Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Mimi nisiyejua kusoma sawa sawa naona kuna conflicting information.Mohamed:Sheikh Hassan bin Amir Muunguja alikuwa ndiye mufti wa Tanganyika na aliwakilisha Waislam ambao hasa ndiyo waliokuwa wakiongoza mapambano dhidi ya serikali. Said Chaurembo aliwakilisha Wazaramo wa Dar es Salaam na vitongoji vyake. John Rupia kutoka Mission Quarter alikuwa mfanya biashara tajiri na mfadhili wa chama. Stephen Mhando Mbondei kutoka Muheza alijulikana kwa misimamo mikali aliwawakilisha wasomi wa Makerere, Dk. Kyaruzi akiwa mmojawapo
Nyerere alikuwa na akina Mwapachu Makerere, bila shaka Makererian wengine kama akina Kyaruzi walimfahamu pia.Mohamed: Hiki ni kitu kikinishughulisha sana. Jambo hili likishighulisha sana fikra zangu kwa kujiuliza mbona Kyaruzi anamruka Abdulwahid Sykes katika historia yao ya uongozi wa TAA mwaka wa 1950 na kumwingiza Nyerere ilhali Nyerere wakati ule hakuwa anafahamika na yeyote katika duru za siasa za Tanganyika? Nikawa nashangaa nikijiuliza kwani Dk. Kyaruzi hajui kuwa Nyerere aliingia katika uongozi wa TAA mwaka 1953? Nilikuwa nikijifariji kwa kusema kuwa haya ndiyo matatizo ya historia ya uhuru wa Tanganyika
Alikuwa katibu wa AA tawi muhimu sana la Tabora.
Alipelekwa kwa Sykes na Kasella Bantu. Nyerere alihudhuria mkutano wa AA iliyozaa TAA.
Hivi mtu akisema hafahamiki na yeyote kuna ukweli hapo!
Mwenyezi mungu anazidi kutuwekea wazi yale yaliyofichwa na yasiyosemwa. Mwenyezi anazidi kuthibitisha ushahidi wetu kuhusu udini. Hapa Mohame anamnukuu Abdul Sykes aliyesema ''kwa ajili ya masilahi ya waafrika na yale ya jumuiya ya waafrika KWA UJUMLA''. Abdul Sykes, mwanaharakati na kiongozi mzalendo hakusema kwa ajili ya Waislam kama Mohamed anavyopotosha umma.Mohamed: Kamati ya siasa ya TAA ilipeleka mapendekezo yake ambayo yalitiwa sahihi na wajumbe wote wa kamati ya siasa. Sheikh Hassan bin Amir, Abdulwahid Sykes, Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, John Rupia, Stephen Mhando na Said Chaurembo. Katika taarifa yake ya TAA ya mwaka ya 1950 Abdulwahid aliandika: "Kwa ajili ya maslahi ya Waafrika na kulinda maslahi ya chama hiki na yale ya jumuiya ya Waafrika kwa ujumla, chama kimeweka wakili atakayeshauri juu ya mambo ya sheria. Wakili huyo ni Bwana E. E. Seaton wa Moshi. Mara kwa mara amekiandikia chama hiki juu ya masuala mbali mbali ya siasa, na kwa kiasi kikubwa ushauri wake umesaidia wakati chama hiki kilipokuwa kikitayarisha mapendekezo juu ya katiba."
Mohamed amesema Waislam ndio walioongoza mapambano, hata kama aliji contradict kwa kuingiza majina ya akina Rupia, Mhando n.k. bado Abdul Syke anamsuta kuwa kazi hiyo haikufanywa kwa masilahi ya Waislam bali Waafrika kwa ujumla.
Hoja ya udini imetoka wapi?