uongozi wa TAA mwaka 1950 pamoja na Abdulwahid Sykes.

Nilikuwa najua kuwa waliomsaidia kuingia katika uongozi walikuwa watu wa mjini akina Plantan na Sykes. Vipi watu hawa hakuwa anawakumbuka? Wakati Nyerere anachukua uongozi wa TAA mwaka 1953 Kyaruzi hakuwa Dar es Salaam. Hiki ni kitu kikinishughulisha sana. Jambo hili likishighulisha sana fikra zangu kwa kujiuliza mbona Kyaruzi anamruka Abdulwahid Sykes katika historia yao ya uongozi wa TAA mwaka wa 1950 na kumwingiza Nyerere ilhali Nyerere wakati ule hakuwa anafahamika na yeyote katika duru za siasa za Tanganyika? Nikawa nashangaa nikijiuliza kwani Dk. Kyaruzi hajui kuwa Nyerere aliingia katika uongozi wa TAA mwaka 1953? Nilikuwa nikijifariji kwa kusema kuwa haya ndiyo matatizo ya historia ya uhuru wa Tanganyika.

Lakini jambo linalonisikitisha sana ni kujua kuwa katika miaka ya 1970 Dk. Kyaruzi alipeleka mswada wa maisha yake kwa mchapaji mmoja wa vitabu ili mswada wake uhaririwe na kuchapwa kitabu. Mchapaji yule ambae lilikuwa shirika la umma lilikataa kuchapa kitabu kile. Sijui kwa nini walikataa kuchapa kitabu kile ambacho kwa hali yeyote ile ingelikuwa hazina kubwa kwa vizazi vijavyo na hii leo wakati wa umauti wake tungelimjua bila wasiwasi Dk. Kyaruzi na mchango wake katika uhuru wa Tanganyika na jinsi kama alivyosema mwenyewe vipi alimwachia TAA Nyerere.



25 May 2012
 
Mkuu WC, umemeliza kazi!
 

Ndugu yangu ukisoma hayo uliyoyaandika wewe mwenyewe utagundua ya kuwa unatoa makosa ya mawazo yako mwenyewe kwa kuonyesha kuwa wakatoliki wanafanya uzuri kuliko waislamu kwa maana hiyo basi kuwa mkatolini ni sawa na kuwa hodari kimasomo. Kinachonishangaza ni kuwa udini gani huo unaoukemea? ama kweli kwa maneno yako mwenyewe. DAIMA udini huendekezwa na watu wenye mawazo ya kimaskini" na kwa hili ndugu yangu mawazo yako umeshayaweka wazi jukwaani.

Na la pili la mwalimu Nyerere hakuwa mchawi na kafanya mengi ya manufaa kwa umma wa wa Tanzania, Afrika na ulimwengu kwa ujumla. Lakini kama mwanaadamu mwalimu alikuwa na kasoro zake. na Kwa sababu hiyo basi kauli ya "Zidumu Fikra Sahihi Za Mwenyeki wa CCM" hazikudumu. Swali la zilikuwa sahihi au siyo wache wana jukwaa waamue kwa ufupi tu Vijiji vya ujamaa vishakufa, Azimio la Arusha lishakufa, Mashirika ya Umma mahututi au yashakufa, majumba waliyonyang'anywa "mabepari" kwa manufaa ya umma sasa yanarejeshwa kwa "mabepari" kwa njia ya ubia.

Kuhusu masikitiko ya waislamu juu ya ubaguzi katika elimu. Tafadhali fanya research ya kwa nini East Africa Muslim Welfare Society ilivunjwa kwa hujuma. Wengine kwa kisingizio ilikuwa ikiongozwa na muhindi Aga Khan, wakati huo huo kanisa likiongozwa na maaskofu wa kizungu na kuchukuwa order kutoka Vatican.

Ndugu yangu kumwita Mtanzania mjinga ati kwa sababu ya dini yake huu si ustaarabu. Haya waachie wale tunaowaita kuwa hawakupata malezi ya wazazi. Kama waislamu wanalalamika, na kama ni sehemu ya jamii ya watu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, basi malalamiko hayo inapaswa yasikilizwe. Tutapanda na kushuka kuonyeshana vidole, lakini mwisho haki itajulikana.

MWENDA TEZI NA OMO MAREJEO NGAMANI
 
K,

Nadhani umefaidika na majibu yangu.

Nifaidike na nini,
mi naona unajichanganya tu, kwa mujibu wa maandishi yako (najaribu kuyatafuta humu ili niyaweke), Vita ya majimaji na ile ya Mkwawa ilikuwa ni vita ya kidini yaani Waislam na Wakristo (Wajerumani),
sasa inakuwaje vita ya kidini wakati Waislamu wakina Sykes, Wamanyema kutoka DRC (including babu yako) na Wale Wanubi (Juba, Darfur) waliwapiga Waislamu wenzao (Mkwawa na Majimaji)

Kama ukweli upo ueleze kama Ukweli, ile vita ya MAjimaji na ya Mkwawa ilikuwa vita kwa Maslahi ya Koloni la Kijerumani wala haikuwa Vita ya kidini kama unavyotaka kutushawishi
 
wewe lazima katika"before life" ulikuwa sangoma
 


Kumekucha...Mohamed Said, hebu tupe kisa cha huyu Sheikh.


[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="width: 601"]
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="width: 601"] Sheikh Suleiman Takadir

Sheikh Haidar Mwinyimvua, a personal friend of Sheikh Suleiman Takadir, member of TANU Elders Council and member of TANU National Executive Committee in 1958, recalls Sheikh Takadir's sudden and seemingly unprovoked attack on Nyerere:

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] ''It was at the TANU old office as we were waiting for the meeting of the National Executive. All of a sudden Sheikh Takadir stood up holding his walking stick pointing it out to Nyerere as he spoke, ‘This man will never come to favour us, he would come to favour his brethren! A stitch in time saves nine.' Sheikh Takadir repeated these words twice. All of us in that meeting room were flabbergasted as to the meaning of those words. I saw Nyerere crying. Nyerere turned to us and asked, ‘Did Sheikh Suleiman speak those words on your behalf?'. We replied in the negative and the meeting broke there and then.''

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Sheikh Takadir was among the early supporters of Nyerere and had campaigned vigorously for TANU addressing meetings on the same platform as him.

He had helped to wipe out the Christian stigma off Nyerere so that people in Dar es Salaam did not associate Nyerere with the Catholic Church but with TANU as a peoples' movement.

Sheikh Takadir's own position as chairman of TANU Elders Council commanded much respect. It was not that all those who were in that room did not understand what Sheikh Takadir had hinted out.

They understood each and every word spoken by him and its implications to the TANU leadership. What they could not grasp, perceive or believe was the fact that Nyerere, their beloved son and leader, would one day turn against Muslims and treat them as his enemies and rivals to his Christian faith.

At that time this was a far-fetched thought to them.

TANU and its precursor, the African Association, were not formed out of sectional interest, despite the fact that Muslims had always initiated their formation and taken active role in the leadership. Sheikh Takadir had touched a raw nerve.

The only way to prevent this new crisis from developing further was for Nyerere to give assurance that Muslims would be treated fairly after independence had been achieved.

In the meantime, unity of the people was important for the struggle ahead. This came to be Nyerere's theme in his speeches since the Takadir episode leading towards the hated tripartite election.

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] TANU-NEC, therefore, decided to form an impromptu committee to go to Sheikh Takadir's house at Msimbazi Street to ask him why he had abused Nyerere. Among the committee members was Idd Faiz, Chairman of TANU-NEC, Idd Tulio and Jumbe Tambaza. Sheikh Takadir told the committee that Nyerere was using the tripartite education condition to put fellow Christians in power on the pretext that they possessed necessary qualifications to assume government responsibility.

Sheikh Takadir then repeated the analogy he had directed to Nyerere, word by word, adding that he has no regrets for his stand.

Committee members, led by Idd Tulio stood up and left in silence. Sheikh Takadir was therefore expelled from TANU for raising the religious issue which, it was alleged, would divide the people. The chairmanship of the Elders Council was passed on to Idd Tulio.


[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Overnight Sheikh Takadir became a political pariah. Sheikh Takadir was an auctioneer and was cunducting his business from his house. Once the auction used to be the meeting place of TANU members. In the early days of TANU Sheikh Takadir was conducting his business from a house situated at Nyamwezi Street belonging to Mwinjuma Digosi, a jumbe appointed by the government.

When Digosi realised that Nyerere was visiting Sheikh Takadir at his place of business, he asked Takadir to seek accommodation elsehwere. He told Sheikh Takadir that he could no longer have him as a tenant because he as a jumbe appointed by the government can not allow his house to be a meeting place of troublemakers like Nyerere. Sheikh Takadir shifted his business to Msimbazi Street.

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] TANU members who used to meet at Takadir's premises to drink coffee, while away the time or discuss political events of the day. After his expulsion from TANU the place was abandoned and nobody went there. When Sheikh Takadir went to Kariakoo Market to buy foodstuff, no merchant would touch his money or even look at him. And when he saluted, people did not respond. Sheikh Takadir was ostracised by TANU and he felt the full weight of isolation. His business began to fail and so did his health. He became very lonely and depressed. Gone where the days when he recited surat fatha and gave dua before introducing Nyerere to the people of Dar es Salaam in the early TANU meetings at Mnazi Mmoja grounds.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Gone were the days when Sheikh Takadir built up Nyerere's image, elevating him to the level of a messiah. Soon after, Sheikh Takadir died. But before he died he left a legacy. A group of Muslims had gone to his house to taunt him, calling him names and ridiculing him, shouting at top of their voices the rhyme, ‘Takadir mtaka dini!' (‘Takadir the religious fanatic').

This group paid him a visit after coming from a rally in which Nyerere delivered a speech attacking Sheikh Takadir. Sheikh Takadir, it is said, came out of his house and told those Muslims, "There will come a day when you will remember me."


[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Mwafrika, the TANU weekly, under the editorship of Heri Baghdelleh and Robert Makange, gave Sheikh Suleiman Takadir front-page coverage, announcing his expulsion from TANU in heavy ink, his photograph in kanzu and Muslim cap staring out of the paper. [1]

Sheikh Takadir's photograph was put there for all to see the face of a ‘traitor' who wanted to slow down the independence process by wanting Muslims to be given assurance of their future because of their contribution in the independence struggle.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[1] Mwafrika, 11th October, 1958.
 

Hapo unajisikiaje? Roho inatamani kuona Founder wa TANU ni Abdu Sykes?
 

Ahsante kwa hili. Bwana Mohamed Said kajibu wengi. Na wengine wakimtukana naye akiwajibu kistaarabu kama mtoto wa kiungwana aliyepewa malezi mema na wazazi wake. Kukhitilafiana katika mas'ala si jambo geni. Hao wanaomwandama kwa matusi hawajaleta mada zao. Bwana Mohamed Said kaandika vitabu na references chungu mzima kwa msomaji mwenyewe kufanya utafiti wake mwenyewe. "Mohamed Said amefungua mlango wa kufanya utafiti katika masuala hayo yote." Haya nayanukuu kutoka katika kitabu chake "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968) Historia ilyofichwa Kuhusu Harakati za Waislamu Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza Katika Tanganyika" lakini badala ya ndugu zetu wengine kufanya huo utafiti wao wanaanza kuvurumisha matusi.

Nadhani topic ya mjadala huu badala ya kuwa "UCHOCHEZI WA MOHAMED SAID" ingelikuwa "CHANGAMOTO YA MOHAMED SAID YA KUFANYA UTAFITI"
[h=2][/h]
 
Hapo unajisikiaje? Roho inatamani kuona Founder wa TANU ni Abdu Sykes?

La Hasha, nadhani nafasi ya Founders isingetosha ndiyo manaa pakaandikwa Leader kinyume na hizo za mbele kuandikwa founders. Hapana shaka Mwalimu alikuwa leader na si hapo tu aliendelea kuwa Leader kama rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mpaka alipoamua kwa khiari yake kung'atuka mwaka 1985.

Aidha roho inatamani au haitamani hili jambo jengine. La muhimu ni kwamba wazee wetu wote waliotoa mchango katika kututoa katika ukoloni wakumbukwe bila ya KUBAGUA na hao kwa uchache tu wakiwemo Sheikh Suleiman Takadir, Mwalimu Julius Nyerere, Sheikh Hassan bin Amir, John Rupia, Dosa Aziz, Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Oscar Kambona, Bibi Titi Mohamed, Bilal Rehan Waikela, Saadani Abdu Kandoro, Kasella Bantu, Na wengine wengi!

MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA
 

"kama umeonewa ni suala la kuappeal tu..."[/QUOTE] ALIYEONEA NI NANI? NA UTA-APPEAL KWA NANI? hapo ndiyo utakapopata jibu nalo ni kugonga ukuta!
 
We tapeli wa kinigeria umeibukia hapa? Humpati mtu hapa kakojoe ipumzishe.

Bwana Yericko tafadhali ondosha jina la muheshimiwa baada ya Yericko. Kwa sababu ya mstari huu tu umetuonesha ni mtu wa aina gani kwa maneno yako. Tafadhali fanya hili kwa heshima ya mwenye jina hilo
 
Kwabahati mbaya kwako nikuwa hujui kuwa wanaukombozi wote wanaenziwa na serikali na sie tuaminio katika historia ya kweli tunawajua.
 
mzee Mohamed Saidi, ni kweli unakiri kwamba hukuwahi kuziona na kuzisoma katiba za TAA na TANU? na bado unajiita umeandika historia ya mapambano ya kudai uhuru wa Tanganyika "objectively"!
 
Bwana Yericko tafadhali ondosha jina la muheshimiwa baada ya Yericko. Kwa sababu ya mstari huu tu umetuonesha ni mtu wa aina gani kwa maneno yako. Tafadhali fanya hili kwa heshima ya mwenye jina hilo
Ndugu yangu utaibiwa wewe, huyo ni mpigaji wa kinigeria wa mitandaoni ameni pm kwa meseji ya wizi kkama demu, lakini hapa anajigeuza kama dume
 
mzee Mohamed Saidi, ni kweli unakiri kwamba hukuwahi kuziona na kuzisoma katiba za TAA na TANU? na bado unajiita umeandika historia ya mapambano ya kudai uhuru wa Tanganyika "objectively"!

Hii ''kukiri'' unakusudia kitu gani?
Kweli sijaziona wala haikunipitia kuzitafuta.

Sijui na hii''objectively'' una kusudia kitu gani.
Mimi sina tatizo na kitabu changu.

Nimekiandika kama nilivyotaka mimi.
Sikukiandika kumfurahisha mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…